Umechanganya mambo mawili kwa wakati mmoja.
Video ya everythingApple pro ni proof kwamba iphone hazina lead tena kwenye optimisation na speed ya simu kwa ujumla nimekupa huyo ni fan wa apple asie na bias ila nyie huku endeleeni tu kutetea.
Are you sure EverythingApple Pro hayupo Bias? inaonekana unajicontradict mwenyewe sasa, ni wewe ndie ulisema kuwa Apple ndio mwenye processor zenye speed kuliko wote, leo hii unasema kuwa hana tena Lead? mhhh
Na fortinite nakujibu sijui mara ya ngapi hiii, lete video inayoonyesha setting usiniletee video za kitoto zinaonesha huku na huku basi,unajua naweza kukutengenezea hapa video kama hio nokia ya tochi inarun hilo game smooth kuliko simu yoyote duniani, ni easy kufake hizo video. Tafuta video moja ya pc gaming review ya vlogger mkubwa kama linus hivi then utaona gaming review inafanywaje.
Lete wewe basi yenye kuonesha settings unazozungumzia. Tujaalie zote mbili zilikuwa zinarun under minimum settings, huoni kuwa iPhone ina perform better na 4GB rams zake over Samsung's 6GB ram? Why?
Ndio nategemea kwa wakati fulani simu ya milioni iwe na kitu fulani kutokana na technology ilipofikia, huwezi ukatoa hela nyingi na kuuziwa kitu kisicho na thamani ya hela.
Sasa kwanini unanambia kuwa mimi ndie niliekariri pesa fulani inanunua nini? wakati ni wewe mwenyewe ndio uliekariri.
Ndio maana nikakuambia hapo juu, unapoipinga kampuni kubwa zaidi ya ram duniani unatakiwa uwe na hoja zenye mashiko,huleti hoja nikuamini wewe ama samsung? Na kuna utofauti baina ya s9 na note 9 wa miezi 6.
Bado mkuu hujatetea unachotetea. nazungumzia Note 9 na sio s9. Note 9 inakuja na version yenye 6Gb of Rams na nyengine inakuja na version ya 8Gb of rams. Sasa kama wewe unasingizia kuwa Samsung hakuweza kuweka 8GB of rams kwenye S9 kwa sababu ramu hazipachikwi tu na huenda akawa hakuwa na hio tech miezi sita iliopita, tena vipi anatoa simu same model, made during same period lakini with different Ram memory? Kwanini asiweke tu 8Gb of rams kwenye note 9 zake zote?
Officially umequalify kuwa isheep mkuu, nimekupa website kibao tena za fans wa Apple na website kubwa kubwa hata google mwenyewe sasa hivi intel kapitwa vibaya vibaya na qualcomm kwenye modems sehemu nyengine mara mbili zaidi bado unabisha.
Ba intel ni mtaalamu wa cpu, haimaanishi ni mtaalamu wa kila kitu.
Nikuulize, what is the reason behind to call me an isheep?
😀
Kwakuwa Apple kaona bora atumie intel instead of Qualcomm ndio amekuwa ana opt for low quality products? Kwaio basi kampuni nyingi wanatumia Low quality products, kwa sababu almost all PCs zinatumia intel chips, that means they are of low quality!!!
hivi mkuu asilimia 1.7 ya mamia ya mamilioni wanayouza Apple ni ndogo?japo hizo data hujazithibitisha ila still ni namba kubwa,ni zaidi ya mkoa wa kawaida wa Tanzania.
Na wewe ni fan wa Apple utaona? Dunia nzima imeona ila wewe hutaona,BBc CNn watareport ila kwako itakuwa ni uzushi tu.
Na hilo ni tatizo la hardware halina uhusiano wowote na software,tatizo linatokea pale unapoziba mkono wako kwenye Antenna,tumia akili angalau kidogo nakuomba. Futa neno Apple kichwani mwako ufikiri angalau sekunde
1.7% out of 100% umeiona ni kubwa sana kuliko 98.3% working phone with similar design... Ata kipofu mkuu hawezi kukubaliana na wewe.
Apple akipiga mayowe tu, media zote na haters kama wewe mnaamka mkiombea liwe baya mpate la kuandika. Kuripotiwa na cnn au bbc ndio ujue kama Apple is a Big company. All eyes on Apple. ukitaka usitake, najua hili linakuuma sana unapoona Apple yupo juu ya Nokia, unapoona iphone ni simu ya juzi tu lakini Nokia ipo zamani kifo cha mende.
Hivi watu wangapi wametekwa Tanzania na Cnn na BBc hawana habari lakini katekwa Mo tu habari imefika kote uko? ndio ujue kuwa Apple ina influence kubwa sana. Habari za nokia sizipati, ni juzi tu hapa naona na wao wameamua kuingia kwenye Notch city, wakati wenzao walipofanya waliwacheka na kuwazomea
😀
Hakuna mahali nimekataa kuwepo kwa tatizo la antenna, au ipo sehemu? kama ipo onesha basi. Mimi nashangazwa na mahaters, mnavolifanya kuwa simu zote mbovu, mapaka ukadai kuwa niende nkanunue simu Aggrey nitaikuta na hilo tatizo. Umemaanisha kuwa every iphone 4 ilikuwa na hili tatizo, na huo ni uongo! kwa sababu binafsi nilikuwa natumia iphone 4 na sijawahi kuexperience hilo tatizo la kwamba eti network bar zinapungua.
Na hilo tatizo linaweza kuwa hardware ONLY na linaweza kuwa Hardware with SOftware issue, hata apple wenyewe walipoletewa hili tatizo katika statement walisema ni software Glitch na watajaribu kutoa update.
Juzi hapa, kulikua na charge gate, mbona tatizo limekuwa solved kwa kutumia software basi wakati port ni harwdare na cable yako ni hardware? lakini Apple wamefix kwa software tatizo lua kucharge. Au njoo uwaambie wasomaji kuwa nalo ni jambo jipya kuwa tatizo la kuchaji simu linasolviwa na software wakati ni hardware.
Hapana unapo preload ramani kwenye simu unataka watu watumie hio, wangapi wana fikra ya kwenda store na kuchagua nyengine?uthibitisho angalia malalamiko waliyoyapata Apple na kesi za polisi zilivyokuwa nyingi.
Sasa jiulize umetoa milioni 2 umenunua simu,unapanda gari lako unaiambia simu ikupeleke morogoro,simu inakupeleka unashuka upo lindi,is this your definition of high quality? Walijua Apple ila they dont care sababu wanajua kuna watu wanaabudu tunda watanunua tu. Wangapi walipelekwa kwenye misitu?wangapi walipata ajali?
Sikiliza mkuu, Tatizo huwajui watumiaji wa Apple products. The only reason, watu walitumia Apple products kwa sababu wanapenda kutumia Apple products, hivo basi wakaona kuwa finally sasa wanayo Map app from the manufacturer, hawa ni watu ambao wanapenda kubaki kwenye eco system ya Apple. Walivotoa Apple maps, kama utaamini, sijawahi kuifungua hio app mpaka ale nilipoona malalamiko ya watu na kusema ngoja nione watu wanacomplain nini, nikafungua maeneo nnapokaa wala sikutaka kwenda kwenye miji nisioijua, nilichokuta nilicheka, kwa sababu wanadata za tangu yaani mji au haukuwa, ni very old data information. I have always been a google map user kwa sababu najua kwanza ipo zamani na wako well experienced na wanajua ku collect data, kama sikosei, its not even apple collecting data for their map app, sijui kuna kampuni walinunua ambayo inahusu maps. Yaani its not something from scratech bali wali acquire from reay made company.
How can a software problem classify a device as low Quality or makes a company low quality? Mbona husemi Nokia kuwa wao ndo one of those with low Quality standards? Unatumia symbian os ambayo iko super vulnarable to virus. No wonder Symbian became a failure!
So umehamia kwenye mauzo na umeshindwa ku compare features? Hata dagaa wanauza sana kushinda nyama ya kuku ama samaki wakubwa it doesnt make dagaa better. Unaweza list ya features ambazo simu yako pendwa ilikuwa inafanya zaidi?
Anae brag Nokia kauza simu milion 500 nani kwani? mie au wewe?
Sina haja ya kulist features ambazo Apple made them better, you can see for yourself. Nokia n9 had no home button, au sio? who cared? iPhone made it better. Nokia n9 ndio ilikuwa na hizo gestures za kunavigate, Apple made them better, multi touch screen were there, Apple made them better, the notch was there au sio? Basi Apple made it better, now even the Android maker ame optimize OS yake for the Notch
😀 the list keeps on Going.
Halafu huo mfano wako wa dagaa, ndugu yangu huoni unakurudia. Wewe unasifia kuwa Nokia kauza simu 300 milioni only one model, hii nokia hapa ndio dagaa lenyewe, hawa kina iphone na samsung ndio nyama na kuku na samaki wakubwa, kwaio vidagaa nokia doesnt mean they are better. Naomba ukae ufikirie tena huu mfano wako ndugu yangu. Unakurudia.
Model za biashara hazifanani na Nokia alikuwa true deicated kwa watu wote duniani? Hakuwa bepari. Kampuni pekee iliokuwa inafanya research za simu za shilingi 30,000.
Na hata mapato yao at that time yalikuwa makubwa.
Kwani Apple hafanyi research au? Mbona apple ina sifa nzuri ya customer care kwanza japo kuwa wanapenda kuwagonga watu kwenye kurepair. Kukiwa hakuna tech ya kutengeza kitu fulani, utafanya research tu hata kama ni cha buku 1, as long as unajua kitakuletea faida. Kwaio wakati Nokia wana wazo la kutengeza nokia tochi, itabidi wafanye research and development kwanza.
Sio Apple tu, kila kampuni inafanya reasearch kwenye product ambayo wanataka kutengeza.
Hapana mkuu kaangalie Aggrey na msimbazi matangazo ya Tecno na itel kama uchafu vile yalivyo mengi.
Inategemea na aina ya tangazo, yapo yanayotafuta wateja wa tochi pia. Na sijaelewa mantiki yako hapa. Unataka kukataa hayo makampuni hayaspend 10b usd kwenye matangazo?
Tecno Spark 8, haina lengo la kumwambia mtumiaji wa nokia tochi ahame atumie tecno k8. ni 2 different market. Tecno, itel na wengine, wanaotumia android, wanawaambia watumiaji wa izi samsung kuwa na sisi tupo tena bei rahisi na unapata all service.
Huwezi kukuta s2 eti inalinganishwa na nokia torch, wakati target market ni tofauti.
Hii ni public forum badala ya kunituhumu kwa heshma na taadhima naomba useme uongo wangu.
Umedai kuwa Apple ditched 3d touch, while ipo kwenye simu zake inaendelea kutumika. Unasema kuwa Nokia akikohoa tu Apple anatoa matrilioni. Mbona haendelei kukohoa basi. Unawaambia watu kuwa iphone 4 (na ulimaanisha in general) kuwa zinatatizo la antenna gate na ukafikia kusema mtu aende aggrey akanunue iphone 4 basi atakuta hilo tatizo. haya uloyasema yana ukweli? 3d touch bado inatumika, Nokia kakohoa mara moja tu na hakohoi tena, iphone 4 sio zote zilizoathirika na unaweza kwenda agrrey ukapata ilokuwa haijaathirika. Ukaenda to the Extreme, eti unaweza kutengeza fortnite ikarun kwenye Nokia torch!
Go through Apple patents.
Kuna utofauti baina ya manufacturing na inventions ni vitu viwili tofauti na kuhusu Nokia na apple unafahamu kila iphone inayouzwa Nokia anapata hela kwa amri ya mahakama?na mwaka jana tu Apple kamlipa nokia 2B (trilioni zaidi ya 2) baada ya figisu za mahakamani tena.
Sio Nokia tu, Apple analipa na wengine, ndio ujue kuwa katika uwanja wa technology kuna kutegemeana. Kama zilivo simu zako za Nokia zenye android, wananunua snapdragon kwa Qualcomm, wangetengeza zao basi.
Mkuu nimekupa ushahidi kipindi elop anaiua symbian Nokia alikuwa anauza simu kuliko samsung na Apple combined, na symbian ilikuwa ni top operating system at that time,kama una data tofauti naomba uzilete hapa na sio maneno matupu.
How old was symbian? and how old was iOs na Android by that time. Hata saivi kama shabiki wa liverpool anakwambia Liverpool ilikuwa ikiongoza, tulia, watu wameanza kuingia sokoni ndani ya muda mfupi tu wamempiga na chini Symbian na nokia wake wakitapatapa taabani, mnamsingizia Elop LOL!
Kama symbian au Meego ilikuwa na uwezo wa kuendelea kudominate manake ingekuwa profit kwa Nokia investors, kwanin hawajaendelea nayo? Izo pesa walizozipata wameenda kuekeza Alcatel. Nlifikiri zimetiwa mfuno kumbe zimerudi tena kwenye uwekezaji. Wamejua kuwa HAWAWEZI KU COMPETE WITH THE RISE OF IOS na ANDROID DEVICES!
Kuna mambo mawili makubwa yametokea duniani mwaka jana.
-Hmd amerudi na simu za nokia
-kutoka kwa jio phone india.
Nokia android kama kawaida, haina ishu.
Mambo hayo yamepelekea.
-kwa mara ya kwanza duniani mauzo ya smartphone yameshuka
-mauzo ya feature phone yamepanda.
Kushukua kwa mauzo ya smartphone haimaanishi kuwa eti features phone (especially Nokia) ndio anatereresha market, tatizo la smartphone ni ghali sio wengi wenye ku affroc na hasa hivi sasa. Hivi unasahau kuwa a phone is more than just a calling an texting device saiv? Facebook kwa sms pia unaweza kwenye nokia torch.