Azam mmejitahidi sana kwenye Mechi ya Ufunguzi AFL

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Kuna siku nilikuwa nabishana tu na mfanyakazi wa Azam, nilimwambia kwamba kamera za HD wanazotumia Multi Choice ni tofauti na wanazotumia Azam, na wanazotumia Multi Choice ni tofauti na zile wanazotumia Sky Sport.

Tulibishana kidogo na alisema kamera za HD zote ni sawa. Nilichouliza kwa nini mechi za Ligi ya Uingereza kimuonekano ni tofauti na Azam akicheza na Yanga Taifa? Mimi nauona utofauti mkubwa sana wa uang’avu lakini jamaa yangu alibisha sana.

Sasa jana nilipokuwa naangalia mpira wa Simba na Al Ahly, nilishangaa kuona kamera zikiwa na muonekano wa tofauti kabisa. Nilipouliza, nilijibiwa kwamba kamera wamezishikilia Wafaransa. Ikanibidi nikubali kwa sababu ya muonekano wake, si ule tuliokuwa tumeuzoea kipindi chote.

Wewe unaweza kuwa na kamera moja na anayotumia mtu fulani Ulaya lakini kwenye setting jamaa akakupiga vibaya sana. Nikakumbuka siku moja nilimpa rafiki yangu Barnaba Salu simu yangu anipige picha. Huyu jamaa ni mtaalamu wa kupiga picha na video, ile picha alivyonipiga na kunionyesha, nikamuuliza ni kamera ya simu yangu ndiyo imepiga hivi? Akajibu ndiyo. Nilishangaa sana, kumbe jamaa aliingia kwenye setting na kufanya mambo yake.

So Azam wana kamera nzuri sana, ila hawana wataalamu wakubwa wa kuweza kuzichezea, yaani ni kamera za HD lakini picha zake si kama za HD tunazozijua, labda niambie kwamba kamera za za jana hazikutumika zile tulizozizoea.

Suala la kamera yoyote duniani ni setting, unasikia tu Bieber amefanya video moja kwa iPhone yake, ila ukichukua iPhone kama ile ukafanya video inaonekana mbaya, kumbe ndugu yangu hujui kuseti kamera.

Kwa jana, kuanzia graphics mpaka uang’avu wa picha ulikuwa mkubwa sana. Wapiga picha wa Azam nahisi watakuwa wamejifunza sana kupitia kwa hao Wafaransa. Kama watakuwa hawajajifunza basi kutakuwa na shida mahali.

Kwa kawaida wanapokuja watalaamu wa kitu fulani nchini, nenda kaungane nao ujifunze mabo madogomadogo kwa ajili ya manufaa yako baadaye, haiwezekani mtu akakubania kwenye vitu vidogo kama hivyo.

Uang’avu wa picha za jana kuanzia mchana mpaka muda wa mechi uwanjani, niliona kabisa kuna utofauti mkubwa sana. Graphic ilikuwa ya kibabe mno yaani mpaka unatamani kila siku ziwe hivyohivyo.

Ni somo kwa wapiga picha. Usijifunze picha studio kwa jamaa halafu ukataka kamera, nenda class kajifunze, siku hizi zipo mpaka course kwenye mitandao, ingia huko, soma sana, nakuahidi hutokuwa kama ulivyo sasa hivi.
 
Wa upgrade camera zao matangazo ya pembeni yalikuwa hayaonekani vizuri

Mpira wa simba uliogonga mwamba na kutaka kuingia golini ilipaswa pia wau zoom kule juu uliko elekea na namna ulivyo rudi golini. Ila kwa sababu camera zao ndo hivyo tena hawakuweza kuonesha engo ile
 
Nje ya mada, hakuna Ligi Kuu ya Uingereza, kuna Ligi Kuu ya England inayozihusisha Klabu mbili za Wales Cardiff na Swansea na hiyo ni kutokana na nchi hiyo kutokuwa na Ligi yake ya soka zaidi ya rugby. Ukisema Ligi Kuu ya Uingereza maana yake ni pamoja na Scotland na Republic of Ireland ambazo zina Ligi zake soka. BBC walishatolea sana ufafanuzi hili.
 
Nilifanikiwa kuangalia, kuna pale wale dancer wakiwa kwenye ule mduara , halafu kamera ikawa inachukua picha kwa juu , huku ikiwa inazunguka degree 360, dah ile view mara ya mwisho kuiona ni kwenye mashindano ya formula one grandprix. Hakika wapewe maua yao wote waliokuwa wapiga picha.
 
Sio kwamba utayarishaji wamehusika watu wengine professional zaidi, tofauti na watu wa Azam kwa tukio la jana na mashindano ya AFL kwa ujumla?
 
Nje ya mada, hakuna Ligi Kuu ya Uingereza, kuna Ligi Kuu ya England inayozihusisha Klabu mbili za Wales Cardiff na Swansea na hiyo ni kutokana na nchi hiyo kutokuwa na Ligi yake ya soka zaidi ya rugby. Ukisema Ligi Kuu ya Uingereza maana yake ni pamoja na Scotland na Republic of Ireland ambazo zina Ligi zake soka. BBC walishatolea sana ufafanuzi hili.
England in swahili, tutajie?
 
umesema ???
 
Wa upgrade camera zao matangazo ya pembeni yalikuwa hayaonekani vizuri

Mpira wa simba uliogonga mwamba na kutaka kuingia golini ilipaswa pia wau zoom kule juu uliko elekea na namna ulivyo rudi golini. Ila kwa sababu camera zao ndo hivyo tena hawakuweza kuonesha engo ile
Kumbe na wewe uliliona hilo kuwa wakati visit saudi nilikuwa napata tabu kuiona.
Ilikuwa inaonekana rangi ya pink tu.
 
Kuna siku nilikuwa nabishana tu na mfanyakazi wa Azam, nilimwambia kwamba kamera za HD wanazotumia Multi Choice ni tofauti na wanazotumia Azam, na wanazotumia Multi Choice ni tofauti na zile wanazotumia Sky Sport.

Tulibishana kidogo na alisema kamera za HD zote ni sawa. Nilichouliza kwa nini mechi za Ligi ya Uingereza kimuonekano ni tofauti na Azam akicheza na Yanga Taifa? Mimi nauona utofauti mkubwa sana wa uang’avu lakini jamaa yangu alibisha sana.

Sasa jana nilipokuwa naangalia mpira wa Simba na Al Ahly, nilishangaa kuona kamera zikiwa na muonekano wa tofauti kabisa. Nilipouliza, nilijibiwa kwamba kamera wamezishikilia Wafaransa. Ikanibidi nikubali kwa sababu ya muonekano wake, si ule tuliokuwa tumeuzoea kipindi chote.

Wewe unaweza kuwa na kamera moja na anayotumia mtu fulani Ulaya lakini kwenye setting jamaa akakupiga vibaya sana. Nikakumbuka siku moja nilimpa rafiki yangu Barnaba Salu simu yangu anipige picha. Huyu jamaa ni mtaalamu wa kupiga picha na video, ile picha alivyonipiga na kunionyesha, nikamuuliza ni kamera ya simu yangu ndiyo imepiga hivi? Akajibu ndiyo. Nilishangaa sana, kumbe jamaa aliingia kwenye setting na kufanya mambo yake.

So Azam wana kamera nzuri sana, ila hawana wataalamu wakubwa wa kuweza kuzichezea, yaani ni kamera za HD lakini picha zake si kama za HD tunazozijua, labda niambie kwamba kamera za za jana hazikutumika zile tulizozizoea.

Suala la kamera yoyote duniani ni setting, unasikia tu Bieber amefanya video moja kwa iPhone yake, ila ukichukua iPhone kama ile ukafanya video inaonekana mbaya, kumbe ndugu yangu hujui kuseti kamera.

Kwa jana, kuanzia graphics mpaka uang’avu wa picha ulikuwa mkubwa sana. Wapiga picha wa Azam nahisi watakuwa wamejifunza sana kupitia kwa hao Wafaransa. Kama watakuwa hawajajifunza basi kutakuwa na shida mahali.

Kwa kawaida wanapokuja watalaamu wa kitu fulani nchini, nenda kaungane nao ujifunze mabo madogomadogo kwa ajili ya manufaa yako baadaye, haiwezekani mtu akakubania kwenye vitu vidogo kama hivyo.

Uang’avu wa picha za jana kuanzia mchana mpaka muda wa mechi uwanjani, niliona kabisa kuna utofauti mkubwa sana. Graphic ilikuwa ya kibabe mno yaani mpaka unatamani kila siku ziwe hivyohivyo.

Ni somo kwa wapiga picha. Usijifunze picha studio kwa jamaa halafu ukataka kamera, nenda class kajifunze, siku hizi zipo mpaka course kwenye mitandao, ingia huko, soma sana, nakuahidi hutokuwa kama ulivyo sasa hivi.

Ila picha ikufikia clear :

  • Source
  • Njia inayokufikia.
  • Inavyopokelewa
  • Chombo chako.

Camera ni component moja.
 
Wabongo kwa kujidharau nawapa salute.

Huo ndo ukweli, ni kama EPL tu DSTV anapewa link za matangazo kwa ajili ya africa, Japani, USA, India wana warushaa matangazo yao. Au unadhani marekani na india wanaangalia EPL super sport 1?

Kinacho fanyika ukishinda haki ya kurusha matangazo wewe unapewa link, sasa wewe ndo utajua unaifanyia nini, hapa kwetu TFF ndo ilitakiwa iwe na jukumu la ku broadcasting michezo alafu wansawapa azam link, kwa kuwa TFF haina ela wameipa mzigo azam
 
Tanzania Football Failure
 
Back
Top Bottom