Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

Mungu hana hasara hata kama mwanadamu atomuabudu anavyo viumbe vingine vingi zaidi ya wanadamu katika atmosphere zingine zinazoonekana na zisizoonekana.

Kama aliweza wafuta majini, shetani na malaika zake ambavyo ni wengi kuliko wanadamu sembuse mwanadamu.

Mungu anataka wanadamu tumuabudu kwa faida yetu, SAwa na mzazi anataka mtoto asome kwa faida ya mtoto mwenyewe.
 
Sio katika perception ya kidini bali katika dhana nzima ya uwepo wake imekaa kimagumashi.

Sababu kuu ni kuwa hakuna uthibitisho wa Mungu kuwepo
Weka vidhibitisho mezani na vitu gani vinakufanya uamini hivyo
 
Mungu ndio mtoa pumzi na chanzo cha upendo kwetu sisi wanadamu.

Ulimwengu si sababu ya Mungu kuwepo kwani yeye ndiye aliyeuumba.
Angeendelea kuwepo hata asingeumba ulimwengu na sisi wanadamu.

Kiukweli imani zetu za kidini hazituweki wazi sana juu ya sababu hasa ya Mungu kuumba ulimwengu.
Kwanini asingeacha tu??
Kuumba ulimwengu kunamfaidisha nini hasa??
Kutokuumba ulimwengu kunahasara gani kwake??
Je, hakujua anguko la mwanadamu kabla ya uumbaji wake??

Zaidi, baadhi ya dini zinatuambia kwamba kulingana na ukuu wa Mungu, baadhi ya maswali hayawezi kujibika kwa akili zetu na tutapata nafasi ya kuuliza maswali yanayo tutatiza tufikapo mbinguni.

NB: Huwezi kuelezea uwepo wa Mungu nje ya imani za kidini (ni swala la imani tu).
Unawezaa vizuri tuu tena Sayansi ndio inaeleza vizurii na kutoa majibu sahii ya uwepo wa Mungu kuliko dini zetu
 
Kabla hajaiumba dunia Yeye alikuwepo,kabla ya kumuumba mwanadamu na viumbe vingine Yeye alikuwepo,wewe na viumbe wengine mtakufa lakini Yeye ataendelea kuwepo

Mungu yupo kwasababu alipenda kuwepo hakuna aliyemuweka hapo alipo mpaka ahoji kwanini yupo,pia hata ukijua kwanini yupo haitakusaidia,cha kukusaidia ni wewe kujiuliza kwanini upo au kwanini uliumbwa,hiki ndicho kitakachokusaidia

Acha kupoteza muda hapa jamii forum kufikiria mambo ambayo hakuna mwanadamu ashibaye wali maharage anaweza kujibu,hata malaika ambao ni watakatifu hawataweza kulijibu swali lako,mambo yaliyoko wazi na yaliyofunuliwa kwenye upeo wa akili zetu na macho yetu hayo ni ya kwetu ila ambayo huna huwezo nayo hayo niya kwake Yeye ambaye Yuko na ataendelea kuwepo

swali ambalo unapaswa ujiulize na litakalokusaidia ni kwanini wewe upo?
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
TUANZIE HAPA... KWANINI WEWE UPO?

KWANINI TUSEME WEWE UNA AKILI...? MIMI NAAMINI WEWE HUNA AKILI? KAMA UTASEMA AKILI ZIPO... KWANINI ZIPO?
 
Hapana Mungu amekuwepo hata kabla ya huu ulimwengu kuwepo, uthibisho huu ulimwengu sio binadamu ndio walianza kuumbwa bali ni majini kwanza kabla ya wanadamu, binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu baada ya majini kugoma kumuabudu Mungu.Kabla ya majini kuwepo duniani,vipo viumbe vingine vingi pia katika sayari zingine nje ya Dunia.
Mfano UFO, malaika,nk.
Na still pana mamilioni ya sayari zingine ambazo hazijagundulika kwa macho ya sayansi ya mwanadamu.
Ebu tuletee vidhibitisho ya hii kauli yako kwamba majini waligoma kumuabudu mungu
 
Mtaongea weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!! lkn Mungu kamwe hatajulikana kwa kondoo wasio wake! kwa sababu kondoo wake wanamjua mchungaji wao!!

Na mbinguni hamwendi ng'oooooooooooo!
Mchungaji hatupo kanisani hapa weka hoja zako sawa zieleweke sio kulazimisha
 
Kabla hajaiumba dunia Yeye alikuwepo,kabla ya kumuumba mwanadamu na viumbe vingine Yeye alikuwepo,wewe na viumbe wengine mtakufa lakini Yeye ataendelea kuwepo

Mungu yupo kwasababu alipenda kuwepo hakuna aliyemuweka hapo alipo mpaka ahoji kwanini yupo,pia hata ukijua kwanini yupo haitakusaidia,cha kukusaidia ni wewe kujiuliza kwanini upo au kwanini uliumbwa,hiki ndicho kitakachokusaidia

Acha kupoteza muda hapa jamii forum kufikiria mambo ambayo hakuna mwanadamu ashibaye wali maharage anaweza kujibu,hata malaika ambao ni watakatifu hawataweza kulijibu swali lako,mambo yaliyoko wazi na yaliyofunuliwa kwenye upeo wa akili zetu na macho yetu hayo ni ya kwetu ila ambayo huna huwezo nayo hayo niya kwake Yeye ambaye Yuko na ataendelea kuwepo

swali ambalo unapaswa ujiulize na litakalokusaidia ni kwanini wewe upo?
Kwann ww upo
 
Majini wao walishahukumiwa tayari kwao ni motoni
Huwezi kwenda motoni bila kuasi
Nmesema utuletee vidhibitisho sio imani yako ww jini umewahi kumuona au nani alikumbia kuwa majini yalikuepo na yalihukumiwa motoni
 
S
Yes sababu ni uzao uliohukumiwa tayari
Sasa huo sio udikteta? Yani kiumbe kimehukumiwa kabla hata hakijazaliwa.
Vipi jini akiamua kutubu na kumrudia mola wake? Hasamehewi?

Au majini hawawezi kutubu? Hawana free will?
 
Back
Top Bottom