Nimesikia story ya mama wa kambo aliyemkata mtoto wa mmewe dudu yake nikaona niweke post ya experience yangu na akina mama wa kambo.
Nakumbuka mdingi alimtema mama angu mzazi alikuwa anamzingua sana mimi nikiwa na miaka kama tano hivi, akavuta mama aliyetulea. Mbona tulionja joto ya jiwe? Unadhani mama wa kambo alinifanya mazuri basi? Mdingi alikuwa anasafiri sana.
Yaani home alikuwa anakaa siku moja au mbili anasafiri halafu huko anakaa hata wiki tatu mpaka sita. alikuwa na wamama wengine huko. Kimaisha hali haikuwa mbaya sana kwani hapo home kulikuwa na lorry tani saba enzi hizo yalikuwa machache sana, kwa hiyo ni full kazi na jumba kuuuubwa ambalo enzi hizo tulikuwa tunaona kama hekalu.
Home store ya misosi ipo full muda wote, mikaa na kuni imejaa kwenye stoo yake kwa sababu kila gari ikisafiri lazima ilete aidha mkaa, kuni, mahindi, mpunga, maharage, kuku, au nyama ya porini. Wakati mwingine vitu kadhaa kati ya hivyo vililetwa kwa pamoja.
Cha ajabu hapo home tulikuwa tunashinda njaa mpaka jioni ndio tunakula! Yaani maskini ya mungu mi sijui hata kosa nililomfanyia huyo mama I was only 5 years old, nashinda na njaa wakati ndani kuna chakula cha kutosha. Wanapewa majirani, vingine vinamwagwa, mi nashinda na njaa mdomo umekaukaaaaa! Siku mshua akirudi ndio napewa kipande cha nyama cha kuzuga.
Akiondoka kesho yake napikiwa maharage ya kula hata siku nne sikumbuki kama hata chumvi yalikuwa yanawekwa yale, na nakula jioni tu, mchana napigishwa pasi ndefu, wakati mdingi ana mahela kibao. Nimepiga hizo since 5 years old mpaka std 7 baada ya kuanza sekondari mateso yalianza kupungua kidogo kidogo.
Acheni utani nyie watu. Kulikuwa na mtoto wa kaka ake hapo home ambaye yeye (maza) ndio alikuwa anasema mwanae, huyo ndio alikuwa anaishi kama mfalme. Akawa anatuonea huruma, akipewa nyama, akipata upenyo anatufichia.
Anajifanya amekula zote baadae tukienda kulala ndio tunakula kitandani huku tumejifunika blanket maza asituone mimi na wenzangu waliokuwapo siku hiyo, hasa ndugu ndugu. Mateso makubwa yalikuwa njaa na vipigo. ​Kakosa kadogo unatandikwa mpaka unajikojolea halafu no msosi siku hiyo.
Siku ambayo siwezi kusahau ni ile ambayo njaa na tamaa viliponizidia nikadokoa nyama aliyokuwa anamuandalia mwanawe. Weee! Alinipa kichapo mpaka nika-faint. Nilipozinduka (hii ndio itafanya nije niue mwanamke siku moja) akanishika mdomo wangu akaniachamisha kwa nguvu halafu akanitemea mate ya kutosha humo.
Sijui yalikuwa makohozi yale, nakumbuka nilitapika mpaka kidogo niteme maini. Nadhani nilifaint, kwa sababu nilikuja shtukia naamshwa asubuhi niende shule tu wakati kipigo kilikuwa jana yake saa mbili usiku nilikuwa std 3.Nakumbuka hata shule sikuenda siku hiyo, nilianza safari ya kwenda kumtafuta mama yangu kwa mguu na hata sijui wapi.
Nilifuata uelekeo flani ambako ndio najua magari ya anakotokea mama angu yanaelekeaga. Nilipoenda kama kilometa tano Wasamaria wakaanza kushangaa huyu mtoto anaelekea wapi wakaanza maswali, nilipowaambia nimetoka wapi na ninaenda wapi na kufanya nini wakanikamata wakanirudisha mpaka home.
Sasa pale tunafika karibu na home akatokea mama mmoja kwa kumbukumbu zangu za wakati huo alikuwa anafanana na mama yangu) nilimrukia vibaya mpaka waliokuwa wananirudisha home wakashangaa. Sasa yule mother aliposema mimi sio mwanae wakakomaa nae mpaka wakapaone nyumbani kwake, tukaenda wote mpaka hapo sio mbali na hapo home kwetu.
Alikuwa ndio amehamia mitaa hiyo hiyo siku si nyingi hivyo nilikuwa sijawahi muona) waliporidhika, na mimi baadae nilipokubali kwamba sio mama yangu wakanirudisha kule home kabisa. Ila niliona aibu sana baadae nilipokuja tambua sasa kuwa yule niliyemkumbatia vile wala sio mama yangu. Yule mama alikuja kunipenda mpaka nakuwa mtu mzima.nadhani huruma ilichangia kwa maisha aliyokuwa anaona naishi.
Ninachotaka kusema ni kwamba muziki wa mama wa kambo mi naujua fresh tu, toka 5 yrs old mpaka form six. Mengine mengi tu inabidi niya-skip kwa sababu story itaboa.