Kamanda Moshi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 2,013
- 3,066
miaka ya 1966 east africa muslim welfare society kwa Tanzania walipata ofa ya kujengewa chuo kikuu na serikali ya misri.kipindi hicho Tewa ndo alikua kiongozi wa jumuia kwa Tanzania.na alikua anafaatilia kwa karibu michakato,Nyerere hajampa transfer akawa balozi wa china ili kudiscourage.bibi Titi akakamata madaraka lakini vikwazo vikawa vingi ili kukwamisha ofa hiyo.isitoshe kipindi hicho viöngozi wa kiislamu walikua wanahusishwa na maasi ya jeshi ya mwaka 64 kwahiyo kamatakamata ilikua inaendelea.ilibidi Tewa na Titi wamuone Nyerere na kumlalamikia kwa mambo yalivyokua yanaenda.
Nyerere akawa mkali akawambia,''nyinyi si mmeamua kutangaza vita na mimi,basi kaeni tayari''.
Toka hapo,zikaanza juhudi za kuivunja jumuia ya kiislamu,ukawepo mgogoro hadi ikavunjwa na kuundwa Bakwata 1968.
mkuu naomba nikukumbushe, thread inasema kwa nini Nyerere hakutaifisha shule za seminary, je haya unayoongea hapa yanahusiana na mada tajwa hapo juu? tafadhali tusitoane nje ya mada husika, anzisha thread ya kusemea haya yako na tutachangia humo badala ya kuanza kupindisha mada hapa.