Majukumu ya Makamu wa Rais ni yapi?

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,196
Asalaam Aleykum.

Leo nimelazimika kuuliza hili swali maana huwa hata sielewi maana ya hiki cheo kuwepo.

Niliwahi kusikia kwamba mojawapo ya majukumu ya Makamu wa Rais ni pamoja na kushughulikia masuala ya mazingira.

Sasa kama ni hivyo kweli, na huko Manyara tumepata mafuriko kutokana huenda na changamoto za kimazingira na hatujamsikia Makamu wetu wa Rais akiongelea chochote, kwa kweli hapo ndo nashindwa kabisa kuelewa.
 
NAANZA NA MASWALI

1. Je uliwahi kusikia makamu wa Rais amemtumbua mtumishi hata walio kwenye wizara zilizo chini ya ofisi zake?

2. Kwa kuwa makamu wa Rais naye ni sehemu ya urais je uliwahi kusikia wapi kuwa yeye ndie amemshauri Rais kuwa waziri hata wale walio katika wizara za ofisi yake?

3. Kwa kuwa Waziri Mkuu, waziri au Makatibu Wakuu hutoa karipia na kusimamisha wazembe na mafisadi uliwahi kuona wapi makamu wa Rais naye kafanya?

4. Je kazi ya Makamu wa Rais ni kula Bata tu na kuwa minimum tour nje ya nchi ?

5.Je tuondoe cheo Cha makamu wa Rais kwenye mabadiliko ya katiba.

Hapa Tanzania kazi ya makamu wa Rais ni kutembea na mkasi kwenye gari kwenda kutaka utepe kufungu,kuzindua,kuweka mawe ya msingi kwenye miradi badala ya kufanya majukumu ya msingi Rais .

Ziara za makamu wa Rais Tanzania hazina kishindo wanazidiwa pawa za ki-kiamri na ma-RC ,manaibu waziri na hata makatibu wakuu huko mikoani , tangu enzi wa makamu hayati DK Omary All Juma labda yeye alijaribu hata kupigwa mkwara hawa wa sasa ni kichekesho na ndio maana waziri mkuu analemewa kipindi Rais akiwa slow kama Rais Samia Saluhu alivyo huko mikoani ni wizi ,uzembe na utoro tu ndio sababu za kuwa na waziri mkuu msasidizi Ili angalau ziara za kutafutana zionekane .

Kwa kuwa makamu wa Rais wengi wametokea ZANZIBAR hii ilidhaniwa kuwa ndio sababu ya kuwa waoga ,kutojiamni na kujikalia kimya ,kipindi hiki tuko na mbara mwenzetu lakini wapi .

Hapa Tanzania kama unakosa sio jambo la kuogopa kiutwa na makamu wa Rais kama unatakavyo ogopa kuitwa na waziri mkuu,waziri,naibu waziri,katibu au naibu katibu mkuu ,nani anahofu ya kuitwa na VP
 
Asalaam Aleykum.
Leo nimelazimika kuuliza hili swali maana huwa hata sielewi maana ya hiki cheo kuwepo.
Niliwahi kusikia kwamba mojawapo ya majukumu ya Makamu wa Rais ni pamoja na kushughulikia masuala ya mazingira!
Sasa kama ni hivyo kweli, na huko Manyara tumepata mafuriko kutokana huenda na changamoto za kimazingira na hatujamsikia Makamu wetu wa Rais akiongelea chochote, kwa kweli hapo ndo nashindwa kabisa kuelewa!!
Hana kazi yoyote ni pambo tu kama alivyokuwa samia
 
Asalaam Aleykum.
Leo nimelazimika kuuliza hili swali maana huwa hata sielewi maana ya hiki cheo kuwepo.
Niliwahi kusikia kwamba mojawapo ya majukumu ya Makamu wa Rais ni pamoja na kushughulikia masuala ya mazingira!
Sasa kama ni hivyo kweli, na huko Manyara tumepata mafuriko kutokana huenda na changamoto za kimazingira na hatujamsikia Makamu wetu wa Rais akiongelea chochote, kwa kweli hapo ndo nashindwa kabisa kuelewa!!
Ni kukakaimu Rais asipokuwepo
 
Jukumu kubwa ni kujaza nafasi ya uraisi kama litatokea la kutokea. Mfano hai ni JPM na SSH. Mengine yote ni mbwembwe tu.
Hili inabidi kama Taifa tuliangalie vizuri, maana kuongozwa na mtu ambaye hamkumchagua kwa nafasi hiyo ni changamoto sana. Hata yeye mwenyewe anakuwa hana uchungu na nyinyi kwa sababu hakuwaomba kura zenu kwa nafasi hiyo bali ni kwa kudra za M/Mungu.
 
Asalaam Aleykum.
Leo nimelazimika kuuliza hili swali maana huwa hata sielewi maana ya hiki cheo kuwepo.
Niliwahi kusikia kwamba mojawapo ya majukumu ya Makamu wa Rais ni pamoja na kushughulikia masuala ya mazingira!
Sasa kama ni hivyo kweli, na huko Manyara tumepata mafuriko kutokana huenda na changamoto za kimazingira na hatujamsikia Makamu wetu wa Rais akiongelea chochote, kwa kweli hapo ndo nashindwa kabisa kuelewa!!
Kuna Vyeo nchi hii hata umuhimu wake havina ni Upigaji tu Mskamu wa Rais wa Tanzania hata kumfukuza kazi Mhudumu wa Ofisi hawezi
Pia kuna Hiki Cheo cha DC mie sielewi kabisa Umuhimu wake kwa Maendeleo ya Nchi Cheo hiki kimekuwa kinatolewa kama ZAWADI na kinatumika kisiasa lakini kinatumia Raslimali za serikali.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom