JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Hivi ni kwanini ndoa nyingi siku hizi zinavunjika? Yaani unakuta watu wameoana haipiti hata miaka miwili unasikia wameachana.
Mfano ni ndoa ya wasanii wetu wa Tanzania , kama Ndoa ya Ali Salehe Kiba maarufu kama “ALIKIBA” na mke wake kutoka Kenya , na ndoa ya Judith Wambura maarufu kama “LADY JAYDEE” na mume wake wa zamani Gardener G. Abashi , na ndoa Zuwena Mohamed maarufu kama “SHILOLE”.
Tatizo hili lipo hata nje ya nchi , mfano ndoa ya mastaa wakubwa wanajulikana kama Kim Kardashian na Kanye West. Na mara nyingi wanawake ndio wanao laumiwa kwa ndoa zao kuvunjika kuwa Ni kosa lao, wao sio wavumilivu na mengine mengi.
Lakini sio kweli kuwa wanawake ndio chanzo cha ndoa hizi kuvunjika, kwasababu kudumutokudumu kwa mahusiano ya ndoa ni tatizo ambalo limetokana na tofauti kati ya nyakati.
Kuna tofauti kubwa kwa jinsi maisha yalivyokuwa nyakati zile na maisha jinsi to alivyo sasa
Nyakati zile wanawake walikuwa hawana ufahamu kuhusu haki zao katika ndoa na maisha yao kwa ujumla, hivyo ilikuwa rahisi kudumu na kuvumilia kwenye ndoa hata kama hunyanyaswa na kukandamizwa kwenye ndoa hizo, kwasababu hivyo ndivyo ambavyo wameambiwa mwanamke anatakiwa awe kutokana na mafundisho ya nyakati hizo.
Ukweli ni kwamba ili ndoa idumu inabidi Kuna upande ukubali kukandamizwa na kuwa chini, na hivyo ndivyo imekuwa kwa muda mrefu Sasa. Na muda wote maisha yamekuwa nyakati hizo yakimuinua mwanaume sana na kumkandamiza mwanamke.
Mfano mzuri wanawake wengi wamekuwa wakiweka maisha yao pembeni na kufuata ndoto za mwanaume baada ya kuolewa, pia walikuwa hawapewi haki hata ya kwenda shule kupata elimu, huku wanaume tu wakiruhusiwa kwenda shule . Lakini kwa nyakati hizi, Kutokana na elimu kutolewa wanawake wamegundua kuwa wao pia ni watu sawa na wenye haki zao za msingi Kama wanaume.
Na sio kuvumilia kila kitu
Wanawake walikuwa hata hawana haki ya kuchagua nani wa kuolewa nae: Zamani wanawake walikuwa hawana haki kabisa ya kuchagua nani wa kuolewa nae na hata Ni muda gani wa kuolewa.
Maamuzi yote hayo yalikuwa katika mikono ya wanaume yaani baba wa mwanamke na upande wa mwanaume ambaye alikuwa antaka kumuoa mwanamke huyo. Ilikuwa nikitendo cha baba kuja na kumtaarifu binti yake na mama wa binti huyo kuwa amepokea mahali kutoka kwa mtu Fulani au familia Fulani hivyo ajiandae kwenda kwa mumewe siku inayofuata au siku iliyopangwa na mwanamke hakuwa na Hali yoyote ya kupinga.
Wanaume kupiga wake zao, wanaume kuzuia wanawake wao kuenda kazini au kufanya kazi za ujasiliamali, wanaume kutoka nje ya ndoa zao na ile Hali ya kwamba kwakuwa mwanaume ndio kichwa Cha familia kila atakachokisema ndio kitakachokuwa hata Kama ni kinyume au ni kibaya au mwanamke hakubaliani nacho na mengineyo.
Haya Ni baadhi ya mambo ambayo wanaume huyafanya ambayo sio sahihi kabisa katika mahusiano ya ndoa lakini kwa nyakati hizo wanawake walifundishwa kuwa haya ni mambo ya kawaida na hutokea Sana kwenye ndoa na hivyo hawana budi kuyavumilia na kuendelea kuheshimu kwakuwa ndivyo wanaume wote walivyo na hatuna cha kufanya zaidi ya kuvumilia.
Kitu ambacho wanawake wa nyakati hizi ambao wameelimika hawako tayari kabisa kukikalia kimya na ndio maana ndoa hazidumu.
Tukija kwenye nyakati tunazoishi hivi Sasa wanawake wanawake wamepewa kipaumbele sana katika sekta mbalimbali, kuanzia kwenye Elimu,Kazi, Ajira Serikalini, kwenye uongozi
Kwahiyo Sababu kuu inayofanya ndoa zivunjike Ni ile dhana ambayo wanaume wa nyakati hizi wanazozichukua wakati wa kuingia katika ndoa. Kama mwanaume anaingia na dhana kwamba, “kwakuwa mimi ndio kichwa cha familia ninachokitaka ndo kitakacho kiwe ndio kitakachokuwa na siwezi kuisikiliza mwanamke, kwakuwa mimi ndio baba”. Hapa tusitegemee kabisa ndoa kudumu kwasababu wanawake wameelimika Sasa na wanajua haki zao na hawako tayari kukandamizwa.
Hivyo ushauri wangu Ni kwamba mnapoingia kwenye ndoa inabidi tujue kuwa nyakati zimebadilika kuondoa hizi fikra za mfumo dume, yule ni mke wako, ubavu wako ni usawa wako na sawa na mwenye haki Kama wewe, muheshimu kama utakavyotaka kuheshimiwa na mtendee yale ambayo utakayotaka kutendewa. Na pia mkimshirikishe Mungu ,Nina amini kuwa ndoa yenu itadumu na itahimili mitikisiko yote.