Kwanini Makamu wa Rais hasemi "Bwana Asifiwe"?

Jane Lowassa

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,760
8,527
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
 
Tuna dini za imani nyingi sana ikiwepo wapagani, ukiamua kutoa salam kwa kuzingatia dini au imani flani, fanya hivyo kwa imani zote kitu ambacho hakiwezekani.

Ingekua amri yangu salam za dini au zenye kuashiria imani flani zisingekuwepo kabisa kwenye hafla za kiserikali, hasa kama tukio halina maudhui ya kiimani.

Hata hivyo hakuapa kulinda salam za kiimani.
 
Hapo cha msingi siku akihudhuria hafla fulani, na wewe hudhuria huku ukiwa na dela lako la CCM na kapelo au kilemba chenye picha ya Rais wako Magufuli!

Halafu jitahidi kujipenyeza mpaka mbele kabisa aliko! Wakati akianza tu kusalimia, kimbia 💃 kwa spidi ya swala na kwenda kumnasa kibao usoni! Hakika baada ya hapo, hatokuja arudie tena kuto kutamka hizo salamu unazo zipenda wewe.
 
Kwenye sera za Chama cha Mapinduzi kuna hicho kipengele cha kusalimia kwa dini zote? Huwa naona kama unafiki fulani tu kuna salamu nyingi tu za kiujumla.
 
Ebu tuondolee kabisa habari zako za ubaguzi wa kidini.

Hivi nyinyi waramba miguu wa lumumba mnakuwaje kila siku ni kuendekeza ubaguzi?

Mlianza kuwabagua wapinzani na sasa mmeanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe ndani ya ccm yenu.
 
Back
Top Bottom