Hadithi: Drug Lords

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
DRUG LORDS

Wanasiasa walilalamika!

Wafanyabiashara walilalamika!

Viongozi wa dini walilalamika!

Kila mtu alilalamika

Yes! Mtu yeyote aliyekuwa kwenye ile orodha alilalamika.

Msingi wa malalamiko yao ukikuwa ni ukiukwaji wa sheria.

Yeyote mliyekuwa hamna mahusiano naye mazuri angeweza kukutaja na ukaandikwa kwenye ile orodha.

Ndio! Ungeandikwa na kutajwa kwenye ile orodha bila ya kuzingatia kama taswira yako mbele ya jamii ingeharibika.

Nia hapa si kubeza, La hasha!

Matokeo tuliyaona,

Lakini kukiukwa kwa haki za watu,kuliondoa uhalali.

Malalamiko ya watu kulilazimu haraka sana Kutekelezwa kwa sheria inayounda Kikosi cha kuzuia na kupambana na mihadarati.

Akateuliwa kamishna wa Idara ile ya DCEA

Baada ya kuundwa Idara hii, Yule aliyekuwa “Advocate” wa mapambano yale bila kutambuliwa na sheria akawekwa kando.

Idara hii imefanya kazi kazi nyingi ambazo bado ninaendelea kuzileta.

Lakini mjue,

Sio kwamba huko nyuma hatukuwahi kuwa na Idara kama hii ikifanya kazi hizi.

Idara hii ni kama tu mvinyo mpya katika chupa ya zamani.

Nia ya andiko la leo ni kuelezea operations za weledi mkubwa zilizokwisha endeshwa miaka ya nyuma.

Tofauti tu ni kwamba, hakuna alijibebesha sifa za ukinara wa kupambana na madawa, Usiri na kuzingatia haki za watu.

11 Jan 2012

MCHINGA MBILI VILLAGE, LINDI

Ni tukio ambalo lilianza mbali kidogo,

Asili ya tukio hili ni kuzurumiana.

Walianza kukamatwa Wapakistani wawili maeneo ya Mbezi Beach Jogoo.

Watu hawa walikuwa wakisifika kwa matanuzi na ukwasi usioelezeka.

Baadaye askari wasio waaminifu wakawatonya wazungu wale wa unga kuwa wameuzwa na wakawatajia aliyewauza

Jamaa waliamini kwa kuwa walikuwa “wamemrusha” mtu waliyetajiwa.

Wakaona wasife peke yao, Wakaamua kuuza ramani ya vita kijijini MCHINGA MBILI

Polisi wakakaa kimasta!

Ni kwamba siku kam tatu zilizopita, kuna binti alivuka boda ya Tanzania kwenda Msumbiji kwa njia ya “kugonga karatasi” pale border.

Kugonga karatasi namaanisha kuvuka kwa hati ya dharula ya kusafiria.

Njia hii huwatoa mashaka maafisa uhamiaji.

Kule Msumbuji binti yule akapokea mzigo kisha akavuka na mzigo mpaka Lindi Kijiji cha Mchinga mbili.

Mzigo ukaachwa pale kisha binti yule akarudi dar.

Usiku wa siku hiyo hiyo bila kujua kama yupo kwenye rada, binti yule na wenzake wakapanda boti ya kasi kurudi mikoa ya kusini.

Mbaya zaidi boti ile ilikuwa ikipeperusha bendera ya nchi nyingine.

Wakawa wanachorwa tu!

Ni mpaka waliporudi na kuingia tena kwenye ile nyumba ikiyokuwa imehifadhi mzigo kule Mchinga mbili.

Ikafanyika Ambush babu kubwa!

Pale ndani yakakutwa Madumu manne ya ujazo wa 60 Lts kila moja yakiwa yamepakiwa unga mweupe.

Mzigo kwa ujumla ulikuwa ni kilo 210 wenye thamani ya Tshs billion 9.6

Hiyo haikuwa habari.

Habari ni yule binti aliyekamatwa.

Alikuwa ni mtoto wa AMATUS LIYUMBA afisa utawala BOT

Binti yule alikuwa akiitwa MOREN AMATUS LIYUMBA akiwa na miaka 22 tu ya kuzaliwa.

Hakukamtwa peke yake!

Mama mwenye nyumba ile PENDO MOHAMED CHEUSI naye alikamatwa.

Huwezi amini kama alikuwa ni mtu mzima wa miaka 67

Kama haitoshi mwane HEMED SAID(27yrs) naye alikamatwa.

Mwanae huyu alikuwa ni dereva mkazi wa Mtoni kwa Azizi Aly Dar es salaam. Alienda Lindi kudownlod pesa na yeye usiku ule.

Subiri, Sijamaliza

Pia pale alikamatwa ISMAIL ADAM Muite ATHUMANI MOHAMED NYAUBI mkazi wa Moroco Dar na mfanyabiashara ya magari nchini Afrika kusini

Sasa nikuambie kitu?

Yaani hapa ni kama picha tu limeanza.

Hawa waliokamatwa, Freezer zao zilikuwa hazipozi.

Namaanisha waliropoka wamiliki halali wa mzigo ule, Wao walikuwa punda tu.

Kilichofata ni Sokomoko mitaa ya Sinza, Ikafatia Mikocheni na Kinondoni

Kabla sijaendelea nitawarudisha nyuma kidogo, Ile siku ya tukio wakati wanakamatwa wale watu pale Mchingambili, Kulikuwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser Iliyokuwa inasogea kwenye ile nyumba yenye mzigo.

Gari ile ilikuwa ndiyo hasa iliyotakiwa kuupakia ule mzigo.

Watu wameumbwa na machale bwana!

Ile gari ilipokaribia ni kama ilisita lakini ikawa imechelewa na polisi waliokuwa wameshafika pale waliipa ishta ya kusimama.

Huwezi amini,Kuna mtu mmoja alishuka kutoka mlango wa mbele wa abiria kwenye gari ile na kutoka “Kiberenge”

Polisi wakamkamata dereva wa gari ile na alipohojiwa alisema aliyetoka kiberenge ni Askofu.

Ndio! Alikuwa Askofu wa haya makanisa yetu ya kisasa ya kiroho ambayo waumini wake husali kwa kelele na “mizuka mingi.

Askofu yule aliitwa MORIS CHARLES. Polisi wakamhusisha pia Askofu yule na mzigo ule na Ikabainika ni mkazi wa Mikocheni jijini Dar es salaam.

Mawasiliano yakafanyika na polisi wakaenda nyumbani kwake na kukamata magari mawili ya kifahari ambayo ni Porsche Cayenne na Jeep Wrangler

Hata hivyo Ilikuja kubainika kuwa Askofu yule alikuwa akitumia hati mbili za kusafiria zenye majina mawili tofauti.

Kuna wakati alikuwa akiitwa MAURICE CHARLES na wakati mwingine aliitwa YUSUPH MOHAMED LUTENGWE.

Yaani alikuwa anaswitch passport akitaka kwenda nchi ya kiislamu au kikristo nakote alikuwa ni kiongozi wa kiroho wa dini husika.

Kwa hiyo polisi walikuja kubaini kuwa askofu yule ameshatoroka nchini tarehe 15 January 2012.

Mbaya zaidi magari yale hayakuwa na jina lake na ukazuka utata mwingine.

Mojawapo ya gari lake lililokamatwa (Land cruiser) iliweza kuuzwa na kubadirishwa kadi ya usajili tarehe 16 Jan 2016 yaani siku moja tu baada ya kusemekana ametoroka nje ya nchi na aliliuza kwa mtu aitwaye ABUSHIRI.

Swali likaja, Huyo ABUSHIRI alinunuaje gari wakati iko mikononi mwa polisi?

Ukisikia vita hii ni ngumu,hii ndio maana yake.

Kupitia taarifa za mmiliki mpya ABUSHIRI akapigiwa simu akapoke mtu aliyesema yuko Morogoro na yeye siye Abushiri lakini akawapatia namba za Abushiri aliyesema yupo Sinza Dar.

Ilipopigwa namba ile akakana kununua gari ile na alipoulizwa kwa nini namba yake amempa mtu mwingine akajibu ni mdogo wake.

Polisi wakaruka naye jumlajumla na wakampata kwa mbinu wanazojua wao.

Alipokamtwa ABUSHIRI naye friji yake ikawa haigandishi akawamwagia data kibao manjagu.

Kutokana na taarifa zile, miezi mitano baadaye Tarehe 8 June manjagu wakamkamata mchungaji KAPUPU DENIS OKECHUKU raia wa Nigeria wa kanisa la kilokole lililokuwepo Biafra Kinondoni akiwa na kilo 81 za Cocaine.

Kikosi cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya chini ya kamanda NZOWA kilitulia kwa muda wa karibu miaka miwili kikichakata taarifa walizozipata mkoani Lindi huku kikiwapeleleza kimya kimya waliotajwa kuhusika.

Hii ni baada ya kujiridhisha kuwa wale waliowakamata ni Punda tu, bali yale mapapa ya biashara hiyo bado yanaranda uraiani.

Polisi wasio waaminifu walikuwa wakitumia mwanya ule kuwakamata mapapa na kulamba mshiko kisha kuwaachia.

Kisha ikafatia kamata kamata nyingine

Taarifa za Intelejensia zilisema wahusika wa mzigo uliokamatwa Lindi(210kgs)ni ALLY HAJI HASSAN aka SHKUBA, LWITIKO ADAMSON MWAKASALA aka TIKO na IDDY MFURU ndio mapapa wa ule mzigo.

Mbaya zaidi mapapa hawa walikuwa wanasakwa kwa udi na uvumba na serikali ya Marekani kiasi kwamba mali zao walizokuwa wakizimiliki Marekani zilikuwa zimetaifishwa na idara ya OFAC inayodhibiti mali haramu za raia wa kigeni.

Yote haya yalitokea kwa sababu pasipo kujua mapapa walitumwa na wapelelezi wa CIA wawaletee mzigo wa Unga nao wakajaa wakapeleka mzigo ule na wakalipwa USD 10,000/=

CIA kwa upande wao wakawa wamefanikiwa kugundua njia wanazotumia kuingiza mzigo ule Marekani na ilijulikana Mzigo ule hutoka Brazil na Pakistan ambapo hupokelewa katika kwa meli katika ufukwe wa MARKAN nchini Pakistani.

Kisha mzigo ule ulikuwa wakipewa watu ambao husafiri na mzigo either kwenda nao DUBAI au Afrika kusini.

Unaopitia Afrika kusini ndio huja Afrika mashariki kupitia Msumbiji hadi Tanzania. Hapa Tanzania ni njia tu, lakini mzigo unatakiwa uende USA, CHINA na Ulaya. Hapa mateja wanakula tu makapi.

Sasa yule anayetoka na mzigo Brazili “kwa Pele” au Pakistani “Kwa Musharaf” huwa anaishia DUBAI au Afrika Kusini na pale anakuwa ameandaliwa mtu mwingine wa kupokea mzigo.

Hii huwezekana kwa “mchongo” yaani maafisa wote wanaohusika kwenye zile nchi wanakuwa wameshawekwa sawa kabla hata mtu hajasafiri.

“Mchongo” wa Dubai au South Africa huwa ni bei nafuu kuliko “mchongo” wa Dar ambao hauaminiki muda wowote vibuyu vinalipuka. Zamani watu walikuwa wanatumia mchongo wa KIA lakini ukashtukiwa.

Ili kuhepuka mambo hayo ndio maana unaona mzigo unazunguka kote huko ili uje Tanzania.

Wale wanaotoka na mzigo “kwa Pele” na “kwa Musharafu” huishia Dubai au SA kwa kuwa mtu mwenye passport iliyogongwa mhuri wa kwa pele au Musharaf huwa anafatiliwa sana kwenye nchi zisizo za “mchongo”

So Mzigo pale utabebwa na mwingine naye akiufikisha Msumbiji biashara yake inakuwa imeishia pale.

Kutoka tz anavuka border ya Msumbiji kwa “kugonga karatasi” so sio vigumu kushtukiwa kama ana mzigo mtu akavuka tu na kurudi kafikaje Kwa Musharaf?

Sasa utaona hivi ndivyo MORINE LIYUMBA alivyoweza kupenya na mzigo.

CIA walishajua yote haya na kabla hawajamkamata SHKUBA akawa amewatoroka na kukimbikia Afrika Kusini akiishi kwa uficho.

Kule ili kujikimu ndio akapush ule mzigo uliokamatwa Lindi na akatajwa.

Sasa kwa presha ya kuwakimbia CIA baada ya kushtukiwa yuko Afrika ya kusini ndipo akafosi akapata hati nyingine ya Tanzania. Akaona bora aje bongo ataumaliza mchezo kwa pesa.

Ni tarehe 28 Feb 2014 Usiku wa manane SHKUBA alitua uwanja wa ndege wa JKNIA akijua safari ile ni siri yake pekee lakini akajikuta anaishia kudakwa na vijana wa kamanda NZOWA na kusafirishwa usiku uleule kwa Helikopter mpaka Gereza la mkoani lindi.

Mali alizokuwa akimiliki hapa nchini ambazo ni majumba na magari ya kifahari,Bureau de Change mbali mbali na makampuni ya ulinzi vyote vikashikiliwa.

Tarehe 13 March 2014 akapandishwa mahakama ya hakimu mkazi Lindi kwa ajili ya kesi kutajwa.

KAMATA KAMATA IKAENDELEA

Mwezi wa 10 tarehe 31 mwaka ule ule wa 2014 akakamatwa mchungaji mwingine mwenye uraia wa Nigeria aliyeitwa EMEKA NWACHUKWU MERT aliyekuwa kiongozi wa kanisa moja la kiroho Sinza.

Mchungaji huyu alikamatiwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga Tegeta ambayo ilikuwa ni mali ya muadhili wa chuo Kikuu cha Dar Es Salaam

Ndani ya nyumba ale alikutwa raia wa Pakistani “Kwa Musharaf” aliyetambulika kama WALYAT KHAN na raia wawili wengine wa Nigeria CHUKSI SYLVESTER AGBAZUO na TONY OLAFOR

Kwenye nyumba ile ukakutwa mzigo wa heroine kilo 35 wenye thamani ya Tshs 2 billion.

Kamanda NZOWA akawa amestaafu huku akiwa amefanya kazi kimyakimya na kwa weredi mkubwa lakini aliacha viporo kadhaa vya kesi ya Lindi vilivyohitajika kumaliziwa.

KUKAMATWA KWA LWITIKO EMANUEL ADAMSON MWAKASALA aka TIKO

Asubuhi Tarehe 25 February mwaka 2016 polisi walivamia nyumba ya LWITIKO iliyopo Magomeni makuti Jijini Dar jirani na kituo cha daladala maarufu “Kwa bibi nyau”

Polisi kutoka kituo cha polisi Oysterbay walifika kwenye nyumba ile wakiwa wameambatana na mjumbe wa shina No. 23 MUHARAMI DAUDI saa moja Asubuhi.

Tukio lile lililovuta mamia ya watu lilisababisha kufungwa kwa barabara itokayo Sinza kwenda Magomeni na lilikuwa na uhusiano na kukamatwa kwa Muuza unga mwingine aliyejulikana kwa jina la HEMED aliyekuwa amekamatwa Mbezi beach.

Nyumba ile ilikuwa ikionekana kwa nje kama nyumba ya kawaida lakini kwa ndani ilikuwa ni ya kifahari sana yenye samani za kisasa na hata bwawa la kuogelea.

Yaani walikuta magari ya kifahari nane ambayo ni BMW X6, Lexus, Lumma CLR RS, Cooper na mengine yakiwa kwenye mazuria ghari.

Katika upekuzi na mahojiano yaliyodumu kwa masaa Saba walimkamata TIKO ili akaelezee chanzo cha utajiri ule wa kutisha usiokuwa na maelezo ya kutosha.

Magari yote na majumba yake mengine ya kifahari vilishikiliwa na kuwa chini ya uangalizi wa polisi.

Mkumbuke huyu TIKO ndiye aliyekuwa mshirika wa SHKUBA na hata CIA walikuwa wakimtafuta kwa kuingiza tani 1.8 ya cocaine jijini Texas na alikuwa akisajwa kwa udi na Uvumba.
Tiko akiwa kwake

Haikuchukua muda,mshirika mwingine papa IDDY MFURU naye akakamatwa baada ya TIKO kubanwa.

Serikali ya Marekani ikaomba mapapa hawa wakashtakiwe Marekani kwa makosa waliyoyafanya kule pia ilikuwa na wasiwasi watu hawa wangeweza kukimbia mkono wa dola ya Tanzania kwa rushwa.

Tarehe 10 April 2017 aliyekuwa waziri wa sheria na katiba Harrison Mwakyembe aliiandikia mahakama kuomba kibali cha kuwasafirisha SHKUBA na wenzake kwenda Marekani kwa sheria ya kubadilishana wafungwa.

Kesho yake tarehe 11 April 2017 ombi lile likasikilizwa Mahakama ya Kisutu.

Siku moja baadaye yaani Tarehe 12 April 2017 Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Kisutu CYPRIAN MHEKA alikubali ombi lile na kuruhusu upande wa utetezi kukatia rufaa uamuzi ule ndani ya muda wa siku 15.

Kumbe kuwekwa kule kwa nafasi ya rufaa kulikuwa kiini macho kwani usiku wake wa tarehe 13 April 2017, SHKUBA,TIKO na IDDY MFURU walisafirishwa kwa ndege hadi Marekani wakiwaacha mawakili wa utetezi MAJURA MAGAFU, HUDSON NDUSYEPO na ADINANI CHITALE wakiwa kwenye mshangao wasiamini kikichotokea.

Washitakiwa wale walikutwa na hatia nchini Marekani na mpaka sasa wanatumikia vifungo katika Magereza mbalimbali nchini humo.

Kwa huku kwetu Tanzania ike kesi ya Lindi inaendelea kuunguruma na huwezi amini nikikuambia jambo!

Leo tarehe 18 November 2021 ndio itasomwa hukumu ya kesi ile katika mahakama kuu ya mkoa wa Lindi ikiwa imetimia miaka tisa tangu kukamatwa kwa mzigo ule.

What a coincidence?

Macho na masikio yangu nayaelekeza huko leo kuona kama Binti LIYUMBA atachomoka au hachomoki? Yule mama mwenye nyumba aliyekuwa na umri wa miaka 67 wakati anakamatwa,alifia mahabusu kabla ya siku ya leo ya hukumu.

MWISHO
 
Directors wa movie script imekamilika hii...bado vitu vichache tuu movie iuze ela kibao
 
Kwahiyo hukumu ikaendaje sasa maana kwa mujibu wa maelezo yako hukumu ni 18 November 2021
 
DRUG LORDS

Wanasiasa walilalamika!

Wafanyabiashara walilalamika!

Viongozi wa dini walilalamika!

Kila mtu alilalamika,

Huyo Tiko kashatoka yupo Magomeni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom