Kwanini sijaonekana kwenye picha za Iftar ya Ikulu siku ya Jana. Nimechukia sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,905
Kwema Wakuu!

Sisi wengine ni Watu wa misifa, Watu wa mitandaoni, Watu wa kujionyesha, Watu wa kujimwambafai tukio kama la jana kwangu lingeniongezea Credit muhimu sana.

Kutokuonekana inamaamisha sikuwepo ama? Kutokuonekana kwenye picha yoyote au video yoyote ya tukio inamaanisha sikuhudhuria ama! Wachukua Kamera mnieleze kwa nini hamkunichukua kwenye Rekodi? Why? Kwamba hamkuniona Ama! Kwamba hamkutaka Watu ambao hawakuhudhuria wasijue nilialikwa Ama!

Kwa ambao hamkuwepo, nilivalia Kanzu yangu safi kabisa ambayo niliinunua Pale Magomeni, mahususi kwaajili ya mwaliko wa heshima wa Iftar. Ilikuwa Kanzu ya Kahawia yenye udarizi mweusi kwenye Kola na sehemu ya vifungo ingawaje haikuwa na vifungo.

Nilinunua pia Sendo nzuri ambazo muuzaji alinijuza zimetokea Uturuki. Kichwani nikanyoa vizuri. Ni kweli nilipendeza na nilifanania mwaliko wa Ikulu.

Nisingepanda Daladala kwa namna ile. Nilikuwa nimependeza na ninanukia marashi mazuri na manukato ya mafuta aghali. Nikachukua Bolt, huyo mpaka kwenye mwaliko.

Kukata Stori isiwe ndefu kwani bado nina Kwikwi za hasira. Vile nimependeza, vile nilivyokuwa natembea kitasha, vile nilivyokuwa nimebeba chakula na ninakula chakula kidizaini na kistaa hivi hakuna mchukua kamera yeyote aliyenibahatisha kuniona?

Humu mtandaoni Watu watahitaji ushahidi. Kule nako sikuruhusiwa kuchukua Kamera. Sasa nitatamba vipi ndugu zanguni? Inamaana hapa sina tofauti na mtu ambaye hakupata Mwaliko.

Mwenye picha yangu nikiwa kwenye mwaliko tafadhali ninaomba. Masuala ya kusema tulikutana wenye uwezo kwenye Iftar na iftar inatakiwa Watu wasio na uwezo hayo tuachane nayo kwanza.

Taikon wa Fasihi
Dar es Salaam
 
Mi pia nilikuwepo ila watu wote walikua hawanijui nikiwasogelea wananiona naharibu stori zao nikaenda kukaa karibu na jokoni
Pole sana
π•Žπ•’π•žπ•–π•œπ•¦ 𝕔𝕣𝕠𝕑 π•’π•šπ•€π•–π•–π•–
Picha moja tuu ingetosha. Mimi sikuwa nahitaji picha nyingi. Moja tuu
 
β„•π•šπ•œπ•¦π•‘π•’π•₯π•šπ•– 𝕖-π•žπ•’π•šπ• π•ͺ𝕒 𝕀π•₯𝕒π•₯𝕖 𝕙𝕠𝕦𝕀𝕖

Nipe ya Wapiga picha. State house Achana nao. Wao ndio wameandaa tukio. Mimi ishu yangu ni kwa wapiga picha na wanaorekodi matukio.
 
Kwema Wakuu!

Sisi wengine ni Watu wa misifa, Watu wa mitandaoni, Watu wa kujionyesha, Watu wa kujimwambafai tukio kama la jana kwangu lingeniongezea Credit muhimu sana.

Kutokuonekana inamaamisha sikuwepo ama? Kutokuonekana kwenye picha yoyote au video yoyote ya tukio inamaanisha sikuhudhuria ama!
Wachukua Kamera mnieleze kwa nini hamkunichukua kwenye Rekodi? Why? Kwamba hamkuniona Ama! Kwamba hamkutaka Watu ambao hawakuhudhuria wasijue nilialikwa Ama!

Kwa ambao hamkuwepo, nilivalia Kanzu yangu safi kabisa ambayo niliinunua Pale Magomeni, mahususi kwaajili ya mwaliko wa heshima wa Iftar.
Ilikuwa Kanzu ya Kahawia yenye udarizi mweusi kwenye Kola na sehemu ya vifungo ingawaje haikuwa na vifungo.
Nilinunua pia Sendo nzuri ambazo muuzaji alinijuza zimetokea Uturuki. Kichwani nikanyoa vizuri. Ni kweli nilipendeza na nilifanania mwaliko wa Ikulu.

Nisingepanda Daladala kwa namna ile. Nilikuwa nimependeza na ninanukia marashi mazuri na manukato ya mafuta aghali. Nikachukua Bolt, huyo mpaka kwenye mwaliko.

Kukata Stori isiwe ndefu kwani bado nina Kwikwi za hasira.
Vile nimependeza, vile nilivyokuwa natembea kitasha, vile nilivyokuwa nimebeba chakula na ninakula chakula kidizaini na kistaa hivi hakuna mchukua kamera yeyote aliyenibahatisha kuniona?

Humu mtandaoni Watu watahitaji ushahidi. Kule nako sikuruhusiwa kuchukua Kamera. Sasa nitatamba vipi ndugu zanguni?
Inamaana hapa sina tofauti na mtu ambaye hakupata Mwaliko.

Mwenye picha yangu nikiwa kwenye mwaliko tafadhali ninaomba.
Masuala ya kusema tulikutana wenye uwezo kwenye Iftar na iftar inatakiwa Watu wasio na uwezo hayo tuachane nayo kwanza.

Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Taiykuon wa kiswahili unadiriki kuandika
""""....Wachukua Kamera....?"
 
Back
Top Bottom