Siamini ktk dhana ya kanisa katoliki kuwa ndilo linaloongoza nchi japo ni dhana ya muda mrefu, japo ni kweli kutokana na ukubwa wake na weledi wa hali ya juu kanisa na viongozi wake wana heshima kubwa na ushawishi ktk serikali za mataifa mbalimbali, kwa hiyo nadhani kinachofanya kanisa lisiparamiwe hovyo ni hicho na sio kwamba ikulu yetu inaongozwa kwa rimoti tokea teki. Na kwa suala la kardinali kusaidia vita ya madawa, si lazima kuitwa publicly, kuna namna nyingi za kupata maelezo yake, cheo cha kardinali ni kikubwa duniani, hapa nchini hapana mtu hata anaekikaribia cheo hicho, mtuma post afikirie kama mkuu wa mkoa angefikiria kuwa maelezo ya raisi magufuli yangesaidia ktk kurahisisha vita hii, angefanya nini, je angemtaja ktk orodha ya 65 au ungetumika utaratibu mbadala, kama hilo lingekuwa gumu kwake, si ni zaidi kwa kardinali alie kiongozi wa wote wakiwemo wakuu wa mataifa na ulimwengu, "ungetambua ukuu wa nafasi ya kardinali ktk ulimwengu wa roho, ungeanguka na kufa" barikiwa.