Kwanini mbuzi tu na si mnyama mwingine?

Kwanini mbuzi tu na si mnyama mwingine?

Mbuzi ni mmojawapo ya wanyama wasumbufu Sana, ni Afadhali hata kuchunga kondoo kuliko mbuzi, hawatulii sehemu moja.. Sasa ukishaona mbuzi ana ratiba maalum tena anayoizingatia vizuri basi ujue huyo si kiumbe wa kawaida, lakini si lazima kuwa anaweza kukudhuru kwa njia yoyote kwakuwa wewe si mlengwa na ndio maana hata kuna vitu vya thamani hutupwa na kuokotwa na wengine na visiwadhuru

dah! Aisee dunia ina mengi
 
Lakn mshana jr hayo mambo ya mbuzi naona kama yanatofautiana kutokana na sehem.

Mambo ya mbuzi wa shughuli mm nmeanza kuyaona maeneo ya pwan na kanda ya kat. Lakn mikoa ya kwetu nmeona kondoo ndio anahusika sana.

Na kwetu zaman chifu akifa alikuwa anazikwa mtu aliyehai pamoja na chifu na ng'ombe wote wanazikwa kaburi moja
 
Last edited by a moderator:

Kwanini mbuzi tu wale wanao taka kuku?
 
Msiwe na hofu, mbuzi nimnyama tu kama wengine na huwa wanajifunza, nilikua na jirani yangu alikuaanafuga mbuzi, baadae akaamua kuwaacha wazurure na walikua wnanrudi nyumbani wenyewe, walikua wanatembea hadi makaburi ya kinondoni na baadae wanarudi, liua ni uvivu wa kuwatafutia chakula, lakini ikifika siku anataka kuchinja, anachinja kama kawaida
 
Lakn mshana jr hayo mambo ya mbuzi naona kama yanatofautiana kutokana na sehem.

Mambo ya mbuzi wa shughuli mm nmeanza kuyaona maeneo ya pwan na kanda ya kat. Lakn mikoa ya kwetu nmeona kondoo ndio anahusika sana.

Na kwetu zaman chifu akifa alikuwa anazikwa mtu aliyehai pamoja na chifu na ng'ombe wote wanazikwa kaburi moja

Yeah ni ukoo mmoja tu ndio maana kwenye mojawapo ya hizo picha ni kichwa cha kondoo
 
Last edited by a moderator:
Marko 16:17 - 18; "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminuo; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, na watapata afya."
 
Yeah ni ukoo mmoja tu ndio maana kwenye mojawapo ya hizo picha ni kichwa cha kondoo

Kwa hiyo una maana mbuzi na kondoo wote wanahusika?

Binafsi nilishashuhudia jamii ya watu fulani wakitumia kondoo katika mambo yao ya mila.
 
Matendo ya mitume 10:9 - 16

V.14; "Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi."

v.15; "Sauti ikamjia mara ya pili ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi."
 
Tatizo hapa ni kwa wale wanao amini ushirikina. Chochote atakiwazia kishirikina..akiumwa mafua atasema kalogwa. Akila uchafu akiumwa tumbo na jirani alikuwepo mtu ataamini kalogwa..akisikia jogoo wa jirani kawika saa 7 usiku huyo mchawi.. Akisikia paka kapita mchawi.. Mbuzi ni mbuzi tu
 
kuna wakati nakuwa na hisia kwamba kuna baadhi ya watu wanataka kupenyeza hofu na imani zao za kishetani katika jamii.
they create fear so that to corrupt people's minds
 
mbuzi kaumbwa na Mungu hana connection na kuzim kama hajakonektiwa binadam ndo wanamuharamisha wenyewe..
 
Kila kitu ni imani
Kama huamini katika hayo mambo hakuna cha mbuzi kondoo wala kuku wa kafara........

Imani
Imani
Imani

Umenikumbusha mwaka flan nikiwa mafinga jkt tulimkuta mbuzi mmoja alikuwa akiishi pangon. Alikuwa beberu mweus na rangi nyeupe shingon. Yule beberu tulimlia timing kwa mda kidogo kila asubuhi alikuwa anakuwa juu ya mlima anakula majan ikifika saa 5 anarudi eneo la pango.

Tukaanza kumuwinda sku ya kwanza alitushinda maana alikuwa anakimbia baraa na alikuwa hatoi saut kama mbuz wengne.

Sku ya pili tukampiga ambush moja matata sana tulifanikiwa kumkamata. Tulimchinja hukohuko porin na tukamla. Japo tulitishiwa sana na baadhi ya wenzet lakn tukawa matomaso.

Lakn hakuna aliyedhulika. Kwa wanaoijua mafinga pale maeneo ya changarawe ukinyooka na mbeya road kuna sehem panaitwa idetero hapo ndipo tulipo vunja matambiko ya watu
 
Back
Top Bottom