Hii ina carbon copy (CC) au Cubic Centimeters = nguvu za mtumiaji + gravity.
Kwa tusiojua vizuri majambo haya copy (kama unavyoitania) ni ni uwezo wa chombo kujenerati pawa. Naambiwa 1,000 CC ni sawa na lita moja.
Kwa vyovyote vile uwezo wa chombo kujenerati pawa inategemea na uzee wa hicho chombo. Kwa bahati mbaya hapa TZ hasa kwenu bongo mnanunua magari yaliyozeeka (mitumba) ingawa mnajisifia ati siwezi kuendesha BW (Baby Walker) aibu kubwa.
Hivi unataka gari la kujenerati pawa kubwa na foleni hizi? Watu wanafikiria kusafiri highway na magari, hawaoni fastjet mtu kutoka Dar hadi mbeya, mwanza au KIA ni shs 43,000 kwa muda wa lisaa! Kwa nini karne hii uhangaike na kununua gari ili uende Kishimundu kuonyesha kuwa na wewe umo, wakati kuna shato za kutoka KIA 10,000 na taxi 2,000 umefika Kishimundu. Jiulize unaenda huko kwenu mara ngapi?
Naona shida na hizi tambo za MMU, pengine ni utafutaji wa free K unatusumbua tulio wengi, karibuni Njinjo