Kwanini Serikali ya CCM haijengi magereza mapya? Je, kiwango cha uhalifu kimepungua au wao ndio wahalifu wenyewe wamehalalisha wizi, na ufisadi?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,907
Ubadhirifu na wizi, matumizi mabaya ya fedha za umma na rasilimali za taifa kutumiwa kwa maslahi ya watu wachache kumeongezeka sana.

Mbaya zaidi Rais amesikika mara kadhaa akisema kwamba upigaji kwenye Halmashauri ni mkubwa sana. Tozo zinapigwa, fedha za miradi zinapigwa, fedha za misaada zinapigwa, yaani mchwa, nzige, tunutu, madumadu, nzige na maparare yako huko.

Ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zimekuwa zikibainisha madudu ya ajabu kwenye idara mbalimbali za serikali.

B. O. T watu waliiba mabilioni wakasingizi kwamba ni hela chakavu. Lakini baada ya uchunguzi ikagundulika kwamba hela hazikuwa chakavu, ila ni fedha mpya zilikuwa zikikatwa.

Wizi umetamalaki kila sehemu, je serikali ya CCM haioni? Au ina faidika na hali hii? Kwanini hawajengi magereza mapya ili mijizi yote ichukuliwe hatua ikapumzishwe huko?

Haya mambo ya mtu akifanya ubadhirifu ahamishwe kituo sasa yafike mwisho.
 
Unajua kwa nini wanaiba?

Jibu ni kwamba hakuna awezaye kuwakamata, so ujenzi wa magereza mapya hauwezekani kabisa kwa ccm government.
 
wamejikita kwenye dora alisikika bashiru kipindi mkate wa siagi na mawaziwa mezani
 
FB_IMG_1669833756053.jpg
 
Sababu wanaopelekwa huko ni raia wa kawaida tena wengi wao nasikia hawana hatia.
 
Ile mahakàma ya mafisadi iliyokua imewalenga wachaga iliishia wapi?
Kidogo tu angejenga gereza kwa ajili ya wachaga..
 
Back
Top Bottom