Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Nilichojifunza katika kitabu cha Enoch ni juu ya origin ya mtu mweupe (kina eleza Mungu aliumba mtu mweusi ila mtu mweupe alitokana na malaika wenye tamaa i.e fallen angels waliokuwa wakiwaingilia kimwili binadamu)

Aliumba mtu mweusi sasa kwanini manabii aliokua akiwatuma walikua ni weupe au baada ya kutokea akawa hana jinsi ikabidi awahalalishe tu?
Wapi imeandikwa kuwa wati weupe wametoka kwa malaika.... Au kitabu cha Henoko kimemuongelea Nuhu kama Nuhu kuhusu issue ya weupe!!! Kma ni hivyo kwanini usiamini Nuhu alikuwa albino ila sio mzungu au mweusi??

Yaani hoja yako kuwa watu weupe wametokana na malaika unatoa mstari gani ili twende pamoja
 
Hahahhaaa mkuu kuna situation ambazo unaamini Mungu yuko... Kuna siku nilikuwa nanyongwa ili nife ila nilipoita jina la Mungu aliyehai yaani aliyekuwa ananinyonga akaachia tu ghafla na kutoweka hapo hapo sasa unafkiri Mimi zitto junior hapo siwezi kuamini kuwa Mungu yupo??

Kuna situation nyingi tu nimepitia nakumbuka hta mtihani wa kidato cha 6 nlikuwa nna shida flani hivyo sikuweza kusoma miezi miwili ya mwisho ila nakumbuka niliandika marks nazotaka Mungu anipe na nliweka kwenye karatasi na nikapeleka madhabahuni tukaiombea..... Ingawa mitihani nilifanya kwa kuunga unga ila marks zilikuja vilevile kma nlivyoandika kwenye ile karatasi sasa unafikiri nikisema NIMEMUONA MUNGU nadanganya???

Anyway haya mambo ni ya kiroho ila cku akitokea mchawi au jini ambao lazima upambane nao kiroho ndio nahisi unaweza kuamini kuwa Mungu naye yupo... Hiyo ni kama unaamini shetani yupo pia!!
Sasa hapo bosi unazungumzia imani jina la mungu ni imani ila mungu humfaamu wala hujawahi mshuhudia so ilikuwa ni IMANI.
 
1. Mkuu kuhusu Yesu kuwa malaika kwanza elewa mimi reference yangu ni biblia na hakuna sehemu kwenye biblia ambapo Yesu anatambulishwa kama malaika tu mara zote anatambulishwa kama mwana wa Mungu yaani Mungu mwana katika ule utatu mtakatifu

2. Huyo anayejiita Henoko sijampinga tu kuhusu kumuita Yesu malaika ila pia nampinga maeneo mengi ikiwemo kusema wanefili walikuwa na urefu mpaka Futi 450!!! Yaani warefu kuliko safina ya Nuhu afu eti wakaomba Nuhu awafungulie waingie???? Yaani aingie kwenye kitu anachokizidi ukubwa???.... Pia nampinga alipotosha kuwa safina ya Nuhu ilijengwa na malaika na sio Nuhu mwenyewe???.... Na mengine mengi tu ikiwemo ya kumfananisha Yesu kma malaika wa kawaida tu ilihali manabii wengine wote walimuona kma Messiah na Mwana wa Mungu atakayekomboa ulimwengu ila Henoko anasema Yesu atakuja kuharibu ulimwengu na wenye dhambi kumalizwa ??!!!!

3. Jehanum hakuumbiwa mwanadamu ilikuwa hukumu kwa Lucifer.... Sema shetani ndio anawadanganya wanadamu toka siku ile amepenyeza dhambi kwenye bustani ya Eden hivyo ukiasi Mungu basi unakuwa mali ya shetani ambaye kwake ni jehanum ila kabla ya anguko la Adam hatukupaswa kwenda jehanum wala hakukuwa na kifo ila shetani ndio anataka kwenda na wenzake huko hivyo sio kweli Mungu aliweka jehanum kwa ajili ya wanadam

4. Kuhusu msamaha..... Kumbuka Mungu alishajua fate yetu kwamba utakuwa moto wa milele maana watu walimuasi na kufanya dhambi ila kwa kuwa ana huruma na upendo akatupa neema ya kuepuka kwenda Jehanum kwa kumtuma mwanaye Yesu kristo aje atuokoe na kweli alikuja akafundisha na kuturudisha kwenye mstari na hata sasa tuna neema ya kwenda mbinguni ambayo zamani haikuwepo sababu dunia nzima hata wayahudi walikuwa wameasi na wanaabudu miungu wa ajabu ajabu..... Sasa bila msamaha angemtuma Yesu??? Kwanini ametupa second chance???

NB: msamaha upo kwa atakayeutaka sio ndio kwamba unasemehewa ilihali hujaungama dhambi
.... Ila ukikiri na kuomba msamaha Mungu anasamehe hapo hapo nafkiri unakumbuka yule jambazi pale msalabani pamoja na madhambi yake yote aliomba msamaha palepale akaambiwa ataenda mbinguni!!!

Ahsante
Maandiko ya mwanzo katika bibilia yaliandikwa na nani?,
 
ulivyofanya utafiti wa awali endelea hivyo hivyo kufanya utafiti ili ujiridhishe na hiyo ''eti wanasema... ''
lisemwalo lipo mkuu.acha dharau.kingine.apo ulipo mengi unayojiamini unayafahamu umeambiwa.na waliokuambia waliambiwa.soo usidharau kitu mtu anachokileta hapa kama a matter of concern...
 
Sasa hapo bosi unazungumzia imani jina la mungu ni imani ila mungu humfaamu wala hujawahi mshuhudia so ilikuwa ni IMANI.
Ok wewe ulitaka umuone uso kwa uso?? Basi naweza kukujibu SIJAWAHI.... Hata wanaoabudu mizimu hawajawahi iona uso kwa uso ila wanaiona PRESENCE ya hiyo mizimu kwenye maisha yao hivyo!!

Hivyo kumuona Mungu haiwezekani kimwili maana yupo kiroho zaidi ni sawa na UKIMWI hakuna aliyewahi kuuona VVU macho kwa macho ila mnaweza ona athari yake kwenye mwili wa binadamu na ndio maana tunaamini UKIMWI upo hivyo ukienda kwenye maombi na ibada au tafakuri ''unamuona'' Mungu kupitia ishara mbalimbali nmekupa mfano wangu nimewahi nyongwa na JITU nikakaribia kufa kabisa ila nlipoita jina la Mungu lile JITU liliniachia mara moja na kutoweka!! Sasa kwa muktadha huo naweza kusema NIMEMUONA MUNGU KUPITIA ISHARA A,B,C....D
 
Ok wewe ulitaka umuone uso kwa uso?? Basi naweza kukujibu SIJAWAHI.... Hata wanaoabudu mizimu hawajawahi iona uso kwa uso ila wanaiona PRESENCE ya hiyo mizimu kwenye maisha yao hivyo!!

Hivyo kumuona Mungu haiwezekani kimwili maana yupo kiroho zaidi ni sawa na UKIMWI hakuna aliyewahi kuuona VVU macho kwa macho ila mnaweza ona athari yake kwenye mwili wa binadamu na ndio maana tunaamini UKIMWI upo hivyo ukienda kwenye maombi na ibada au tafakuri ''unamuona'' Mungu kupitia ishara mbalimbali nmekupa mfano wangu nimewahi nyongwa na JITU nikakaribia kufa kabisa ila nlipoita jina la Mungu lile JITU liliniachia mara moja na kutoweka!! Sasa kwa muktadha huo naweza kusema NIMEMUONA MUNGU KUPITIA ISHARA A,B,C....D
iyo ni IMANI.
 
Maandiko ya mwanzo katika bibilia yaliandikwa na nani?,
Sio mwanzo tu kama hoja yako ni kujifichua hapo ila kuanzia Isaya.... Jeremiah.... Micah.... Kina daudi etc wanachosema kinaendana na Genesis ilihali haviendani kabisa na anachosema huyo aliyeandika kitabu cha Henoko
 
Mwanzo 6:1-8
[1]Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,

[2]wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

[3]BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

[4]Nao Wanefili
walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

[5]BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

[6]BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.

[7]BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.

[8]Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA...


HAPO INAJIDHIHIRISHA WAZI BINADAMU SI WANA WA MUNGU WANA WA MUNGU NI MALAIKA PEKEE.
 
iyo ni IMANI.
Kwahiyo wewe ulitaka nimuone face to face wakati Biblia inasema kwa utukufu wake ukimuona uso kwa uso HAKIKA UTAKUFA!!

Hata wana waisrael walitaka wamuone kma wwe unavyotaka.... Ila walipoona linaanza tetemeko zitro na radi za maana wakaomba poo na wakamwambia Mussa kuwa wameshaamini hivyo asishuke

Ni kama Medusa wa greek mythology yaani ukimuangalia tu na uso wake unaganda kuwa jiwe la chumvi .....
 
Hebu tupunguze ubishi tuzidi kupiga hatua kadha wa kadha...binadamu tusijing'ang'anize nasi ni wana wa mungu wakati sisi ni walaamiwa.

Origin yetu ni ya laana ila sasa tujitambue wapi tuendako ni salama na nini tufanye ili tuweze kupunguza machafu tuliyo nayo...


Tutazidi saka mchawi nani wakati wachawi ni sisi wenyewe.....never give up tuwashe moto...
 
Ni hv kwa kifupi tu huko nyuma kuna tukio kubwa sana lilitokea na hadi leo athari zake zinatawala maisha yetu.tukio hilo ni interaction kati ya binadamu na viumbe fulani wengine wa Mwenyezi Mungu(huwa tunawaita tu malaika hii inatupa upofu sana)walikuwa 200 wakiongozwa na mkuu wao Azazel waliposhuka ktk kilele cha mlima Hermon na kuigiza maumbile ya kibinadamu.kilichowaleta ni kutamani binadamu.walitaka kukaa nao,wawatawale,wazae nao,waanzishe empire yao tofauti na utaratibu waliopangiwa na Mungu.wakafanya hivyo.ikazaliwa offspring ya ajabu,majitu makubwa yenye nguvu za kutisha na akili za ajabu na roho za ajabu maana nusu binadamu nusu malaika.waliitwa nephilims,leo tunawaita titans(usifikiri hadithi ya kigiriki hii)!kutokana na hiyo offspring kuwa imbalance,ilileta vurugu kubwa duniani,na kama Mungu asingeingilia kati mbegu ya binadamu pure ingetoweka.hao malaika pamoja na hayo matoto yao ndio walifundisha binadamu mambo meengi ambayo leo yana sehemu kubwa ktk sayansi,elimu na tamaduni zetu hasa mashariki ya mbali,India na america.base yao kuu ilikuwa bara la Atlantis lililokuwepo katikati ya america na ulaya.kitendo hiki kilimchukiza Mungu mno akaamua kutuma gharika ya maji na kuteketeza dunia nzima pamoja na bara la Atlantis isipokuwa binadamu mmoja anaitwa Nuhu na watoto wake na baadhi ya wanyama ambao hawakuchafuliwa(nephilims walizaana hata na mijusi,kilichotoka hapo ni balaa).LAKINI kuna laana alitamka Mungu,kwamba roho za viumbe hao hataziangamiza,ataziacha na zitakuwa chanzo cha kila uovu duniani kwa umri wote wa dunia hadi mwisho ili viumbe wake wote wapate darasa how serious was this mistake!roho hizo ndizo zilimuongoza Nimrod kuijenga Babylon na kuanzisha idol worshiping na tamaduni za Atlantis zikaanza kurudi taratibu huku spidi yake ikivurugwa na elimu ya dini ya mitume na manabii wa Mungu.ilibidi utaratibu wa kuinteract na binadamu ili kutimiza lengo lao waufanye kwa siri,taratibu,miaka na miaka,wakiibadili dunia taratibu hadi mazingira yakiruhusu,roho hizi zikiwa ndani ya miili ya kibinadamu,zitaigeuza dunia nzima kuwa kama Atlantis!ndipo hapa vyama vya siri na dini zisizoeleweka vinaposhamiri underground.
Mkuu umechimba sana! ndo maana hata vyakula sahihi vimepungua duniani tukaanza kula ugali na ubwabwa (starch in general) maziwa na nyama kama chakula hivi ndo vinatupa maradhi mengi.

Kama kweli Mungu ndo ametupa hivi ndo viwe vyakula basi God is not fair.Yeye alitupa matunda na mboga tu viwe vyakula, leo tuna hybrid ndo chakula. Twafaaa
 
Kwenye kitabu cha enoki ameandika kwambali alipokwenda mbinguni alionyeshwa mwisho wa dunia nina mashaka na hii dunia kuwa hata sio tufe HILI NALA TATIZO hiki kitabu cha enoki kina jambo la siri sana.
 
Kila nikisoma hicho kitabu nabaki kichwa kinauma,inaonekana mwandishi alikuwa na knowledge ya ulimwengu tofauti na tunavyojifunza na kuelewa sasa hivi.

Kupingwa hiki kitabu na kanisa kuna jambo kubwa, si bure.
 
Mkuu humu watu ni vifuata upepo na hawajui wanamini nini, akiona mtandaoni wameandika hv yy anachukua na kukariri.
Good point man most Africans are so dull
They almost take everything written in internet as facts and its so tough arguing with them
 
Nimegundua kitu apa...bibilia inatuongopea,iv safina kubwa kiasi kile wanaweza kujengwa watu 4-7 na ilichukua muda gani?


,alafu kwny dhambi hapa ivi mtu unaweza kufanya uovu wowote ule ili hali uamini utasamehewa kwa kuwa mungu ni mwenye kusamehe basi hata waovu hawatapewa hukumu watasamehewa tu.


Kitabu cha enock kinaonekana na ukweli fulani hivi endapo utatathimini kwa makini...hata uyu yesu sizani kama atarudi kwa mema lazima aangamize tuliolaanika wote....nipo nawasoma endelezeni hoja ila nimehisi bibilia inadanganya sana kwanza ina mistari inayojipinga yenyewe.
We ndo uelewi kabisa safina ilichukua 120 years hata watu wanashindwa????? Ingawa sijui hip fact yako ya wtu tano hadi saba umeitoa wapi
 
Kama mungu alimuumba mtu mweusi kabla ya hao fallen angels kuwaingilia kimwili binadamu(blacks) kwa nn idadi ya mtu mweupe ni kubwa zaidi ukilinganisha na mweusi?
 
Kama mungu ni mwenye kusamehe uko mnapopaita jehanam kwa kazi gani si autoe hata uo moto maana hatamuhukumu mtu wote tutasamehewa.

Na swala la mbinguni wewe unaamini vipi kuwa mbinguni ni kwa wanadamu wakati hiyo bibilia inasema kuwa mbingu ni mahala na makazi ya malaika,je itawezekana kweli malaika wakachangamana na wanadamu na kuishi pamoja?.

Kuna mambo ukiyasoma inaonesha wazi tunalishwa matongo pori si ndo hiyohiyo bibilia inasema dhambi zote ni sawa sasa hapa unamfunza mwanadamu nini ndipo unakuta mtu anabaka na kujiamanisha kuwa endapo alipitiwa na uovu ata samehewa lakini pia licha ya msamaha kiutendaji dhambi yuko sawa hata na yule mtu muongofu(mdanganyaji)


embu tuwe tunajitoa tongotongo kwa ishu nyingine sio ushabiki tu usio na mbele wala nyuma,bibilia inazingua sana na nadiliki kusema imeharibu watu na imewapaka dhambi zaidi na dhambi kuu iliowapaka watu ni hii MUNGU NI MWENYE KUSAMEHE NA SISI NI WANA WAMGU.


wana wa mungu haitakuja iwe na haitatokea akawa mwanadamu,mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake/wao....(kwenye bibble uko kumejikanya two place ya kwanza wao ikaja wake)sasa kama mimi niliumbwa kuwa kama mfano ni vipi aniite mwana wake?,katka kushushwa kwa yesu ambaye pia ni malaika,hapa niwe mtulivu kuna sehemu uko juu umempinga enock alipomtaja yesu kama malaika umebisha kuwa sio malaika,sasa wewe kama unabisha yesu si malaika mbona shetani alikuwa malaika miongoni mwa malaika wenzie,na bibilia inasema yesu alikuwako na aliitwa NENO,basi katka hili neno kuna kitu humu,maana mungu aliumba dunia kwa kutumia neno kumbe kama alitumia neno alisaidiyana na huyu yesu ambaye aliitwa neno,kwa hiyo yesu na ni malaika na ana uungu ndani yake.
Nimefatilia ur arguments nimegundua uwezo wako wakufikiri ni wakutilia mashaka


Kwanza u lack basic bible knowledge and pili sina uhakika hata kama hivi vitabu huwa unasoma nahisi ni mfuata upepo ,

Nahisi hata Mimi nikiandika kitabu kizuri kuhusu dini na kujiita kuwa Mimi ni yohana au Ibrahim utaamini kabisaaa

Tatu anae take time Ku argue nawewe is surely wasting his/her precious time
 
kuna majadiliano yaliwahi kufanywa na CNN kuhusiana na kuharibiwa old bible ambayo inasemekana ilikuwa inamzungumzia zaidi mtu mweusi na pia wazungu ni uzao uliolaaniwa uliotokana na wale malaika waliowaingilia watoto wa binadamu
Kwanini mnaenda kwa wazungu tyu kwani wachina na waarabu ni watu weusi???
Hata waarabu ni weupe kama wazungu tyu sasa mkiamini hivo yani inamaanisha Mungu aendelee kutuma viumbe vyenye laana kuleta ujumbe
 
Back
Top Bottom