Ingetangulia Kigoma mngeendeleza uzushi wenu kuwa Rais wetu(kipenzi) ni mburundi hivyo anaunganisha TZ na nchi yake...imetangulia Mwanza bado mnaleta kelele.!!!!
Binadamu hamridhiki..
Mizigo inayosafirishwa kuanzia na kuishia Mwanza ni mingi mno kuliko Kigoma kwa kutumia barabara na reli ya kati.
Mwanza ni economic potential hub kubwa kwa mazao ya Kanda ya ziwa kama pamba, kokoto,samadi,mbao,ngozi,katani,mahindi,mchele,ndizi,kahawa,samaki,wasafiri,kuelekea mashariki ya Tanzania na kwinginepo
Pia mizigo ya kutokea Mashariki ya nchi kwenda Kanda ya ziwa kama mafuta,saruji,nondo,mitambo,wasafiri,hardware,mabati,Fertilizern.k
Lakini ni kiungo muhimu kwa usafirishaji wa mizigo ya Uganda kwa kutumia bandari ya Dar-es-salaam na Tanga.
Mjomba Magu anacheza mchezo wa kumvutia Uganda atumie Mwanza kama njia mbadala ya kusafirisha mizigo yake kutumia Marine Ferries.
Kumbuka mizigo mizito ikisafirishwa kwa reli itaokoa barabara zetu na matengezo ya mara kwa mara.