Kwanini mbuzi tu na si mnyama mwingine?

Kwanini mbuzi tu na si mnyama mwingine?

Na kuku imekaaje maana waganga wanazipenda sana

Ndio kiumbe kidogo zaidi ambacho tunaweza kuita kuwa ndio msingi wa kuanza kuingia maagano na nguvu za giza, pia gharama yake ni ndogo lakini kadiri unavyozidi kuzama kwenye hayo mambo hasa kibiashara nguvu na mamlaka ya uongozi hupanda hatua mpaka kumaliza wanyama kama mbuzi na Ng'ombe na kuingia kwa binadamu
 
Umenikumbusha mwaka flan nikiwa mafinga jkt tulimkuta mbuzi mmoja alikuwa akiishi pangon. Alikuwa beberu mweus na rangi nyeupe shingon. Yule beberu tulimlia timing kwa mda kidogo kila asubuhi alikuwa anakuwa juu ya mlima anakula majan ikifika saa 5 anarudi eneo la pango.

Tukaanza kumuwinda sku ya kwanza alitushinda maana alikuwa anakimbia baraa na alikuwa hatoi saut kama mbuz wengne.

Sku ya pili tukampiga ambush moja matata sana tulifanikiwa kumkamata. Tulimchinja hukohuko porin na tukamla. Japo tulitishiwa sana na baadhi ya wenzet lakn tukawa matomaso.

Lakn hakuna aliyedhulika. Kwa wanaoijua mafinga pale maeneo ya changarawe ukinyooka na mbeya road kuna sehem panaitwa idetero hapo ndipo tulipo vunja matambiko ya watu


Mweeh ...ila nanyie ni makauzu.....yaani mkajitoa fahamu kabisa......au mlishapiga kijiti cha bobu?:A S-rap:
 
Hahahahahah
Na ukitaka kujua akili za kilozi na kishirikina tuma neno ULOZI kwenda msichanajr@upumbavu.com

Imethibitika una hizi tabia 1444801454444.jpg @holygrail katika ubora wake
 
Mshana Jr ... Tatizo La Mtu Inapofika Mchana Yeye Anaona Kama Ni Usiku Na Inapofika Usiku Yeye Anaona Kama Ni Mchana ... Je, Hili Ni Tatizo Gani Na Tiba Yake Ni Ipi ... ?
 
Hivi kuna anayejua wale kondoo waliokuwa wanapiga kambi pale barabara ya sita Dodoma mjini wameishia wapi?
 
Mshana Jr ... Tatizo La Mtu Inapofika Mchana Yeye Anaona Kama Ni Usiku Na Inapofika Usiku Yeye Anaona Kama Ni Mchana ... Je, Hili Ni Tatizo Gani Na Tiba Yake Ni Ipi ... ?
Mmh hili nilishawahi kulisikia mahali ngoja nisilitolee majibu sasa ila nitalitafiti na kurejea hapa
 
Nilishawahi kuweka mada ya mbuzi wa ndafu kuwa ni ibada ya kishetani, mjadala ulikuwa mzito na nilishutumiwa sana mpaka pm, hii ni kwa sababu iligusa Mila na tamaduni za makabila ya watu.

Kulikuwa pia na mada ihusuyo mbuzi wanaozurura mitaani, wanaitwa wa laana ikawa nayo ni mjadala uliogusa hisia za wengi
Si mara moja au mara mbili kusikia kuhusu mbuzi wa shughuli... Ni shughuli gani hiyo??? Kwanini asiwe kondoo au punda au Ng'ombe?

Mbuzi hasa beberu ni alama ya kuzimu, ni alama ya shetani na imani za kishetani na dunia ya giza, ndio maana laana na mapepo yote hutupiwa mbuzi kwakuwa kule ni Kama nyumbani kwao.

Mbuzi hawa wanaoitwa kwa jina lingine mbuzi wa albadiri hawafi hawaugui hawagongwi na magari na kamwe huwezi kuwakuta kwenye sehemu zisizo na watu, kamwe huwezi kukuta Mzoga wa hawa wanayama, na kama ukiukuta basi huyo alikuwa kenge kwenye msafara wa mamba.

Waganga wengi wa kienyeji na mambo ya Kiza humtumia Sana mbuzi Kama sehemu ya kafara na kinachochukuliwa ni damu na Kichwa tuu, hiki ndio hutengeneza muungano na nguvu za kuzimu.

Cha kushangaza ni kwamba mapepo huwaingia wanawake zaidi kuliko wanaume, na kwa wanyama mbuzi ndio hutumika zaidi kuliko wanyama wengine unajua ni kwanini?

Mniwie radhi kwa picha nitakayoweka, ni sehemu ya kuelimishana na kujuzana visivyosemwa, Nina Heshima na adabu kwa kila mtu, hasa mama zetu, picha hii isitafsiriwe Kama dhihaka... Nimetoa angalizo hili mapema.

Mfanano wa via vya uzazi vya mwanamke na kichwa cha mbuzi beberu ndio vinatengeneza colabo ya ajabu unaovutia nguvu za kuzimu na mapepo
hivi mshana....we ni mganga wa kienyeji au mwanasayansi?
 
Tatzo Tilio Wengi Tunakariri Alichosema Mshana Badala Ya Kuelewa.

Swala La Wanyama Kutumika Lipo Tena Kwa Wanyama Tofauti Kulingana Na Hitaji La Imani Ama Tukio Husika.

Mtu Hawez Kuvunjika Mguu Akapewa Mseto Na Hawezi Kuugua Malaria Akavalishwa POP, So Tunapaswa Kuelewa Kwmb Viumbe Wengi Hutumika Kwny Matambiko Ama Uchawi Lakn Msingi Wa Hayo Yote Hutokana Na Mahitaji Ya Swala Husika.

Kuki, Paka, Bundi, Dudumizi, Mbuzi, Kondoo, Fisi Na Wengineo Hutumika Kulingana Na Mahitaji Ya Shughuri.

Kaka Mshana Endelea Kutupa Darasa.
 
hatukudhulika tulimgonga supu na nyingine iliyobaki tulichoma hukohuko
Duh!umesema supu ya mbuzi nimekumbuka mbali enzi za utoto tumeingia chaka kuwinda ndege mara tukakurupusha katoto ka mbuzi tukakakamata faster dogo mmoja akajipa jukumu la kurudi kwao kuchukua sufulia akaelekezwa qibla na mambo yakajipa tumekaa tunapiga story ili tule nyama kuni za kutosha zimechochewa.Jamaa kuja kufunua ili aone nyama imeiva anakuta uji watu tukapagawa kuwahadithia washkaji ndo kutuambia kalikuwa hakajakomaa.
 
apa mikuamua ujifunze kitu au uache kwasababu ya kujifanya mjuaji mi nimejifunza kitu elimu aina mwisho
 
Yeah mshana, tupatie mambo, hio mbuzi hata sis hutumia Sana kwa matambiko, so kuna ukweli nwingi sana hata Ile pentagram hufanana Sana,
 
Back
Top Bottom