Kwanini mazao yote ya kibiashara tunategemea kuuza nje ya nchi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,330
33,958
Kabla ya Mwaka 1968 Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi yenye akiba kubwa ya fedha za kigeni. Zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo zilitokana na kuuza nje zao la Mkonge. Bei ya zao la mkonge lilipoporomoka na uchumi wa Tanzania nao ukatisika.

Ni kwa nini soko la ndani siyo imara sana na la kutegemeka kwa mazao ambayo tunayaita ya kibiashara? Yaani Kahawa, Korosho, Parachichi, na mazao mengine mengi,soko lake ndani ya nchi ni dogo sana chini ya asilimia tano.

Jee hali hiyo inatokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kwa watanzania kiasi cha kushindwa kununua mazao hayo au ni ukosefu wa tamaduni wa kutumia mazao hayo??
 
Uchumi wa chini unakua kwa.kuuza bidhaa nje. Just imagine kama wewe ungekuea unalima ili kukidhi mahitaji ya familia yako tu. Je, unaweza tajirika kwa kilimo hicho? Kwa hiyo ni muhimu sana kuwa na mazao ya Biashara hata hayo ya kula ili kukuza samani yetu na utajiri wa nchi.

Jambo pekee linalonikera mimi ni Uuzaji wa dhahabu nje ambazo wao wanahifadhi kubwa katika hazina zao wakati sisi hatuhifadhi.

Ikiwa wao wanachukua dhahabu na kuihifadhi sio fedha zao lazima kuna siri kubwa ambayo sisi hatuifahamu na nsuo maana tunahifadhi karatasi za dollar. Siku dollar ikiporomoka hayo.makaratasi yatakuwa hayana thamani tena..
 
Kabla ya Mwaka 1968 Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi yenye akiba kubwa ya fedha za kigeni. Zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo zilitokana na kuuza nje zao la Mkonge. Bei ya zao la mkonge lilipoporomoka na uchumi wa Tanzania nao ukatisika.

Ni kwa nini soko la ndani siyo imara sana na la kutegemeka kwa mazao ambayo tunayaita ya kibiashara? Yaani Kahawa, Korosho, Parachichi, na mazao mengine mengi,soko lake ndani ya nchi ni dogo sana chini ya asilimia tano.

Jee hali hiyo inatokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kwa watanzania kiasi cha kushindwa kununua mazao hayo au ni ukosefu wa tamaduni wa kutumia mazao hayo??
Wewe ulitakaje?
 
Uchumi wa chini unakua kwa.kuuza bidhaa nje.
Nakubaliana na wewe kuhusu suala la Dhahabu. Kama unakumbuka baada ya Augustine Mrema kukamata dhahabu pale uwanja wa Ndege, serikali ikasema inunue yenyewe dhahabu ili kukuza akiba ya dhahabu Benki Kuu.

Kilichotokea sote tunakikumbuka, Kulitokea ubadhirifu na ufujaji mkubwa wa fedha za umma kulikotokana na utapeli uliogubika zoezi zima la ununuzi wa dhahabu kupitia Benki Kuu. Kwa maana nyingine hapo tena tatizo liko kwetu sisi.

Kuhusu uuzaji nje ili kukuza utajiri wetu nakubaliana na wewe, lakini jee sisi kama taifa baada ya kuuza nje ndiyo hatupati uwezo wa kununua mazao tunayoyazalisha sisi wenyewe??
 
Zamani tulikuwa na BIT na BET
Kuna watu hawakuwahi kujua kama tulikuwa na Board of Internal Trade (BIT) na Board of External Trade (BET), ambazo zilishughulika na uuzaji wa mazao yetu. Lakini jee ni kwa nini BIT ilifeli kuendesha RTCs?

Lakini hili la kutokutumia hayo tunayoyaita mazao ya kibiashara kabla ama baada ya kuyachakata ni udhaifu mkubwa sana kwetu kama Taifa.
 
Nakubaliana na wewe kuhusu suala la Dhahabu. Kama unakumbuka baada ya Augustine Mrema kukamata dhahabu pale uwanja wa Ndege, serikali ikasema inunue yenyewe dhahabu ili kukuza akiba ya dhahabu Benki Kuu.

Kilichotokea sote tunakikumbuka, Kulitokea ubadhirifu na ufujaji mkubwa wa fedha za umma kulikotokana na utapeli uliogubika zoezi zima la ununuzi wa dhahabu kupita Benki Kuu. Kwa maana nyingine hapo tena tatizo liko kwetu sisi.

Kuhusu uuzaji nje ili kukuza utajiri wetu nakubaliana na wewe, lakini jee sisi kama taifa baada ya kuuza nje ndiyo hatupati uwezo wa kununua mazao tunayoyazalisha sisi wenyewe??
Kwanza tosheleza nyumbani, halafu uwe na biashara ya kuuza nje. Tatizo letu ni umaskini. Maskini siku zote hutazama anawezaje kutoka hata kama anaishusha hadi yake mwenyewe. Ndio maana tuna shida ya chakula, mafuta ya kula, sukari n.k. nchi inaishi kwa mission town kinachoingia ndio unajua utakacho kula, hatuna maandalizi
 
Kweli kabisa, Umaskini ndiyo chanzo chake. Huwa nawauliza watu inawezekanaje kwa mama ntilie kuendelea kuuza wali kwa kati ya shilingi 1,000 hadi 1,500 kwa sahani kwenye mazingira ambapo bei za mchele na mboga anazotumia zinapanda kila siku?

Lakini kwa mtazamo wangu mama ntilie wanajua wateja wao wengin ni maskini kiasi kwamba wakipandisha bei za vyakula vyao wanavyouza watapoteza wateja. Mtu atawezaje kula Parachichi la 1,000 wakati nyumbani kwake katoka hajaacha hata senti??
 
Kabla ya Mwaka 1968 Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi yenye akiba kubwa ya fedha za kigeni. Zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo zilitokana na kuuza nje zao la Mkonge. Bei ya zao la mkonge lilipoporomoka na uchumi wa Tanzania nao ukatisika.

Ni kwa nini soko la ndani siyo imara sana na la kutegemeka kwa mazao ambayo tunayaita ya kibiashara? Yaani Kahawa, Korosho, Parachichi, na mazao mengine mengi,soko lake ndani ya nchi ni dogo sana chini ya asilimia tano.

Jee hali hiyo inatokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kwa watanzania kiasi cha kushindwa kununua mazao hayo au ni ukosefu wa tamaduni wa kutumia mazao hayo??
Kipato kidogo cha,mtanzania..
Ukiwa na watu wako wana kipato kidogo maana yake soko lako la ndani ni dogo pia.

Jiulize mara ya mwisho umenunua nguo lini kwa familia yako ukiacha sare za shule .
 
Shida tuna viongozi wenye IQ kubwa wanaojua, kilimo, udaktari, sheria, usanifu majengo, uinjinia, ufundi umeme n.k.

Hawafanyi tafiti, kazi yao nikupiga meza bungeni na kutoheshimu taaluma za watu.
 
Back
Top Bottom