Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

S

Sasa huo sio udikteta? Yani kiumbe kimehukumiwa kabla hata hakijazaliwa.
Vipi jini akiamua kutubu na kumrudia mola wake? Hasamehewi?
Au majini hawawezi kutubu? Hawana free will?
Si dikteta thus walipewa mda wa kutubu wakagoma.

Ukishakuwa kuzimu Neema ishafungwa. Majini ndio waliumbwa kabla ya uwepo wa wanadamu
 
Si dikteta thus walipewa mda wa kutubu wakagoma.
Ukishakuwa kuzimu Neema ishafungwa. Majini ndio waliumbwa kabla ya uwepo wa wanadamu
Sasa jini aliezaliwa leo kapewa lini muda wa kutubu?
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
We jamaa mbona unauliza mwanadamu maswali yanayomuhusu Mungu!? Ni nani aliwahi kukaa na Mungu mpaka akujibu maswali yako.

Majibu mengi humu ni mapokeo kutoka kwa wagiriki na waarabu! sasa nashangaa unamuuliza mwanadamu mwenzako swali la Linalomuhusu Mungu ambaye wengine tunamuona kwa vitendo na miujiza tu.

Nadhani kaa fikiria upya na uamue upande utakao amini, wengine tumeamua kuyapokea tu, kuhoji hakutakusaidia sana maana hakuna mwenye evidence za moja kwa moja juu ya maswali uliyouliza.

Ndio yale mtu anauliza eti ivi ukifa unaenda wapi? as if wanao jibu waliwahi kufa wakaenda kisha wakarudi kutoa taarifa
 
Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe)
Alikuwa na uamuzi wa kuumba au kuacha. Alichagua kuumba!

Je yeye kwanini yupo?
Kwa sababu Yupo!

Nini kilipekea yeye kuwepo?
Hakukuwa na nini, hakukuwa na kutokea kabla ya Mungu kuumba. Kabla hajaumba alikuwepo Mungu peke yake na kabla hajaumba hakukuwa na nafasi ambapo matokeo unayoyazungumzia yangetokea. Kabla ya Uumbaji hakukuwa na muda wala nafasi. so maswali yote yanayohusu muda na nafasi ni meaningless!


Kwanini Mungu yupo?
Mungu yupo kwa sababu haiwezekani Mungu kutokuwepo
 
Sababu katoka uzao wa laana uendelea kulaanika
Kwani jini ndio anaepanga kuzaliwa jini? Jini anajizaa?
Kama jibu ni hapana, je ni nani anaemuumba jini?
Kama ni Mungu, je huoni Mungu ndio mwenye makosa?

Chukulia mfano wewe ni kinyozi... ujitengenezee sheria kuwa mtu yeyote hatakiwi kuwa na kipara, akinyoa kipara asiingie kwenye saluni yako. Umeshawaambia walinzi wakiona mtu ndani ya saluni yako ana kipara apigwe.

Halafu wewe huyohuyo ukaendelea kunyoa watu vipara kwenye saluni yako. Na ukishawanyoa wanapigwa.
Sasa hapo kosa linakuwa la nani? Wewe unayenyoa vipara? Wanaonyolewa, au sheria yako mbovu?
 
Kwani jini ndio anaepanga kuzaliwa jini? Jini anajizaa?
Kama jibu ni hapana, je ni nani anaemuumba jini?
Kama ni Mungu, je huoni Mungu ndio mwenye makosa?

Chukulia mfano wewe ni kinyozi... ujitengenezee sheria kuwa mtu yeyote hatakiwi kuwa na kipara, akinyoa kipara asiingie kwenye saluni yako. Umeshawaambia walinzi wakiona mtu ndani ya saluni yako ana kipara apigwe.
Halafu wewe huyohuyo ukaendelea kunyoa watu vipara kwenye saluni yako... Na ukishawanyoa wanapigwa.
Sasa hapo kosa linakuwa la nani? Wewe unayenyoa vipara? Wanaonyolewa,, au sheria yako mbovu?
Mbwa uzaa mbwa hawezi zaa mbuzi
 
Mbwa uzaa mbwa hawezi zaa mbuzi
Mbwa anaezaliwa qlipanga kuzaliwa mbwa? Kama hakupanga, kwanini aadhibiwe kwa kosa ambalo hakuwa na uwezo/choice ya kutokulifanya? (kuzaliwa mbwa)
 
Mbwa anaezaliwa qlipanga kuzaliwa mbwa? Kama hakupanga, kwanini aadhibiwe kwa kosa ambalo hakuwa na uwezo/choice ya kutokulifanya? (kuzaliwa mbwa)
Ipo hivi waliopewa uchaguzi wa kuzimu au paradise ni binadamu sababu mlango wa rehema aujafungwa.majini au uzao wa majini wao hawana choice.
 
Mchungaji hatupo kanisani hapa weka hoja zako sawa zieleweke sio kulazimisha
Aseee?? Kwanza jua nimefurahi saaaana! ndani ya Moyo wangu kunipatia hicho cheo tukuka! hujui tu kuwa nina furaha!.. Na kweli cheo iko nina kipenda/Tamani mnoo! Mungu ana jua!

Naomba siku moja iwe km ulivo tamka!...Biblia naipenda sana, kuisoma hasa Mimi Binafsi!...Kufundishwa na Mtu/Mwinjilist/Mchungaji hainipagi raha km nikisoma binafsi!

Haya nayo yasema siyo ya kwangu ni kwa mujibu wa Neno lili lovuviwa na Roho Mtakatifu! Biblia!...Cain, Esau, Lilith nk! hawa wana watoto humu Duniani,.....

..kwa sababu baada ya Gharika kamwe Biblia haikusema walikufa au walipotezwa kwa namna yeyote ile!...Bali waliendelea kuishi, (The desire of Ages volume II) na mpaka sasa....''ke ni Mama waviumbe wote''!

Tunao, hata hapo ulipo wapo! humu JF Ndo kabisaa.... Biblia hiyo hiyo inasema ivi nanukuu...''Nefilim walikuwepo Kabla na Baada ya Gharika''!...

je unawezaje kuwa jua leo, kuwa huyu ndiyo Nefilimu? na huyu siyo?......

simple tu sikia sasa, Mungu alivo sema simple tu kuwa ''utawajua kwa Kauli na Matendo yao'' ...hata Misikitini Makanisani wamoooo! tena akaongezea..... ''Muwajaribu''.... sasa hata kuwa jaribu hujui ndg?????
 
Ww jini umewahi kumuona
Mbona meeengi tu yanazurula Mitaani humo!! km hujawahi kuliona jini Basi jua kabisaa huna Nyota ya Mafanikio/Uungu! Jini pia halikutaki?

sababu yale yana akili sana!! yanatafuta watu wenye Potential/wenye vismart/Maono...haya hata hapo kwa Gwajima tu pia hujayaona?? WKT yana zurula hovyo?? pole sana!

Jini akili mingi linataka ambao Mungu amewapanga wenye maono/Mambo makubwa Duniani,...ni sawa na kaka Jambazi. ivi? una dhani ataenda kuvunja kwa Maskini??...Never!!

Maskini mlevi wa DSM hana hela!!,....... DSM/Mbagala nk! kuna vibaka/jambazi hatare! lkn maskini wa huko atakuona Muongo! ukisema huko kuna majambawazi!

maskini hana cha kuibiwa!...Tukija kwako sasa na wewe ni sawa na hao walevi maskini wa mbagala! kiimani!

Nakuomba uli- relux!.... jini hakutambui??, ukiwa na bahati, uta kuwa kuni siku ya kiama, za kuteketeza wenye dhambi!! kwenda Mbinguni utastukia, tunarudi kula Bata! kutawala!

Si ajabu Malaika hawajishughulishi nawe! fikiria, Hata majini (mtaji wa mbinguni) yana kudharau! hayakujaribu? sasa je? Ufalme wa Mbinguni utaujuaje? wkt hupati majaribu??.....

Na majaribu ndo mtaji Wa mbinguni? ......Majini yanajua mbinguni kulivyo kutamu, weye ni toto lao! wamekunyima ufahamu wa uzuri wa Mbinguni! ili usije yageuka!!.... stuka dogo!

Mie siyo mchoyo! nasema sana sababu hivi nakutakia Mema! uende Mbinguni! mwenzako Kiranga Ameokoka kilazima!...ndo maana hasikiki kupinga neno! siku hizi.....

Baada ya kugundua kuwa alikuwa akifanya makosa akatubu! ....ayaa! usije sema sikukwambia!..maana mie siyo mchoyo wa neno!...sometimes ni Malaika wanakuita kwa kulia machozii kupitia hili bandiko ! lkn huoni!

siku ukivunjika shingo lita vunjika ghafla huta pata Dawa!...Muda ni sasa! na kama wewe na Mtu yeyote huta/hata sikia sauti hii, huna/hana wokovu! na uzima wa Milele!

JUA KM UJUAVYO Yesu amenituma nikuokoe wewe na Wenzako wote wenye myoyo migumu km wewe! ukizingatia kwamba MUNGU HADHIHAKIWI!
 
Nguvu yenye uhai isoyoonekana itendayo kazi. Mfano mtu ni muunganiko wa vitu vitatu navyo ni MWILI, ROHO na NAFSI ufanya Kazi kwa kushirikiana
1. Wewe umejuaje kuwa ipo wakati ni nguvu isiyoonekana ? Na inatenda kazi zipi ?

2. Nini tofauti Kati ya nafsi na roho ?

3. Unathibitishaje kuwa mtu ni muunganiko wa mwili, roho na nafsi zinazo fanya kazi kwa kushirikiana ?
 
Kwahyo Mungu ni mtazamo tu wa Wanadamu
Nje ya Huu mtazamo Mungu Hana sababu?

Inamaana bila sisi, Mungu Hana maana yoyote?
Inategemea kwako maana ya "maana yoyote" ina maana gani hasa kwako, uwepo wake tosha unaweza kuwa maana ya yeye kuwepo lakini kwako hiyo maana inaweza isiwe maana ya maana.

Hivyo unamaanisha nini hasa unaposema "bila ya sisi mungu hana maana yoyote?

Na sijasema mungu ni mtazamo tu wa binadamu bali nimesema uwepo wa mungu ili kusimiamia binadamu ndio mtazamo wa binadamu juu ya uwepo wa mungu.

Nikikuuliza kwanini wewe upo hai sasa hivi utajibu nini?
 
1. Wewe umejuaje kuwa ipo wakati ni nguvu isiyoonekana ? Na inatenda kazi zipi ?

2. Nini tofauti Kati ya nafsi na roho ?

3. Unathibitishaje kuwa mtu ni muunganiko wa mwili, roho na nafsi zinazo fanya kazi kwa kushirikiana ?
1.Kupitia elimu ya kiroho,yaani ulimwengu usioonekana.
ROHO ni nguvu ya uhai ndiyo uongoza mwili bila roho mwili si kitu ni SAwa na gari bila injini.

2. Nafsi ni uwezo, ufahamu,nadhiri, akili ya kujua au kuhisi uwepo

3. Mfano roho ikitoka, mtu huwa maiti, mwili kupumzika lakini nafsi na roho zipo active hadi mwisho wa maisha yako, nafsi ni copy yako au kivuli chako ktk ulimwengu usioonekana ambacho ucontrol mwili wa nje mfano kuwaza, ndoto

Hili somo ni pana zaidi.

Kwa kirefu pitia hapa ROHO,NAFSI NA MWILI
 
Alikuwa akifanya nini katika hicho kipindi?
Hauwezi kujua usichokijua.

Hakuna binadamu anayejua alikuwa anafanya nini hasa, sababu binadamu ameanza kujua uwepo wa mungu na kuhusu mungu punde tu binadamu huyo alipoanza kuwepo hayo mengine ni yeye mwenyewe ndio anajua alikuwa anafanya nini hasa.

Labda siku moja atokee na atuambie alikuwa anafanya nini kabla ya uwepo wa binadamu.
 
Anawasimamia binadamu katika lipi?

Ukraine kuna massive murders watu wanakufa afu we unasema anatusimamia.

Ukiniuliza kwanini nipo hai jibu ni moja tu

Nipo hai kwasababu ya juhudi zangu binafsi za kuepukana na hatari zinazoweza nisababishia nisikuwepo though active cells nazo zinanifanya nizidi kuongeza number ila zikichoka nitakufa tu
Anawasimamia juu ya uwezo wa utambuzi wa mema na mabaya.
Huko ukraine wanajua kuua ni kitu kibaya lakini wanafanya bila mungu kuingilia sababu amewapa free will lakini malipo watapewa siku ya mwisho.

Mwanafunzi uliyempa mtihani na akajaza majibu siyo hauwezi kumsahihisha na kumuadhibu hapohapo wakati anafanya huo mtihani bali utasubiri mpaka muda sahihi uliopangwa wa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom