Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Mama yangu! Nashukuru bado nilikuwa ni mdogo kipindi hicho labda na miye yangenikuta

Pole sana ila comment za JF siku hizi ni zaidi ya Punch we angalia watu wanavyotukanwa bila hatia, nyie kizazi kipya ni makauzu zaidi hata yangekukuta unakomaa zaidi check FB na whatzapp sahau uwazi yaani ni hatare.
 
Asante sana kwa aliyeleta mada hii. Hii kesi ilinigusa sana pamoja na wana TAMWA wenzangu. Rest in peace Levina Mukasa.
 
ROBO KARNE SASA-7-2-2015
Historia yako na ya kifo chako haitafutika vichwani mwetu kamwe.
Leo ni miaka 25 kamili tangu wanadamu wabaya walipokulazimisha kuicha dunia kwa njia chungu na inayoumiza, ukimaliza safari yako na hisia za upweke na kutengwa kukubwa.
Tunakuombea huruma ya Mungu ikuelekee wewe na hao waliokufanyia ukatiri. Tunawaombea na wote wanaoumizwa na vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia na wa namna nyingine zote, Mungu awajaze ujasiri wa kuvumilia na faraja ya kutumaini.
Upumzike kwa amani dada LEVINA KAGEMURO MUKASA

Copied Somewhere.

R.I.P Levina
 
Inasikitisha sana. Pumzika kwa amani Levina.
 
apumzike kwa amani

"Sisi wana wa dunia, tukumbuke maneno aliyosema Bikira Maria. Alipowatokea Francisca na Yasinta..... Alisema tusali, tusali Rozari........"

Haya ni baadhi ya maneno ya wimbo ambao dada huyu alipenda kuimba wakati wa sala za jioni kwa wakatoliki tulipokuwa Chuo Cha Ualimu Korogwe. Sad, so sad that she is no more!

Nilijiunga na Chuo cha Ualimu Korogwe mwaka 1988. Yeye alikuwa mwaka wa tatu akisoma Diploma wakati huo na kama sikosei alikuwa akisoma KL. Alikuwa Choir Mistress wa kwaya ya wakatoliki pale chuoni. Alikuwa na sauti nzuri sana, kwa kweli alijaliwa kuimba. Kila nisikiapo wimbo huo hapo juu, namkumbuka Levina. Alikuwa mpole sana na mnyenyekevu. Alimaliza Korogwe akejiunga UDSM. Na huko ndiko alipopatwa na masahibu hayo.

Nikiwa bado Korogwe na wenzangu ambao tulimjua dada huyu, tulilia sana. Tulipatwa na uchungu. Na hata sasa mada hii imenikumbusha mabali sana. Kwa jinsi, nilivyo mjua, kwa akili zangu za kibinadamu nitabisha hadi mwisho wa maisha yangu ya kwamba "alikula vya watu ndiyo akafanyiwa hivyo". Hakuwa mtu wa aina hiyo. Bila shaka wana KOCET ambao ni wana JF waliokuwepo wakati huo, watakubaliana na mimi.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.
 
Inasikitisha kwakweli na wote walio fanya tukio hiko Damu ya mtu haipotei itawafuata popote mlipo.

M/Mungu akulaze sehemu stahiki.
 
Hao Saloti na Victor sijui wanajisikiaje sasa!!?? Hivi familia haiwezi kufungua kesi ya madai Chuo Kikuu au against these people??

Nimewaza kitu kama hicho familia ya Levina inaweza kuwafungilia mashitaka watu hawa dhidi ya unyanyasaji na mauaji inasikitisha sana Sababu wanafahamika
Ili tumuenzi kwel tumpe support hii
 
mungu amrehemu Levina ....amfpunguzie adhabu za umauti kadri ya utukufu wake....nawaombea na wale waliosababisha kifo chake wabadilike na kuwa wajumbe wazuri kwenye utetezi wa unyanyasaji wa kijinsia....sisi sote ni binadamu tukubali tusikubali hivyo kasoro zetu na tofauti zetu ni utukufu wa mungu tu ili ajulikane kwa wote.


lala mahari pema peponi Levina
 
ROBO KARNE SASA-7-2-2015
Historia yako na ya kifo chako haitafutika vichwani mwetu kamwe.
Leo ni miaka 25 kamili tangu wanadamu wabaya walipokulazimisha kuicha dunia kwa njia chungu na inayoumiza, ukimaliza safari yako na hisia za upweke na kutengwa kukubwa.
Tunakuombea huruma ya Mungu ikuelekee wewe na hao waliokufanyia ukatiri. Tunawaombea na wote wanaoumizwa na vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia na wa namna nyingine zote, Mungu awajaze ujasiri wa kuvumilia na faraja ya kutumaini.
Upumzike kwa amani dada LEVINA KAGEMURO MUKASA

Copied Somewhere.

R.I.P Levina

Shukrani kwa kuikumbuka siku.
 
Uchunguzi ufanyike wakamatwe hao watu naamini wapo baadhi kama siyo wote wafunguliwe mashtaka ya kusababisha kifo cha huyu dada. Rest in peace Levina
 
Back
Top Bottom