Kwanini Magufuli hataki kuongea Kiswahili?

Sijui shida ni nini tu? Maana Kiswahili ni lugha nzuri tu yenye hadhi na viwango stahiki vya lugha bora.

Magufuli haishi kuchomekea vimaneno vyake vya broken English ; hata kwenye mkutano wa wakuu wa jumuiya ya Afrika mashariki alinishangaza kwa kuingiza vijimaneno vyake vibovu vya kiingereza!

Lugha ya Kiswahili ikizungumzwa kwa ufasaha unaotakiwa ni lugha nzuri mno na ya heshima! Nilitegemea kwenye mkutano ule akiwakilishe Kiswahili kwa mbwembwe na madaha yote ya kisarufi lakini akaishia kukoroga tu mara achomekee vimisamiati vyake vya hovyo! Vimisamiati vyenyewe broken! Hata tenses tu hawezi!

Yule mwanamama wa kirusi alipokuja ikulu, Rais akawaponda wanaoongea kiingereza, eti 'wanajifanya'! Ebo!!? Juzi katutia aibu, badala ya kusema "air hostesses" kasema air 'hostages'!

Ningemshauri Rais aongee Kiswahili, tena Kiswahili sanifu!!

Kiingereza chake hafifu sana, hawezi kabisa sarufi! Tutaepuka "intaprentinyuwa" , "fenti fodi" na matakataka mengine ya dizaini hiyo!
Yule jamaa ni maji kupwa maji kujaa
 
Katika ma Rais waliokuwa wanajua Lugha ya Kiingereza kwa Ufasaha zaid Ni Mzee Julius Nyerere Na Mzee Mkapa Na Mara zote huwakuti wakichanganya lugha

Wakizungumza Kiswahili kinakuwa Kiswahili sanifu Na wakiongea Kiingereza utadha hawajui Kiswahili

Mseto wa Lugha Mara nyingi ni kuficha udhaifu wa kilugha
Ila Mkapa alikuwa na eloquent matata sana. Kiswahili fasaha na kimenyooka na kujiamini. Akiongea kingereza utafurahi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui shida ni nini tu? Maana Kiswahili ni lugha nzuri tu yenye hadhi na viwango stahiki vya lugha bora.

Magufuli haishi kuchomekea vimaneno vyake vya broken English ; hata kwenye mkutano wa wakuu wa jumuiya ya Afrika mashariki alinishangaza kwa kuingiza vijimaneno vyake vibovu vya kiingereza!

Lugha ya Kiswahili ikizungumzwa kwa ufasaha unaotakiwa ni lugha nzuri mno na ya heshima! Nilitegemea kwenye mkutano ule akiwakilishe Kiswahili kwa mbwembwe na madaha yote ya kisarufi lakini akaishia kukoroga tu mara achomekee vimisamiati vyake vya hovyo! Vimisamiati vyenyewe broken! Hata tenses tu hawezi!

Yule mwanamama wa kirusi alipokuja ikulu, Rais akawaponda wanaoongea kiingereza, eti 'wanajifanya'! Ebo!!? Juzi katutia aibu, badala ya kusema "air hostesses" kasema air 'hostages'!

Ningemshauri Rais aongee Kiswahili, tena Kiswahili sanifu!!

Kiingereza chake hafifu sana, hawezi kabisa sarufi! Tutaepuka "intaprentinyuwa" , "fenti fodi" na matakataka mengine ya dizaini hiyo!

Kiswahili chenyewe kwake ni taabu, bora aongee Kisukuma kwa sababu hapo yuko fasaha sana.🤔
 
Makosa ya matamshi hasa kwa lugha ambayo si ya kwanza kwako ni jambo la kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom