Watanzania wenzetu sijui nani katuloga. Mbona tunasahau mapema sana kiasi hiki. Hivi leo tumesahau kuwa chanzo kikuu cha ufisadi hapa nchini ni mfumo uliopo serikalini?
Swali dogo naomba kuuliza:
Ni waziri mkuu gani mwenye rekodi ya kipekee ya kuwa mkali zaidi tena kwa vitendo kwa watendaji wa serikali? Sio Lowassa huyu huyu aliekaa madarakani kama mtendaji mkuu wa serikali kwa muda mchache zaidi, na ndie huyu aliweka rekodi ya kuwa mkali zaidi kwa watendaji wa serikali wanaopenda kufanya kazi kwa mazoea?
Ni waziri mkuu yupi aliekuwa na uwezo wa kumwajibisha mkuu wa wilaya on the spot? Halafu leo mnasema Lowassa hajawahi kupambana na ufisadi!
MEMBE , PINDA na LOWASSA wana tofauti gani katika hili???
hapa ni MAKONGORO tu
ninaungana nawe kabisa kwenye hoja yako ya utangulizi niliyo highlight in RED. Wewe mwenyewe una tatizo hilo hilo la kusahau mapema......maana jibu la swali lako juu ya Waziri Mkuu gani mwenye rekodi ya kipekee ya kuwa mkali zaidi, tena kwa vitendo kwa watendaji wa Serikali- Jibu sahii ni EDWARD SOKOINE
jambo la pili, muhimu kuclarify.....UFISADI na UZEMBE japo vyote vinaathiri maendeleo ya nchi, ni vitu viwili tofauti. Mifano uliyotoa kwenye uzi wako ni rekodi ya Mhe Lowassa kushughulikia UZEMBE, na sio kushughulikia UFISADI.
Ni kweli kabisa kwamba mifumo Serikalini inaweka mazingira ya kulea rushwa.....kwa mfano.....Maslahi duni Serikalini, hupelekea baadhi ya wauguzi au mapolisi kuchukua rushwa....na hizi ndio rushwa zinazowakera na kuwaumisa wananchi kila siku mijini na vijijini- ningetegemea kuona mifano ya Mhe Lowassa alivyotetea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma.
mfano mwingine wa mfumo wa Serikali unaochochea rushwa upo kwenye sheria zilizopo....mfano Sheria ya Manunuzi ya Umma......Mhe Lowassa na Wagombea wengine wote wanaojipambanua na rushwa, wamechukua hatua gani (wakiwa kama Wabunge) kupendekeza mabadilisho ya sheria hiyo na nyinginezo kuziba mianya ya rushwa?
Tatizo lingine lililopo ni rushwa kubwa (Grand Corruption)- ununuzi wa Rada, Deep Green, EPA, Land grabbing ni mifano michache- ni vema rekodi za wanaojipambanua na rushwa zikapimwa kwa hatua/misimamo walioyochukua kushughulikia na madhira haya.
Nimalizie kwa kueleza maoni yangu na swali kwa Mhe Lowassa. Sina shaka yoyote na uwezo wa Mhe Lowassa kuongoza nchi; Sina shaka yoyote juu ya dhamira ya Mhe Lowassa kuona nchi hii inasonga mbele kwa kasi zaidi.
Swali langu ni je atawezaje kuwakwepa baadhi ya watu wanaomzunguka ambao hawana uwezo na dhamira njema kama yake- baadhi yao rekodi zao za utendaji na uadilifu ni za kutiliwa shaka?
Kwenye kundi lake kuna walioshiriki kikamilifu kwenye GRAND CORRUPTION, kuna watu wenye rekodi za kukwepa kodi na kuinyima serikali mapato zinafahamika wazi. Je watu hawa wana share njozi yake ya matumaini kwa watanzania wote au wataendelea na njozi yao ya matumaini kwao peke yao?
Anawatosaje watu hawa? Haya maswali watanzania wengi wangependa kujua!
Nanze mada yangu kwa kuuliza maswali la kipuuzi hivi.
1. Ni kweli lowasa amenuia kuingia ikulu?......
2.Ni kweli watanzania wanapenda lowasa awe rais wao?....
3.Je,lowasa atambua kuwa watanzania wana mtaka awe rais?...
4Je,wapambe wa lowasa,wafadhili wake pamoja marafiki wake wanatambu hilo?.
5.Je,lowasa amejiandaa vizuri kukabidhiwa nchi?....
6.Je,lowasa anatambua kuwa yeye ndiye mtia nia mwenye sifa kuzidi watia nia wengine?....
7.Je,lowasa anatambua kuwa endapo watanzania wataamua kumchagua mgombea mwingine,lowasa atafanya nini?...
Maswali yote hayo,jibu ni moja tu.Jibu hilo ni kuwa,' HANA SIFA.
Edwaed ngoyai lowasa hajanuia kuingia ikulu baada ya uchaguzi huu,kwa sababu,Kwa sababu kama angelikuwa na nia thabiti ya kuingia ikulu basi,lowsa angeanza kujisafisha machoni pa watanzania hasa kuhusiana na tuhuma mbalimbali zinazo mwandama...rushwa,ufisadi na mashaka ya mali alizonazo.Kuhusu watanzania kumtaka awe rais wao,lowasa na wapambe wake bado hajatambua kuwa,watanzania hamtaki rais ambaye anakabiliwa na tuhuma za ufisadi,rushwa na staha hafifu ,kitu ambacho lowasa na wafuasi wake halitambui hata kidogo.
kuhusu utayari wa kukabidhiwa nchi,lowasa hajajiandaa kukabithiwa ikulu,Kwani angelikuwa tayari,lowasa asingepingana na sera/ilani ya ccm kuhusiana na elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.Hii inaonyesha kuwa,lowasa haiheshimu ccm na dira ya maendeleo ya ccm,Na kwamba,endapo ccm itamsimamisha lowasa na kushinda katika uchaguzi hou,Basa,lowasa ataacha kufuata na kutekeleza ilani na maagizo ya ccm,badala yake ataendesha nchi kwa ilani yake anayoijua yeye.
Ni kweli kabisa kuwa lowasa ndiye mtia nia ambaye ana sifa kuliko watia nia wengine....richmond ni sifa yake...alphatel. ni sifa yake...kuratibu kumchafua dr salim 2005 ni sifa yake....Uhusiano!/ na batilda burian ni sifa yake...bety mkwasa...sifa yake...kagoda ni shombo yake....makundi ya urais yanayo tukana pale wanapoombwa majibu kuhusiana na mgombe wao ni sifa yake...kutoa hongo ili adhaminiwe na chama ni sifa yake..kujisahau na kuongelea habari fulani kwa majibu tofauti ni sifa yake.Watanzania wenzangu,Naomba tuinuke na kwa sauti moja kuanzia sasa popote ulipo..TUMKATAE LOWASA KUWA RAIS WETU,................
Ikulu sio wodi ya Wagonjwa
Kweli ukuwadi ni jambo baya sana! Yaani umelishwa sumu mpaka umejisahau!
Watanzania sio makuwadi wala wajinga kama wewe! wala hatuna akili za kushikiwa kama wewe!
Kabla ya kuanza kubwabwaja na kutema pumba na hoja zako dhaifu! kwanza ungejiuliza maswali yafuatayo;
(1).Kuhusu rushwa na ufisadi ni mahakama gani iliwahi kumkuta EL na hatia?! wewe unao ushaidi wa tuhuma hizo au unaleta ushabiki maandazi?!
(2).Kutokufuata ilani ya ccm; Hivi Membe aliposema atabadili sheria na kumfunga mtoa rushwa tu badala ya mtoaji na mpokeaji alifuata ilani ya chama?! Usiwe kilaza mpaka unajisahau! watanzania wa-leo sio wale wa mwaka 1961..!
Majungu, chuki na wivu ni sumu ya maelendeleo ya nchi, tutoe hoja facts na sio tetesi za mitaani na kwenye kahawa! kuhusu afya EL yuko fit kama anavyoonekana! angekuwa mgonjwa angeweza kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini?! Na wakusema afya ya mtu ni yeye mwenyewe au daktar wake! wewe daktar wake?!
Acha Kutumiwa kama toilet paper tumia ufaham wako mzuri aliokupa muumba!
Kama kigezo ni kujiuzuru uwaziri kwa tuhuma tu! hata Mwinyi aliwahi kujiuzuru uwaziri na baadae akaja kuwa Raisi!
Na kama hoja ni kashfa' hata membe hafai kuwa raisi maana ana kashfa ya fedha za ghaddaf..!