Kwanini Mpendazoe hakupewa mafao Zitto apewe?

Naomba niweke sawa kidogo tu kuondoa upotoshaji wa makusudi. Kwanza mimi nasikia tu kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la mafao. Halinisumbui. Nawakumbusha;

  1. Toka mwaka 2011 mwezi Juni niliacha kupokea posho za vikao. Kwa mwaka posho za vikao ni takribani shs 24 milioni.
  2. Wabunge hupewa msamaha wa kodi kwenye magari wanayonunua. Kwa kuwa napinga misamaha ya kodi nilikataa na mpaka namaliza ubunge sijatumia msamaha huo wa kodi.

Kwa hiyo suala la fedha sio suala la msingi kabisa kwangu kwenye maamuzi yangu.

Fact: Mpendazoe alilipwa kiinua mgongo chake kwa muda wa miezi aliyotumikia Bunge. Sio kweli kwamba hakupewa kiinua mgongo chake. Alipewa na tunaweza kuthibitisha

ZZK Usitake kutudanganya hapa.uliacha kuchukua fedha za posho za vikao huku unapokea fedha nyingine nyingi tu maradufu zaidi ya hizo toka CCM na serikali. Bisha hapa kama Rostam hakuwa anakupa fedha nyingi zaidi ya hizo posho ili kukihujumu chama chako kwa faida yako??!!watu sio wajinga wanaona kaka.
 
Acha unafiki bwana mdogo, you think you smart and you can let us rest on complacent, we are no fools to idiotically let that deadly combination live even for a second, we know the eagle in the name of ACT has landed the menace to the political struggle

O.P umebaki chuki tu
 
ZZK Usitake kutudanganya hapa.uliacha kuchukua fedha za posho za vikao huku unapokea fedha nyingine nyingi tu maradufu zaidi ya hizo toka CCM na serikali. Bisha hapa kama Rostam hakuwa anakupa fedha nyingi zaidi ya hizo posho ili kukihujumu chama chako kwa faida yako??!!watu sio wajinga wanaona kaka.

mkuu mnatuaibisha sana watanzania wenzenu, mbona nyie wenzetu huwa mnadanganyika kirahisi hivi? wewe binafsi unao uthibitisho au umesikia tu??

kwa akili hizi CCM wameishawabemenda sana
 
.....Msiamini maneno ya wanasiasa...., hilo gari nilipewa zawadi/ nunuliwa na rafiki zangu....., nionyesheni hilo gari liko wapi......!?!?!

Mimi nasema hivi ikiwa kweli umesaliti mageuzi kwasababu yeyote ile, ilihali ukijua fika hata wewe kwa wakati fulani uliishi maisha magumu yasiyokuwa na matumaini mpaka mageuzi yakakubadilishia history...... Mungu mwenyewe ajuaye mambo ya sirini akuhukumu!

What will it profit a man if he gains the whole world and loses his life/personality?

Mkuu Ame, mageuzi nini???
Je lengo la vuguvugu la mabadiliko ni kuitoa tu CCM madarakani halafu tunaingia nchi ya maziwa na asali.
Katika uongozi wa taifa, ni kipi hasa kinatoa nchi kutoka hatua moja kwenda nyingine? Je, ni dhamira safi ya chama au ni dhamira safi ya kiongozi/ viongozi??
Na mwisho ni nani hapa ana first hand information juu ya Zitto?? Tunanunua uongo kamili au ukweli kamili, au nusu uongo nusu ukweli??? Are we infatuated by the lie?????
 
Last edited by a moderator:
ZZK Usitake kutudanganya hapa.uliacha kuchukua fedha za posho za vikao huku unapokea fedha nyingine nyingi tu maradufu zaidi ya hizo toka CCM na serikali. Bisha hapa kama Rostam hakuwa anakupa fedha nyingi zaidi ya hizo posho ili kukihujumu chama chako kwa faida yako??!!watu sio wajinga wanaona kaka.
Hivi hizi ndio mnaziita akili za ukombozi!!!!!!!
 
Katika mambo ambayo kamwe sitakuja kuamini:
1) Zito ni mtu safi
2) Zito ni mjamaa

a) Kuna uthibitisho wa kibenki kuwa Zito alikuwa akipokea hela toka serikalini toka kwa viongozi wa TIS, Zito hajawahi kukanusha wala kukubali
b) Kuna uthibitisho kuwa Zito anayejidai kuwa huwa hapokei posho za vikao vya Bunge, ndiye mbunge wa upinzani anayeongoza kuwatumia watu pesa kwa njia ya MPESA. Zito hajawahi kukanusha au kukubali. Mbunge asiyepokea posho ya vikao vya Bunge halafu anaongoza kwa kugawa pesa, hiyo pesa anayogawa anaipata wapi?
c) Zito ndiye mbunge pekee wa upinzani ambaye anaongoza kwa kuwasiliana na maafisa wa juu wa usalama wa Taifa, hakuna anayejua huwa wanawasiliana kuhusiana na nini
d) Zito ndiye mbunge pekee wa upinzani mwenye ukaribu mkubwa na viongozi wa CCM, Zito hajawahi kueleza ni kwa nini na kwa maslahi ya nani
e) Zito ndiye mbunge pekee wa upinzani ambaye kwa maelezo yake aliwahi kukiri kupewa gari na kada wa CCM
f) Zito ndiye kiongozi pekee wa upinzani ambaye hajawahi kupata misukosuko yoyote toka polisi
g) Zito ndiye mbunge pekee aliyeupata umwenyekiti wa PAC kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM kwa wabunge wa CCM

Huyo ndiyo Zito. Lakini watanzania na CHADEMA wamekwishamfahamu. Sasa atalazimika kufanya harakati zake za kupambana na wapinzani wa CCM akiwa mahali wazi, nje ya vyama vya upinzani. ACT ni mwavuli uliotatuka, hauwezi kumsitiri Zito asionekane kiurahisi katika jitihada zake za kupunguza kasi ya mageuzi. Ni aheri sana adui aliye nje ya nyumba yako kuliko adui uliye naye ndani ya nyumba.
 
ngoja tukuletee ushahidi hapa msaliti mkubwa wee.acha kutapeli watu kwa kujiita mjamaa.mjamaa gani anafanyia mikutano Serena Hotel?uliuza majimbo ya chadema unajifanya una mapenzi na chama,umewauza mpaka wapiga kura wako kwa ccm na kukimbilia kigoma mjini.je umekuwa wa mwisho kutoka chadema?
Nyie mateka wa Mbowe na Dr.Slaa akili zenu za kushikiwa soma hii hapa chini.

mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m zauchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni.
 
Mkuu namswali machache kwako!....ningependa kupata majibu....

1. Kwanini chama chako kinaungwa mkono na makada wengi wa CCM?..

2. Kwanini chama chako kina pambana na Chadema tu na sio CCM walio shika dola?

3 . kwanini watu walio kuzunguka na wenye kukunga mkono katika siasa zako hasa kwenye chama chako, Wana Watusi viongozi walio kulea kisiasa tena kwa dharau?...
Mfano...Msondo ambae ni mwanasheria wako.
Habibu mchange, na hawa wote ni makada wa Act!
Hili swali la kwanza sidhani kama ni la zito kabwe maana kwa mantinki tu siku zote kunapokuwa na mafahari wawili wanapambana akitokea mmoja akachomoka kutoka kundi moja na kwenda kwingine tule mwingine hufurahi kwa kuwa anapata sehemu ya kuanzia kupiga propaganda zake
 
ngoja tukuletee ushahidi hapa msaliti mkubwa wee.acha kutapeli watu kwa kujiita mjamaa.mjamaa gani anafanyia mikutano Serena Hotel?uliuza majimbo ya chadema unajifanya una mapenzi na chama,umewauza mpaka wapiga kura wako kwa ccm na kukimbilia kigoma mjini.je umekuwa wa mwisho kutoka chadema?

Mkuu ushahidi unao? Tuusubirie toka kwako?
 
Sio kawaida yangu kukimbia mijadala. Mimi ni mtu wa mijadala. Chama cha ACT Tanzania kinaungwa mkono na wanyonge. Hakina ugomvi na chama kingine chochote cha upinzani. Ninawasihi tuelekeze nguvu dhidi ya CCM na sio kushinda kutwa kushambuliana.
Tunaweza kuwa na tofauti lakini tukawa tunalenga shabaha kwa adui mmoja. Tukomae kidemokrasia. Hii sio zero sum game. Tunaweza kufikia malengo yale yale hata kama tuna tofauti zetu. Nkrumah alisema One struggle Many fronts. Zingatieni hilo na acheni kusambaza chuki.

Nilikuuliza huko pm lakini naona kimya,sasa lini mtatangaza kujiunga na UKAWA ili tuitoe CCM madarakani? Ningekuomba juu ya hili uwe direct kuliko kupinda pinda,ukubali ni lini au ukanushe haiwezekani kwa sababu ya nini? Asante!
 
ZZK Usitake kutudanganya hapa.uliacha kuchukua fedha za posho za vikao huku unapokea fedha nyingine nyingi tu maradufu zaidi ya hizo toka CCM na serikali. Bisha hapa kama Rostam hakuwa anakupa fedha nyingi zaidi ya hizo posho ili kukihujumu chama chako kwa faida yako??!!watu sio wajinga wanaona kaka.

teh teh uliona wapi??
na kwa nini usiripoti takukuru
na kama unavidhibitisho kwa nini usipeleke kamati ya maadili ya bunge????
 
Naombeni tutafakari ni kwanini Mpendazoe hakupewa mafao yake ya ubunge wakati ule,Lakini Zitto anapewa?

Hili si jambo la kupuuza kwa ustawi wa Demokrasia yetu na sheria za nchi.

Ni vema tujadili kujua kama bunge letu lina upendeleo wa sheria au kanuni?

Tujiulize angekuwa Lissu Mnyika,Wenje au Mnyaa wangepewa?

*************** Majibu kutoka kwa Zitto ****************

Mzee Kibo10 umenikumbusha jina nililoanza kulisahau.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuuliza huko pm lakini naona kimya,sasa lini mtatangaza kujiunga na UKAWA ili tuitoe CCM madarakani? Ningekuomba juu ya hili uwe direct kuliko kupinda pinda,ukubali ni lini au ukanushe haiwezekani kwa sababu ya nini? Asante!

Hilo sahau mkuu ACT kujiunga ukawa ni sawa na Kusema Ccm waungane na ukawa.
 
Back
Top Bottom