ASIWAJU
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 1,939
- 1,625
Maswali kwa Wizara ya Elimu Tanzania na kwa wadau wote humu Jamiiforums:
Kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya kidato cha nne 2022.
1. Kwanini wizara haijaamuru matumizi ya lugha ya kiswahili katika kufundisha na kuondoa matumizi ya lugha ya kiingereza katika ngazi zote za kielimu hapa nchini?
2. Je, Serikali inafahamu madhara ya kufundisha kupitia lugha isiyo na matumizi makubwa na kuacha lugha yenye utumizi mkubwa katika taifa?
3. Kwanini kuna matumizi ya lugha ya Kiingereza katika kufundishia huku mazingira ya kazi yakihitaji zaidi matumizi ya lugha ya kiswahili?
4. Kwanini Kiingereza kisibaki kama yalivyo masomo mengine kama Kichina, Kifaransa, Bailojia, Fizikia, Kemia n.k