Kwanini SGR inatangulia Mwanza kabla ya Kigoma?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Kigoma imetengwa kwa muda mrefu, kwenye miradi yote ya maendeleo imepelekewa ikiwa ýa mwisho. Barabara ya lami imepelekewa baada ya mikoa yote kuwa imeshaunganishwa. Umeme wa gridi, itakuwa ya mwisho kuunganishiwa, na hata reli ya SGR itakuwa ya mwisho maana shurti ifike Mwanza kwanza.

Kigoma imepakana na nchi mbili- Burundi na Kongo, Mwanza imepakana na nchi moja pekee Uganda. Pili, Kigoma ina changamoto nyingi za miundombinu, ilipaswa ipewe kipau mbele kuliko Mwanza ambayo ina miundombinu yote, Uwanja wa Ndege na barabara za lami zinazoiunganisha na mikoa yote.

Napenda kujua, kwa nini Mwanza wanatanguliziwa SGR kabla ya Kigoma wakati Kigoma ni lango kuu kupeleka na kupokea mizigo kutoka Burundi na Congo ukilinganisha na Mwanza ambayo ni Uganda pekee?

Vv
 
Mkuu ongea na figures badala ya hisia.
 
Ingeanza Kigoma mngeuliza tena kwa nini Kigoma
Sio kosa, tungeweka vigezo na kuuliza kwa nini Kigoma kwanza badala ya kwingine.

Nimejitahidi kuweka vigezo/hoja, hoja hujibiwa kwa hoja, sio kwa blah blah.

Vv
 
Back
Top Bottom