Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

Yupo kwa ajili ya kuchoma moto wale watukutu tukutu kama morrison
 
Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
Jibu langu ni, sifa ya Mungu ni upendo na upendo ni utoaji. Tena haswaa ni ule ujitoleaji au ujitoaji kuwa na hakika (to be exact)

Uumbaji sio sababu ua Mungu kuwepo, ni uamuzi wa hiyari kabisa wa Mungu kujitolea kujipa kazi ya kulea viumbe na mifumo inayowabeba.

Ndiyo, Mungu angeweza tu kuamua kukaa peke yake na kufaidi utukufu wake lakini amechagua kutugawia nasi uhai ili tufaidi pamoja naye.

Ndiyo maana cha msingi kwetu katika sala ni hasa shukrani tu kwa tukichokipewa tayari. Uhai.

Nilichokieleza hakitaeleweka sana kwa maskini(wanaoishi katika hali ya kuhitaji, lack) hawa huwaza kujikusanyia tu. Lakini kwa aliyeonja kuwa tajiri ataelewa haraka sana(Being rich, living in abundance). Maana siku zote mwenye uwezo mkubwa hutaka kujitengenezea mazingira ya kutoa kuwapatia anaowapenda.

So Mungu hahitaji sababu ya kuwepo, Mungu yupo. Sema sisi na uumbaji tumekuja kutokana na sifa hiyo ya kupenda kujitoa. U P E E E N D O nukta.
 
Sasa Mungu aliyetuumba sisi wanadamu na hatutegemei, Je ni kwanini alituumba? Tuna faida Gani kwake?
Haya yote bado ni mawazo ya umasikini/uhitaji ndio maana a priori yake ni kwamba kwa kuwa hatujakamilika ndio maana tunahitaji vitu fulani vitupe faida ili tuongezeke. Tukifanya chochote ni ili kitusaidie kitu fulani.

Ni tofauti na mwenye kuwa tajiri (being rich) mind you sio kuwa na(having) utajiri au kuumiliki, La. Ni kuwa tajiri being rich, living in abundance. Hapa ndio utajikuta unatafuta wasiojiweza na kuwasaidia na wewe unajiskia vizuri tu kufanya hivyo.

Ndivyo ilivyo kwa Mungu, kwa kuwa amekamilika hahitaji kujikusanyia faida ndio maana anatoa kwa upendo kamili...out of pure undiluted LOVE.

Mimi experience yangu ni nimewaona watu wenye elimu kubwa. Au hikma. Hawa watu hupenda sana kutoa hiyo elimu yao kwa watu na hujisikia raha sana kwa kufanya hivyo tu. Sikatai, kuna faida nyingine wanapata lakini raha inaanzia pale tu kwenye kuweza kutoa kitu. Itabakia kuwa ni ukweli milele na milele kwamba Ni heri zaidi kutoa kuliko kupokea.
 
Na kama hapati faida...Inamaana huku kumuabudu,kumsifu,kumlilia,kumuimbia ni kazi bure
No kwa kufanya hivyo ni sisi ndio tunaofaidika yaani kila kitu ni kwa ajili yetu. Yeye hahitaji chochote yeye ni mtoaji wa upendo wote asiyehitaji chochote
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
Nafikiri hili linakaribia kuwa swali la msingi zaidi kuliko yote manake linamgusa yule aliye chanzo cha yote. Lakini jibu lake laweza tu kuwa hivi: Mungu yupo kwasababu yote yapo. Kwanini iko hivyo? Mungu ndiye aliyesababisha yote kuwapo, hivyo kuna mantiki kusema Mungu yupo kwasababu yote yapo.
 
Kwahyo Jibu lako ni kuwa binadamu hatuwezi kung'amua swali langu??
Kwanini hatuwezi? Je Quran imesema hatuwezi kung'amua swali langu?

Kama tumeumbwa kuabudu...kwanini tunaabudu? Mungu anapata faida Gani na ibada zetu?
Nakazia "Mungu anapata Faida gani ya sisi kumuabudu/ya ibada zetu"??
 
Jibu hoja kama huwezi kaa pembeni usubili wenye uwezo wa kufikili na sijui kwa nini upo humu maana huna faidi humu tunaelimishana tunataka wenue hoja ngumu kqma hizi
 
Back
Top Bottom