Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 7,262
- 12,620
- Thread starter
- #161
Mzee unanitisha Sasa ...Kuna mtu unaemjua alieuliwa?.Sikia sasa; .Ukisema neno ''mungu''!! hatujui una maanisha mungu gani!! bado weye mwenyewe hujui unacho uliza!! kwa sababu Miungu wapo weeengi tangia zama,
Hata Biblia Takatifu imewataja baadhi ya miungu wengii tu kuwa walikuwepo na wapo.. km mungu Baal, Osilis nk!...na hao miungu iliwasaidia sana walio iamini! Mfano mungu wa Misri huyu alishindana na Musa sana tu!!
mungu wa wafilist waliye muamini mpaka akawasaidia kumtia hatiana mbaya wao samsoni, huyu alimshinda Mnadhili wa Mungu tangu tumboni Bwana Samson, kupitia Delila mpaka akatobolewa Macho.
hivo samsoni akasota kweli kweli! nadhani unajua! Washami pia walikuwa na mungu wao aliye washindisha vita...wahaya wana mungu wao wa mazao mpaka leo anaitwa ''Umukama we charo''
Wakurya wana ''Nyanokwe'' anae wapa, Mazao, mvua, nguvu vitani, ndo maana wakurya wanapenda jeshi! na hawashindwi mstari wa mbele!...
Wabondei, wasambaa, wazaramo nk! wana mungu wao maarufu kama ''kiti'' huyu wanamjengea vinyumba vidogo! vidogoo! vya nyasi
size ni usawa wa ugoko! wanapalilia pale na huyo mungu wao anawalinda kweli kweli! Wachaga ndo usissikie wao kila December lazima wanaenda kuonana na kumchinjia Mungu wao Wanyama km ng'ombe mbuzi,
Hapo wanapata damu ya utakaso maarufu wanaita kisusio! lengo ni ili wafanikiwe ktk Maisha yao na Biashara zao! na kweli wako mbali ktk hii Biashara!
Wazungu wao wana muabudu mungu wao, Mzungu vilevile! huyu wanamuomba ili awape nguvu watawale Dunia ktk nyanja zooote!! na kweli kawapa miguvu tele!! hakuna wa kupinga ktk hili!
na wao wanaenda kuhiji Vatican kila mda unapo waruhusu kufanya ivo!...hapo nimekupa kwa kiasi tu, na kuna mungu mwingine yeye huyo hafananishwi na kitu chochote huyo yuko kivyake vyake tu!!
na huyo haoni tabu watu wake kuua wasio muamini, na kumsema hovyo! hovyo!! hata weye leo hii ukimsema hovyo! watakusaka mpaka wakuue popote ulipo hapa Duniani! na Listi ya wanao windwa ni kubwaa!
kusema kweli huyo simtaji nisije uawa Bureee!! wanakula kichwa........ sasa weye ndugu yangu sema wewe unamsema mungu gani huyooooo! kati ya hao wooote hapo juu? make list ni kuuubwa sana?
ila ujichunge mno kuhusu hao miungu make kuna maeneo ukigusa tu unaliwa kichwa hapo hapo mbele ya computer yako!! hayaa yangu ni hayo!
Ila Mimi Ningeuliza Kwa Yule Mungu aliwaumba watu wote wa dini zote, wazungu Kwa wahindi Kwa waafrica.