Jinsi ya kupata marafiki na kushawishi watu (Tafsiri ya kitabu How to win friends and influence people cha Dale Carnegie)

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,233
12,742
Pictuspublishers tumefasiri kitabu How to win friends and influence people. Kila wiki siku ya ijumaa tutasoma sehemu moja. Unaweza kusoma sehemu iliyofasiriwa ndani ya maktabaapp. kuungwa tucheki whatsapp 0715278384.

71vK0WVQ4rL.jpg


Muandishi: Dale Carnegie, 1936.
Mtafsiri: Pictus Publishers ltd
Email: pictuspublishers@gmail.com.
©Pictus Publishers ltd2022.
Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli, kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.

MAPENDEKEZO TISA YA JINSI YA KUFAIDIKA NA KITABU HIKI

  • Kama unataka kufaidika vilivyo na kitabu hiki, kuna jambo moja la lazima. Ni la muhimu kuliko kanuni au mbinu yoyote ile. Bila hilo, kanuni elfu za jinsi ya kusoma na kufaidika hazitakuwa na msaada wa maana kwako. Kama unalo jambo hili, basi utafanya maajabu bila hata ya kusoma mapendekezo yoyote juu ya usomaji wenye faida.
  • Ni takwa gani hilo la ajabu? Ni hili: Tamaa kali ya kutaka kujifunza, nia hasa ya kutaka kuongeza uwezo wako wa kushughulika na watu.
  • Unawezaje kukuza tamaa hiyo? Kwa mara zote kujikumbusha jinsi ambavyo kanuni hizi ni muhimu kwako. Fikiria jinsi ambavyo kuzimudu kutafanya maisha yako yawe ya furaha na ya kuridhisha zaidi. Jiambie tena na tena, “Furaha yangu, kukubalika kwangu na thamani yangu kwa kiasi kikubwa kunategemea uwezo wangu wa kushughulika na watu.
  • Soma kila sura kwa haraka ili kupata wazo kuu. Pengine utashawishika kukimbilia sura nyingine. Usifanye hivyo—labda kama unasoma tu kujifurahisha. Lakini kama unasoma ili kuongeza uwezo wako kwenye mahusiano na binadamu wengine, rudi na usome kila sura kwa kina. Baada ya muda, hili litakuokolea muda na kukupatia matokeo.
  • Simama kusoma mara nyingi na tafakari kile ulichosoma. Jiulize ni jinsi gani na wapi unaweza kutumia mapendekezo yaliyotolewa.
  • Soma ukiwa na penseli, kalamu ya wino au ya rangi. Kama ukikutana na pendekezo ambalo unahisi unaweza kulitumia, chora mstari pembeni yake. Kama ni pendekezo lenye hadhi ya nyota nne, basi pigia mstari kila sentensi au liwekee alama “****.” Kuwekea kitabu alama au kukipigia mistari inafanya kivutie na iwe rahisi kurejelea.
  • Namfahamu mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni meneja wa kampuni ya bima kwa miaka kumi na mitano. Kila mwezi alisoma mikataba yote ya bima ambayo kampuni yake ilikuwa imeingia. Ndiyo, alisoma mikataba inayofanana tena na tena kila mwezi na mwezi, mwaka na mwaka. Kwa nini? Kwa sababu uzoefu ulikuwa umemuambia kuwa hiyo ndiyo njia pekee wa kuiweka vizuri akilini mwake.
  • Kuna wakati nilitumia miaka miwili kuandika kitabu juu ya kuzungumza na umati, lakini bado nilihitajika kurudi nyuma kuangalia nimeandika nini ndani ya kitabu change mwenyewe. Kasi ambayo tunasahau vitu inastaajabisha
  • Hivyo basi, kama unataka kupata faida ya kweli na kudumu kutoka katika kitabu hiki, usidhanie kuwa kukipitia tu mara moja kutatosha. Baada ya kukisoma chote, pengine utahitajika kukipitia kwa saa chache kila mwezi. Kiweke mezani pako kila siku. Kichungulie mara kwa mara. Endelea kuwazia juu maboresho mengi unayoweza kufikia. Kumbuka kuwa kanuni hizi zinaweza jengeka kuwa tabia kwa kuzirejelea na kuzitumia mara kwa mara tu. Hakuna njia nyingine.
  • Bernard Shaw amewahi kusema: “Kama ukimfundisha mtu jambo lolote lile, hatajifunza kamwe.” Shaw alikuwa sahihi. Kujifunza ni jambo linalohitaji kutenda. Tunajifunza kwa kufanya. Hivyo basi, kama nia yako ni kuzimudu kanuni unazosoma kwenye kitabu hiki, zifanyie kazi. Zitumie kwenye kila fursa unayopata. Usipofanya hivyo, utazisahau haraka sana.
  • Pengine utaona kuwa ni vigumu kutumia kanuni hizi kila wakati. Nafahamu, sababu ndiye nimeandika kitabu lakini bado mara nyingi napata ugumu kutumia kila pendekezo. Kwa mfano, unapokasirishwa, ni rahisi kushutumu na kulaani kuliko kujaribu kuelewa mtazamo wa mtu mwingine; mara nyingi ni rahisi kutafuta makosa kuliko kuliko kutafuta jambo la kupongeza; ni jambo la asili kuongea kuhusu unayotaka kuliko anayotaka mwingine nk. Kwa hiyo unavyosoma kitabu hiki, kumbuka kuwa hujaribu tu kupata habari. Unajaribu kujenga tabia mpya. Ndiyo, unajaribu aina mpya ya maisha. Jambo hilo litahitaji bidii, muda na kutumia kila siku yale uliyojifunza.
  • Basi rejelea kurasa hizi mara kwa mara. Chukulia kitabu hiki kama maelekezo ya kila siku juu ya mahusiano wa binadamu. Na kila unapokutana na tatizo fulani—kama kushughulika na mtoto, kumfanya mwenzi wako aunge mkono wazo lako au kumridhisha mteja mwenye hasira—jizuie kufanya jambo la asili, jambo linaloongozwa na hisia. Jambo ambalo huwa si sahihi. Badala yake, rudi kwenye kurasa hizi na rejea kwenye aya ulizopigia mistari. Jaribu kutumia mbinu hizi na angalia zinapokutendea maajabu.
  • Mpatie mwenzi wako, mtoto wako au mfanyakazi mwenzako senti kumi kila mara anapokukuta ukikiuka kanuni fulani. Fanya kuzimudu kanuni hizi iwe burudani.
  • Rais wa benki moja maarufu ya huko Wall Street aliwahi eleza, mbele ya moja ya darasa langu juu ya mfumo wenye ufanisi sana aliotumia kuboresha utu wake. Mtu huyu alipata elimu kidogo tu, lakini aliweza kuwa mmoja wa wasimamizi wa fedha muhimu sana katika Marekani, na alikiri kuwa sehemu kubwa ya mafanikio yake ni sababu ya mfumo huo alioubuni. Hiki ndicho alichofanya, nitaelezea kama alivyosema kadri ninavyokumbuka.
“Kwa miaka mingi nimekuwa na kitabu kinachoonyesha miadi niliyokuwa nayo siku hiyo. Familia yangu haikunipangia jambo lolote jioni ya jumamosi, maana walifahamu kuwa nilitumia jioni ya jumamosi kujitathmini. Baada ya chakula cha jioni nilienda sehemu yap eke yangu, nilifungua kitabu cha miadi na kutafakari juu ya mikutano yote, mahojiano na usaili uliotokea kwenye juma zima. Nilijiuliza:

“Kosa gani nilifanya wakati ule?”

“Kitu gani nilifanya sawa—na kwa namna gani ningeweza kuboresha mambo?”

“Ni somo gani ninapata kutokana na mambo yaliyotokea?”

“Mara nyingi kujitatmini huku kulinifanya nifedheheke sana. Mara nyingi nilistaajabishwa na makosa yangu ya kizembe. Lakini kadri miaka ilivyozidi kwenda makosa haya yakaanza kupungua. Ikafika wakati nilitaka hata kujipongeza mwenye baada ya kumaliza kujitathmini. Kujitathmini huku na kujielimisha kuliendelea mwaka hata mwaka. Kumenisaidia kuliko jambo lolote lile nililowahi kufanya.

“Kulinisaidia kuongeza uwezo wangu wa kufanya maamuzi—na kulinisaidia sana katika kushughulika kwangu na watu. Napendekeza sana matumizi ya mbinu hiyo.”

Kwa nini usitumie mfumo kama huo kuangalia jinsi unavyotumia kanuni zilizomo ndani ya kitabu hiki? Kama ukifanya hivyo, mambo mawili yatatokea.

Kwanza, utajikuta unapata elimu kwa njia ambayo ni bora na ya kufurahisha.

Pili, uwezo wako wa kukutana na kushugulika na watu utaboreka sana.

Mwishoni mwa kitabu hiki utakutana na kurasa tupu, humo unaweza kuandika mafanikio yako katika kutumia kanuni zilizoandikwa humu. Andika kwa kina, andika tarehe, majina, matokeo. Kutunza kumbukumbu hizo kutakusukuma kufanya bidii hata zaidi; na jinsi zitakavyokufurahisha taarifa hizo ikitokea umeziona jioni moja miaka kadhaa mbele!

Ili kufaidika na kitabu hiki:

  • Jenga tamaa kali ya kumudu kanuni za mahusiano ya binadamu.
  • Soma kila sura mara mbili kabla ya kwenda inayofuata.
  • Unaposoma, simama mara nyingi na kujiuliza ni jinsi gani unaweza kutumia kila pendekezo.
  • Pigia mstari kila wazo muhimu.
  • Rejelea kitabu hiki kila mwezi.
  • Tumia kanuni hizi kila upatapo fursa. Tumia kitabu hiki katika kutatua matatizo yako ya kila siku.
  • Fanya kujifunza kuwe burudani kwa kumpatia rafiki yako senti kumi, au dola moja kila mara anapokukuta ukikiuka moja ya kanuni hizi.
  • Andika kumbukumbu nyuma ya kitabu hiki kuonyesha ni lini na kwa namna gani ulitumia kanuni hizi.
 
SEHEMU YA KWANZA

KANUNI ZA MSINGI ZA JINSI YA KUSHUGHULIKA NA WATU





KAMA UKITAKA KURINA ASALI USIPIGE TEKE MZINGA

Tarehe 7 mwezi wa tano mwaka 1931 kulikuwa na msako wa aina yake wa mhalifu ambao New York halijawahi kushuhudia. Baada ya msako wa wiki kadhaa, mhalifu aliyejulikana kama Crowley “Bunduki mbili”, muuaji na jambazi wa kutumia silaha ambaye hakutumia wala kuvuta kilevi chochote alikuwa amepatikana. Alikuwa amezingirwa katika makazi ya mpenzi wake katika mtaa wa West End.

Polisi mia moja na hamsini walizingira maficho yake yaliyokuwa kwenye ghorofa ya juu kabisa. Walikuwa wametoboa matundu kwenye paa. Walikuwa wanajaribu kumtoa Crowley “Muua polisi” kwa kutumia gesi ya kutoa machozi. Walitega bunduki katika majengo yanayozunguka. Kwa zaidi ya saa nzima, eneo tulivu la jiji la New York lilirindima kwa milio ya bastola na bunduki za rasharasha. Crowley alijificha nyuma ya sofa na kuwarushia polisi risasi mfululizo. Watu elfu kumi walikuwepo kushuhudia mapambano hayo. Kitu kama kile hakijawahi kutokea katika jiji la New York.

Crowley alipokamatwa, kamishna wa polisi, E. P. Mulrooney alikiri kuwa jambazi Crowley “Bunduki mbili’ ni moja ya wahalifu hatari zaidi kuwahi kutokea katika historia ya jiji la New York. “Huyu haoni taabu kuua,” alisema kamishna.



Lakini Crowley “Bunduki mbili” alikuwa na maoni gani kujihusu? Tunafahamu maoni yake kwa sababu wakati polisi wanarusha risasi kwenye makazi yake, yeye aliandika barua kwa “Yeyote atayejali.” Wakati anaandika barua hiyo, damu kutoka kwenye majeraha yake iliacha alama katika karatasi. Kwenye barua hiyo Crowley alisema: “Katika kifua changu mna moyo uliopondeka lakini wenye rehema, moyo usioweza kumdhuru yeyote.”

Kabla ya tukio hili Crowley alikuwa anafurahia maisha na mpenzi wake katika barabara moja huko Long Island. Ghafla polisi aliwafuata kwenye gari na kusema: “Naomba kuona leseni yako.” Bila kujibu kitu, Crowley alitoa bunduki na kummiminia mvua ya risasi. Polisi yule alipokuwa anakufa, Crowley alitoka ndani ya gari na kuchukua bastola ya polisi na kuumiminia risasi mwili uliokuwa umelala chini, huyo ndiye muuaji aliyesema: “Moyo wangu umepondeka lakini ni wenye rehema, hauwezi kumdhuru yeyote.”

Crowley alihukumiwa kifo kwa kiti cha umeme, alipokuwa anaingia kwenye gereza la wafungwa wanaosubiria kifo alisema, “Je hiki ndicho malipo ya kuua watu? Hapana, haya ni malipo ya mimi kujilinda.”

Lengo la hadithi hii ni kuonyesha kuwa: Crowley “Bunduki mbili” hakuona kama ana kosa lolote.

Je hilo ni jambo lisilo la kawaida kwa wahalifu? Kama unafikiri si la kawaida sikiliza haya:

“Nimetumia miaka yangu kuwapa watu furaha, na kuwasaidia kuwa na maisha mazuri na malipo niliyopata ni uonevu.Kuishi kama digididi.”

Hayo yalikuwa ni maneno ya Alcapone. Muhalifu hatari kabisa Marekani. Kiongozi wa genge la uhalifu hatari kabisa kuwahi kutokea katika jiji la Chicago. Capone hakujilaumu, badala yake alijiona ni mtu anayesaidia jamii. Msaidia jamii asiyeeleweka na asiyethaminiwa inavyostahili.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Dutch Schultz kabla ya kuuwawa na mwanachama wa genge la uhalifu huko Newark. Mtu mmoja alisema katika mahojiano kuwa Dutch Schultz alikuwa ni mtu anayesaidia jamii na aliamini hivyo.

Nimewahi kuzungumza kuhusiana na hili suala na Lewis Lawes ambaye alikuwa ni mkuu wa gereza maarufu huko New York la Sing Sing kwa miaka mingi, alikiri kuwa ni “Wahalifu wachache sana wanajiona kuwa ni watu wabaya. Wanajiona ni watu wa kawaida kama mimi na wewe tu. Wanajiona kuwa wana sababu za msingi za kufanya wanayoyafanya. Wanaweza wakakuambia ni kwanini wanavunja sanduku la pesa, au kwanini ni wepesi kufyatua risasi. Wengi wao hujitahidi kutafuta sababu za uwongo na kweli kutetea uovu wao. Hata wakijaribu kujiaminisha wao wenyewe kuwa hawana hatia. Hupaza sauti wakisema hawakustahili kufungwa.

Iwapo Al Capone, Crowley “Bunduki Mbili,” Dutch Schultz na wanaume na wanawake wengine waliojaa magerezani hawajilaumu kwa chochote, vipi kuhusu watu ambao mimi na wewe tunakutana nao?

Muanzilishi wa maduka ya Wanamaker, John Wanamaker aliwahi kiri hivi: “Nilijifunza miaka thelathini iliyopita kuwa ni ujinga kushutumu. Ninapata ugumu wa kutosha katika kukabiliana na mapungufu yangu, siwezi anza kuhangaika na ukweli kuwa Mungu aliamua kutogawa akili kwa usawa.”

Wanamaker alijifunza jambo hilo mapema sana, lakini mimi imenichukua kufanya makosa kwa theluthi ya karne kabla sijaanza kuelewa kuwa kati ya mia moja, mara tisini na tisa, watu huwa hawajishutumu kwa chochote. Haijalishi ni kibaya kiasi gani. Kushutumu hakusaidii lolote, na zaidi zaidi kunamfanya mtu ajitahidi kujitetea. Shutuma ni hatari kwa sababu zinaharibu heshima ya mtu, inampunguzia kujithamini na huleta chuki.

Mwanasaikolojia maarufu, B. F, Skinner alithibitisha kupitia majaribio aliyoyafanya kuwa, mnyama anayezawadiwa kwa kuwa na tabia njema hujifunza haraka, na hukumbuka vizuri kile alichojifunza kuliko mnyama anayeadhibiwa kwa kuwa na tabia mbaya. Tafiti zilizofuatia zilionyesha kuwa hata kwa binadamu iko hivyo. Kwa kushutumu hatuleti mabadiliko ya kudumu, na mara nyingi tunaishia tu kujenga chuki.

Mwanasaikolojia mwingine maarufu, Hans Selye alisema, “Kama ambavyo tunapenda kukubalika, ndivyo tunavyochukia kushutumiwa.”

Chuki inayoletwa na na shutuma, inaweza athiri ari ya wafanyakazi, washiriki wa familia na marafiki, na bado ikawa haijarekebisha jambo au hali ya mambo iliyosababisha shutuma.

George B Johnston kutoka Enid Oklahoma ni msimamizi wa masuala ya usalama katika kampuni ya uhandisi. Moja ya majukumu yake ni kuhakikisha wafanyakazi wanavaa kofia ngumu kila wanapokuwa kazini.Alisema kuwa, kila alipokuwa anakutana na mfanyakazi ambaye hajavaa kofia ngumu, alikuwa akimwambia kama mtu mwenye mamlaka kuhusu sheria ya kuvaa kofi na kuwa anapaswa aifuate. Matokeo yake ni kuwa walimkubalia kwa shingo upande, na mara tu alipotoka wafanyakazi walivua kofia zao.

Akaamua kutumia mbinu nyingine. Alipokutana tena na wafanyakazi ambao hawajavaa kofia zao, aliwauliza iwapo kofia zinawatinga au haziwatoshi vizuri. Kisha kwa kauli nzuri aliwakumbusha kuwa kofia zimetengenezwa kwa namna itakayowalinda na madhara, na kushauri kuwa zivaliwe mara zote wawapo kazini. Matokeo yake ni kuwa watu wakaongeza uvaaji wa kofia bila kinyongo wala kujihisi vibaya.

Katika historia unaweza kuona mifano mingi ya jinsi ambavyokushutumu kusivyo na faida. Chukulia mfano wa ugomvi wa Theodore Roosevelt na Rais Taft, ugomvi ambao ulikigawa chama cha Republican, ukasababisha Woodrow Wilson kuwa Rais na kubadili historia. Hebu acha tuuchunguze vizuri mfano huo. Punde tu baada ya Theodore Roosevelt kuachia urais mwaka 1908, akaanza kumuunga mkono Taft ambaye alichaguliwa kuwa Rais. Baada ya hapo Theodore Roosevelt akafunga safari kwenda Africa kutalii na kuwinda. Aliporudi aliwaka kwa hasira, akatangaza kutomuunga mkono Taft kwa sababu ya uhafidhina wake, na akajaribu kuingia madarakani kwa muhula wa tatu na akaunda chama kilichoitwa Bull Moose, hilo halikusaidia kitu zaidi ya kukidhoofisha chama cha Republican. Katika uchaguzi uliofuata, William Howard Taft na chama cha Republican walishinda katika majimbo mawili tu, Vermont na Utah. Chama hakijawahi shindwa namna hiyo. Theodore Roosevelt alimlaumu Taft. Lakini je, Rais Taft alijilaumu mwenyewe? Hapana hata kidogo, kwa machozi Taft alisema: “Sioni kama kulikuwa na namna bora ya kufanya mambo zaidi ya nilivyofanya.”

Ni nani wa kulaumiwa? Roosevelt au Taft? Kwa kweli sijui na sijali. Jambo ninalotaka kueleza na kuwa, shutuma zote za Theodore Roosevelt hazikuweza kumuaminisha Taft kuwa alikosea. Badala yake zilimfanya Taft ajitahidi kujitetea hadi kwa machozi akisema: “Sioni kama kulikuwa na namna bora ya kufanya mambo zaidi ya nilivyofanya.”

Au fikiria juu ya kashfa ya Teapot Dome. Kashfa iliyopamba magazeti mwanzoni mwa miaka ya 1920. Ilitingisha nchi. Na katika kumbukumbu za watu leo, jambo kama lile halijawahi kutokea ndani ya Marekani. Kashfa yenyewe ilikuwa namna hii: Waziri wa mambo ya ndani wa Marekani katika baraza la rais Harding, bwana Albert B. Fall alipewa jukumu la kukodisha visima vya mafuta vya serikali huko Elk Hill na Teapot Dome ambavyo viliwekwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye ya jeshi la majini. Je Fall aliruhusu mnada kufanyika? Hapana. Alimpatia mkataba huo mnono rafiki yake aliyeitwa Edward L. Doheny. Na Doheny alifanya nini? Alimpatia Fall “mkopo” wa dollar laki moja. Na kwa kutumia madaraka vibaya, Fall akaagiza kikosi cha jeshi la Marekani kuwaondoa wachimbaji wengine wa karibu ambao visima vyao vilikuwa vikinyonya mafuta kutoka ukanda wa Elk Hill. Wachimbaji hawa baada ya kufukuzwa kwa mtutu wa bunduki na singe wakaamua kwenda mahakamani na kufumua kashfa ya Tea Dome. Kashfa yenye harufu mbaya sana kiasi cha kuharibu uongozi wa Rais Harding na kuitia kichefuchefu nchi nzima. Ilisababisha Albert B. Fall kufungwa, na ilitishia kusambaratisha chama cha Republican.

Fall alishutumiwa vikali sana, ni watu wachache sana wamewahi shutumiwa namna ile. Je alitubu? Hata kidogo! Miaka kadhaa baadaye Herbert Hoover alisema hadharani kuwa Rais Harding alikufa sababu ya matatizo ya kiakili yaliyosababishwa na kusalitiwa na rafiki. Mke wa Fall aliposikia jambo hili aliruka kitini, alilia, alijipigapiga na kusema kwa hasira: “Nini! Harding alisalitiwa na Fall? Hapana! mume wangu hajawahi msaliti yeyote. Nyumba iliyojaa dhahabu isingeweza mshawishi mume wangu kutenda ndivyo sivyo. Yeye ndiye aliyesalitiwa na kutolewa kafara.”

Basi hiyo ndiyo hulka ya binadamu, waliofanya makosa hulaumu kila mtu isipokuwa wao wenyewe. Sote tupo namna hiyo. Kwa hiyo, kama kesho tukitaka kumshutumu mtu, acha tuwakumbuke Al Capone, Crowley “Bunduki Mbili” na Albert Fall. Tuelewe kuwa kushutumu ni kama njiwa wa kufugwa. Siku zote hurudi nyumbani. Acha tuelewe kuwa mtu tunayeenda kumshutumu na kumsahihisha labda atajaribu kujitetea, na kutushutumu sisi badala yake: au kama ni mstaarabu kama Taft atasema: “Sioni kama kulikuwa na namna bora ya kufanya mambo zaidi ya nilivyofanya.”

Katika asubuhi ya tarehe 15 mwezi wa nne mwaka 1865 Abraham Lincoln alipokuwa karibu kufa kwenye makazi duni yaliyokuwa ng’ambo ya barabara kutoka ukumbi wa Ford ambako John Wilkes Booth alimpiga risasi. Lincoln akiwa amelala kwa ulalo kitandani kwa sababu mwili wake ulikuwa mrefu sana kutosha kitandani. Mchoro mbovu wa Rosa Bonheur, The Horse fair ukining’inia ukutani mbele ya kitanda na karabai ikitoa mwanga hafifu wa njano.

Lincoln alipokuwa hoi kitandani, waziri wa mambo ya vita , bwana Stanton alisema, “Hapa amelala kiongozi bora kabisa kuwahi kutokea duniani.”

Ni siri gani iliyomfanya Lincoln aweze kuchukuana na watu vizuri? Nimetumia miaka kumi nikisoma maisha ya Abraham Lincoln. Kwa miaka mitatu nilishughulika na kuandika kitabu kiitwacho Usiyoyajua kuhusu Lincoln. Nafikiri nimegusa maisha ya Lincoln kwa undani kadri inavyowezekana. Kwa upekee kabisa, nilijikita kusoma jinsi Lincoln alivyoshughulika na watu. Je alijihusisha na kushutumu? Ndiyo, alipokuwa kijana huko Pigeon creek Valley, Indiana, alijihusisha na sana na kushutumu watu, na siyo kushutumu tu, bali alikuwa akiandika barua na mashairi ya kuwadhihaki watu. Alitupa barua na mashairi hayo barabarani ambako alijua watu watazipata kirahisi. Moja ya barua hiyo ilisababisha kinyongo ambacho kilidumu maisha yote.

Hata baada ya Lincoln kuwa mwanasheria huko Springfield, Illinois, bado alikuwa na tabia ya kuwashambulia wapinzani wake kwa barua alizozichapisha katika magazeti. Lakini mtindo huu haukuwa na mwiho mzuri. Katika majira ya kupukutika ya mwaka 1842 alimshambulia kwa dhihaka mwanasiasa mmoja mkali na mwenye majivuno aliyeitwa James Shields. Alimshambulia kwa barua ya siri iliyochapishwa gazeti la Springfield journal, mji wote ulilipuka kwa vicheko kutokana na barua hiyo. Sababu Shields alikuwa ni mwenye majivuno, akawaka hasira kwa kudharauliwa. Akachunguza na kugundua aliyeandika barua ile, akamuendea Lincoln na kumwambia wapambane ana kwa ana. Lincoln alikuwa hataki kupambana, na alikuwa ni mpinzani wa mapambano kama hayo. Lakini pia haikuwezekana aepuke jambo hilo na kubaki na heshima yake. Aliambiwa achague silaha yake. Kwa sababu alikuwa na mikono mirefu alichagua panga lililotumika na jeshi la wapanda farasi, na akapata mafunzo ya kupigana kwa mapanga kutoka kwa mhitimu wa chuo cha jeshi cha West Point. Siku ya pambano, yeye na Shields wakakutanakwenye mchanga katika mto Mississipi, wakiwa wamejiandaa kupambana hadi kifo. Lakini mwishoni kabla ya pambano, wapambe wao waliingilia kati na kusimamisha pambano.

Hiyo ilikuwa ni hali tete kabisa kwa Lincoln kuwahi kujikuta katika maisha yake binafsi. Lakini alipata somo muhimu sana kuhusiana na kushughulika na watu. Hakuandika tena barua ya dhihaka, wala hakumdhiki yeyote tena. Na kuanzia wakati huo hakumshutumu mtu yeyote.

Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe, Lincoln alibadilisha majenerali wake walioongoza mara kwa mara. Na mara zote, majenerali wote—McClellan, Pope, Burnside, Hooker, Meade—Walivurunda vibaya na kumuacha Lincoln akihangaika asijue la kufanya. Nusu ya nchi iliwashutumu vikali majenerali hao kwa uzembe, lakini Lincoln, “Bila ubaya kwa yoyote, na kusaidia wote,” hakutoa shutuma. Moja ya nukuu alizozipenda sana, “Usihukumu nawe hutahukumiwa.”

Na hata mke wake na watu wengine walipowaongelea watu wa kusini kwa ubaya, Lincoln alijibu: “Msiwashutumu, hata sisi tungekuwa katika hali yao tungetenda kama wao.”

Pamoja na hayo, kama kuna mtu alikuwa na haki ya kurusha shutuma basi alikuwa ni Lincoln. Acha tuone mfano mmoja:

Pambano la Gettysburg lilipiganwa katika siku tatu za mwanzo za mwezi wa saba wa mwaka 1863. Katika usiku wa tarehe 4 ya mwezi huo, jenerali Lee, akiwa na jeshi lake lililoshindwa alianza kurudi kusini, mvua kubwa ilikuwa inanyesha. Alipofika kwenye mto Potomac, alikuta umefurika haupitiki, huku jeshi la muungano likiwa nyuma yake. Lee alikuwa amebanwa kwenye kona bila njia ya kutorokea. Lincoln aliona jambo hilo. Ilikuwa ni fursa adhimu ya kuteka jeshi la Lee na kukomesha vita mara moja. Kwa hiyo kwa matumaini makubwa ya ushindi, Lincoln alimuamuru Meade kutoitisha baraza la vita na badala yake amvamie Lee mara moja. Alimtuma mjumbe maalumu na aliyepeleka amri kwa Meade akimtaka avamie jeshi la Lee mara moja.

Lakini Jenerali Meade alifanya nini? Alifanya kinyume kabisa na alichoagizwa. Aliitisha baraza la vita, akikiuka amri ya Lincoln waziwazi. Alisita na kujizungushazungusha. Alituma ujumbe akitoa visingizio kibao. Alikuwa amekataa kutii amri waziwazi. Mwishowe maji yalipungua na Lee akavuka mto Potomac na jeshi lake na kutoroka.

Lincoln alikasirika sana, “Nini maana ya jambo hili?’” alipiga kelele akimwambia Robert, mtoto wake. “Mungu wangu! Nini maana ya jambo hili? Walikuwa wetu kabisa, tulihitaji tu kunyoosha mkono na kuwakamata, lakini hakuna ambacho ningefanya au kusema kulifanya jeshi livamie. Kwa hali aliyokuwa nayo Lee, jenerali yoyote angemshinda. Hata mimi mwenyewe ningekuwepo pale ningemtandika.”

Katika hali hiyo, Lincoln akaketi na kuandika barua kwenda kwa Meade. Na kumbuka kuwa wakati huo Lincoln alikuwa mhafidhina hasa, na alijizuia katika maneno yake. Kwa hiyo barua hii ya mwaka 1863 kutoka kwa Lincoln inaonyesha shutuma kali zaidi alizoweza kutoa.

Mpendwa Jenerali

Siamini kama huelewi hali mbaya aliyokuwa nayo Lee kabla ya kutoroka. Alikuwa kaingia mikononi mwetu. Na kumkamata, pamoja na ushindi tuliopata hivi karibuni, kungemaliza vita. Lakini kwa sababu hilo halikutokea, inaonekana vita hii itaendelea kwa muda mrefu sana. Kama hukuweza kumvamia Lee jumatatu iliyopita, sehemu yenye usalama. Utawezaje kumvamia huko kusini ya mto, sehemu ambayo unaweza kwenda na si zaidi ya theluthi mbili ya jeshi lako? Haiingii akilini kutarajia, na wala sitarajii kama utakuwa na manufaa ya maana. Fursa nzuri ya kufanya hivyo imekwishapita, na hilo jambo limenikoseha amani kabisa.


Unafikiri Meade alifanya nini baada ya kusoma barua hiyo?

Meade hakupata barua hiyo. Lincoln hakuituma. Ilipatikana katika nyaraka zake baada ya kifo chake.
 
Mimi nadhani-na huku ni kudhani tu- kuwa baada ya kuandika barua ile. Lincoln alitazama nje kupitia dirishani na kujisemea, “Ngoja kwanza, labda sitakiwi kuwa na haraka hivi. Ni rahisi kwa mimi kukaa hapa katika usalama wa ikulu kumuamuru Meade avamie: lakini kama ningekuwepo Gettysburg, na kama ningeona umwagaji wa damu kama alioona Meade wiki iliyopita, na kama masikio yangu yangekuwa yamechomwa na vilio vya majeruhi na wanaokufa, pengine hata mimi nisingekuwa na mshawasha wa kuvamia. Vyovyote vile, yaliyopita si ndwele. Kama nikituma barua hii, itatuliza hisia zangu, lakini itamfanya Meade ajaribu kujitetea. itamfanya anishutumu. Itafanya kuwe na kinyongo kati yetu na na kufanya iwe ngumu kumtumia kama kamanda, na pengine itamfanya ajiuzulu toka jeshini.”

Kama nilivyokwisha sema, Lincoln aliiweka barua hiyo pembeni, alikuwa amekwishajifunza kwa uchungu kuwa shutuma kali na kusuta karibu mara zote huwa na mwisho mbaya.

Theodore Roosevelt aliwahi kusema kuwa alipokuwa anakabiliwa na jambo tata wakati alipokuwa rais, alikuwa akikaa na kuangalia picha kubwa ya Lincoln iliyokuwa imeningi’nizwa juu ya meza ofisini kwake kisha akajiuliza, “Kama Lincoln angekuwa kwenye viatu vyangu angetendaje? Angetatua vipi tatizo hili?”

Wakati ujao tukishawishika kumsuta mtu, tutoe noti ya dola tano kutoka mfukoni na kuangalia picha ya Lincoln kwenye noti hiyo na tujiulize. “Kama tatizo hili lingemkuta Lincoln, angeshughulika nalo namna gani?”

Mark Twain alikuwa ni mtu wa kulipuka hasira mara kwa mara, aliandika barua zenye maneno makali yaliyoweza kubadilisha rangi ya karatasi. Kwa mfano; kuna kipindi alimuandikia mtu aliyemuudhi maneno haya: “Jambo linalokufaa ni kibali cha mazishi yako tu. Sema nami nitahakikisha unakipata.” Wakati mwingine aliandika hivi kwa mhariri baada ya mtu anayehakiki habari kujaribu kurekebisha baadhi ya maneno aliyoandika. Alisema: “Acha hiyo kazi kama nilivyoiandika, na mwambie huyo uliyempa kazi ya kuhakiki abaki na maoni yake katika matope ya ubongo wake uliooza.”

Barua hizi kali zilimfanya Mark Twain ajihisi vizuri. Zilimfanya atoe dukuduku lake, lakini barua hizo hazikuwa na madhara yoyote sababu mke wake alizitoa zisitumwe kwa siri.

Je, unamfahamu mtu yeyote ambaye ungependa kumrekebisha na kumfanya awe bora? Vema! Hilo ni jambo zuri na naliunga mkono. Lakini kwanini usianze na wewe mwenyewe. Kwa mtazamo wa kibinafsi kabisa, hilo ni jambo lenye faida zaidi kuliko kutaka kufanya wengine wawe bora, na pia ni salama zaidi. Mwanafalsafa wa China, Confucius aliwahi kusema: “Usilalamike juu ya theluji iliyo juu ya paa la jirani yako wakati njia ya kuingia ndani kwako ni chafu.”

Nilipokuwa kijana, nilipokuwa najitahidi sana kukubalika na watu niliandika barua ya kipumbavu kwenda kwa bwana Richard Harding Davi, mwandishi ambaye kuna wakati alikuwa mtu mkubwa katika fasihi ya Marekani. Nilikuwa naandaa makala kuhusu waandishi na nilimuomba bwana Davis anieleze kuhusu mbinu za kazi zake. Wiki chache zilizopita nilikuwa nimepokea barua kutoka kwa mtu fulani ambayo mwishoni ilikuwa imeandika, “Maneno ni yangu, lakini barua hii sijaiandika wala kuihariri.” nilistaajabu sana, nilihisi muandishi atakuwa ni mtu mkubwa, na mwenye majukumu mengi sana.

Mimi sikuwa na majukumu yoyote ya kunitinga lakini nilitaka kuonekana wa maana kwa Richard Harding Davis, hivyo mwisho wa barua yangu niliandika: “Maneno ni yangu, lakini barua sijaiandika wala kuihariri.”

Hakujishughulisha na kujibu barua yangu. Badala yake aliirudisha ile niliyoandika chini yake akiwa ameandika: “Tabia yako mbaya inazidiwa ubaya na tabia yako tu.” Ni kweli nilikuwa nimefanya kosa kubwa, na pengine nilistahili kukosolewa. Lakini kwa sababu nami ni binadamu nilichukia hilo. Nilichukia kiasi kwamba nilipopata habari ya kifo cha Richard Harding Davi miaka kumi iliyofuata, kwa aibu nikiri kuwa kitu kilikilichokuwepo kichwani mwangu ni jinsi alivyoniumiza.

Kama mimi na wewe kesho tunataka kutengeneza chuki itakayodumu miongo na miongo mpaka kifo, basi tujihusishe na ukosoaji wenye kuumiza. Haijalishi tunaamini kiasi gani kuwa ukosoaji huo ni muhimu.

Tunaposhughulika na watu inatakiwa tuelewe kuwa hatushughuliki na kiumbe anayeongozwa na mantiki, bali anayeongozwa na hisia, kiumbe aliyeharaka katika kunyanyapaa, anayechochewa na majivuno na kujikweza.

Shutuma kali zilimfanya Thomas Hardy, moja ya waandishi bora kabisa wa fasihi ya kiingereza, kuachana kabisa na kazi ya kundika riwaya. Shutuma zilimfanya Thomas Chatterrton, mshairi wa kiingereza kujiua.

Wakati angali kijana, Benjamin Franklin hakuwa na ujuzi wowote wa maana, lakini baadaye akawa mwanadiplomasia mzuri na mtu mwenye uelewa sana wa jinsi ya kushughulika na watu, hata akafanywa kuwa balozi wa Marekani nchini Ufaransa. Siri ya mafanikio ? Alisema: “Sitamuongelea yoyote kwa ubaya, na nitaongelea mema yote ninayoyafahamu ya watu wote.”

Mpumbavu yoyote anaweza kushutumu, kulaumu na kuhukumu—na wapumbavu wengi hufanya hivyo. Lakini inahitaji uungwana wa hali ya juu kujizuia, kuwa muelewa na mwenye kusamehe.

Caryle aliwahi kusema: “Mtu mkuu huonyesha ukuu wake kwa jinsi anavyowatendea watu wa chini.”

Rubani maarufu na mshiriki wa mara kwa mara wa maonyesho ya anga, Bob Hoover alikuwa anarudi nyumbani kwake huko Los Angeles kutoka katika maonyesho ya anga huko San Diego. Kama habari yake ilivyoandikwa kwenye jarida Flight Operations, ilisemwa alipokuwa kimo cha futi mia tatu angani, injini zote ziliacha kufanya kazi. Kwa utaalamu wake aliweza kuitua ndege lakini iliharibika vibaya, japo hakuna aliyejeruhiwa.

Jambo la kwanza alilofanya Hoover baada ya kutua ni kuchunguza mafuta ya ndege. Kama alivyokuwa amehisi, ndege yake yenye injini ya mapanga, ya zama za vita ya pili ya dunia ilikuwa imewekewa mafuta ya ndege zenye injini ya jet badala ya petrol.

Aliporudi uwanja wa ndege akaomba kuonana na fundi aliyehudumia ndege yake. Fundi mwenyewe alikuwa kijana mdogo tu. Alikuwa amefadhaishwa sana na kosa lake. Machozi yalikuwa yakimtoka Hoover alipokuwa akimfuata. Alikuwa amesababisha uharibifu wa ndege ya gharama sana. Na alikuwa karibu kusababisha vifo vya watu watatu. Unaweza hisi hasira aliyokuwa nayo Hoover. Unaweza kudhania maneno makali ambayo rubani huyu makini na aliyejivuna angetoa juu ya uzembe ule. Lakini Hoover hakumsema fundi huyu wala hata hakumshutumu. Badala yake aliweka mkono wake kwenye bega la fundi yule na kusema, “Kuonyesha kuwa nina hakika hutarudia kufanya hivi tena, nataka kesho uhudumie ndege yangu aina ya F-51.”

Mara nyingi wazazi hushawishika kuwashutumu watoto wao. Labda unategemea niseme, “Wasifanye hivyo.” Hapana hata kidogo. Nitachosema ni kuwa, “Kabla ya kuwashutumu, wasome moja kati ya makala ya maana sana kuwahi kuandikwa na wanahabari wa Marekani, ‘Baba husahau.’ ”

Kwa mara ya kwanza iliandikwa katika gazeti People’s home Journal. Tutaiandika tena hapa kwa ruhusa ya muandishi, kama ilivyofupishwa kwenye jarida la Reader’s Digest.

“Baba husahau’ ni moja ya makala zinazohamsha hisia kwa wasomaji wengi sana kiasi kwamba inachapishwa kila mwaka. Toka ilipochapishwa kwa mara ya kwanza. “Baba husahau” imeandikwa tena na tena, anasema muandishi wake, W. Livingston Larned, “Imeandikwa kwenye mamia ya majarida, vipeperushi na magazeti nchini kote. Pia imeandikwa na kufasiriwa katika lugha nyingi sana. Nimetoa ruhusa kwa maelfu waliotaka waliotaka kuisoma wakiwa kanisani, shuleni au kumbi za mihadhara. Imetangazwa katika vipindi mbalimbali. Na hata vijarida vya vyuo na shule za upili vimeitumia



BABA HUSAHAU

W. Livingston Larned

Nisikilize mwana wangu: ninasema haya ukiwa umelala, kiganja kimoja kikiwa shavuni mwako na nywele zako zikiwa zimeng’ang’ania kwenye paji lako la uso. Nimeingia chumbani mwako peke yangu. Dakika chache zilizopita nilikuwa maktaba nikisoma gazeti. Wimbi la hisia likaniingia. Kwa kuhisi hatia, nikaja hapa pembeni ya kitanda chako.

Kuna mambo nilikuwa nikifikiria mwanangu: nimekuwa kauzu kwako. Nimekufokea unapokuwa akijiandaa kwenda shule. Sababu umejifuta tu kijuu juusoni kwa taulo. Nimekufokea kwa kutosafisha viatu vyako. Nimekupigia kelele unapotupa vitu vyako sakafuni.

Wakati wa kifungua kinywa nilikukosoa pia, ulimwaga vitu. Ulimeza chakula kwa sauti. Uliweka viwiko mezani. Ulijaza siagi kwenye mkate. Na ulipokuwa ukienda zako, nami nikielekea kituo cha garimoshi, uligeuka na kunipungia mkono na kusema, “Kwa heri baba!” Nami nilikasirika na kusema, “Simama kwa kunyooka!”

Kisha hayo yakajirudia tena jioni. Nilipokuwa nakuja nilikuona. Umepiga magoti ukicheza gololi. Suruali yako ilikuwa na matundu. Nilikudhalilisha mbele ya rafiki yako kwa kukuongoza kuingia ndani. Suruali ni gharama, kama ni wewe ungekua unanunua, ungekuwa makini nazo! Fikiria mwenyewe mwanagu, eti baba anaongea hayo!

Unakumbuka baadaye nilipokuwa nikisoma kwenye maktaba, jinsi ulivyokuja kwa uoga na macho yako yakionyesha kuna jambo linakutatiza? Nilipoacha kusoma na kukuangalia, nikiwa nimeudhika kwa kukatishwa, ulisita mlangoni. “Unataka nini?” Nilifoka.

Hukusema kitu, kwa hisia kali ulinikimbilia na kunikumbatia shingoni na kunibusu, mikono yako midogo ilinikumbatia kwa nguvu na hisia ambazo Mungu mwenyewe amezifanya zichanue ndani ya moyo wako. Hisia ambazo hata kupuuzwa hakuwezi kuzizima. Kisha ukawa umeondoka, ukipanda sauti ya kupanda kwako ngazi ikisikika.

Punde baada ya hapo gazeti lilinitoka mkononi, hofu kuu ilinijaa. Hii tabia imenifanya kuwa mtu wa aina gani? Tabia ya kutafuta makosa, tabia ya kushutumu—hiyo ndiyo zawadi yangu kwako kwa kuwa mwana wangu. Ni si kwamba sikupendi; ni sababu nilitarajia mambo mengi kutoka kwa kijana. Nilikupima kwa kutumia kipimo cha miaka yangu.

Ukweli ni kuwa kuna mengi ambayo ni mazuri katika tabia yako. Moyo wako japo mdogo, lakini ni mkuu kama machweo ya jua kwenye vilima. Hili lilionyeshwa na tendo lako la kunikimbilia, ukinibusu na kunitakia usiku mwema. Usiku wa leo sijali chochote mwanangu. Nimefika hapa pembeni ya kitanda chako, nimepiga magoti gizani, nikiwa nimejawa na aibu.

Ni ishara ya kujuta na kuomba msamaha; najua hutaelewa
mambo haya iwapo nitakuambia ukiwa macho. Lakini kesho nitakuwa baba hasa. Nitakuwa rafiki yako, nitateseka utesekapo na kucheka uchekapo. Nitauma ulimi wangu iwapo maneno ya kukosa subira yatanijia. Nitaendelea kusema kama vile ni sala: “Bado ni mvulana tu—mvulana mdogo.”

Nina wasiwasi kuwa nilikua nikikuchukulia kama mwanaume, lakini ninapokuona sasa, ukiwa umejikunja kitandani kwako, natambua kwamba bado ni mtoto mdogo. Jana tu ulikuwa katika mikono ya mama yako, umelaza kichwa chako begani mwake. Nimetaka mengi, mengi kupita kiasi.


Badala ya kushutumu na kuhukumu watu, acha kwanza tujaribu kuwaelewa. Tuelewe kwanza kwanini wanafanya yale wanayofanya. Hilo ni jambo lenye faida na linavutia kuliko kushutumu; nalo huzaa huruma, kuvumiliana na rehema. “Kujua yote ni kusamehe yote.”

Kama Dr. Johnson alivyowahi kusema: “Mungu mwenyewe hamhukumu mtu mpaka mwisho wa maisha yake.”

Kwanini mimi na wewe tuhukumu wengine?



KANUNI YA 1

Usishutumu, usihukumu wala usilalamike.
 
Pictuspublishers tumefasiri kitabu How to win friends and influence people. Kila wiki siku ya ijumaa tutasoma sehemu moja. Unaweza kusoma sehemu iliyofasiriwa ndani ya maktabaapp. kuungwa tucheki whatsapp 0715278384.

71vK0WVQ4rL.jpg


Muandishi: Dale Carnegie, 1936.
Mtafsiri: Pictus Publishers ltd
Email: pictuspublishers@gmail.com.
Pictus Publishers ltd2022.
Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli, kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.

MAPENDEKEZO TISA YA JINSI YA KUFAIDIKA NA KITABU HIKI

  • Kama unataka kufaidika vilivyo na kitabu hiki, kuna jambo moja la lazima. Ni la muhimu kuliko kanuni au mbinu yoyote ile. Bila hilo, kanuni elfu za jinsi ya kusoma na kufaidika hazitakuwa na msaada wa maana kwako. Kama unalo jambo hili, basi utafanya maajabu bila hata ya kusoma mapendekezo yoyote juu ya usomaji wenye faida.
  • Ni takwa gani hilo la ajabu? Ni hili: Tamaa kali ya kutaka kujifunza, nia hasa ya kutaka kuongeza uwezo wako wa kushughulika na watu.
  • Unawezaje kukuza tamaa hiyo? Kwa mara zote kujikumbusha jinsi ambavyo kanuni hizi ni muhimu kwako. Fikiria jinsi ambavyo kuzimudu kutafanya maisha yako yawe ya furaha na ya kuridhisha zaidi. Jiambie tena na tena, “Furaha yangu, kukubalika kwangu na thamani yangu kwa kiasi kikubwa kunategemea uwezo wangu wa kushughulika na watu.
  • Soma kila sura kwa haraka ili kupata wazo kuu. Pengine utashawishika kukimbilia sura nyingine. Usifanye hivyo—labda kama unasoma tu kujifurahisha. Lakini kama unasoma ili kuongeza uwezo wako kwenye mahusiano na binadamu wengine, rudi na usome kila sura kwa kina. Baada ya muda, hili litakuokolea muda na kukupatia matokeo.
  • Simama kusoma mara nyingi na tafakari kile ulichosoma. Jiulize ni jinsi gani na wapi unaweza kutumia mapendekezo yaliyotolewa.
  • Soma ukiwa na penseli, kalamu ya wino au ya rangi. Kama ukikutana na pendekezo ambalo unahisi unaweza kulitumia, chora mstari pembeni yake. Kama ni pendekezo lenye hadhi ya nyota nne, basi pigia mstari kila sentensi au liwekee alama “****.” Kuwekea kitabu alama au kukipigia mistari inafanya kivutie na iwe rahisi kurejelea.
  • Namfahamu mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni meneja wa kampuni ya bima kwa miaka kumi na mitano. Kila mwezi alisoma mikataba yote ya bima ambayo kampuni yake ilikuwa imeingia. Ndiyo, alisoma mikataba inayofanana tena na tena kila mwezi na mwezi, mwaka na mwaka. Kwa nini? Kwa sababu uzoefu ulikuwa umemuambia kuwa hiyo ndiyo njia pekee wa kuiweka vizuri akilini mwake.
  • Kuna wakati nilitumia miaka miwili kuandika kitabu juu ya kuzungumza na umati, lakini bado nilihitajika kurudi nyuma kuangalia nimeandika nini ndani ya kitabu change mwenyewe. Kasi ambayo tunasahau vitu inastaajabisha
  • Hivyo basi, kama unataka kupata faida ya kweli na kudumu kutoka katika kitabu hiki, usidhanie kuwa kukipitia tu mara moja kutatosha. Baada ya kukisoma chote, pengine utahitajika kukipitia kwa saa chache kila mwezi. Kiweke mezani pako kila siku. Kichungulie mara kwa mara. Endelea kuwazia juu maboresho mengi unayoweza kufikia. Kumbuka kuwa kanuni hizi zinaweza jengeka kuwa tabia kwa kuzirejelea na kuzitumia mara kwa mara tu. Hakuna njia nyingine.
  • Bernard Shaw amewahi kusema: “Kama ukimfundisha mtu jambo lolote lile, hatajifunza kamwe.” Shaw alikuwa sahihi. Kujifunza ni jambo linalohitaji kutenda. Tunajifunza kwa kufanya. Hivyo basi, kama nia yako ni kuzimudu kanuni unazosoma kwenye kitabu hiki, zifanyie kazi. Zitumie kwenye kila fursa unayopata. Usipofanya hivyo, utazisahau haraka sana.
  • Pengine utaona kuwa ni vigumu kutumia kanuni hizi kila wakati. Nafahamu, sababu ndiye nimeandika kitabu lakini bado mara nyingi napata ugumu kutumia kila pendekezo. Kwa mfano, unapokasirishwa, ni rahisi kushutumu na kulaani kuliko kujaribu kuelewa mtazamo wa mtu mwingine; mara nyingi ni rahisi kutafuta makosa kuliko kuliko kutafuta jambo la kupongeza; ni jambo la asili kuongea kuhusu unayotaka kuliko anayotaka mwingine nk. Kwa hiyo unavyosoma kitabu hiki, kumbuka kuwa hujaribu tu kupata habari. Unajaribu kujenga tabia mpya. Ndiyo, unajaribu aina mpya ya maisha. Jambo hilo litahitaji bidii, muda na kutumia kila siku yale uliyojifunza.
  • Basi rejelea kurasa hizi mara kwa mara. Chukulia kitabu hiki kama maelekezo ya kila siku juu ya mahusiano wa binadamu. Na kila unapokutana na tatizo fulani—kama kushughulika na mtoto, kumfanya mwenzi wako aunge mkono wazo lako au kumridhisha mteja mwenye hasira—jizuie kufanya jambo la asili, jambo linaloongozwa na hisia. Jambo ambalo huwa si sahihi. Badala yake, rudi kwenye kurasa hizi na rejea kwenye aya ulizopigia mistari. Jaribu kutumia mbinu hizi na angalia zinapokutendea maajabu.
  • Mpatie mwenzi wako, mtoto wako au mfanyakazi mwenzako senti kumi kila mara anapokukuta ukikiuka kanuni fulani. Fanya kuzimudu kanuni hizi iwe burudani.
  • Rais wa benki moja maarufu ya huko Wall Street aliwahi eleza, mbele ya moja ya darasa langu juu ya mfumo wenye ufanisi sana aliotumia kuboresha utu wake. Mtu huyu alipata elimu kidogo tu, lakini aliweza kuwa mmoja wa wasimamizi wa fedha muhimu sana katika Marekani, na alikiri kuwa sehemu kubwa ya mafanikio yake ni sababu ya mfumo huo alioubuni. Hiki ndicho alichofanya, nitaelezea kama alivyosema kadri ninavyokumbuka.
“Kwa miaka mingi nimekuwa na kitabu kinachoonyesha miadi niliyokuwa nayo siku hiyo. Familia yangu haikunipangia jambo lolote jioni ya jumamosi, maana walifahamu kuwa nilitumia jioni ya jumamosi kujitathmini. Baada ya chakula cha jioni nilienda sehemu yap eke yangu, nilifungua kitabu cha miadi na kutafakari juu ya mikutano yote, mahojiano na usaili uliotokea kwenye juma zima. Nilijiuliza:

“Kosa gani nilifanya wakati ule?”

“Kitu gani nilifanya sawa—na kwa namna gani ningeweza kuboresha mambo?”

“Ni somo gani ninapata kutokana na mambo yaliyotokea?”

“Mara nyingi kujitatmini huku kulinifanya nifedheheke sana. Mara nyingi nilistaajabishwa na makosa yangu ya kizembe. Lakini kadri miaka ilivyozidi kwenda makosa haya yakaanza kupungua. Ikafika wakati nilitaka hata kujipongeza mwenye baada ya kumaliza kujitathmini. Kujitathmini huku na kujielimisha kuliendelea mwaka hata mwaka. Kumenisaidia kuliko jambo lolote lile nililowahi kufanya.

“Kulinisaidia kuongeza uwezo wangu wa kufanya maamuzi—na kulinisaidia sana katika kushughulika kwangu na watu. Napendekeza sana matumizi ya mbinu hiyo.”

Kwa nini usitumie mfumo kama huo kuangalia jinsi unavyotumia kanuni zilizomo ndani ya kitabu hiki? Kama ukifanya hivyo, mambo mawili yatatokea.

Kwanza, utajikuta unapata elimu kwa njia ambayo ni bora na ya kufurahisha.

Pili, uwezo wako wa kukutana na kushugulika na watu utaboreka sana.

Mwishoni mwa kitabu hiki utakutana na kurasa tupu, humo unaweza kuandika mafanikio yako katika kutumia kanuni zilizoandikwa humu. Andika kwa kina, andika tarehe, majina, matokeo. Kutunza kumbukumbu hizo kutakusukuma kufanya bidii hata zaidi; na jinsi zitakavyokufurahisha taarifa hizo ikitokea umeziona jioni moja miaka kadhaa mbele!

Ili kufaidika na kitabu hiki:

  • Jenga tamaa kali ya kumudu kanuni za mahusiano ya binadamu.
  • Soma kila sura mara mbili kabla ya kwenda inayofuata.
  • Unaposoma, simama mara nyingi na kujiuliza ni jinsi gani unaweza kutumia kila pendekezo.
  • Pigia mstari kila wazo muhimu.
  • Rejelea kitabu hiki kila mwezi.
  • Tumia kanuni hizi kila upatapo fursa. Tumia kitabu hiki katika kutatua matatizo yako ya kila siku.
  • Fanya kujifunza kuwe burudani kwa kumpatia rafiki yako senti kumi, au dola moja kila mara anapokukuta ukikiuka moja ya kanuni hizi.
  • Andika kumbukumbu nyuma ya kitabu hiki kuonyesha ni lini na kwa namna gani ulitumia kanuni hizi.
Salute kwako ndugu!
 
2

SIRI KUBWA YA JINSI YA KUSHUGHULIKA NA WATU

Kuna njia moja tu chini ya mbingu ya kumfanya mtu kufanya jambo lolote. Umewahi kaa na kufikiria kuhusu hilo? Ndiyo, ipo njia moja tu. Nayo ni kumfanya mtu huyo atake mwenyewe kufanya jambo hilo.

Kumbuka kuwa hakuna njia nyingine.

Ni kweli kuwa unaweza mfanya mtu akupe saa yake kwa kumuwekea bastola ubavuni. Unaweza kuwafanya wafanyakazi wako mpaka pale utakapo wapa mgongo kwa kuwatishia kuwafukuza kazi. Unaweza kumfanya mtoto afanye kile unachotaka kwa vitisho au fimbo. Lakini njia hizi za mabavu zina matokea mabaya.

Njia pekee ya kukufanya ufanye kitu chochote ni kwa kukupatia kile unachotaka.

Unataka nini?

Mwanasaikolojia Sigmund Freud alisema kuwa vitu vyote ambavyo mimi na wewe tunafanya vinachochewa na mambo mawili: Tamaa ya ngono na tamaa ya kuwa wakuu.

Mmoja kati ya wanafalsafa maarufu nchini Marekani, John Dewey alisema jambo hilohilo, kwa namna tofauti kidogo. Dr Dewey alisema kuwa tamaa kubwa kabisa ya binadamu ni “Tamaa ya kujihisi una umuhimu.” Kumbuka sentensi hiyo: “Tamaa ya kujihisi una umuhimu.” Ni ya muhimu. Utaiona mara nyingi sana ndani ya kitabu hiki.

Unataka nini? Si vitu vingi, ni vichache tu. Lakini vitu hivyo vichache unavyotaka unavitafuta kwa nguvu na bidii sana. Baadhi ya vitu ambavyo watu wanataka ni pamoja na:

  • Afya na kuwa hai
  • Chakula
  • Kulala
  • Pesa na vitu ambavyo pesa hununua
  • Maisha baada ya kifo
  • Kutimiziwa tamaa ya ngono
  • Maisha bora kwa watoto wetu
  • Kujihisi una umuhimu
Karibu matakwa yote haya huwa yanatimizwa kwa ukawaida isipokuwa takwa moja. Nalo ni muhimu na karibu linaweza kufanana na takwa la chakula au kulala, lakini linatimizwa mara chache sana. Ni takwa ambalo Freud aliliita “Tamaa ya kuwa mkuu.” Ni hilo ambalo Dewey aliliita “Tamaa ya kujihisi una umuhimu.”

Kuna barua Lincoln alianza kwa kuandika: “Kila mtu anapenda kupongezwa.” William James aliwahi kusema: “Kanuni kuu katika silka ya binadamu ni njaa ya kuthaminiwa.”

Kumbuka kuwa hakuzungumzia “Tamaa” au “Takwa” ya kuthaminiwa. Alisema “Njaa” ya kuthaminiwa.

Akimaanisha kuna njaa inayouma bila kikomo, na mtu adimu ambaye anaweza kuikomesha njaa hii bila unafiki, atawaweka watu wengine kiganjani mwake na “Hata malaika wa kifo atahuzunikia kifo chake.”

Tamaa ya kuhisi una umuhimu ni moja ya tofauti kuu kati ya binadamu na wanyama. Kwa mfano: Nilipokuwa kijana nikifanya kazi za shamba huko Missouri, baba yangu alikuwa akizalisha nguruwe bora aina ya Duroc-Jersey na ng’ombe weupe wazuri. Tulikuwa tukiwapeleka nguruwe na ng’ombe hao kwenye maonyesho ya kilimo huko Magharibi ya Kati. tulishinda nafasi ya kwanza mara nyingi. Baba yangu aliweka medali zake kwenye kitambaa cheupe. Marafiki au wageni walipokuja kututembelea, baba alitoa kitambaa hicho kirefu na kukikunjua. Alishika upande mmoja nami nilishika mwingine tukionyesha medali hizo.

Nguruwe hawakujali juu ya tuzo walizoshinda. Lakini baba yangu alijali. Tuzo zile zilifanya ajihisi ana umuhimu.

Kama mababu zetu wa kale wangekuwa hawana tamaa hii ya kujihisi wana umuhimu, isingewezekana kufikia ustaarabu na maendeleo. Bila tamaa hiyo tungekuwa kama wanyama tu.

Ni tamaa hii ya kujihisi una umuhimu ndiyo inamfanya karani wa duka maskini na asiye na elimu kusoma vitabu vya sheria alivyovipata kwenye rundo la vitu vya zamani alilonunua kwa senti hamsini. pengine umewahi sikia kuhusu karani huyo. Jina lake aliitwa Lincoln.

Ilikuwa ni tamaa yake ya kujihisi ana umuhimu ndiyo iliyomchochea muandishi Charles Dickens kuandika riwaya zake maarufu. Tamaa hii ndiyo ilimfanya msanifu majengo, bwana Christopher Wren kufanya kazi bora kabisa. Tamaa hii ndiyo ilimfanya Rockefeller kujilimbikizia mamilioni ya pesa ambazo hata hakuzitumia! Na tamaa hii ndiyo inaifanya familia tajiri katika mji wako kujenga nyumba kubwa kuliko mahitaji yao. Tamaa hii ndiyo inakufanya utake kuvaa mitindo mipya kabisa ya mavazi, kuendesha gari la kisasa, na kuongelea jinsi watoto wako walivyo na akili.

Ni tamaa hii ndiyo inayowaongoza vijana wa kiume na wa kike kujiunga katika magenge ya kihalifu. Aliyewahi kuwa mkuu wa pilisi wa jiji la New York, E. P. Mulrooney aliwahi sema kuwa, kwa wastani, wahalifu vijana huwa wamejaa na majivuno, na ombi lao la kwanza baada ya kukamatwa ni kuomba gazeti ambalo limemuandika kama shujaa. Jambo la kufungwa huonekana kuwa mbali na akili yao kadri wanavyoweza kujisifu kwa picha zao kuwa gazetini na wanamichezo, waigizaji wa filamu na wanasiasa.

Kama ukiniambia jinsi unavyopata hisia za kuwa na umuhimu, nitakuambia wewe ni mtu wa namna gani. Jambo hilo ndilo linaonyesha tabia yako. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi kukuhusu. Kwa mfano, John D. Rockefeller alipata hisia za kuwa yeye ni muhimu kwa kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya kisasa huko Peking, China. Hospitali itakayohudumia mamilioni ya watu maskini ambao hawajawahi kuwaona wala hangeweza kuwahi kuwaona. Kwa upande mwingine, Dillinger alipata hisia za kuwa yeye ni wa muhimu Kwa kuwa jambazi, mpora benki na muuaji. Maafisa wa FBI walipokuwa wanamtafuta, aliingia kwenye nyumba moja ya mashambani huko Minnesota na kusema, “Mimi ndiye Dillinger!” aliona fahari kuwa mtu anayetafutwa sana na vyombo vya dola. Alisema, “Sitawadhuru, lakini mimi ndiye Dillinger!”

Tofauti moja ya muhimu kati ya Dillinger na Rockefeller ni jinsi walivyopata hisia za kujiona ni watu wa maana. Historia imejaa mifano ya watu maarufu waliohangaika ili kupata hisia za kujiona kuwa wao ni watu wa maana. Hata George Washington alitaka aitwe “Mtukufu rais wa Marekani”; na Columbus alishawishi aitwe: jemedari wa bahari na liwali wa India.” Catherine Mkuu alikuwa akikataa kufungua barua ambazo hazikuandikwa, “Kwenda kwa mtukufu mtawala.” Na mke wa Lincoln kuna kipindi ndani ya ikulu ya Marekani alimfokea mke wa Grant kwa ukali, “Unawezaje kukaa kabla sijakwambia ukae!”

Matajiri walimpatia besa jemedari Byrd kwenda kufanya utafiti katika bara la Antarctic mwaka 1928 kwa makubaliano kuwa safu za milima barani humo zitapewa majina yao. Na Victor Hugo hakutaka chochote zaidi ya mji wa Paris kupewa jina lake. Hata Shakespeare, mkuu wa wakuu alijaribu kulikweza jina lake kwa kununua nembo ya familia

Muda mwingine watu hufanya mambo ya aibu ili kupata huruma na hisia za kuonekana kuwa wana umuhimu. Mke wa McKinley alipata hisia za kuwa yeye ni wa muhimu kwa kumlazimisha mume wake, Rais wa Marekani kupuuza mambo ya msingi ya taifa na kukaa kitandani tu pamoja naye. Muda mwingine kwa masaa kadhaa, akiwa amemkumbatia na kumbembeleza hadi alale. Alitimiza tamaa yake hiyo kwa kumsisitiza amsubiri alipokuwa akirekebishwa meno yake, na kuna wakati alizua tafrani kubwa baada ya bwana wake kutaka kumuacha kwa daktari wa meno ili kuwahi miadi muhimu na waziri wa mambo ya ndani, John Hay.

Muandishi, Mary Roberts Rinehart amewahi kunisimulia kisa cha kijana mmoja mwanamkea mwenye akili, mbaye ili kupata hisia za kujiona ana umuhimu alifanya mambo ya kushangaza sana. Alisema kuwa, “Siku moja mwanamke huyo alilazimika kukubaliana na ukweli fulani, labda miaka yake. Miaka yake ilikuwa imeenda na matarajio yake yalizidi kudidimia. Akajidai ni mgonjwa wa kulala tu. Kwa miaka kumi mama yake alipanda na kushuka ngazi akimhudumia. Siku moja, mama yule mzee kwa kuchoka alifariki. Kwa majuma kadhaa mwanamke yule aliendelea na mtindo wake wa maisha, lakini mwishowe aliamka, alivaa nguo na kuanza kuishi tena.”

Baadhi ya mamlaka zinasema kuwa watu wanaweza kupatwa na kichaa ili kuingia kwenye ulimwengu wa kuwaziwa, na kupata hisia za kuwa wao ni wa maana ambazo hawakuzipata katika ulimwengu halisi. Kwa Marekani, wagonjwa wa akili ni wengi kuliko wagonjwa wote wa magonjwa mengine wakijumlishwa.

Ni nini kinasababisha hali hiyo?

Hakuna mtu anaweza kujibu swali hilo, lakini tunajua kuwa baadhi ya magonjwa kama kaswende huharibu seli za ubongo na kusababisha kichaa. Karibu nusu ya magonjwa yote ya akili husababishwa na athari kama hiyo kwenye ubongo, sumu, majeraha kwenye ubongo, maambukizi na pombe. Lakini nusu nyingine, nusu ya watu wanaopata magonjwa ya akili huwa hawana tatizo lolote katika seli za ubongo. Wakati wa uchunguzi baada ya kufa, pale ambapo hadubini zenye nguvu zinapotumika kuchunguza ubongo wao, huonyesha kuwa ubongo una afya kama wangu na wako tu. Sasa kwa nini watu hawa hupata kichaa?

Nilimuuliza swali hili daktari wa moja ya hospitali maarufu ya magonjwa ya akili katika nchi yetu. Daktari huyu, ambaye amewahi kupata tuzo ya juu kabisa katika eneo la afya ya akili aliniambia kuwa hafahamu kwa nini watu huwa vichaa. Alisema kuwa hamna mtu anayejua kwa uhakika, lakini watu wengi ambao hupatwa na kichaa, katika kichaa chao wanapata hisia za kwamba wao ni watu wa muhimu, hisia ambazo hawakuzipata walipokuwa na akili timamu. Kisha alinisimulia hadithi ifuatayo:

“Kwa sasa nina mgonjwa ambaye ndoa yake ilikumbwa na matatizo. Alikuwa anataka kupendwa, kutimiziwa tamaa ya ngono, kupata watoto na kuwa mtu wa kuheshimika katika jamii. Lakini maisha hayakuwa kama alivyotarajia. Mume wake hakumpenda. Na hata alikataa kula naye, akimwambia ampelekee chakula chake chumbani kwake ghorofani. Hakuwa na watoto wala heshima yoyote katika jamii. Alipatwa na kichaa; na katika mawazo yake, alikuwa anaona kuwa amemtaliki mume wake, na ameachana na jina la mumewe. Sasa anaamini ameolewa katika familia ya kifalme ya Uingereza na anasisitiza kuitwa Bibi Smith.

“Na kuhusu watoto, anadhani kwamba anazaa mtoto kila usiku. Kila mara ninapomwita husema: ‘Daktari, jana usiku nilijifungua mtoto.’ “

Maisha yamevunja meli zake zote za ndotoni kwenye mwamba wa uhalisia; lakini katika kisiwa kizuri cha ukichaa, mashua zake zote zinakimbia kuelekea bandarini huku tanga zikipepea kwa upepo.

“Inahuzunisha? Oh, sifahamu.” Daktari wake aliniambia: “Kama ningeweza kumtibu kichaa chake, nisingefanya hivyo. Anafuraha hivyo alivyo.”

Kama baadhi ya watu wana njaa ya kuhisi wao ni muhimu hadi wanakuwa vichaa, wazia muujiza ambao mimi na wewe tunaweza kufanya kwa kuwaonyesha watu kuwa wana umuhimu watu bila ya unafiki.

Mmoja kati ya wamarekani wa kwanza kulipwa mshahara wa zaidi ya dola milioni moja kwa mwaka(wakati ambapo kulikuwa hakuna kodi ya makato. Na mtu aliyepata dola hamsini kwa wiki alionekana yuko vizuri) alikuwa ni Charles Schwab, mwaka 1921 alikuwa amewekwa na Andrew Carnegie kuwa rais wa kwanza wa kampuni mpya ya United States Steel Company. Wakati huo Schwab alikuwa na miaka thelathini na nane tu. (Baadaye Schwab aliondoka U. S. Steel na kwenda kuongoza kampuni iliyokuwa inatetereka ya Bethlehem Steel company, na alifanikiwa kuijenga upya na kuifanya kuwa moja ya makumpuni yanayoingiza faida kubwa katika Marekani )

Kwa nini Andrew Carnegie alimlipa Charles Schwab dola milioni moja kwa mwaka, au zaidi ya dola elfu tatu kwa siku? Kwa nini? Kwa sababu Schwab alikuwa na akili nyingi? Hapana. Kwa sababu alijua kutengeneza chuma kuliko watu wengine? Upuuzi. Charles Schwab aliwahi kuniambia yeye mwenyewe kuwa alikuwa na watu wengi chini yake waliokuwa wanajua habari ya kutengeneza chuma kuliko yeye. Schwab alisema kuwa analipwa mshahara huo mkubwa sababu ya uwezo wake wa kushughulika na watu. Nilimuuliza anafanyaje hivyo. Hii ndiyo siri yake kwa maneno yake mwenyewe—maneno ambayo yanatakiwa kutengenezwa kwa shaba na kutundikwa katika kila nyumba, shule, kila duka na ofisi nchini kote—maneno ambayo watoto wanatakiwa kuyakariri badala ya kupoteza muda wao wakikariri misamiati ya Kilatini au kiasi cha mvua kinachonyesha kwa mwaka huko Brazil—maneno ambayo yatabadilisha maisha yangu na yako iwapo tutayatumia maishani:

“Nachukulia uwezo wangu wa kuhamaisha watu kama kitu cha thamani kabisa nilichonacho,” alisema Schwab. “Na njia ya kuwafanya watu wakuze ubora ulio ndani yao ni kwa kuwathamini na kuwatia moyo.”

“Hakuna kitu kingine kinachoua ari ya mtu kama kuchambuliwa-chambuliwa na wakubwa zake. Kamwe simchambui-chambui yeyote. Naamini katika kumpa mtu motisha ya kufanya kazi. Kwa hiyo muda wote nina shauku ya kupongeza lakini nachukia kupata makosa. Nikisema nijielezee, Nina moyo wa kuthamini na ni tajiri wa pongezi.”

Hivyo ndivyo alivyofanya Schwab. Lakini watu wa kawaida hufanya nini? Kinyume chake kabisa. Kama hawajapenda kitu huwafokea walio chini yao; na kama wakipendezwa nacho hawasemi chochote. Ni kama mstari fulani wa shairi la zamani unavyosema: “Nilipokosea mara moja, nilisemwa siku zote/nilipofanya vizuri mara mbili, sikusikia kitu kamwe.”

Schwab aliendelea kusema, “Katika maisha yangu ya kuchangamana na watu wengi wenye vyeo na maarufu sehemu mbalimbali duniani, bado sijaona mtu, haijalishi cheo chake, ambaye hafanyi kazi yake vizuri na anayetia bidii kubwa pale anapothaminiwa—kuliko vile angefanya chini ya shutuma na kuchambuliwa-chambuliwa.”

Alisema hiyo ndiyo moja ya sababu iliyomfanya Andrew Carnegie kuwa na mafanikio makubwa aliyopata. Carnegie aliwapongeza washirika wake mbele za watu na katika faragha. Carnegie alitaka kuwapongeza wasaidizi wake hata kwenye jiwe la kaburi lake. Aliandika maneno ya kuandikwa kwenye jiwe hilo yakisema: “Hapa amelala mtu aliyejua jinsi ya kuzungukwa na watu waliokuwa na akili kuliko yeye.”

Kuthamini bila unafiki ilikuwa ni moja ya siri yaliyomuwezesha John D. Rockefeller kushughulika na watu kwa mafanikio. Mfano; mmoja wa washirika wake, Edward T. Bedford alipopoteza mamilioni ya pesa za kampuni baada ya kufanya manunuzi ya hovyo huko Amerika ya kusini, John D angeweza kumshutumu vikali; lakini alijua kuwa Bedford alijitahidi kufanya vizuri kadri awezavyo—jambo hilo likaishia hapo. Kwa hiyo Rockefeller alitafuta jambo la kupongeza; alimpongeza Bedford kwa sababu aliweza kuokoa asilimia 60 ya pesa alizowekeza. “Kazi nzuri.” Alisema Rockefeller. “Hata huku kwenye uongo si mara zote tunafanya vizuri hivyo.”
 
Katika makabrasha yangu nina kisa kimoja ambacho najua hakikuwahi kutokea, lakini inaongelea jambo la kweli hivyo nitakirudia hapa:

Kulingana na kisa hiki cha ajabu, mwanamke mmoja mkulima, baada ya kazi ngumu za shambani akawatengea jamaa zake rundo la nyai kama chakula. Wanaume walipomuuliza kama amepatwa na kichaa, akawajibu: “Kwa nini, ningejuaje kama mtagundua? Nimekuwa nikiwapikia kwa miaka ishirini iliyopita na katika muda wote huo sijasikia neno lolote la kunifanya nijue kuwa mlikuwa hamli nyasi.”

Kuna utafiti kuhusu wake waliokimbia waume zao ulifanyika miaka michache iliyopita, unafikiri ni sababu gani kubwa iliyosababisha wake kukimbia iligunduliwa? “ Ilikuwa kutothaminiwa.”

Na naamini kuwa kama utafiti kama huo ukifanywa juu ya waume wanaokimbia wake zao, sababu itakuwa hiyohiyo. Mara nyingi ‘tunawachukulia poa’ wenza wetu kiasi kwamba hatuwafanyi wajue kuwa tunawathamini.

Mshirika mmoja wa madarasa yetu alisimulia kuhusu jambo lililoombwa na mke wake. Mke wake na baadhi ya wanawake kanisani kwake walikuwa wanafanya zoezi la kuboresha utu wao. Alimuomba mume wake amsaidie kwa kumtajia vitu sita ambavyo anaamini akivifanya vitamfanya kuwa mke bora. Mume yule alisema darasani: “Nilishangazwa sana na ombi lile. Ukweli ingekuwa ni rahisi kwangu kuorodhesha mambo sita anayotakiwa kuboresha ili kuwa mke bora. Nina hakika angeweza kuorodhosha mambo elfu ninayotakiwa kuboresha. Lakini sikuorodhesha, nilisema: ‘Acha niyafikirie na nitakupa jibu asubuhi.’

“Asubuhi iliyofuata nilimpigia simu muuza maua na kumuambia atume maua waridi sita kwa mke wangu yakiwa na ujumbe usemao: ‘Sijaona mambo sita ambayo ningependa ubadilike. Nakupenda jinsi ulivyo.’

“Jioni niliporudi nyumbani unafikiri ni nani alikuwepo mlangoni kunipokea: bila shaka! Mke wangu alikuwa mlangoni machozi yamemlengalenga. Nilishukuru kuwa sikumchambua-chambua kama alivyoomba.

“Jumapili iliyofuata, mara baada ya kuwaeleza matokeo ya zoezi lake, wanawake kadhaa ambao alijifunza nao walinifuata na kuniambia, ’Ulilofanya ni jambo la kiungwana kabisa kuwahi kusikia.’ Hapo ndipo nilipogundua nguvu ya kuthamini wengine.”

Florenz Ziegfeld alikuwa ni mtayarishaji hodari kabisa katika historia ya sanaa ya maigizo, alipata umaarufu mkubwa kwa uwezo wake wa ‘kumheshimisha msichana wa Marekani.’ Mara nyingi alikuwa akichukua wasichana wa kawaida na kuwafanya kuwa waigizaji wakubwa. Akitambua nguvu ya kuthaminiwa na kujiamini, aliwafanya wanawake wajihisi warembo kwa uungwana wake na kuonyesha kujali kwake. Hakuwa mtu wa maneno matupua: alipandisha mshahara wa wasichana waimba kwaya kutoka dola thelathini kwa wiki hadi dola mia moja na sabini na tano. Mara nyingi aliwatumia waigizaji jumbe za telegrams na kuwapa maua waridi waimbaji wote.

Kuna kipindi nilipatwa na ‘mzuka wa kufunga’, nilifunga kwa siku sita, usiku na mchana bila kula, haikuwa vigumu. Mwishoni mwa siku ya sita njaa haikuwa kali kama mwishoni mwa siku ya pili. Laki ninafahamu, na najua nawe unafahamu watu ambao watahisi wana hatia iwapo watafanya familia zao au wafanyakazi wao kukaa siku sita bila chakula, lakini watu hao hao wanaweza kukaa siku sita, wiki sita na mara nyingine hata miaka sitini bila kuwaonyesha kuwa wanawathamini, kitu ambacho wanakihitaji sana kama tu chakula.

Mmoja wa wa waigizaji wakubwa wa wakati wake, Alfred Lunt, alipocheza kama muigizaji mkuu kwenye filamu ya Reunion in Vienna alisema: “Hakuna kitu nahitaji sana kama virutubisho vya kunifanya nijiamini na kujithamini.”

Tunarutubisha miili ya watoto wetu, rafiki zetu na wafanyakazi wetu, lakini ni mara ngapi tunawapa virutubisho vya kuwafanya wajiamini na kujithamini? Tunawapatia chipsi na nyama choma kuongeza nguvu, lakini tunapuuzia kuwapa maneno mazuri ya kuonyesha tunawathamini, maneno yatakayoimba masikioni mwao miaka na miaka kama mziki wa nyota za asubuhi.

Paul Harvey, katika kipindi chake cha redio, “Hadithi kamili,” alisema jinsi ambavyo kuonyesha uthamini kunavyoweza badilisha maisha ya mtu. Alisema kuwa miaka kadhaa iliyopita mwalimu mmoja huko Detroit alimuomba Stevie Morris amsaidie kutafuta Panya aliyekuwa amepotea darasani. Ukiangalia utaona kuwa alikuwa anathamini karama alizojaaliwa nazo Stevie, ambazo hakuna mwingine darasani mule aliyekuwa nazo. Stevie alikuwa na uwezo mkubwa wa kusikia, pengine ili kufidia upofu wake. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Stevie kuonyeshwa kuthaminiwa sababu ya uwezo wa masikio yake. Miaka mingi baadaye Stevie alisema kuwa kitendo hicho cha kuthaminiwa ilikuwa ndiyo mwanzo wa maisha mapya. Kutoka hapo alizidi kukuza kipaji chake na baadaye kuja kujulikana kama Stevie Wonder, moja kati ya waimbaji na waandishi wakubwa wa muziki wa pop katika miaka ya sabini.

Kuna baadhi ya watu muda huu wanaposoma hii mistari watakuwa: “Oh, sifa za kinafiki! Kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Nimejaribu hiyo mbinu. Haifanyi kazi—si kwa kwa watu werevu.” Ni kweli kuwa sifa za kinafiki hazifanyi kazi dhidi ya watu werevu. Ni dalili ya ubinafsi, utapeli na uzembe. Kitu cha hivyo lazima kifeli, na mara nyingi zinafeli. Ni kweli kuwa kuna watu wana hamu sana ya kusifiwa na kukubalika kiasi kwamba wako tayari kumeza sifa zozote zile, kama tu mtu mwenye njaa kali anavyoweza kula nyasi na minyoo.

Hata Malkia Victoria wa Uingereza aliathirika na sifa za kinafiki. Waziri mkuu wake, Benjamini Disraeli alikiri kuwa alitumia sana aliposhughulika naye. Kwa maneno yake mwenyewe alisema, “Nilizisambaza kama kwa mwiko wa kujengea.“ Lakini Disraeli alikuwa ni moja ya watu werevu na wajanja sana waliowahi kutawala himaya ya Uingereza. Alikuwa anaijua kazi yake barabara. Hivyo, kwa sababu mbinu hiyo ilifanikiwa kwake haimaanishi itafanikiwa kwangu mimi na wewe. Na baada ya muda mrefu, sifa za kinafiki zina madhara kuliko faida. Sifa za unafiki ni kitu bandia, na kama pesa bandia, mwishowe zitakutia matatani kama ukizipeleka kwa mwingine.

Ni nini tofauti ya sifa za kweli au kuthamini kikweli na sifa za kinafiki? Swali hilo ni rahisi. Kimoja kinatoka moyoni na kingine ni kujifanya tu; kimoja kinatoka moyoni na kingine kinatoka mdomoni; kimoja kinatokana na ubinafsi na kingine sivyo. Kimoja kinakubalika na watu wote, na kingine kinashutumiwa na kila mtu.

Hivi karibuni nimeona sanamu ya kichwa cha jenerali shujaa wa Mexico, Alvaro Obregon katika ikulu ya Chapultepec huko katika jiji la Mexico. Chini ya sanamu hiyo yameandikwa maneno ya busara yanayoonyesha falsafa ya Obregon: “Usiogope adui zako wanaokushambulia. Ugopa marafiki wanaokupa sifa za unafiki.”

Kwahiyo basi, sizungumzii kabisa kuhusu sifa za kinafiki! Badala yake nazungumza kinyume chake. Naongelea kuhusu namna mpya ya maisha. Naomba kurudia. Nazungumza juu ya namna mpya ya maisha.

Mfalme George V alikuwa na kanuni sita ambazo alizibandika ukutani katika maktaba yake ndani ya ikulu ya Buckingham. Moja ya kanuni hizo ilisema: “Nifundishe kutotoa wala kupokea sifa za kunipamba.” Zifa za kupamba ndizo hizo sifa za kinafiki. Tafsiri inasema kuwa sifa za kinafiki ni kumwambia mtu vile vilevile anavyofikiri kujihusu.”

“Tumia lugha yoyote upendayo,” alisema Ralph Waldo Emerson, “Kamwe huwezi sema chochote tofauti na ulivyo.”

Iwapo kitu ambacho tunatakiwa kufanya kingekuwa ni kutoa sifa za kinafiki tu, kila mtu angeanza kufanya hivyo, na watu wote tungekuwa manguli wa mahusiano ya binadamu.

Iwapo hatufikiri juu ya jambo fulani hususa, kawaida huwa tunatumia asilimi 95 ya muda tukiwaza kujihusu. Iwapo tukiacha kufikiria kujihusu na kuangalia mambo kwa mtazamo wa mwingine, hatutafikia kutoa sifa za kinafiki. Sifa ambazo ni za kitapeli na duni kiasi kwamba zinagundulika hata kabla ya kutoka mdomoni.

Moja ya vitu ambavyo tunapuuuza katika maisha yetu ya kila siku ni kuonyesha uthamini. Kwa namna fulani tunapuuza kuwapongeza watoto wetu pale wanapofanya vizuri shuleni, tunashindwa kuwatia moyo wanapofanikiwa kuoka keki au kujenga kijumba cha ndege. Hakuna kitu kinawafurahisha watoto kama jambo la kukubaliwa na kupongezwa na wazazi wao.

Wakati ujao ukifurahia nyama choma, jaribu kumpongeza mpishi kuwa amepika vyema, na muuzaji aliyechoka anapokuonyesha uungwana, mpongeze kwa hilo.

Mhubiri yeyote, mhadhiri au mtu yoyote anayeongea kwenye hadhara anajua jinsi inavyokatisha tama kujitoa kwa hadhara ambayo haitoi maoni yoyote ya kutia moyo. Kama jambo hilo lina ugumu kwa wataalamu, ni gumu hata zaidi kwa wafanyakazi ofisini, viwandani na kwa ndugu na marafiki. Tunaposhirikiana na wengine yatupasa kukumbuka kuwa, washirika wetu wote ni binadamu hivyo wana njaa ya kukubalika. Ni kitu cha asili kwa nafsi zetu kufurahia.

Jaribu kuacha alama na cheche za urafiki katika shughuli zako za kila siku. Utashangaa jinsi zitakavyowasha moto wa urafiki ambao utakuwa moto mkubwa sana mtakapokutana kwa mara ya pili.

Mkazi mmoja wa New Fairfield huko Connecticut aitwaye Pamela Dunham alikuwa na majukumu mengi sana. Moja ya majukumu hayo ilikuwa ni kumsimamia mfanya usafi ambaye alikuwa anafanya kazi hovyo sana. Wafanyakazi wengine walimsema na kuchafua korido makusudi kumuonyesha ni jinsi gani alikuwa akifanya kazi yake vibaya. Hali haikuwa nzuri, muda mwingi wa kazi ulikuwa ukipotea.

Pam alijaribu njia mbalimbali kumchochea mfanyakazi Yule afanye kazi yake vizuri bila mafanikio. Lakini alikuja kutambua kuwa kuna nyakati chache mfanyakazi yule alifanya kazi yake vizuri. Hivyo akaamua kuwa anamsifu nyakati hizo, tena mbele ya watu wengine. Mfanyakazi Yule akaanza kuboresha kazi yake kila siku, na ndani ya muda mfupi akawa akifanya kazi yake vizuri kabisa, na wengine wakaanza kumkubali na kumpongeza, kupongeza kutoka moyoni kulileta matokeo, kushutumu kulishindwa.

Kuwaumiza wengine kwa shutuma si tu hakuwezi kuwabadilisha, lakini pia hakuhitajiki. Kuna msemo wa zamani ambao nimeuweka kwenye kioo changu, mahali ninapoweza kuuona kila siku, nitake nisitake, unasema:

Kama nitapita njia hii mara moja: basi kama kuna jambo zuri naweza kulifanya, au kama kuna rehema naweza kumuonyesha binadamu yoyote, acha nilifanye sasa. Nilisilipuuze wala kulihairisha. Maana sitpita njia hii tena.

Emerson alisema, “Kila mtu ninayekutana naye, kwa namna fulani ni bora kuliko mimi, hivyo nalazimika kujifunza kumhusu.”

Kama hilo lilikuwa kweli kwa Emerson, si litakuwa kweli hata mara elfu kwako na kwangu? Hebu tuache kufikiri juu ya mafanikio yetu, na matakwa yetu. Tujaribu kutambua mtazamo wa watuwengine. Tusahau kuhusu unafiki. Toa pongezi kutoka moyoni. “Kuwa mwingi wa sifa za kutoka moyoni na usiwe mbahili wa pongezi,” na watu watathamini maneno yako kama hazina. Watayarudia maisha yao yote—watayarudia miaka mingi baada ya wewe kuyasahau.



KANUNI YA PILI

Toa pongezi kutoka moyoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom