Kwanini SGR inatangulia Mwanza kabla ya Kigoma?

Mwanza ndiko kwenye shehena kubwa ya mizigo, Hapa tunapambana na Mombasa maana wanataka kuhodhi mizigo yote ya Uganda, Sasa sisi SGR ikiwahi kufika Mwanza maana yake mizigo mingi ya Uganda itakuwa inapita kwetu ambako mabehewa ya mizigo ya Uganda yatakuwa yanaingia moja kwa moja kwenye meli na kwenda kuunganisha na reli ya Port Bell.
Mombasa port wanatuzidi kwa kupokea mizigo mingi ya Uganda kwa ajili ya SGR yao? Kwani SGR ya Kenya inafika Uganda? Hizo ni sababu duni sana, tunashindwa na Mombasa kwa sababu ya kushindwa kwetu kujipanga sawasawa. Kama hatujipangi sawasawa, hata tukishakuwa na SGR, bado wataendelea kutuburuza.

Vv
 
Tumia akili ndugu,kumbuka huduma inapopelekwa pia mji huo uchangie kurudisha hizo gharama kiasi fulani.so Mwanza ni mji mkubwa na wa kibiashara ukiondoa Dar es Salaam na kuipelekea reli ni sawa ili kuwahisha mambo na wingi wa wafanya biashara watachangia pia kurudisha gharama kwa kiasi fulani kulingana na safari zao,nje na mjo kama Kigoma mkoa ambao bado umelala kiasi fulani huo itafuata baadae.
Kigoma imetengwa kwa muda mrefu, kwenye miradi yote ya maendeleo imepelekewa ikiwa ýa mwisho. Barabara ya lami imepelekewa baada ya mikoa yote kuwa imeshaunganishwa. Umeme wa gridi, itakuwa ya mwisho kuunganishiwa, na hata reli ya SGR itakuwa ya mwisho maana shurti ifike Mwanza kwanza.

Kigoma imepakana na nchi mbili- Burundi na Kongo, Mwanza imepakana na nchi moja pekee Uganda. Pili, Kigoma ina changamoto nyingi za miundombinu, ilipaswa ipewe kipau mbele kuliko Mwanza ambayo ina miundombinu yote, Uwanja wa Ndege na barabara za lami zinazoiunganisha na mikoa yote.

Napenda kujua, kwa nini Mwanza wanatanguliziwa SGR kabla ya Kigoma wakati Kigoma ni lango kuu kupeleka na kupokea mizigo kutoka Burundi na Congo ukilinganisha na Mwanza ambayo ni Uganda pekee?

Vv
 
Sgr ikija kgm hakuna cha maana itasaidia uzoefu wa reli ya mkoloni mnayo,piga kelele mkoa ufunguke kwa barabara ndio itawasaidia
Leo hii mikoa mipya ya Geita njombe na simiyu wanajengewa barabara zingine nyie hakuna hata moja ya zamani iliyokamilika
Umeongea point mkuu. Ndio maana nawapigia kelele Watanzania wenzangu waliopo Kigoma kuwa wanastahili upendeleo maalumu ili nao wapigie hatua zaidi kimaendeleo.

Vv

Vv
 
Naona baadhi munafuata upepo. huko Rwanda kuna watalii maelfu wangapi unaowasikia? Hizo hadithi za Kagame tu. They are nothing! Absolutely nothing! Wanachofanya ni usumbufu EAC tu na kutaka kila sehemu wawepo wakati ni member wa hivi majuzi. Wakipata mradi wanafanya promo utadhani kweli wako fit!
Soma magazeti ya jana ya Kiingereza, Daily News na Guardian.

Vv
 
Tumia akili ndugu,kumbuka huduma inapopelekwa pia mji huo uchangie kurudisha hizo gharama kiasi fulani.so Mwanza ni mji mkubwa na wa kibiashara ukiondoa Dar es Salaam na kuipelekea reli ni sawa ili kuwahisha mambo na wingi wa wafanya biashara watachangia pia kurudisha gharama kwa kiasi fulani kulingana na safari zao,nje na mjo kama Kigoma mkoa ambao bado umelala kiasi fulani huo itafuata baadae.
Hebu nisaidie kujua ndugu yangu, SGR ikifika Mwanza itarudisha gharama kivipi na Kigoma inashindikana vipi kurudisha hizo gharama.

Mwanza kuna Reli ya Kati, kuna barabara za uhakika kutoka na kuingia kutokea mikoa yote, pia kuna Uwanja wa Ndege mkubwa. Vyote hivyo vipo tayari, SGR itaongeza nini/ itabeba nini ambacho hakibebwi sasa?

Kigoma hawana barabara za uhakika kuingia na kutokea mkoa wowote, wakati wa mvua kunakuwa na upungufu wa bidhaa kutoka mikoa mingine. Je, huoni SGR italipa haraka kuliko Mwanza?

Hoja ambayo unaweza kuijenga hapa ni mizigo ya kwenda na kutoka Rwanda kupitia Isaka. Lkn haina maaana kuwa kwa kuwa Isaka itarejesha gharama za SGR haraka kwa ajili ya mizigo ya Rwanda basi ndio hivyo kwa Mwanza, sio kweli. Mwanza ni zaidi kilometa 200 kutoka Tinde (njia panda ya kwenda Mwanza), SGR ingeweza kuishia Isaka na Tinde, na hizo kilometa 200 -300 zinazisalia, zingeelekezwa Kigoma.

Vv
 
Kigoma imetengwa kwa muda mrefu, kwenye miradi yote ya maendeleo imepelekewa ikiwa ýa mwisho.

Napenda kujua, kwa nini Mwanza wanatanguliziwa SGR kabla ya Kigoma wakati Kigoma ni lango kuu kupeleka na kupokea mizigo kutoka Burundi na Congo ukilinganisha na Mwanza ambayo ni Uganda pekee?
Mkuu Vyama Vingi,
Utekelezaji wa miradi yoyote, hutegemea mambo matatu, 1.progression, 2. logistics na 3. econimic viability.

1. Kwa vile Kigoma ni pembezoni, ujenzi wa mradi wowote utaanzia mwanzo na kumalizikia mwisho. Hivyo ndivyo ilivyo, kama ujenzi wa nyumba, unaanzia chini unakwenda juu. Barabara na reli, unaanzia mwanzo, unamalizia na Mwisho, Kigoma iko mwishoni, hii inaitwa logical progression, huwezi kuanza mwisho ukaruka katikati.

2. Logistics zina determine mradi uanzie wapi, mfano ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima Uganda hadi Chongoleani, Tanga, japo mwanzo wa mradi ni Uganda, kufuatia logistics za kupokea mzigo ni bandari ya Tanga, then ujenzi utaanzia Tanga kwenye easy logistics kuelekea Uganda. Kigoma ingekuwa na easy logistics, SGR ingeanzia Kigoma. Japo Tanzania tuna Bandari, mizigo mingi ya Tanga, Moshi na Arusha, inapitia bandari ya Mombasa kwa ajili ya proximity for logistical reasons, kuliko bandari ya Dar ambayo ni mbali zaidi.

3. Economical viability. Ili SGR yoyote iweze kuoparate kwa faida, it has to link up na nchi nyingine. Plan ya SGR ya Mombasa ilikuwa i link up na Uganda, Uganda i link up na Rwanda. Kitendo cha Kagame kujitoa ku link up na Uganda, na badala yake SGR yetu ndio ita link up na Rwanda, kumepelekea SGR ya Mombasa kuwa a loss making white elephant. Baada ya Rwanda kujitoa, Uganda inasua sua, funders wa kipande cha kuunganisha Mombasa na Kampala kagoma kutoa pesa kwa sababu it will be loss making.

Hata SGR yetu, kipande cha Dar-Moro-Dodoma ni loss making hadi itakapo cross Isaka na link up na Rwanda.

SGR ya Mwanza ni more economic viable kwa sababu itakwenda hadi Uganda. SGR ya Kigoma is just a dead end unless in future East DRC ita link. Hivyo ni faida zaidi kuanza na Mwanza kuliko Kigoma for economical viability.
Pole.
P
 
sote watanzania ukabila na ukanda tulishauacha tangu Uhuru. Ata ingepelekwa Zanzibar sawa tu.
Kigoma imetengwa kwa muda mrefu, kwenye miradi yote ya maendeleo imepelekewa ikiwa ýa mwisho. Barabara ya lami imepelekewa baada ya mikoa yote kuwa imeshaunganishwa. Umeme wa gridi, itakuwa ya mwisho kuunganishiwa, na hata reli ya SGR itakuwa ya mwisho maana shurti ifike Mwanza kwanza.
Kigoma imepakana na nchi mbili- Burundi na Kongo, Mwanza imepakana na nchi moja pekee Uganda. Pili, Kigoma ina changamoto nyingi za miundombinu, ilipaswa ipewe kipau mbele kuliko Mwanza ambayo ina miundombinu yote, Uwanja wa Ndege na barabara za lami zinazoiunganisha na mikoa yote.
Napenda kujua, kwa nini Mwanza wanatanguliziwa SGR kabla ya Kigoma wakati Kigoma ni lango kuu kupeleka na kupokea mizigo kutoka Burundi na Congo ukilinganisha na Mwanza ambayo ni Uganda pekee?
Vv
 
mtoa post hajielewi reli ya Kati wakati inajengwa ikafika adi kigoma kwanini mikoa mingine hawakulalamika ishie kwao
Hivi hamna reli inayo enda Kigoma kweli.. Nakumbuka kwenye maarifa ya jamii.. Wale wenzangu tukumbushane hapa
 
Kigoma wachawi wengi hata Mh. Zitto alishamtishia Mwanaharakati Huru Musiba kuwa atamroga. Hivyo serikali iliogopa reli ya SGR itarogwa na Zitto and his Company!
😂😂😂😂😂😂
 
Maswali ya kijinga kamulize mkeo au ndugu zako
 
Mkuu Vyama Vingi,
Utekelezaji wa miradi yoyote, hutegemea mambo matatu, 1.progression, 2. logistics na 3. econimic viability.

1. Kwa vile Kigoma ni pembezoni, ujenzi wa mradi wowote utaanzia mwanzo na kumalizikia mwisho. Hivyo ndivyo ilivyo, kama ujenzi wa nyumba, unaanzia chini unakwenda juu. Barabara na reli, unaanzia mwanzo, unamalizia na Mwisho, Kigoma iko mwishoni, hii inaitwa logical progression, huwezi kuanza mwisho ukaruka katikati.

2. Logistics zina determine mradi uanzie wapi, mfano ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima Uganda hadi Chongoleani, Tanga, japo mwanzo wa mradi ni Uganda, kufuatia logistics za kupokea mzigo ni bandari ya Tanga, then ujenzi utaanzia Tanga kwenye easy logistics kuelekea Uganda. Kigoma ingekuwa na easy logistics, SGR ingeanzia Kigoma. Japo Tanzania tuna Bandari, mizigo mingi ya Tanga, Moshi na Arusha, inapitia bandari ya Mombasa kwa ajili ya proximity for logistical reasons, kuliko bandari ya Dar ambayo ni mbali zaidi.

3. Economical viability. Ili SGR yoyote iweze kuoparate kwa faida, it has to link up na nchi nyingine. Plan ya SGR ya Mombasa ilikuwa i link up na Uganda, Uganda i link up na Rwanda. Kitendo cha Kagame kujitoa ku link up na Uganda, na badala yake SGR yetu ndio ita link up na Rwanda, kumepelekea SGR ya Mombasa kuwa a loss making white elephant. Baada ya Rwanda kujitoa, Uganda inasua sua, funders wa kipande cha kuunganisha Mombasa na Kampala kagoma kutoa pesa kwa sababu it will be loss making.

Hata SGR yetu, kipande cha Dar-Moro-Dodoma ni loss making hadi itakapo cross Isaka na link up na Rwanda.

SGR ya Mwanza ni more economic viable kwa sababu itakwenda hadi Uganda. SGR ya Kigoma is just a dead end unless in future East DRC ita link. Hivyo ni faida zaidi kuanza na Mwanza kuliko Kigoma for economical viability.
Pole.
P
Mkuu Pasco, Mwanza imeondokaje kutoka kuwa mkoa wa pembezoni? Hizo zote ni itiatiatives za serikali, serikali ndio nayohusika na kutengeneza mazingira ya hizo viabilities ili kukuza uchumi, leo wabunge na wananchi wanapiga kelele kuwa biashara nchini zinadorora serikali nayo imekubali na kuitaka TRA ichukue hatua za kukabiliana na mdororo huo.

Serikali isipoandaa mazingira ya kiuwezeshaji: miundombinu na sheria za kusimumua uchumi wa sehemu husika, Kigoma itaendelea kuwa pembezoni na Mwanza itaendelea kuwa strategic town. Usishangae hata Katavi na Geita mikoa ya juzijuzi tu inaenda kuwa mbele ya Kigoma.

Hivi unajua kuwa mfanyakazi wa serikali anayeishi Kigoma ni masikini kuliko anayeishi Mwanza? Wanaweza kulipwa kima kimoja cha mshahara, lakini kwa uwezo wa kukidhi mahitaji, yule wa Mwanza anahimili zaidi kuliko yule wa Kigoma maana wa Mwanza ananunua kilo ya sukari kwa sh. 2700/= wakati yule wa Kigoma, kwa mshahara uleule analipa sh.3000/- !

Sasa bila serikali kutengeneza mazingira wezeshi kwenye mikoa hiyo ya pembezoni na kuendelea kutoa kipaumbele kwa mikoa iliyo kwenye kitovu, hiyo mikoa ya pembezoni itabaki kuwa masikini na ile mingine itaendelea kufanikiwa zaidi.

Hapo ndipo lile andiko kuwa ' mwenye vingi ataendelea kuongezewa, na yule mwenye vichache hata hivyo vichache atang'anywa na kupewa yule mwenye vingi ".

Vv
 
Acha zako basi [emoji53]
Ubishi mwingine hauna maana. Kupeleka Mwanza inamaanisha wanufaika ni shinyanga, simiyu, mwanza, geita, kagera, mara.

Tabora- Kigoma mnufaika ni kigoma tu. Leo hii kusafirisha mizigo ya congo imekuwa ni bora kuliko watanzania walipa kodi!!
 
Kigoma imetengwa kwa muda mrefu, kwenye miradi yote ya maendeleo imepelekewa ikiwa ýa mwisho. Barabara ya lami imepelekewa baada ya mikoa yote kuwa imeshaunganishwa. Umeme wa gridi, itakuwa ya mwisho kuunganishiwa, na hata reli ya SGR itakuwa ya mwisho maana shurti ifike Mwanza kwanza.

Kigoma imepakana na nchi mbili- Burundi na Kongo, Mwanza imepakana na nchi moja pekee Uganda. Pili, Kigoma ina changamoto nyingi za miundombinu, ilipaswa ipewe kipau mbele kuliko Mwanza ambayo ina miundombinu yote, Uwanja wa Ndege na barabara za lami zinazoiunganisha na mikoa yote.

Napenda kujua, kwa nini Mwanza wanatanguliziwa SGR kabla ya Kigoma wakati Kigoma ni lango kuu kupeleka na kupokea mizigo kutoka Burundi na Congo ukilinganisha na Mwanza ambayo ni Uganda pekee?

Vv

Kwa kigezo cha wingi wa abiria Mwanza sio then Kg Mwanza itabeba abiria wa Kahama,shinyanga,bukoba,Na Mara. Plus waganda.
 
Back
Top Bottom