Kwanini nyumba yako unaiita "kakibanda kangu"? Mungu hapendi kujishusha sana. Having too much humility is self destructive

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,963
2,000
S.hikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania jifunzeni kujishusha lakini isiwe too much. Mungu hapendi mjishushe sana. Having too much humility is self destructive;

Unakuta mtu alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga vyumba viwili chumba na sebule, lakini kwa bahati nzuri akajinyima kisha kwa uwezo wa Mungu akajenga nyumba yake self-contained ya vyumba vitatu vya kulala.

Siku ama weeks kadhaa baada ya kuhamia unasema ngoja niende nikamtembelee ndugu, jamaa au rafiki yangu nifahamu anapokaa. Baada ya kufika na kusalimiana anakukaribisha ndani kisha anakwambia "karibu, haka ndio kakibanda kangu najifichamo na kafamilia kangu, si unajua tena ujenzi wa kimasikini"

Kwanini nyumba yako nzuri Mungu aliyokubariki uiite kakibanda? Au baadhi ya watu wanafikiri huko ndio kujishusha kwenyewe na ndio uungwana? Why don't you feel proud of what God blessed you with? Au haujui kuwa hata vinyonge havitaenda Mbinguni. Mtu amekuja kukutembelea mwambie kwa kujiamini kwamba, "hii ndio nyumba yangu. Nimeijenga mpaka stage hii ila Mungu akinijalia nitaimalizia taratibu tarabitu kwa maana pesa ngumu sana siku hizi"

Au unakutana na dada classmate wako wa secondary school na ulisikia aliolewa punde tu baada ya kumaliza shule. Unamuuliza "hongera Fatuma ninasikia uliolewa na fulani na umebarikiwa mtoto mmoja" utamsikia atakavyokujibu kwa kinyonge "kuolewa wapi kaka yangu, nipo tu ninasogeza naye maisha, si unajua tena mambo ya sogea tukae"

What the hell is "Sogea tukae"? Hiyo ndio ndoa yako ndugu yangu ambayo Mungu ameona inafaa uwepo mpaka wakati huo. Kuwa na shukrani kwa mume/mke uliyenaye na usimuite tena SOGEA TUKAE. Kwani kuna akina dada/kaka wangapi wanatamani wangekuwa katika ndoa ila wameshindwa kwa sababu mbalimbali?

A thankful heart is one that is grateful and appreciative of who God is and the life He has given them despite the storms of life.

Having too much humility is self destructive. Humility has to be practiced with care. Humility requires boundaries.

Watanzania msipende kujiweka kinyongenyonge na kujishusha saana. Jivunie kile ambacho Mungu amekubariki kwa wakati huo huku ukizidi kupambana ili usonge mbele zaidi.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO. MUNGU IBARIKI NCHI YANGU.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
4,403
2,000
Tatizo Watanzania ni wanafiki. Una chumba 2 na sebure ukiita nyumba mbele anakwenda kukusemanga.

Cha msingi mtu aite nyumba yake kadri apendavyo maana ni yake. Na kusema anenavyo mtu ndivyo atakavyokuwa ni uongo, ukitaka kuamini jinenee kuwa wewe ni tajiri wa Afrika then baada ya miaka kumi utajiona.
 

parts

JF-Expert Member
Mar 31, 2018
2,048
2,000
Kuna watu wanaoishi vizuri na wanajiweza, lakini kuna wengine wapo tu kwa sababu walizaliwa. Kuna wenye nyumba na wanao miliki vibanda. Nadhani kila mtu anatakiwa kujitathimini kwa kuzingatia uhalisia.

Kibanda ni kibanda tu, hata ukiite ghorofa.
 

RReigns

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
16,785
2,000
Kinachoepukwa ni kuonekana unajimwambafy. Lakini si kwamba hawathamini nyumba zao. Si unajua watu bana. Ukisema nyumba nyuma wataanza kukung'ong'a.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom