Mkuu Vv, kwanza nakubaliana na wewe, serikali za awamu zote zilizopita, ziliutelekeza mkoa wa Kigoma, kwa kutousisimua uchumi wa Kigoma. Tanzania tunatumia fedha nyingi sana kuagiza mafuta ya kula, Kigoma zao la chikichi linastawi, zao hilo lingeendelezwa kama chai na kahawa, lingekuwa na manufaa makubwa kwa taifa kuliko zao jingine lolote na Kigoma would have been the richest region, lakini mkoloni alijikita kwenye cash crops za demand yake na sio demand yetu kama kahawa, as a result, mikoa wazalishaji wa kahawa ndio the richest regions wakati hiyo kahawa tunawazalishia wazungu, halafu foreign currency yote ya kahawa tunaitumia kuagiza mafuta ya kula ya mawese kutoka Malaysian wakati Kigoma ilianza kustawisha mawese kabla ya Malaysia.
Tulipopata uhuru hadi leo tumeendelea kutembea mule mule wakoloni walimotutembeza.
Tuna agitation mchele wakati bonde Ruvu pekee lingetosha kulisha Tanzania nzima, achilia bonde la Usangu na bonde la Kilombero.
Tunaagiza sukari, wakati tuna aridhi ya kutosha kulima miwa kujitosheleza kuuza nje, Anglian ka nchi kadogo kama Cuba, kanatuuzia sukari, ni aibu.
Tanzania sio masikini ni sisi wenyewe tuu na mipango yetu, akina sisi kazi yetu kuuliza, baada ya rais Magufuli kuamua kujenga Tanzania ya viwanda, kwa nchi inayotegemea kilimo, then Tanzania ya viwanda vya ukweli, ni Tanzania ya agro processing industries, kulikuwa na haraka gani kukimbilia kununua midege, na kutengeneza SGR ukilinganisha na fedha hizo zingewekezwa kwenye kilimo?.
Tuna chuma cha kutosha pale Liganga na Mchuchuma, mali ghafi kuu ya reli ni chuma, na ndio the most expensive na most costly kwenye ujenzi wowote wa reli, chuma tunacho kwanini hatukitumii, ni poor planing tuu na ndio hii imepelekea Kigoma kutelekezwa.
Poleni sana wana Kigoma.
P.