Silicon valley sio wabunifu kama mnavyofikiri, ila wana access kubwa sana ya hela.
Fikiria kampuni kama Uber ambayo haijawahi kupata faida inaweza kupata wawekezaji waliowapa $8 billion!
WhatsApp kabla haijanunuliwa walipewa $60 million na wawekezaji kujikuza, wabongo tukianzisha hizo kampuni hakuna hata wa kutupa senti, mwisho wa mwezi hatuwezi hata kulipia servers.
Hongera zake ila hiyo ni $400,000 before taxes, developer aliyeajiriwa Sillicon Valley anaitenegeneza hiyo ndani ya miaka kama miwili/mitatu bila kujisumbua kuendesha biashara. Of coz sisemi kuwa hakuna atakayetoka bongo ila sio kwa rate na viwango wa SV na tusijifananishe kabisa.Inawezekana bongo hapa. Your network determines your networth. Edwin Bruno Smart Code deal ya M-paper alipigwa kama Million 900 hivi na vodacom. Nakumbuka alivuta Range mpyaaa 0km hadi mzee mengi aliongea. Ahah big up kwake edwin. Ishu ni kujipanga mzee proffessionally and unatoboa. Sio una andaa mzigo hafu ujanja ujanja tu bila kuandaa proper presentation kutoboa inakua ngumu sana. Pia muhimu kushirikisha watu sio coder wewe, graphics wewe, marketing wewe yani kila kitu unajikuta juajua hapa you r likely to fail.
Hongera zake ila hiyo ni $400,000 before taxes, developer aliyeajiriwa Sillicon Valley anaitenegeneza hiyo ndani ya miaka kama miwili/mitatu bila kujisumbua kuendesha biashara. Of coz sisemi kuwa hakuna atakayetoka bongo ila sio kwa rate na viwango wa SV na tusijifananishe kabisa.
mkuu ulikuwa na level gan ya elimu kufanya kazi kama consultantMa-IT watanzania wako wengi. Check github ujionee mwenyewe kuwa wabongo wako wengi. Ila kwa kifupi shida ni moja; kama wewe ni software developer mzuri, hauna sababu ya kubaki bongo. Nchi kibao duniani zitakupigania na kukupa visa karibu bure.
Nikupe mfano. Nilirudi bongo baada ya kusoma nje kwa muda mrefu. Nilitaka kuanzisha kampuni ya software na kujitegemea. Nilianzisha kampuni na kuanza kuzunguka mtaani kuuza solution yangu. Tatizo kubwa nililiona ni kuwa wabongo hatuna uwezo wa kuona solution mpaka inapofika too late (hii ni shida kubwa duniani kote ila bongo nimeliona zaidi). Kwa maana nyingine, mpaka tuone wengine wanatumia kitu ndio tunaanza kudandia. Idea zetu za software ni za kizamani sana. Na software development ni eneo ambalo linakuwa na kubadilika haraka. Mfano ni baadhi ya kampuni na sekta kibao serikalini zinang'ang'ania kuwa na server kwenye ofisi zao. Mambo ya kuwa na cloud computing ni kitu kigeni. Wengi wanabaki kuhofia security ya cloud computing. Ukijaribu kuwaelewesha kuwa security ni balaa zaidi unapokuwa na server zako mwenyewe, wanabaki kufikiri kuwa mradi unaiona server kila siku basi hiyo ndio security (kana kwamba server ikiibiwa ndio security imefeli). Baada ya kusota miaka kadhaa kujaribu biashara bongo bila mafanikio nikaamua kupiga kazi na kampuni za nje ya nchi kama consultant nikiwa bado bongo (remote working). Mshahara wangu wa kwanza ulikuwa $3000 kwa mwezi. Kipindi nasota na wabongo, nikipata $800 kwa mwezi nilikuwa najiona mjanja. Huo mshahara wa kampuni za nje hata sikupigania na tayari nilikuwa napiga hela mara nne ya nilichozoea. Nilikuwa single, sina demu wala mtoto. Naomba niwaulizeni, utabaki kujaribu kupiga dili na wabongo baada ya hapo? Baada ya kama mwaka hivi nikaanza kudai hela ambayo ni halali kwa experience yangu. Bila mabishano mshahara ulipanda hadi $4800 kwa mwezi ($30/hr).
Unauliza ni kwanini hakuna matajiri wa IT bongo? Jibu hilo hapo juu 😀 Mpaka siku bongo tutapoanza kuona umuhimu wa IT, vijana wote wanaoweza hizi kazi tutabaki kupiga biashara na nchi ambazo zinafadhili kazi zetu.
Mmiliki wa jf sio IT guy! Ni civil engineer by professional!kwani mmiliki wa jf sio tajiri? wapo ma IT matajiri pia Tanzania, kama vile ambavyo kuna Ma IT masikini huko Duniani ambao wanaishia tu kuwa wauzaji/wazungumzaji kwenye show room.
Watu wa IT wenyewe tulishakimbia nchi.IT ni fani ambayo ina nafasi kubwa sana za kutanua kimataifa.Kuna fursa kubwa sana yani pesa mingi ya duniani ipo katika sekta ya teknolojia. Fursa inazidi kukua kila siku but why jamaa zetu bongo hapa hawana mpunga yani kuunga unga kwingi.
Personally am not an IT but i love this profession. Nchi kama bongo ipo nyuma sana lakini yenye matamanio makubwa yakufahamu teknolojia then whats pulling us back.?!
Mi ishu nimeona kwenye management ya hawa talented stars pia na wengi wao kuto fahamu marketing and advertisement.
Costech wanafeli na hubs zingine the push is not that hard. Hebu tuimarishe huu mfumo vijana wapige hela. Mifumo user friendly ambayo kila mwananchi hata mwenye elimu ndogo ya teknolojia anaweza master. Kwa research nliyofanya tech is not that expensive nkimaanisha kuna softwares, systems and tools zinawwza patikana in a cheaper way ughaibuni kwa njia tofauti(kijanja).
Na madini yote haya tufungue cyber mall moja kubwa sana, wajae wabongo humo, wachina na warusi wa kutosha. [HASHTAG]#YouthWeCan[/HASHTAG]