Kwanini mbuzi tu na si mnyama mwingine?

Kwanini mbuzi tu na si mnyama mwingine?

Nilishawahi kuweka mada ya mbuzi wa ndafu kuwa ni ibada ya kishetani, mjadala ulikuwa mzito na nilishutumiwa sana mpaka pm, hii ni kwa sababu iligusa Mila na tamaduni za makabila ya watu.

Kulikuwa pia na mada ihusuyo mbuzi wanaozurura mitaani, wanaitwa wa laana ikawa nayo ni mjadala uliogusa hisia za wengi
Si mara moja au mara mbili kusikia kuhusu mbuzi wa shughuli... Ni shughuli gani hiyo??? Kwanini asiwe kondoo au punda au Ng'ombe?

Mbuzi hasa beberu ni alama ya kuzimu, ni alama ya shetani na imani za kishetani na dunia ya giza, ndio maana laana na mapepo yote hutupiwa mbuzi kwakuwa kule ni Kama nyumbani kwao.

Mbuzi hawa wanaoitwa kwa jina lingine mbuzi wa albadiri hawafi hawaugui hawagongwi na magari na kamwe huwezi kuwakuta kwenye sehemu zisizo na watu, kamwe huwezi kukuta Mzoga wa hawa wanayama, na kama ukiukuta basi huyo alikuwa kenge kwenye msafara wa mamba.

Waganga wengi wa kienyeji na mambo ya Kiza humtumia Sana mbuzi Kama sehemu ya kafara na kinachochukuliwa ni damu na Kichwa tuu, hiki ndio hutengeneza muungano na nguvu za kuzimu.

Cha kushangaza ni kwamba mapepo huwaingia wanawake zaidi kuliko wanaume, na kwa wanyama mbuzi ndio hutumika zaidi kuliko wanyama wengine unajua ni kwanini?

Mniwie radhi kwa picha nitakayoweka, ni sehemu ya kuelimishana na kujuzana visivyosemwa, Nina Heshima na adabu kwa kila mtu, hasa mama zetu, picha hii isitafsiriwe Kama dhihaka... Nimetoa angalizo hili mapema.

Mfanano wa via vya uzazi vya mwanamke na kichwa cha mbuzi beberu ndio vinatengeneza colabo ya ajabu unaovutia nguvu za kuzimu na mapepo

Pumba tupu PUMBAVU
 
Mkuu mshana jr inaelekea unauelewa sana nahaya mambo Usiache kuelimisha haya mambo Unajua tatizo watu hatuamini km Shetani ana ufalme wake kamili na anamajeshi yake humu duniani sasa watu wengi hawapendi kujifunza haya mambo ninachotaka watu wajue Ulimwengu wa Roho unanguvu kuliko watu wanavyidhani so Nivyema kujifunza haya mambo
 
Last edited by a moderator:
Umenikumbusha mwaka flan nikiwa mafinga jkt tulimkuta mbuzi mmoja alikuwa akiishi pangon. Alikuwa beberu mweus na rangi nyeupe shingon. Yule beberu tulimlia timing kwa mda kidogo kila asubuhi alikuwa anakuwa juu ya mlima anakula majan ikifika saa 5 anarudi eneo la pango.

Tukaanza kumuwinda sku ya kwanza alitushinda maana alikuwa anakimbia baraa na alikuwa hatoi saut kama mbuz wengne.

Sku ya pili tukampiga ambush moja matata sana tulifanikiwa kumkamata. Tulimchinja hukohuko porin na tukamla. Japo tulitishiwa sana na baadhi ya wenzet lakn tukawa matomaso.

Lakn hakuna aliyedhulika. Kwa wanaoijua mafinga pale maeneo ya changarawe ukinyooka na mbeya road kuna sehem panaitwa idetero hapo ndipo tulipo vunja matambiko ya watu

Aaaaaamen.
 
Huyo walishamaliza naye shughuli ni Sawa na ile methali isemayo ganda la mua la Jana...chungu kaona kivuno...!!!

Kama wamemiza shuguli mbona damu haikutoka kwa huyo ng'ombe? kafara ni damu, na hiyo damu ndo inatenda kazi.
Hata Yesu alimwaga damu yake kwa kujitoa kafara na kinachotenda kazi ni damu yake ndo maana tunasema damu ya Yesu inanena.
Kwahiyo huyo mbuzi kama hakuchinjwa basi tambua kuwa hakuwa amefanyiwa shuguli zozote kafara, au labda walimnenea kuwa atamayemla basi moja kwa moja ameunganishwa mahala flani.
 
Mkuu waswahili wanasema huwezi kumjua mchawi kama na Wewe sio member. Vp umemchungulia kwenye Rada nini?

Kumjua mchawi sio lazima na wewe uwe mchawi, ukiwa na nguvu kubwa ya rohoni unaweza ukawajua wachawi na ukawatesa saaana.
Mambo ya rohoni yanafahamika kwa namna ya kiroho, hata wale wachawi nguli huwa wanawatambua watu wenye Mungu, wakiwaangalia tu huwa wanawatambua.
 
Lakn mshana jr hayo mambo ya mbuzi naona kama yanatofautiana kutokana na sehem.

Mambo ya mbuzi wa shughuli mm nmeanza kuyaona maeneo ya pwan na kanda ya kat. Lakn mikoa ya kwetu nmeona kondoo ndio anahusika sana.

Na kwetu zaman chifu akifa alikuwa anazikwa mtu aliyehai pamoja na chifu na ng'ombe wote wanazikwa kaburi moja

Kina kitu kinaitwa MADHABAHU.
Sifa ya madhabahu yoyote ni kusema au kutoa majibu ya watu juu ya eneo flani.
Unapoambiwa au mnapoambiwa mpeleke mbuzi, ng'ombe, kuku, binadamu basi tambua kuwa yule mganga au huyo mzee hasemi kwa mapenzi yake ila ni ile madhabahu ya miungu ndo inasema kupitia hiyo madhabahu kuwa inataka sadaka ya aina gani.

Madhabahu za mkoa wa lindi zinaweza zikapendekeza sana kafara za wanadamu ila madhabahu za Arusha zikataka sana mbuzi. kwahiyo ni vitu vinavyotofautiana.
Kumbuka madhabahu zimegawanyika ktk sehemu mbalimbali, kuna madhabahu za kifamilia, madhabahu za kiukoo, madhabahu za kimkoa, madhabahu za kitaifa n.k
Na hizi madhabahu zinakuwa na hiyo miungo, kwa ngazi ya kifamilia au kiukoo hiyo miungu inaweza ikavaa sura ya mtu yoyote ambae amekufa ktk huo ukoo au familia.
 
Last edited by a moderator:
Nilishawahi kuweka mada ya mbuzi wa ndafu kuwa ni ibada ya kishetani, mjadala ulikuwa mzito na nilishutumiwa sana mpaka pm, hii ni kwa sababu iligusa Mila na tamaduni za makabila ya watu.

Kulikuwa pia na mada ihusuyo mbuzi wanaozurura mitaani, wanaitwa wa laana ikawa nayo ni mjadala uliogusa hisia za wengi
Si mara moja au mara mbili kusikia kuhusu mbuzi wa shughuli... Ni shughuli gani hiyo??? Kwanini asiwe kondoo au punda au Ng'ombe?

Mbuzi hasa beberu ni alama ya kuzimu, ni alama ya shetani na imani za kishetani na dunia ya giza, ndio maana laana na mapepo yote hutupiwa mbuzi kwakuwa kule ni Kama nyumbani kwao.

Mbuzi hawa wanaoitwa kwa jina lingine mbuzi wa albadiri hawafi hawaugui hawagongwi na magari na kamwe huwezi kuwakuta kwenye sehemu zisizo na watu, kamwe huwezi kukuta Mzoga wa hawa wanayama, na kama ukiukuta basi huyo alikuwa kenge kwenye msafara wa mamba.

Waganga wengi wa kienyeji na mambo ya Kiza humtumia Sana mbuzi Kama sehemu ya kafara na kinachochukuliwa ni damu na Kichwa tuu, hiki ndio hutengeneza muungano na nguvu za kuzimu.

Cha kushangaza ni kwamba mapepo huwaingia wanawake zaidi kuliko wanaume, na kwa wanyama mbuzi ndio hutumika zaidi kuliko wanyama wengine unajua ni kwanini?

Mniwie radhi kwa picha nitakayoweka, ni sehemu ya kuelimishana na kujuzana visivyosemwa, Nina Heshima na adabu kwa kila mtu, hasa mama zetu, picha hii isitafsiriwe Kama dhihaka... Nimetoa angalizo hili mapema.

Mfanano wa via vya uzazi vya mwanamke na kichwa cha mbuzi beberu ndio vinatengeneza colabo ya ajabu unaovutia nguvu za kuzimu na mapepo

mbuzi mimi basiiii.
 
Pumba tupu PUMBAVU

Mkuu sijui kama umemuelewa mshana jr vizuri..........haya mambo hajahitaji elimu kubwa sana kuyafahamu.......yapo mitandaoni mengi ya kutosha........ni upekuzi wako tu.........ndio maana kuna nuru na giza........
sijui kama umenielewa.......au na mimi ni pumbavu tu..........
 
Last edited by a moderator:
Kuna vitu ukivichunguza sana hautaweza kuishi kwa amani.
 
Mchana Jr wewe unaweza hata kutuagua hebu tusaidie hili je Lowasa atashinda??? Kweli???
 
Back
Top Bottom