Joannah
JF-Expert Member
- May 8, 2020
- 18,372
- 42,384
Kuna siku nilikuwa kwenye ibada za Hawa manabii wa kizazi kipya,kwenye maombi nabii akawa akisema"Mungu baba, sisi ni Kama sisimizi,ni wadudu tu mbele zako"nikapoteza network nikakumbuka tuliambiwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, Sasa kwa Nini hata tusiseme "Mimi ni pendo,Mimi ni nuru kwa kuwa nimeumbwa kwa mfano wako"nikawaza hata kujishushusha kuwe na kiasi,kujishushusha Sana mwishowe utakufuru.Moyo wenye shukrani humpendeza Mungu na Jamii yake.
Hakika friend. Upo sahihi. Tujifunze kushukuru katika kila hali.