Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

nikiwa field yangu august 2015 mzee mmoja alinisimulia hii hadithi ya LEVINA (RIP)na habari za mzee PUNCH..zinasisimua...mzee yule alisimulia jinsi Punch walivyosababisha wanafunzi wa UDSM wakafukuzwa chuo mwaka mzima kisa punch kumdhalilisha Rais Mwinyi..

Mimi nlipokuwa fild mwaka 2013 nakumbuka mzee mmoja officin alituuliza vijana tuliokuwa pale wangapi wanatokea udsm? Tulipojitaja..

Akanza kushusha stori ile, nayeye alikuwa mwanafunzi kipindi hicho.

ingawa sikumuelewa sana, ila alisimulia kama tukio fulan la historia ya kukumbukwa.

Nimefarijika saana kuiona hii stori na kuielewa vema.
 
Dah hakika stori ya Levina imenisikitisha hivi hao waliotajwa ndio wahusika wanajiskiaje ?? Natumaini nao sasa hivi watakua na watoto wa kike na kama ilivyo kawaida ya Karma watavuna tu walichopanda
kweli mkuu Mungu atawalipa, nimeshangaa naanza kufanisha hii story na ndugu wa mama yangu katali sana huyu jamaa, pia alisoma miaka hiyo ya mwinyi, ukute nae ndo punch. Huyu jamaa kichwani smart sana kazi nzuri maisha mazuri, ana watoto wawili pasua kichwa sana, wakiume mdokozi balaa hajawahi maliza kidato cha nne, wa kike anapigwa miti na vijana ile mbaya, sasa ana mimba.

r i p dada Levina
 
Huo ni ushamba sana waliokuwa wanafanya watu wa PUNCH, actually ni ujinga na udhaifu. Kumbaka mwanamke kwa nguvu, mtu mzima msomi wa chuo, unaejiita umeelimika! Natumaini wahusika karma inawaandama huko waliko.
 
kweli mkuu Mungu atawalipa, nimeshangaa naanza kufanisha hii story na ndugu wa mama yangu katali sana huyu jamaa, pia alisoma miaka hiyo ya mwinyi, ukute nae ndo punch. Huyu jamaa kichwani smart sana kazi nzuri maisha mazuri, ana watoto wawili pasua kichwa sana, wakiume mdokozi balaa hajawahi maliza kidato cha nne, wa kike anapigwa miti na vijana ile mbaya, sasa ana mimba.

r i p dada Levina

Dah aisee ndio hivyo Mkuu ni mavuno ya baba yao huenda ,Mwisho wa amri Mungu anasema hivi nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne wanichukizao nami nawerehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu
Baba yao inabidi atubu tu kwa alichokifanya
 
Elimu ya zamani ilikuwa tamu sana. Ubabe ubabe na akili zinachaji.

RIP Levi. Sad memories.
 
na kuna shule zilikuwa zinasikika kuwa mwanafunzi wa kike akifika anakuwa ameshachaguliwa na mwanamme, hakuna kusema hapana maana mateso yake hayavumiliki, mojawapo ilikuwa mkwawa high school

nimesoma mkwawa high school aka complex n casino.....hayo unayosema sio kweli.
 
Kwa kawaida retariation dhidi ya shujaa yeyote yeyote duniani huwa na misukosuko mikubwa mawili, moja ni DiScrimnation, na nyingine ni victimization. unatakiwa kuwa na moyo wa kishujaa sana ili kuweza kubabiliana na hayo mambo makuu mawili. ni lazima uwe na ngozi ngumu na moyo mgumu wenye kuhimili mathara hayo makubwa mawili. Ni lazima moyo wako uwe na shock absorber amabayo nadani yake iwe imebeba kusamehe na kudharau unayofanyiwa.

Levina alikuwa mtoto, ambaye pia inwezekana alipitia maisha ambayo hayakuwahi kuwa na misukosoko mikubwa kama hiyo aliyokutana nayo. Najua watu wengi wakati huo walikuwa wanawaogopa sana akina mzee Punch kwa kugopwa nao kuning'nizwa, lakini ni lazima kuna watu walishindwa kutimiza majukumu yao mpaka hayo yakatokeo kwenye jamii na kwa Levina. Nimezaliwa kutetea wanyonge kwa nguvu zote, wate tunapaswa kuwa na moyo huo.

Kama japo mtu mmoja tu angejitokeza na kukabiliana na hilo, Leo tungekuwa tunachati na mwanauzi mwenzetu Levina. Lakini kwa sababu tulishindwa kuzuia hilo lisitokee kwake, tujitahidi hilo lisitokee tena na mtu yeyeote wa karibu yako. RIP Levina.
 
Nliona kwenye Facebook page ya Bernard Mukasa(wakatoliki wanamfahamu sana huyu Bwana kupitia Tungo sake za nyimbo) kumbe ni Dada yake
 
Very touching and sad story RIP levina.Kumbe udsm kuna background ya kutisha hivi i was there for four years ila sijawahi isikia story hii,Engineering bado wana elements za kibabe kumbe ni toka vizazi
 
!.

Wanafunzi wanaosoma boys only, wanakabiliwa na tatizo la kisaikolojia liitwalo "male chauvinism", wanapontaka msichana, hujiona its their right kumpata, na akikataa pia its right kumbaka!, na wengi hubakwa hawasemi, hawalalamiki na baadhi ya mahusiano huanza kwa kumbaka ndipo kisha hupenda!. !".

Naona unatetea ubakaji. I'm very sure hao vijana wanaobaka wanajua vizuri kuwa ni kosa ila wanajipa moyo hawatokamatwa. Wala si kuwa wanaona ni halali yao kubaka. Hapo Kuna kijana kakusoma sasa anaanza kuEntertain mawazo ya kubaka akijipa moyo kuwa ana tatizo na linaeleweka.

Tunashukuru hatuishi enzi ambazo sexual harassment kwa wanawake ni kawaida

NB:male chauvinism ni sawa na sexism. Si hadi mwanaume asome boys school ndo awe chauvinist. Inawezekana toka home kulelewa kuwa wanawake ni inferior na ni sawa kuwaMistreat
 
Mkuu umenikumbusha battle ya Tambaza Vs Azania. Kule Moshi kulikuwa na wababe wa Kibohehe / (Kolila?) na Kilimanjaro Boys. Kuna kipindi pia Lyamungo Vs Umbwe, Moshi Tech Vs Old Moshi. Ilikuwa full burudani.
Tabora School vs Mirambo Sec
 
Hahaha!! hayo majina ukiyasikia tu unajua kabisa si salama

Kuna siku mwaka 1993 au 1994 wanafunzi wa WU-TAMBA walitembeza mkong'oto karibia shule zote za msingi na sekondari.

Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni hekaheka mjini hapa, wanafunzi na waalimu walipigwa bila kusahau mali za shule nyingi ziliharibiwa.
milikua likizo na b mkubwa wangu na mbilinge hili lilitukuta town wakatushusha kwenye dala dala...asnate Mungu hatukupigwa ila since the nikasema mwakani lazima nije kusoma Tamba!
 
Kumbe haya mambo yanaanzia mbali sana , wengine huwa wanaiga kwa mtindo tofauti tofauti.
Hiki kisa cha PUNCH -UDSM kimenikumbusha ule mtindo uliokuwepo mika flani ya nyuma kidogo
wakati tupo chuo kikuu cha MZUMBE , ulifahamika kwa jina la "KATA KIU" , yaani taa zinazimwa na
kisha mtu au watu wanakuwa wamjifunika usoni au wanavaa mavazi ambayo huwezi kumtambua
kisha wanaanza kumkatia kiu muhusika, wanawake walikuwa wahanga sana wa 'KATA KIU".
 
Nataman ningekutana nao hao watajwa wa hao punch ...huku nimebeba 45 caliber yangu ningewafyatulia wote ....hii tukio hua linansikitishaga sana
 
Quite thrilling, yet a saddening story.

Kimsingi haya mambo bado yapo sana, ni kwa namna tofauti tu. Siku hizi kuna cyber bullying, thanx to Jamii Forums and other socializing media platforms. Humo watu wananyanyasa na kunyanyaswa directly ama indirectly, intentionally and unintentionally.

Kuna mwanamama mmoja hapo 2013 au '14 sikumbuki vizuri kifo chake kilikuwaje, ila ilikuwa ni foul play mtindo kama huu. It started off as a subaru on twitter, developed into a tweef, and she ended up in the dirt. Kwa wapenzi wa Crime Investigation channel, ukipitia timeline yake unaona main suspects + motives. Sijui hata hii issue iliishia wapi. Alizikwa Dodoma nadhani.

Yapo matukio mengi ya unyanyasaji yanaendelea na tunayafumbia macho. Visa vingi naamini vinapita untold and unrecorded.

Truth be told, japo ukatili dhidi ya wanawake unaongozwa na wanaume, ila katika kila visa 10, zaidi ya nusu kuna wanawake wenzao nyuma wanahusika kwa namna moja ama nyingine.

It's a freakin' jungle out there.
 
Back
Top Bottom