Kwanini ndege haiwezi kufikia anga ya bluu?

Wakuu kuna una uzoefu wa kusafiri kwa ndege, hivi ulishawahi kujiuliza kwa nini ndege ina uwezo wa kufikia mawingu meupe ya mvua lakini haina ubavu wa kufikia anga/mawingu ya bluu? Why?

Kwani ile blue ni anga au mbingu? Mwezi mungu ameumba mbingu saba.
 
Duuu anga ya mawingu ya samawati!!!!
Wakuu kuna una uzoefu wa kusafiri kwa ndege, hivi ulishawahi kujiuliza kwa nini ndege ina uwezo wa kufikia mawingu meupe ya mvua lakini haina ubavu wa kufikia anga/mawingu ya bluu? Why?
 
anga halina mwisho wala rangi. Huko unakotaka ndege ifike hakuna kani uvutano - sijui kani uvutano inaitwa nini kingreza mii nilisoma kayumba na kuishia huko.

Inaitwa gravitation force.
 
Wakuu kuna una uzoefu wa kusafiri kwa ndege, hivi ulishawahi kujiuliza kwa nini ndege ina uwezo wa kufikia mawingu meupe ya mvua lakini haina ubavu wa kufikia anga/mawingu ya bluu? Why?

Kwa nini mlima ukiwa jirani unaonekana wa kijani, ila ukiwa mbali huonekana wa blue?
 
sasa mkuu ile ya blue ni kitu gani?
Jiulize kwanza kwa nini maji ya bahari au ziwa ukiyaangalia kwa mbali unaona kama ya bluu...ulishawahi kufika baharini ukayachota na kukuta ni ya bluu?

Au ukiangalia kwa mbali hata sasa angalia mbele yako utaona kama anga linashuka kugusa ardhi na kutengeneza dome..ulishawahi kukimbia (kwa miguu au kwa gari) ukagusa lile anga kule linakoonekana kugusa ardhi?

Kwa mifano hiyo utagundua kuwa pale uwezo wa macho ya binadamu kuona ndipo yanapofunga ukurasa na hapo utaona bluu au anga kugusa ardhi. Kaka yangu mmoja kipindi ana akili za ki-teenager alikimbia kilometa za kutosha kwa lengo la kushika anga kule linakoshukia, aliishia kurudi nyumbani amechoka ile mbaya!
 
Elimu ya bure kijana hicho unachokiona kama blue sio anga ila Ni rangi ya miale mifupi itokayo kwenye jua (Short wave radiation) yenyewe ina rangi ya blue kwa asili na kwakua haina uwezo wa kusafiri umbali mrefu usambaaa angani na kufanya anga liwe la blue (scattering process ) kitendo hicho hakina totauti na urushaji wa mafataki ya rangi angani ambayo usababisha anga kuwa na rangi ya fataki asante wako ktk kujenga taifa mkatagogo kwa wembe

Iko poa hiyo
 
Jiulize kwanza kwa nini maji ya bahari au ziwa ukiyaangalia kwa mbali unaona kama ya bluu...ulishawahi kufika baharini ukayachota na kukuta ni ya bluu?

Au ukiangalia kwa mbali hata sasa angalia mbele yako utaona kama anga linashuka kugusa ardhi na kutengeneza dome..ulishawahi kukimbia (kwa miguu au kwa gari) ukagusa lile anga kule linakoonekana kugusa ardhi?

Kwa mifano hiyo utagundua kuwa pale uwezo wa macho ya binadamu kuona ndipo yanapofunga ukurasa na hapo utaona bluu au anga kugusa ardhi. Kaka yangu mmoja kipindi ana akili za ki-teenager alikimbia kilometa za kutosha kwa lengo la kushika anga kule linakoshukia, aliishia kurudi nyumbani amechoka ile mbaya!

mkuu bahari ni kama kioo na ndo maana ukitazama maji ya bahari unaona uso wako, kwa hiyo maji ya bahari kama kioo yana hakisi na kuchukua taswira rangi ya anga ambalo ni la blue na kufanya maji ya bahari yaonekane ya blue na ndio maana ukiyachota uwezi kuona rangi ya blue tena sawa mkuu
 
Hapo jikite atmospheric level, troposphere,stratosphere,mesosphere&meterosphere.Hivo air bus fly at troposphere kutokana anga zingine kuna uvutano
 
Back
Top Bottom