Majibu Kuntu ya kwanini ndoa nyingi zinavunjika sana siku hizi haya hapa

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,176
2,279
Ndoa nyingi za sasa zimekuwa zikivunjika kwa sababu mbalimbali ikiwemo wanandoa kuishi maisha ya kuigiza kabla ya kuoana na baada ya kufunga ndoa kujikuta wakifahamiana kwenye uhalisia hivyo kuondoa kabisa yale matarajio ya mmoja kwa mwenzake. Hii ina maana wakati wa uchumba sehemu kubwa ya maisha yao ilikuwa ni kufeki kwa kila kitu;

UVAAJI
Unakuta mwanamke au mwanaume alikuwa anaonekana ni mwenye kupenda kuvaa mavazi ya staha, mavazi ambayo kila mwanaume au mwanamke anapenda kuwa naye, lakini baada ya kuingia kwenye ndoa, kila mtu anaonesha uhalisia wa mavazi anayo-penda. Mwanaume anashangaa kumuona mkewe ghafla ameanza kuvaa vinguo ambavyo vinambana au vinaonesha sehemu kubwa ya maungo yake.

Kwa tabia hizo, ni dhahiri watashindana au kila mtu atataka mwezake asifanye jambo fulani na hapo ndipo mgogoro na mfarakano unapotokea na matokeo yake ndoa inasambaratika.

UTII
Wakati wa kutafutana katika urafiki wa mapenzi au uchumba, kila mtu anakuwa na utii wa kipekee kwa mwenzake ili kumfanya mwenzake amvutie. Kwa hiyo baadhi ya tabia zile za asili, wapenzi wengi huzificha ili wasije wakashindwa kutimiza azma zao. Lakini wakishaingia kwenye ndoa, tabia halisi hujidhi-hirisha kwa wanandoa, ule utii aliokuwa nao mwanamke kwa mumewe au mume kwa mkewe hupotea, kila kitu inakuwa ni kuulizana na kujibizana kwa hasira.

HURUMA
Katika kipindi cha urafiki au uchumba, kila mtu anakuwa tayari kuonesha huruma kwa mwenziye. Hata kama kiasili hana huruma lakini kwa kuwa anakuwa na lengo maalum, basi hujifanya ana huruma ilimradi tu afanikiwe.

Lakini baada ya muda uhalisia wa tabia za kila mmoja hujidhihirisha na hapo ndipo kila mtu huhisi kuwa mke au mume aliyenaye si sahihi, si yule mwenye sifa alizozihitaji.

KUONGEA
Wakati mwingine wapenzi hufeki hata namna ya kuongea, huongea kwa ustaarabu, huongea kwa kujifanya muungwana, mwenye hekima, anajiamini lakini katika uhalisia si mtu wa hivyo, pengine ni mtu wa kuropoka. Lakini anakuwa ameamua ‘kujikontro’ ili amteke vizuri mwenza wake. Kimbembe ni pale watakapokuwa kwenye ndoa, kwani baada ya miezi kadhaa, tabia halisi au asili ya mhusika kujitokeza na wakati huo hujikuta hawezi kufeki tena maisha kwa sababu muda mwingi anaishi na mpenzi wake, tofauti na kipindi kile ambacho wako kwenye uchumba ambapo kila mmoja alikuwa mbali na mwenza wake.

MATUMIZI
Kipindi cha uhusiano baadhi ya wapenzi hujifanya ni watu wenye matumizi mazuri ya fedha na rasilimali nyinginezo lakini akishaingia ndani basi huonesha utumiaji wake mbovu wa rasilimali hizo. Kwa mtu mwenye malengo, mtu wa namna hiyo hana nafasi katika maisha yake.

FARAGHA
Kuna wapenzi wengine hudiriki hata kufoji namna ya kushughulika wanapokuwa faragha, utakuta anajitutumua ilimradi asioneshe udhaifu wake na kwa mtu ambaye yuko naye, anaona huyu ndiye anafaa lakini anapomuweka tu ndani basi uwezo wake wa faragha udhihirika na hapo ndipo mmojawao anaanza kutamani kutoka nje kwa sababu alichokiona siku za awali sicho alichokutana na nacho.
 
Kwenye mavazi sina uhakika sana maana nimeshuhudia watu wengi wa karibu wakishaolewa ndo wanaanza kuvaa stara.
 
Back
Top Bottom