Kwanini Magufuli hataki kuongea Kiswahili?

Regnatus Cletus

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2018
Posts
1,114
Reaction score
959
Sijui shida ni nini tu? Maana Kiswahili ni lugha nzuri tu yenye hadhi na viwango stahiki vya lugha bora.

Magufuli haishi kuchomekea vimaneno vyake vya broken English ; hata kwenye mkutano wa wakuu wa jumuiya ya Afrika mashariki alinishangaza kwa kuingiza vijimaneno vyake vibovu vya kiingereza!

Lugha ya Kiswahili ikizungumzwa kwa ufasaha unaotakiwa ni lugha nzuri mno na ya heshima! Nilitegemea kwenye mkutano ule akiwakilishe Kiswahili kwa mbwembwe na madaha yote ya kisarufi lakini akaishia kukoroga tu mara achomekee vimisamiati vyake vya hovyo! Vimisamiati vyenyewe broken! Hata tenses tu hawezi!

Yule mwanamama wa kirusi alipokuja ikulu, Rais akawaponda wanaoongea kiingereza, eti 'wanajifanya'! Ebo!!? Juzi katutia aibu, badala ya kusema "air hostesses" kasema air 'hostages'!

Ningemshauri Rais aongee Kiswahili, tena Kiswahili sanifu!!

Kiingereza chake hafifu sana, hawezi kabisa sarufi! Tutaepuka "intaprentinyuwa" , "fenti fodi" na matakataka mengine ya dizaini hiyo!
 
Acha upumbavu, raisi kukosea neno moja katika 1000 , ndio uanzishe Uzi, yaani chadema mmekosa hoja, kila kitu mnadandia , badala mjadili kuhusu mustakabali wa kupoteza jimbo la Arumeru kijinga, unaanzisha Uzi kumkebehi raisi,

Pumbaff

'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
 
His English is poor, and his Swahili is not even better. Vumilia kusikia ukweli.
 
Chadema siku hizi hawaikosoi serikali pamoja na makosa kibao inayofanya, wako busy na kukosoa point za kijinga,

Hapo ilibidi ukosoe jambo la maana

Kwahiyo kazi ya kukosoa umewaachia cdm tu. Inapidi ww ukosoe ili cdm wajifunze toka kwako. Humu jf ni ofisi ya cdm mpaka uone maoni ya humu ndani ni ya chama cha cdm?
 
Sijui shida ni nini tu? Maana Kiswahili ni lugha nzuri tu yenye hadhi na viwango stahiki vya lugha bora.

Magufuli haishi kuchomekea vimaneno vyake vya broken English ; hata kwenye mkutano wa wakuu wa jumuiya ya Afrika mashariki alinishangaza kwa kuingiza vijimaneno vyake vibovu vya kiingereza!

Lugha ya Kiswahili ikizungumzwa kwa ufasaha unaotakiwa ni lugha nzuri mno na ya heshima! Nilitegemea kwenye mkutano ule akiwakilishe Kiswahili kwa mbwembwe na madaha yote ya kisarufi lakini akaishia kukorogo tu mara achomekee vimisamiati vyake vya hovyo! Vimisamiati vyenyewe broken! Hata tenses tu hawezi!

Yule mwanamama wa kirusi alipokuja ikulu, Rais akawaponda wanaoongea kiingereza, eti 'wanajifanya'! Ebo!!? Juzi katutia aibu, badala ya kusema "air hostesses" kasema air 'hostages'!

Ningemshauri Rais aongee Kiswahili, tena Kiswahili sanifu!!

Kiingereza chake hafifu sana, hawezi kabisa sarufi! Tutaepuka "intaprentinyuwa" , "fenti fodi" na matakataka mengine ya dizaini hiyo!
Nafikiri anafanya kusudi kujidai hajui neno la Kiingereza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom