Kwanini siku hizi wanandoa wengi hawapendi kuvaa pete za ndoa?

Hyrax

JF-Expert Member
May 20, 2023
604
1,534
Kuna jambo linanitatiza sana maana nimefanya research kiasi nikuwa huko mikoani na hata nilipofika huku Dar hili nimeliona sana.

Kwa mujibu wa utafiti wangu nilioufanya kwa kiasi toka miaka ya 2000 wanandoa wengi japo sio wote hawaonekani kuwa na pete za ndoa kwenye mikono yao, nilijaribu kuuliza baadhi ya wanandoa upande wa jinsia ya Me wengi walitoa sababu mbambali japo nyingi hazina mashiko na Kwa jinsia ya Ke ni hivyo hivyo.

Nimejaribu kutafakari ila naona kama kuna sababu zingine zenye uzito zaidi ambazo zinawafanya wawe si watu wa kuvaa pete za ndoa japo wanaishi wote kama wanandoa na wengi wakiwa sawa tu.

Hii kitalaamu imekaaje wajuvi mje mnifundishe Je, kuvaa pete ya ndoa ni Ushamba? Au si kitu cha maana kwenye utamaduni wetu sisi waafrika?
 
wapo wasiotaka kufukuza michepuko isiyofahamu kuhusu ndoa za
Dah kizazi hiki cha zinaa unadhani kinaweza dhibitiwa kwa kuvaa pete?. Hata Pete uzivae mwili mzima, kama huna hofu ya Mungu aliyesema ndoa na iheshimiwe na watu wote ni kazi bure tena hiyo michepuko ndio iko confortable zaidi na hao wenye Pete kuliko hata wasionazo.
 
Hapana,lile ni agano lako na umpendaye,pia ni udhihirisho ya kwamba ur already taken🤣🤣🤣🤣unataka tu kumsaliti mama yeyoo
Hamna Joannah, nilishamwambia kuwa hii kitu sitavaa, nilivyoivua sikuwahi kuirudia tena, huenda hata ishauzwa na sijui. Agano langu lipo moyoni...

Halafu ujue kusaliti haina cha pete wala nini, ukiamua kusaliti ni unasaliti tu. Hata hivyo kidume kudumu na Ke mmoja ni mtihani mkubwa sana kuwahi kutokea duniani, nilijaribu nimeshindwa😀😀
 
Back
Top Bottom