Maisha ya chuo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya chuo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tumsifu Samwel, Mar 10, 2010.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  J

  umamosi moja tulivu Janet akiwa na wazazi wake walifika Stendi ya mabasi ubungo kama ilivyo kawaida ndani ya stendi hiyo magari huwa mengi kama siku za kawaida ,Kwa mtu mgeni anaweza kushangaa pilika pilika zilizopo ndani ya stendi hiyo iliyojaa wasafiri na wasio wasafiri kwani sio wote wanaokuwepo stendi hapo ni wasafiri.
  Wengine wapo pale kuuza vitu vidogo dogo kwa wasafiri mfano kijana mmoja aliyekuwa amevaa nguo zilizo katika malalamiko ya kukosa maji kwa muda mrefu,alikuwa akipita na kusimama kwa mtu yeyote akimuonesha simu aliyokuwa akiiuza.Watu waliokuwa karibu na kijana huyu walijaribu kujiuliza alipata wapi simu hiyo ilihali anaonyesha hana hata ela ya kununua sabuni na kufua nguo zake.
  “Mzee simu hii ntoe basi”sauti ilitoka kwa huyo kijana pale alipomsogelea baba Janet .

  Muda wote huo baba yake Janet alikuwa akikatisha huku na huko kumtafutia mwanae tiketi ya basi la kwenda chuo morogoro katika chuo cha elimu ya juu Mzumbe kwa ajili ya masomo yake ya juu,
  Hatua tatu tu mbele walisikika watu wakisukumana kama wenye kugombania kitu “Sogea huko wewe!Mzee….Mzee……unataka gari? Eeeh…..sema mzee….Arusha?,Moshi mh…..mara!Mzee gari Dodoma ile pale imebakia siti mbili mzee….mmh……..”. kwa kuogopa kutapeliwa alimuita pembeni kijana aliyekuwa akiuza tiketi na kumtaka waende wote mpaka kwenye ofisi zao iliakampatie tiketi kwakuwa ndio njia ya kujipatia pesa kijana huyo hakuwa mbishi akaongozana na baba Janet mpaka ofisini nakumpatia tiketi .
  Muda wote huo Janet alikuwa pembeni na mama yake wakisubiri tiketi iliyoenda katwa na baba yake Janet.
  Mama Janet aliutumia muda huo kumpa mwanae nasaha za maisha kwani huko aendako atakutana na watu asiowajua na wenye tabia tofauti na yeye ,
  “Mungu kakujaalia mwanangu sura na umbo zuri,najua watakufuata wanaume mabalimbali elewa kwamba wengi watakuwa wanakutamani nasio kukupenda mama,jihadhari sana na watu hao kwani watakuharibia malengo yako na mwisho wasiku dira yako ya maisha itavurugika .
  Kafuate kinachokupeleka, shinda vishawishi na epuka marafiki wabaya ,najua ni vigumu mwanangu kumtambua rafiki mzuri ila jitahidi kuchagua rafiki mnae endana nae kimwenendo na tabia” mama Janet alijitahidi kumsihi mwanae wa pekee.
  Janet alikuwa kimya akimsikiliza mama yake,baada ya dakika chache baba yake alifika na kumpatia Janet tiketi

  BABA JANET: Mwanangu inabidi usogee pale kwenye basi(akionyesha lilipo basi)muda si mrefu litaondoka

  JANET: Asante baba

  BABA JANET: Mwanangu kasome ,usihadaike na mambo ya dunia kwani muda wake bado utayakuta tu,nakutegemea mwanangu.

  JANET: “Sawa baba,nawaahidi kufuata kile kinachonipeleka,niamini sitawaangusha wazazi wangu wapenzi” Janeti aliongea huku akiwa anafuta machozi yaliyokuwa yakidondoka mashavuni mwake kama maji yaliyokosa njia maalumu, Janet alikuwa akitiririkwa na machozi .
  Uzuri wa uso wake haukuweza kufichika hata kidogo, kitambaa cheupe kilichokuwa katikati ya mikono yake kiki tumika kufuta machozi taratibu kama mtu akandae kidonda .

  BABA JANET: Sawa mwanangu,usilie mama najua ni mara yako ya kwanza kukaa mbali na sisi ila inabidi uende chuo ukasome

  MAMA JANET:Baba Janet mwanao ataachwa na basi,

  Wanamsaidia kubeba mizigo ,Kondakta wa basi anaichukua na kuweka sehemu ya mizigo.
  Janet anaagana na wazazi wake kisha anapanda ndani ya basi,dakika chache mbele basi linaanza safari ,Janet anawapungia mikono wazazi wake.
  ***********************************************************


  Janet alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga chuoni Mzumbe, alikuwa tishio kwa kila msichana katika chuo hicho hasa katika kitivo cha sheria,kwani alikuwa binti mrembo hakuna mvulana chuoni hapo alithubutu kupishana nae bila kugeuza shingo.
  Uzuri wake ulimfanya afuatwe na wavulana wengi wanafunzi chuoni hapo na hata wanafunzi wavyuo jirani na wanaume wengine waliokuwa wakikutana nae njiani .
  Siku za mwanzoni ilimuwia vigumu kukabilia na hali hiyo lakini ilimbidi aizoee,Janet alikuwa mtulivu kipindi cha mwanzoni Janet alikuwa mtulivu alipenda kuutumia muda wake mwingi kwa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyo husu masomo yake na wakati mwingine alikuwa akisoma kitabu chake cha mafundisho ya dini.Hali hiyo ilikuwa ikiwakera rafiki zake kwani walimuona mtu asiyeenda na wakati,taratibu wakaanza kumshabulia na maneno ya kejeli ilitu awe anafuatana nao na kuishi kama wao.Ilichukua muda kidogo kumbadilisha janet ,hawakukata tamaa mwishowe walifanikiwa kumuingiza kwenye kundi lao, mwanzoni walianza kumrushia vijembe vya hapa na pale hasa pale alipokuwa akiishiwa ela ya matumizi.

  ZAITUNI: Janet huu ndio muda wako wakula maisha ,jiachie mtoto mzuri ujana hauji mara mbili.

  JOYCE: Ujue ujana ni kama moshi ukienda haurudi

  VERO : Utakuja wa hadithia nini watoto wako kama utakuendelea kujifungia ndani na vitabu ?

  Walimaliza kumweleza Janet kisha wakavaa na kuondoka zao wakimwacha Janet amejilaza kitandani akiwa na kitabu chake mkononi.
  Yale maneno yalianza kuzunguka kichwani mwake.

  “ila kweli,mhm!! Kila siku ntabaki humu ndani mpaka lini,mbona wenzangu wanatoka nabado wanafanya vizuri kwenye masomo yao”
  Alibaki akijisemea mwenyewe Janet.
  Siku hiyo Janet alikuwa ameishiwa pesa ya matumizi,kila akijaribu kuwakumbusha wazazi wake walikuwa wakimwambia avute subira kwani hawakuwa na ela ya kumtumia,Janet hakuwa na budi ya kuwa subiria wazazi wake wamtumie kwani hakuwa na njia nyingine ya kupata ela zaidi ya wazazi wake.
  Baada ya masaa kadhaa rafiki zake walirudi na vyakula na baadhi ya vitu kadhaa kwa ajili ya mapambo ya kike,Janet alitamani awaombe chakula lakini alihofi kashfa,kama vero alijua alitafuta sahani akamuwekea Janet chakula na kumpa ,Janet alishukuru sana akaanza kula huku moyoni akiona aibu .
  kidogo kidogo akaanza kutoka na wenzie kwenda sehemu mbalimbali,mabadiliko hayo hayakumshangaza mtu yeyote kwani ni kawaida kwa jambo hilo kutokea katika chuo chochote ni wachache wenye uwezo wa kubaki na misimamo yao thabiti.
  Janet akawa mtu wa kwenda kwenye kumbi za starehe za usiku,yale yote aliyokatazwa na wazazi wake akaya puuza kwa kuwa ona wazee wasiojua nini maana ya ujana.Janet akalivamia jiji la morogoro ,alitaka kuwa zidi walimu zake .
  Katika pita pita zake Janet aliweza kumnasa mfanyabiashara mmoja maarufu jijini hapo ,mara moja akajikita kwenye mahusiano ya kimapenzi na jamaa huyo almaarufu kama Awarding p.degAwarding alimjali Janet na kumpa kila alichokihitaji,ile hali ya kukaa na njaa kidogo dogo Janet alianza kuisahau .Janet alibadilika kuanzia mavazi mpaka tabia,akawa mtu wa nyodo kwani alihisi pesa ndio kila kitu na kuusahau utu.waliomjua walimuonea huruma kwani walijua marafiki wabaya wamesha mpoteza.
  Siku moja Janet akiwa na rafiki zake wakiangalia mashindano ya mpira wa kikapu kati ya wavulana wa chuoni hapo waishio ndani ya chuo yani on campus boys na wale waishio nje ya chuo ambao wanajiita off campus boys,wakati wanaendelea kuangalia mashindano hayo kukazuka kamjadala kati yao wane yani vero,zaituni,Janet na joyce juu ya mvulana aliyekuwa akicheza mpira wa kikapu.

  JANET: mmh yule mwenye namba 4 mtamu

  VERO: wa timu gain?

  JANET: on campus

  JOYCE: mhm yule yupo hot best,moyo umemdondokea nini?

  ZAITUNI: mambo hayooo!!

  JANET: nisimsifiee jamani mbona hivyo?

  Wakacheka kwa pamoja!!!

  Wakati mpira wa kikapu unazidi kupamba moto huku on campus ikiwa inaongoza ,mchezaji wa timu ya nje yani off campus anamgonga kwa bahati mbaya mchezaji mwenye nambari 4 mgongoni na kusababisha aanguke ,Janet anapiga ukulele uliosababisha watu waliopo pembeni yao wacheke ,yeye mwenyewe hakujali ndio kwanza akasimama na kusema “ mtaniumizia jamani” alisema Janet kisha akakaa chini,watu wengi walijiuliza maswali juu ya kauli aliyoitoa Janet.
  Kutokana na kuangua na kuumia Victor alienda kukaa pembeni kabisa,muda wote aliokaa pembeni alikuwa akimwangali Janet kwani alikuwa akijiuliza maswali mengi.
  “ mmmh,yule dada kwani nini alisema vile je kama ningekuwa na mchumba hapa chuo alafu anasikia kile alichokisema siingekuwa balaa leo,ila mzuri cheki anavyocheka na wenzie sijui ameshajua na mwangalia yeye?” alikuwa akijisemea Victor peke yake bila mtu kusikia.
  Baada ya dakika kadhaa mpira ukaisha timu ya on campus ikaibuka kidedea .Janet hakusita kumfwata Victor na kumpongeza juu ya ushindi waliowapatia wanafunzi wa on campus.

  JANET: mambo,pole kwa kuumia na hongera kwa kuwashinda off campus

  VICTOR: asante,

  JANET: am Janet(akimpa mkono huku akitabasamu)

  VICTOR: victor (akitabasamu kichovu)

  JANET: ngoja nikuache ukapumzike

  VICTOR: poa,upo on campus or?

  JANET: on campus

  VICTOR: oh poa,ntakutafuta sijui upo bweni gain?

  JANET:Karume

  VICTOR: mimi nipo kibasila

  JANET: naweza kukupa namba ya simu ili iwe rahisi kwako kunitafuta?

  VICTOR: das gud,yangu 071391…..

  JANET: thanks ,ngoja nikubeep then utaisave

  Baada ya tukio la kupeana namba kuisha,rafiki zake Janet waliokuwa wanamsubiri pembeni wanamuita.Janet anmuaga Victor kasha kila mtu anaendelea na safari yake,huo ndio ukawa mwanzo wa urafiki kati ya Janet na Victor.
  Kidogo kidogo hisia za mapenzi zikaanza kujitokeza kwa marafiki hao,Janet ilibidi amwambie rafiki yake mpenzi Vero.

  JANET: best Victor ameniapproach?

  VERO: umemjibu nini?

  JANET: wakati akiniambia ,nilikosa jibu ila sasa hivi ninalo lakini naogopa awarding akijua

  VERO: unahisi unampenda?

  JANET: NAMPENDA!!

  VERO: kama wampenda ni bora umkubalie,kwa akili yako yule mtu mzima atakuoa ?

  JANET: eeeh,ujana wake ale na nani alafu uzee wake aje kula na mimi.pale nataka pesa ambazo zitanisaidia ila nikimaliza mwaka wa mwisho na yeye atakuwa mwisho (anacheka)

  VERO: bora uwe na kijana mwenzio atakupunguzia stress za hapa na pale,tena mnaendana kweli

  JANET: nimwambie Victor kuwa nina mtu ?

  VERO : Usijaribu kwani hakuna mwanaume anayependa kushare penzi

  JANET : akija jua je ?

  VERO : haitakuwa leo hiyo,na pia unaweza tumia ujanja kwani wewe mtu mzima sasa hautashindwa mdaganya


  JANET : hivi inawezekana Victor akaja kunioa eeh

  VERO : shosti yamekuwa hayo ?

  JANET :nakuuliza jamani

  VERO : ni wachache wanaokuwa wapenzi chuo nakuja kuoana

  JANET : kwa hiyo tunapotezeana muda

  VERO : sina maana hiyo,wewe kama unampenda Victor jitose kwenye penzi lake mkiwa mnamalengo ya kujaoana inawezekana ikaja kuwa poa

  JANET : asante mpenzi kwa ushauri wako, nisindikize library nikachukue kitabu cha administrative law maana kesho tunaweza kuwa na pepa alafu sijasoma .

  VERO :poa ila fasta sio unaremba

  JANET : Usijali mama

  Wananyanyuka na kuelekea library
  Jumapili moja victor alimuomba Janet waende kupata chakula cha usiku nje ya campus,Janet hakuwa na kipingamizi.walitafuta hoteli nzuri kisha wakatafuta sehemu iliyokaa vizuri wakakaa ,mhudumu alifika na kuanza kazi yake nao bila hiyana wakampa ushirikiano wakagiza chakula na vinywaji.walipo maliza,Victor akamuomba Janet watembee kidogo alafu warudi chuo Janet hakuwa na kipingamizi huo ndio muda alioutaka a Victor kwani aliweza kumweleza Janet hisia zake nae janet bila kipingamizi akamkubali,ukawa mwanzo wa mapenzi yao.
  VICTOR: i love you Janet!!( nakupenda Janet)

  JANET: I love you too my love,please be faithful to me and our love (nakupenda pia mpenzi wangu,tafadhari kuwa mwaminifu kwangu na penzi letu)

  VICTOR: I will my love and you too you have to do that (ntafanya hivyo mpenzi wangu,nawe ufanye hivyo)

  JANET: worry out my love trust me,(ondoa shaka mpenzi wangu,niamini)

  Hii ni sehemu ya viapo walivyopeana mwanzoni mwa penzi lao ambalo lilikomaa siku hadi siku ,maisha yao yalijaa furaha mno kiasi cha marafiki zao kuwa onea wivu .walishirikiana kwa kila kitu hakuna mtu aliyekuwa na wazo la wapenzi hao kuja kusalitiana ama kuachana.Victor alijitahidi kumtimizia kila alichohitaji Janet ili mradi mpenzi wake afurahi na kutulia.
  Victor hakuwa anajua kama Janet alikuwa akitembea na mwanaume mwingine tena aliyempita umri ,alijitahidi muda wote kuwa mwaminifu kwa Janet ,kwani alitokea kumuamini Janet alikuwa na matumaini ya kuishi nae kama mke wake pindi watakapo maliza masomo yao ya chuo.
  Siku zote aliitilia maanani ahadi walizokuwa wakipeana na Janet hasa ile yakuja kuishi wote kama mume na mke.
  “Janet will you marry me after the college ?”( Janet utakubali nikuoe baada ya kumaliza chuo )
  “I will marry you Victor” (nitaolewa nawe Victor)
  Victor aliheshimu ahadi hii kwani alitamani siku moja amuoe Janet na kuishi nae nyumba moja.
  Miezi ilienda hatiamye waka wanakaribia kumaliza masomo yao, Kama Janet alivyopanga kuachana na Awarding pindi akaribia apo kumaliza akaanza kumletea jeuri na maudhi mbalimbali ili mradi apate chanzo cha kumuacha.Awarding akaamua amchunguze Janet ili ajue kinachomfanya abadilike hivyo.
  Awarding akiwa ofisini kwake anapata simu kutoka kwa mtu aliyempa kazi ya kumchunguza Victor.

  AWARDING: huyo mwanaume anaitwa Victor ,aah sasa cha kufanya kuwa karibu nao ili uweze jua wikiendi hii watakuwa wapi.Huyo binti hanijui vizuri ,haya kijana fanya kazi hiyo jioni ufuate pesa yako.

  Awarding anamaliza kuongea na simu na kukata simu,kisha anazama kwenye dimbwi la mawazo.

  “ntamtolea mfano kwa wasichana wote wanaofika vyuoni na kupapatikia maisha ,na huo ndio utakuwa mwisho wa furaha yake na ndoto zake,atajua kwa nini najiita Awarding p. deg,kwa akili yake fupi anajua ndio jina langu halisi ha! Ha! Ha! Ha!(anacheka kwa nguvu)

  *********************************************************

  Wikiendi moja Janet akiwa na mpenzi wake wakisheherekea siku ya kuzaliwa ya mmoja wa rafiki wa Victor ,kulikuwa na watu wengi siku hiyo na kila mtu alikuwa na mpenzi wake kwani moja ya sheria ya shughuli hiyo ni kuja na mpenzi wako.
  Si Victor wala Janet alikuwa akijua kama kuna mtu alikuwa akiwafwatilia,waliendelea kufurahi na wenzao.wakati shughuli ikizidi kupamba moto,Awarding alifika akiwa na kundi la vijana bila uwoga alipita mpaka mbele ya ukumbi na kumpokonya kipaza sauti Mc wa shughuli hiyo kisha akaanza kumuita Janet

  “habari mabibi na mabwana,naitwa Awarding”alipofika hapo akavuta pumzi nakupumzika
  ,Janet alikuwa kifuani kwa mpenzi wake baada ya kusikia Jina la Awarding anajitoa kifuani kwa Victor kisha anamuomba mpenzi wake watoke nje mara moja lengo nikumkimbia Awarding lakini hawakufanikiwa kwani walijikuta wakiwa wamezungukwa na vijana wakiume watatu,Janet alikuwa akitoka jasho.muda wote huo Victor alikuwa hajui kinachoendelea .
  VICTOR: kwani vipi mbona mnatuzuia kutoka?

  JANET: tupisheni tupite( anamsukuma mmoja wa vijana hao)

  KIJANA WA KWANZA: tena utulie hivyo hivyo kwani leo ndio siku yako,kwani umezoea kula vya watu wewe

  VICTOR: janet mbona si elewi,hawa akina nani?

  Wakati wanaendelea kubishana watu wakaanza wasogelea kujua kulikoni,ili kuepusha aibu ilibidi Victor ajitutumue kuepusha aibu.anawasukuma wale vijana,unazuka ugomvi wale vijana wanampiga vibaya Victor,wakiwa wanaendelea kumpiga Janet alijuwa ameshikwa na Awarding .masikini Janet kwani alikuwa akipiga kelele lakini hakuna mtu kati ya marafiki zake aliyejitokeza kuwa saidia mpaka pale wale vijana walipo acha kumpiga Victor nakumuacha hoi pale chini,Awarding anamsukumiza Janet,anashindwa kujizuia anamwangukia Victor
  Muda wote watu walikuwa wakiangalia kinachoendelea kwani wale vijana wa Awarding waliwatishia kuwa piga risasi kama wataleta fujo,hawakuwa na la kufanya zaidi ya kutii amri hiyo.
  Awarding anawasogelea Victor na Janet waliokuwa wamekaa kwenye sakafu
  Kwa sauti ya chini iliyojaa kebehi na dharau , “ janet unajina mjanja kutumia ela zangu alafu unanichanganya na huyu mtoto mdogo,sikia lengo sio kuwatisha ama kuwatia aibu kama ilivyo tokea,mmmmhmm.najua mmebakisha miezi kadhaa mpewe digirii zenu sijui za uwana sheria ,ila leo hii napenda nikutaarifu Janet wangu kuwa nimekupa digrii tena bure bila hata kwenda darasani na kumeza maneno,umesikia mpenzi?
  Janet alikuwa kimya kichwa kikiangalia chini,muda wote huo Victor alikuwa kimya akiona aibu pale chini.
  Awarding anaendelea, “ naitwa Kelvin nasio Awarding.Awarding ni a.k.a kama msemavyo watoto wa kisasa,unajua nini kesho nenda na mpenzi wako ha!ha! (anacheka) Victor mkapime afya zenu alafu ndio mtajua kwa nini naitwa Awarding p.degree (awarding private degree ,especially to young girls like you Janet ,that is H.I.V / AIDS)
  najua utashaanga kwa kuwa ulikuwa ukijua naitwa Awarding p.deg.niliambukizwa na mwanafunzi kama wewe na mimi naamua kushare na wanafunzi wa vyuo kama wewe ilikupunguza machungu.

  “hivi unaakili timamu wewe mzee?” anafoka Victor akitaka kunyanyuka,vijana wa Awarding wanamsukumiza,victor anabaki amekaa chini akitetemeka kwa hasira.

  Awarding anaondoka zake lakini kabla hajafika nje anageuka kisha kwa sauti ya juu “ Victor tulikuwa tunammiliki Janet kwa wakati mmoja ila leo hii nimeamua kukuachia” alipomaliza kusema maneno hayo ya kejeli anaondoka zake akiwaacha watu wakiwa wamepigwa na bumbuwazi.
  Victor ananyanyuka nakutoka nje ya ukumbi huku Janet akimfuata nyuma ,Victor alitoka nje na kukodi gari akimuacha Janet aliyekuwa akimfuata kwa nyuma .Victor anamwambia dereva ampeleke hospitali ya taifa,bila hiyana dereva anampeleka mpaka hospitali bila hata kulipa Victor anashuka mbio na kwenda mapokezi.


  VICTOR: samahani dada nahitaji kupima damu yangu

  DADA WA MAPOKEZI: huduma hiyo mpaka kesho asubuhi

  VICTOR: tafadhali dada naomba nisaidie

  DADA WA MAPOKEZI: mtu wa maabara hayupo mpaka kesho kaka yangu.

  Victor anajishika magoti nakuinamisha kichwa chini,anashtushwa na sauti ya dereva akidai pesa yake.

  VICTOR: samahani kaka yangu,ni kiasi gani?

  DEREVA :elfu saba
  Bila ubishi Victor anatoa wallet yake na kumpa pesa dereva,kabla dereva hajafika mbali .
  VICTOR :naomba nipeleke lodge yeyote ya karibu

  DEREVA : sawa

  VICTOR :dada nitakuja kesho

  DADA WAMAPOKEZI: sawa kaka

  Wakati wanaondoka simu ya Victor inaita ,anaitoa mfukoni anapoanglia anaona jina la mpenzi wake ,anakata simu na kuizima kabisa.
  Usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana hasa kwa Victor na Janet kwani maneno waliyo ambiwa na Awarding yaliwasumbua sana ,kila mmoja kwa wakati wake alipanga kwenda kucheki afya yake asubuhi na mapema siku iliyo fuatia.


  Asubuhi ya siku iliyofuata victor alienda kupima afya yake katika hospitali ya mkoa wakati Janet alienda kwenye kituo maalumu cha kupima damu.
  Majibu waliyo yapata hawakuamini macho yao kwani waligundulika wanavirusi vya ugonjwa wa ukimwi ,walichanganyikiwa sana victor alinusurika mara mbili kugongwa na gari .
  Alivyotoka hospitali alienda moja kwa moja mpaka hosteli,akiwa njiani watu walikuwa wakimwangalia wengi wao walimsikitikia kwa kile kilichomtokea jana kwani karibu chuo kizima walijua.Victor hakujali macho ya watu aliendelea na safari yake mpaka alipofika kwenye bweni analoishi na kuingia chumbani kwake.
  Alilia sana nakujuta kutembea na Janet,wakati akiendelea kulia mlango wa chumba chake unafunguliwa Janet anaingia akiwa analia .

  JANET: victor naomba nisamehe(analia)

  VICTOR: janet naomba uondoke mbele ya macho yangu kwani sihitaji kukuona tena ,umeniharibia dira ya maisha yangu.kwani nini lakini Janet,nini ulitaka sikukutimizia(analia)


  JANET: najuta Victor,nisamehe mpenzi wangu

  VICTOR: futa hilo neno mpenzi,nenda kamuite yule mzee anayejiita awarding (analia)
  Janet anamsogelea Victor ,victor anamsukumiza Janet anaanguka chini janet akiwa anendelea kujizoa zoa pale chini Victor anachukua kisu na kumsogelea Janet ,Janet anapiga kelele akiomba msaada.
  Victor anarudi nyuma na kujichoma yeye kile kisu,masikini janet anamkimbilia Victor nakutaka kukichomoa kile kisu ili amnusuru mpenzi wake na kifo wakati anajitahidi kukitoa kile kisu ndio damu zina zidi kutoka nakumchafua mwilini mwake,kumbe zile kelele zake ziliwashitua watu waliokuwepo bwenini humo wakaitana na kwenda mpaka chumbani kwa Victor walipofungua mlango wanamkuta Janet akiwa amelowa damu huku mkononi akiwa na kisu pembeni yake ulikuwepo mwili wa victor ukiendelea kuchuruzika damu.
  Wanafunzi wakaanza kupiga kelele wengine wakipiga simu polisi,kuna wengine walithubutu kukimbia vyumba vyao.
  Baada ya robo saa mapolisi walifika kwenye tukio na kuuchukua mwili wa victor pamoja na mtuhumiwa,chuo kilizizima kwa huzuni vilio vilitawala chuoni hapo,hakuna alie amini kilichotokea.

  Magazeti ya kesho yake yalipambwa na vichwa vya habari vinavyo mtuhumu Janet kumuua mpenzi wake kwa kumchoma kisu,kila gazeti thubuliliandika vile lilivyopata habari .Magazeti mengine yalithubutu kuandika kuwa wivu wa mapenzi ndio chanzo cha kifo cha Victor.
  Watu wengi walivutiwa na tukio hilo hivyo basi walijitahidi kununua magazeti mbalimabli yenye habari hiyo ilikupata undani wa tukio zima.
  Mida ya saa nne alipelekwa mahakaman kujibu shitaka lake,wakat akipandishwa karandinga janet anawaona wazazi wake .Anagoma kupanda.
  “mama na baba ,si husiki mimi na singiziwa .Victor alijichoma mwenyewe kisu baada ya kugundua nimemwambukiza ukimwi sijauwa mimi jamani” janet alitamka maneno hayo huku akilia.
  Askari ana msukumiza ili apande karandinga,janet anajingonga kweny ngazi za karandiga.damu nyingi zinaanza kumtoka anaanguka chini.
  Wazazi wake wanazuiwa wasimsogelee,mama yake anashindwa kujizuia anaanza kulia watu waliokuwepo karibu nae walimuonea huruma sana kwani kilio chake kiliamsha hisia za wengi.
  Janet anafungua macho kwa tabu sana ,huku akikunja sura yake inaonyesha maumivu anayoyapata .
  “oooh naona giza mbele yangu namfwata mpenzi wangu Victor .Najua huko aliko atakuwa amensamehe”
  Maaaamaa…………nakufa nikiwa nimeathirika na virusi vya ukimwi,najuta mimi kwa kuyapuuza yale mliyonieleza ,makundi yameniponza mi…………..miii……ahh!!
  Janet anashidwa kumalizia kile alicho kuwa akisema.ana funga macho ukimya unatawala .vilio vinasikika

  Mipango ya mazishi inapangwa chini ya uangalizi wa polisi.hatimaye Victor na janet wanazikwa karibu karibu.huzuni inatawala chuooniii.
  Haikupita muda mrefu mzee Kelvin almaarufu kama Awarding anafariki kwa kifo cha ghafla akiwa ofisini kwake,mipango ya kusafirisha mwili wake inapangwa na kwenda kuzikwa kwao Mbeya.


  *********************END**************************
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  CarthbertL hadithi yako imeniliza ..maskini Janet ,Maskini Victor ..
  Hongera kwa utunzi wa hadithi nzuri na yenye fundisho kwetu ....
   
 3. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #3
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante FirstLady1, mara hii umemaliza kuisoma? kaa tayari kusoma nyingine nyingi tu nzuri kuliko hii.
   
 4. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2010
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Mh! inasikitisha sana, yaani ndoto zao zimezimika kama mshumaa((
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  nimemaliza hivi huu ni mfano hai ama hadithi ya kutunga ..inapain sana !
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kodabosi ..mbona mdomo wako uko wazi masaa yote :)
   
 7. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #7
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni story ya kweli kabisa,watajwa hapo juu sio wausika wa mkasa huu...Haya mambo yapo sana kwenye jamii zetu.
   
 8. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  Mahusiano, mapenzi, urafiki Tubadilishane mawazo kuhusu mahusiano, mapenzi, urafiki, n.k na kushauriana. TAFADHALI: Hii si sehemu ya kuweka picha chafu ama kutumia lugha kali sana. Zitafutwa!....

  kwa urefu wa hadithi hii nadhani ni busara kuwa najukwaa la hadithi...hadithiiii...hadithi njoooo uongo njoooo utamu koleaaaa....hapo zamani za kaleeeee.....

  ni maoni tuu
   
 9. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,266
  Trophy Points: 280
  Hii ni zaidi ya mshumaa...
  nice one mtunzi thanks!
   
Loading...