Aliyejiuzuru Uwaziri Mkuu kwa kashfa za Richmond alizotuhumiwa bungeni Edward Lowasa, ametengeneza mtandao mkubwa kupenya ateuliwa kuwa mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM.
Kimsingi Lowasa ana jina kubwa lakini hana sifa au sera anazoeleza wazi atakachofanya akiwa rais kama ilivyo kwa wagombea wengi wanaowania nafasi hiyo kupitia CCM kutotuhakikishia Watanzania watabadilishaje kile tunacholalamikia serikali inayoongozwa na CCM kufumbia macho urasimu na ufisadi.
Sera tunazozisikia ni kutoka upinzani, labda kwa vile wako jukwaani wakiwaangalia wachezaji uwanjani wanaona makosa yanayofanyika kuliko Lowasa aliyoko uwanjani akiwa mchezaji hawezi kuona makosa wanayoyafanya.
Lowasa hana sera ni kujipitishapitisha na kuhudhuria mikusanyika Tanzania ya leo si ile ya kuchagua umaarufu wa mtu au umaarufu wa kujulikana, tunahitaji sera. Tanzania ya leo si ya Kitudumu Chama Cha Mapinduzi, Zidumu Fikra Sahihi Za mwenyekiti wa CCM, kila mgombea uraisi anayepitishwa na CCM kujihakikishia kuwa Rais wa Tanzania.
Tanzania ya leo hatuhitaji kujionyesha kwa kupitapita kila sehemu na kuhudhuria kila tamasha na matukio ili wapiga kura wakuone, tunahitaji uuzaji wa sera utaibadilishaje Tanzania ya leo tuwe na Tanzania tuioteayo.
Tuanataka uonyesha mapungufu kiuongozi ndani ya CCM utayashughulikiaje.Utuonyeshe kwa nini hukuweza kushughulikia matatizo hayo ulipokuwa waziri mkuu, mbunge kamati ya bunge na uongozi katika ngazi mbalimbali chamani.
Kama hayo hukuweza kuyashughulikiwa upokuwa Waziri Mkuu, Waziri, Mbunge, mwenyekiti kamati ya bunge, ngazi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na kuhitimishwa kwa kashfa ya Richmond hadi ukajiuzuru, utawezaji kurejesha imani kwa wananchi na kuondoa uchafu unaoendelea ndani ya serikali inayoongozwa na CCM hasa ubadhilifu wa mali ya umma?