Tusiuze mazao ghafi nje ili kulinda ajira za ndani

Wamanyaki

New Member
Mar 25, 2024
3
3
Serikali yashauriwa kuongeza thamani katika mazao inayouza nje ya nchi kulinda ajira za ndani

Na Mwandishi wetu

Serikali ya Tanzania imeshauriwa kuongeza thamani katika mazao inayo uza nje ya nchi ili kulinda ajira na soko la ndani.

Katika mahojiano maalumu na Mwandishi wa habari hii, Mhadhili Mwandamizi wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abel Kinyondo amesema nchi inapo uza mazao ghafi nje ya nchi, ina safirisha mambo mawili makuu: Ajira ya ndani na thamani.

Kinyondo anasema unapopeleka korosho ghafi na mbaazi ghafi nje ya nchi, unapeleka pia mambo mawili kwa wakati huo huo.

Kwanza, unapeleka nje ajira/kazi ambazo zilipaswa kufanywa na wazawa hapa hapa nchini. Lakini badala yake kazi hizo kuongeza thamani kwa hayo mazao ghafi zinakwenda kufanywa na watu wa huko kwao.

Lakini kitu cha pili, una safirisha ubora/thamani yenyewe. Maana ubora/thamani ikiisha ongezwa kwenye zao ghafi bidhaa yake huwa ina thamani/bei yake huwa kubwa sana.

Katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwaka jana nchini India, pamoja na makubaliano mbali mbali ya kibiashara [MoU]iliyo ingia kati ya Serikali ya Tanzania na India , India imekubali kununua tani 200,000 za mbaazi.

Profesa Kinyondo amempongeza Rais kwa jitihada zake za kufungua uchumi wa nchi.

Hata hivyo ameshauri kuwa unapofanya biashara na India lazima uangalie wao wana kitu gani unacho kihitaji hapa nchini kwetu na wewe unakitu gani wanacho kihitaji ili mbadilishane. Lazima tujiulize hayo mambo!

India ni taifa kubwa lenye uchumi mkubwa. Inatabiliwa kuwa na uchumi mkubwa wa tatu baada ya Marekani na China.

India inaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu duniani.

Bahati mbaya tumekuwa tunapeleka na kuuza India mazao mbali mbali ya kilimo yakiwa ghafi, kama korosho, uwele, mbaazi, na mengine mengi.

Kwahiyo ili biashara iwe na maana inabidi tuwaombe badala ya kuchukua mazao ghafi bila ya kuyaongezea thamani tuwaombe watusaidie sisi tuweze kuongeza thamani kwenye hayo mazao ghafi kabla ya kufanya biashara nao.

Kwahiyo, huyu Profesa nguri wa uchumi anashauri kuwa unapofikiria kufanya biashara na India fikiria juu ya kuongeza thamani au ubora kwenye hicho kitu ili kupata kitu cha thamani. Na siyo kufikiria ukubwa wa fedha, kwamba biashara kati ya India na Tanzania itaingiza kiasi hiki!

Ni jambo lisilopingika kwamba India ni nchi yenye teknolojia ya hali ya juu sana, yenye maendeleo makubwa katika mambo ya madawa na tiba.

Sasa unapofanya naye biashara lazima useme, bwana wewe unafanya biashara na sisi.

Kwahiyo tuwaambie tunataka teknolojia yako, watalaam wako wa tiba.

Tunakuomba uje hapa kwetu uwajengee uwezo watu wetu hapa. Hii mikataba ya kibiashara kwa Tanania kuuza bidhaa ghafi au malighafi kwao na wao kukupatia bidhaa iliyotokana na malighafi hiyo (finished product).. Hiyo, haijawahi kufanyika popote duniani.

Tutakuwa tunatumiwa-hii ni sawa sawa na ukoloni mambo leo.

Ameongeza kuwa, kwake yeye mikataba mingi ya kibiashara tunayoingia na nchi nyingine haina tija mpaka tutakapofikiria nje ya wingi wa namba.

Tunataka vitu vinavyonekana. Mimi nina maligahfi unazozitaka na wewe unavitu ninavyo vitaka, mathalani, Nyanja ya madawa na teknolojia. Hebu tusaidiane kwenye eneo hili.

Unapofanya hivyo mikataba ya kibiashara inakuwa na maana zaidi kuliko kuingia hati za makubaliano [MoUs] lukuki ambazo hazina tija kwa nchi na watu wake.

“Kuna hati za makubalino nyingi zimekwisha ingiwa tokea uhuru enzi za awamu ya kwanza ya utawala wa Rais wa Kwanza Mwl Julius Kambarage Nyerere hadi awamu hii ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan, lakini cha kushangaza bado hatuendi popote na tumeendelea kuogelea ndani ya lindi la umasikini. Kwanini? Kwasababu hatufanyi kama inavyotakiwa.

Ameshauri kuwa nchi inapoingia hati za makubaliano ya kibiashara na nchi nyingine lazima ijuulize, nitapata nini?

Jiulize baada ya kuingia hati za makubaliano baada ya miaka sita naweza kuonesha kitu gani cha mfano kwamba hiki kimetoka na hati za makubaliano niliyoinga na nchi ya India.

Je, unaweza kujivunia nini. Je, unaweza kusema kiwanda kile , teknolojia ile iliyopo Hospitali ya Mlonganzila, imetokana na makubaliano Kati ya Tanzania na India, n.k. Hiyo ndiyo hatua tunayopaswa kufikia kama nchi, vinginevyo tutaishia kwenye matokeo hasi.

Nchi inapoingia makubaliano ya kibiashara [MoUs] mwisho wa siku tunataka tuseme tumepata hiki kwenye makubaliano ya kibiashara. Pia Inabidi tuwe na vipengele vya sheria vitakavyo turuhusu kuvunja mikataba hiyo kama upande mwingine utakiuka makubaliano.

Wahindi wana sera kwaajili ya Afrika. Kwahiyo maranyingi tunapo kwenda kuingia nao mikataba ya kibiashara tayari wao wanafahamu wanataka nini.

Kwahiyo kuuza korosho ghafi, mbaazi ghafi, hayo siyo makubaliano ya kibiashara. Lazima ifike mahali tuseme sisi tunapambana kwenye medicine, na wewe India una mafanikio makubwa. Naomba watalaam wako waje huku kuwafundisha watu wangu.

Tuwambie sisi tuna dhahabu, almasi na tanzanite, lakini wewe una utalaamu mkubwa katika teknolojia na tehama. Naomba watalaam kutoka vyuo vikuu vyenu waje kufundisha watu wangu kwenye vyuo vyetu vikuu na taasisi zingine za elimu. Waje wajenge vituo vya tehama hapa kwetu.

Kama tukifanya hivyo makubaliano ya kibiashara tunayoingia na nchi zingine yatakuwa na maana zaidi.

Mwisho.
 
Back
Top Bottom