Kwanini Makamu wa Rais hasemi "Bwana Asifiwe"?

Inategemea kikao kinafanyika wapi.

Amandla...

..tuna salamu ambazo zinawaunganisha waTz wote.

..nadhani ni vizuri tukazitumia hizo badala ya zile zinazowagawa Watanzania.

.."asaramareko" na "bwana yesu asifiwe" ni utaratibu mbaya ulioanza hivi karibuni.

..wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, na Mzee Mkapa, kulikuwa hakuna salamu za namna hiyo.

..lakini hata ktk awamu hii wako viongozi wazungumzaji wazuri kama Prof.Kabudi, Tundu Lissu, ambao ni nadra kutumia salamu za kidini-dini. Naamini hao ni mifano mizuri ya kuigwa kwa weledi wao wa kuzungumza mbele ya hadhira.
 
Hayo mambo ya kuanza na maneno ya dini niyakipuuzi sana hayatakiwi, sema yapo awamu hii sana........hii nchi haiamini dini yoyote, huwa yananikera sana kwakweli
 
Ingeekuwa vizuri kama angekuwa analitamka hivyo hivyo kwa kiswahili.
"Amani iwe juu yenu" ingeleta salamu za jumla kwa wanaomsikiliza, lakini akiingiza maneno ya kiarabu tayari inakuwa imegeuka salamu ya watu wenye imani fulani.
Hiyo ndiyo imeshakuwa salamu ya waswahili, na kwa kuwa asilimia kubwa ya waswahili ni waislamu na waswahili wamepokea maneno mengi kutoka kwa waarabu. Hivi huwezi kukataa kutumia neno kama sala, ibada au imani kutumika katika ukristo sababu tu maneno haya yana asili ya kiarabu au yanatumiwa na waislamu.
 
Mbona watu wanasalimiwa kwa kisukuma, kwa kihaa, kimakonde n.k. na hatuoni tatizo? Waarabu ni sehemu ya jamii yetu kama walivyo wasukuma, waha na wamakonde. Usiopopendezwa na hizo salamu usijibu.

Amandla....
Ni kweli, tumesikia huko usukumani watu wakisalimiwa kisukuma; buhaya watu wakisalimiwa kihaya nk. Tatizo huyu mama husalimia kiarabu hata akiwa kwa waha wasiofahamu kabisa hicho kiarabu.

Hivi kiongozi akisimama jukwaani akasalimu hadhira mbele yake kwa kiingereza ataeleweka kweli?!
 
..lakini hata ktk awamu hii wako viongozi wazungumzaji wazuri kama Prof.Kabudi, Tundu Lissu, ambao ni nadra kutumia salamu za kidini-dini. Naamini hao ni mifano mizuri ya kuigwa kwa weledi wao wa kuzungumza mbele ya hadhira.
Naona taratibu umeanza kumkubali.
 
Wapinzani waliokuwa wanawachelewesha hawapo ! visingizio hakuna sasa na hata cha kujadili hakipo badala yake yanajadiliwa mambo yasiyo na msingi wowote ! jiwe shikilia hapo hapo 5 tena au nasema uongo ndugu zangu?
 
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
Aseme bwana Yesu asifiwe kwani yeye ni Mkristo? Swali gani hilo.
 
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
VERY STUPID QUESTION. YAANI BADALA TUJADILI JUHUDI ZA MHESHIMIWA WEWE UNALETA MASWALI YA KIPUMBAVU.... NYUMBU KWELI MNA KAZI.MNAKOSOA TU KILA KITU SABABU HAMNA AKILI.
 
Inajenga picha kwamba sio mnafiq.

Huyo mama kwanza sio muongo muongo maana kama mnakumbuka alivyosema kipindi kile cha kampeni kwamba hata mkimpgia kura mgombea mwingine lakini wa CCM ndio atakayeshinda. Kwani aliongopa?
Madaraka ni kilevi.

Kauri mbaya sana wakati ule nilishangaa kwamba, imesemwa na yeye, na nyingine ya polepole about V8.

Viongozi wawe wanyenyekevu, msijigambe sana. Ni sisi maskini tunaonunua V8.
 
Jitahidi kujikita kwenye mada.
 
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
Acha Uwongo Mimi ni Mkristo tena Mkatoliki Mkomavu kabisa nimeshawahi Kumsikia Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisalimia hivyo Bwana Yesu Asifiwe katika Hafla kadhaa za Kiserikali.

Ni vyema kabla ya Kukurupuka hivi kama Makimba ya Alfajiri mkawa mnajiridhisha Kwanza. Na unaonekana kuwa una Chuki nae tu Binafsi. Halafu naomba unionyeshe katika Vipengele vya Katiba ya Tanzania ni wapi Kiongozi asiposalimia Hadhara kwa Lugha za Kiimani ni Kosa la Jinai?

Mada zingine JF ni za Kitoto sana tu.
 
Weka ushahidi ewe utopolo
 
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mkichoma nyumba za wapemba zikimalizika mtaanza kujiuliza mbona za wachaga hatuchomi.
Mlifanya kila aina ya figisu kuondoa upinzani kwenye gemu, sasa hakuna wakumshambulia mmeanza kutafutana wenyewe kwa wenyewe.
Tukija kwenye hoja yako, kwanza ungeangalia maana halisi ya hizo ulizoita salamu kuu za kidini.
"Tumsifu yesu kristo au Bwana yesu asifiwe" kwa muislamu sio salamu bali ni kumtukuza yesu. Na salamu anayoikubali muislamu ni ile ya yesu mwenyewe alipo watokea wanafunzi na kuwaambia "Amani ya bwana iwe nanyi" na hii ndio maana ya neno Assalaamu alaykum.
Kwa maana hiyo hakuna picha yoyote mbaya anayoijenga makamu wa rais.
 
Back
Top Bottom