Kwanini Ikulu inaendelea kuudanganya ulimwengu?

Kwanini Ikulu inaendelea kuudanganya ulimwengu?

Ndugu wewe unamatatizo kwelikweli,

Pokea darasa hili huru,

Mchwe, kipindi hicho Kabila alikuwa kijana, ndicho kipindi Che Guevara alikuja Dar akipita kuelekea Congo akitokea Msumbiji, Hapa Dar alikaa kwa siku tatu akila na kulala pale Fast food jengo la mavuno pale posta, wakati akiwa Dar, manowari za kivita za USA zilikuwa kilimita chache ya mwambao w bahari ya Tanzania, na USA ikamshinikiza Nyerere amkamate Che, lakini Nyerere alikataa na kumuongezea ulinzi, ikiwemo kusindikizwa hadi Kigoma mpaka misitu ya Kongo ambako alikutana na Kabila huko,

Che hakumaliza kazi ya ukombozi DRC, aliondoka baada ya kushindwana na Laurant Kabila akaondoa kwenda Bolivia

Anapoondoka Kongo alitoa hotuba thabiti kule msituni na moja ya nukuu muhimu katika hotuba ile ni hii:

"...Ni vigumu kutegemea vijana waliogubikwa na mawazo ya ngono na wasio na elimu endelevu kuleta mapinduzi katika nchi maskini! Mapinduzi hayaletwi na watu wanaoabudu `Ngono' na `Pombe!" ~ CHE GUEVARA".

kipindi hicho che guevara alipokuwa congo. vita vilikuwa vinaongozwa na nani?kabila alikuwa na cheo gani?kabila hakuwa na nguvu yoyote kipindi hicho.che guevara alikuwa anatoa tu mafunzo ya vita vya msituni kwa vijana wa congo na wala hakushiriki kwenye mapinduzi.mapinduzi yalifanyika baadae sana
 
Mkuu ndo vijana wetu hao mashuleni wanapenda kusoma summary ndo maana vitabu vya Nyangwine vinauzika sana. Tuna Taifa la vijana wasiopenda shughulisha mbongo zao.
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

una hakika kwamba che guevara hakuwai kumsaidia ndugu kabila (father)? mijitu iliyosoma PCM udogoni inapenda sana kubishana.
 
kipindi hicho che guevara alipokuwa congo. vita vilikuwa vinaongozwa na nani?kabila alikuwa na cheo gani?kabila hakuwa na nguvu yoyote kipindi hicho.che guevara alikuwa anatoa tu mafunzo ya vita vya msituni kwa vijana wa congo na wala hakushiriki kwenye mapinduzi.mapinduzi yalifanyika baadae sana

Nitaendelea kujitahidi kukufungua akili japo umekomaa kwa ujingaa,

Unaposema,

"Che guevara alikuwa anatoa tu mafunzo ya vita vya msituni kwa vijana wa congo na wala hakushiriki kwenye mapinduzi"

Hapo unamaana alikuwa akiwafundisha vita vya nini?

Jitahidi kutumia akili hata hiyo ya kuzaliwa tu ikiwa ya darasani ilikupiga chenga.
 
Historia ina nadharia ya ajabu sana, haitofautiani na nadharia ya hisabati,

Ikulu ya Dar es Salaam inaendelea kuaminisha watu kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliongozwa na Sheikh Karume ama mwanaharakati mashuhuru kutoka kundi la makuli ndani ya Bandari ya Zanzibar,

Na mwendelezo huo umo katika lamgambo lililo tawazwa leo mbele ya kadamnasi ya walimwengu.

Hili hapa:

Hebu tujikumbushe ukweli unaouma kwa ikulu ya Jamhuri,

Kwanini Ikulu inadanganya? Karume hakuongoza mapinduzi wala hakuyaona mapinduzi yale ndani ya miezi mitatu, yeye alikuwa Dar, Muasisi halisi na aliyeweza kuwanyoosha wabwanyenye ni Field Marshal John Okello, akaitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma ndani ya miezi mitatu, na zaidi John Okello ndie Mwenyeiti wa kwanza wa baraza la Mapinduzi,

Abdulhman Babu ndie aliyepewa idara ya propaganda kuutangazia umma kuwa Karumena ASP ndio waliofanya mapinduzi, ni uongo mtupu, historia huwa haifichiki, Karume alikabidhiwa Zanzibar na Julius Nyerere hapa Uwanja wa Ndege wa Dar ule wa Zamani, tena kwa makubaliano kuwa Okello atakuwa Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi na Karume atakuwa Rais wa Zanzibar. Baada ya siku tatu Okello alipigwa ambushi na mtaalamu wa shabaha Emilio Mzena (TISS) au wengine katika idara walipenda kumuita the snake, huyu alimteka Okello kwa agizo la Nyerere na Karume kisha wakampeleka Kenya, walifika Nairobi Kenyatta akakataa kuwa huyo sio Mkenya, ndipo akarudishwa rasmi kwao Uganda, Huyo ndie Baba HALISI wa taifa la Zanzibar.

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.

Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.

Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka, 2000. Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.

Ni ukweli usiopingika kuwa, John Okelo ndo mleta mapinduzi na mwenyekiti wa kwanza wa SMZ
 
ya zitto yamekushinda sasa umeona uhamie kwa wazenji? hebu tueleze ukweli pia wa shekh suleiman taqdiir na akina bilal waikela walivyopigania uhuru wa tanganyika na nyerere akaitwa baba wa taifa wakati si kweli? nyani haoni ....
 
kipindi hicho che guevara alipokuwa congo. vita vilikuwa vinaongozwa na nani?kabila alikuwa na cheo gani?kabila hakuwa na nguvu yoyote kipindi hicho.che guevara alikuwa anatoa tu mafunzo ya vita vya msituni kwa vijana wa congo na wala hakushiriki kwenye mapinduzi.mapinduzi yalifanyika baadae sana

Main point ni kua John Okello ndio kiongozi wa Mapinduzivl ya Zanzibar, Period!!
 
Nitaendelea kujitahidi kukufungua akili japo umekomaa kwa ujingaa,

Unaposema,

"Che guevara alikuwa anatoa tu mafunzo ya vita vya msituni kwa vijana wa congo na wala hakushiriki kwenye mapinduzi"

Hapo unamaana alikuwa akiwafundisha vita vya nini?

Jitahidi kutumia akili hata hiyo ya kuzaliwa tu ikiwa ya darasani ilikupiga chenga.

ngoja nikukumbushe.vuguvugu la mapinduzi lilipoanza congo ndio muda che guevara alipokuja congo kuhamasisha mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuwatoa uoga vijana wa congo kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi.kipindi hicho mabutu alikuwa anaogopwa sana ndio maana hata kabila alikimbilia tanzania kwa kuogopa nguvu ya mobutu.mapinduzi ya congo yalifanikishwa kwa kiwango kikubwa na kagame kwa kuwatumia enterehamwe ndio maana mpaka leo kagame bado anaingilia mambo ya congo kwa kiasi kikubwa kwa sababu anajua udhaifu wake
 
Dada kwa niaba yangu na wengine namuombea msamaha huyo ndugu,hata mimi huwa nakereka na matusi kwenye sehemu ya kuelimishana!,akitamka hayo inabidi amfikirie mama,dada,shangazi,bibi,mke nk kisha aone anawaheshimu vipi!
Hivi Maku iliwakosea nini?mbona maku imekuleta Duniani maku inaleta familia maku inawajengea watu nyumba inasababisha watu wamiliki magari pasipo kutarajia Maku kwa kuheshimika imekatazwa isibakwe wala kukeketwa Sasa Mbona wewe unafananisha maoni ya mtu na kiungo cha mama yako Mzazi kiungo cha shangazi yako dada yako nk jaribuni Kuwa na mbinu digital za matusi staili hii imepitwa na wakati
 
Historia iliyopo kichwani kwako ni half baked. Study harder and dig deep.
ngoja nikukumbushe.vuguvugu la mapinduzi lilipoanza congo ndio muda che guevara alipokuja congo kuhamasisha mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuwatoa uoga vijana wa congo kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi.kipindi hicho mabutu alikuwa anaogopwa sana ndio maana hata kabila alikimbilia tanzania kwa kuogopa nguvu ya mobutu.mapinduzi ya congo yalifanikishwa kwa kiwango kikubwa na kagame kwa kuwatumia enterehamwe ndio maana mpaka leo kagame bado anaingilia mambo ya congo kwa kiasi kikubwa kwa sababu anajua udhaifu wake
 
Historia ina nadharia ya ajabu sana, haitofautiani na nadharia ya hisabati,

Ikulu ya Dar es Salaam inaendelea kuaminisha watu kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliongozwa na Sheikh Karume ama mwanaharakati mashuhuru kutoka kundi la makuli ndani ya Bandari ya Zanzibar,

Na mwendelezo huo umo katika lamgambo lililo tawazwa leo mbele ya kadamnasi ya walimwengu.

Hili hapa:

Hebu tujikumbushe ukweli unaouma kwa ikulu ya Jamhuri,

Kwanini Ikulu inadanganya? Karume hakuongoza mapinduzi wala hakuyaona mapinduzi yale ndani ya miezi mitatu, yeye alikuwa Dar, Muasisi halisi na aliyeweza kuwanyoosha wabwanyenye ni Field Marshal John Okello, akaitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma ndani ya miezi mitatu, na zaidi John Okello ndie Mwenyeiti wa kwanza wa baraza la Mapinduzi,

Abdulhman Babu ndie aliyepewa idara ya propaganda kuutangazia umma kuwa Karumena ASP ndio waliofanya mapinduzi, ni uongo mtupu, historia huwa haifichiki, Karume alikabidhiwa Zanzibar na Julius Nyerere hapa Uwanja wa Ndege wa Dar ule wa Zamani, tena kwa makubaliano kuwa Okello atakuwa Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi na Karume atakuwa Rais wa Zanzibar. Baada ya siku tatu Okello alipigwa ambushi na mtaalamu wa shabaha Emilio Mzena (TISS) au wengine katika idara walipenda kumuita the snake, huyu alimteka Okello kwa agizo la Nyerere na Karume kisha wakampeleka Kenya, walifika Nairobi Kenyatta akakataa kuwa huyo sio Mkenya, ndipo akarudishwa rasmi kwao Uganda, Huyo ndie Baba HALISI wa taifa la Zanzibar.

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.

Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.

Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka, 2000. Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.

Sheikh Mohammed Said, hebu njoo utupe ukweli kuhusu hili la Okello na Mzee Karume. Tunaomba a Real History, who actually was behind Mapinduzi Matukufu siku hizo yaani vuguvugu lote hadi siku ya kilele yaani 12 Jan 1964. Ama utawala na yaliyojiri baada ya 12/01/1964 yaani kuanzia 13/01/1964 hadi leo hii usigusie sana. Naomba nani alikuwa100% mastermind huko nyuma hadi 12/01/1964 halafu ishia hapo, maana makala ya mdau hapo inaleta mkanganyiko, kwa sisi ambao historia tunaijua juu juu tu! Ufafanuz Sheikh.
 
ngoja nikukumbushe.vuguvugu la mapinduzi lilipoanza congo ndio muda che guevara alipokuja congo kuhamasisha mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuwatoa uoga vijana wa congo kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi.kipindi hicho mabutu alikuwa anaogopwa sana ndio maana hata kabila alikimbilia tanzania kwa kuogopa nguvu ya mobutu.mapinduzi ya congo yalifanikishwa kwa kiwango kikubwa na kagame kwa kuwatumia enterehamwe ndio maana mpaka leo kagame bado anaingilia mambo ya congo kwa kiasi kikubwa kwa sababu anajua udhaifu wake

Naomba nikufungue akili yako kwa mapana zaidi,

Soma makala haya niliyoyaandika siku za nyuma.

Yericko Nyerere: Ijue Rwanda, Kagame na Museveni

13/08/2013

1 Comment

Rwanda ilikuwa eneo penye utawala wa kifalme tangu karne ya 16 BK kabla ya kufika kwa ukoloni. Mwanzo wake ni katika eneo la Ziwa la Muhazi. Watawala wenye cheo cha "mwami" kutoka kikundi cha wafugaji (Watutsi) walitanua himaya zao tangu miaka ya karne ya 16 BK hadi kufika eneo la leo hii. Wafugaji wa ng'ombe Watutsi walikalia nchi pamoja na wakulima wa Kihutu na wawindaji Watwaa.

UKOLONI WA KIJERUMANI

Ukoloni ulichelewa kufika Rwanda, mwaka 1890 Ujerumani na Uingereza walipatana ya kuwa Rwanda na Burundi ziwe ni sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Lakini ilikuwa mwaka 1908 tu ya kwamba Wajerumani walimtuma afisa wa kudumu aliyekaa Rwanda kama mwakilishi wa serikali ya Ujerumani. Mwaka 1916 Ubelgiji na Uingereza walivamia Rwanda katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baadae ikawa chini ya Ubelgiji pamoja na Burundi kama "Rwanda-Urundi" katika hali ya eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa (UNO).

Utawala wa Wabelgiji ulikuwa wa moja kwa moja na mkali zaidi kuliko wa Wajerumani. Wabelgiji walijaribu kutoa faida ya kiuchumi wakilazimisha wenyeji kupanda mikahawa na kutekeleza kazi za serikali ya kikoloni. Katika utawala wao Wabelgiji walitumia zaidi Watutsi wakiwapa nafasi za elimu na kuwatumia katika shughuli za serikali. Wataalamu wengine huamini ya kwamba siasa hii ilisababisha kukua kwa chuki dhidi ya Watutsi kwa upande wa wakulima Wahutu iliyoleta kumwaga kwa damu baadaye.

Katika miaka ya 1950 ilionekana na kudhihirika ya kwamba ukoloni unaelekea mwisho wake. Uhusiano kati

ya Wahutu na Watutsi ukawa vigumu kwa sababu Wabelgiji walibadilisha siasa yao yakupendelea Watutsi wakidai haki zaidi kwa ajili ya Wahutu waliokuwa wengi. Ni hasa wamisionari wa katoliki Mapadre Weupe waliosimama upande wa Wahutu wakiona ndio wagandamizwa.

Mwami Mutara Rudahigwa aliyejiita pia Charles alijaribu kuleta upatanishi kati ya vikundi katika nchi. 1954 aligawa nchi ya kifalme kati ya Wahutu na Watutsi. Lakini alikuwa na wapinzani Watutsi waliomua mwaka 1959. Mtoto wake Mwami Kigeri V. alisimikwa kwenye kiti hicho. Hatua hii ilisababisha ghasia na vurugu nchini kwa sababu Wahutu walidai kuwa na neno katika mabadiliko ya serikali. Mwezi wa Novemba 1959 Mwami Kigeri V. alilazimishwa kuondoka nchini akikimbilia Uganda. Watutsi wenye siasa kali walijaribu kumwua kiongozi wa Mouvement Democratique Republicain (MDR) chama kikubwa cha Wahutu. Wahutu walijibu kwa kuwashambulia na kuua Watutsi. Wabelgiji walitumia wanajeshi wao kupoza hali hiyo nchini Rwanda. Katika uchaguzi wa kwanza wa halmashauri ya tarafa na miji kabla ya uhuru chama cha Parmehutu ndicho kilichopata kura nyingi. Viongozi wa Parmehutu walitangaza serikali mpya mwaka 1961. Uchaguzi wa Bunge ulileta kura ya 77% kwa ajili ya chama cha Parmehutu kilichomchagua kiongozi wake Grégoire Kayibanda kuwa Rais.

Tarehe 01.07.1962 Rwanda ilipata uhuru wake kamili. Wakati huo zaidi ya Watutsi 350,000 tayari walishakuwa wamekimbilia nchi za jirani. Mwaka uliofuata vikundi vya Watutsi kutoka nchi hizo za jirani walijaribu kufanya mapinduzi kwa kushambulia serikali mpya wakitokea uhamishoni. Kitendo hicho kilifuatiwa na uangamizaji wa kwanza wa Watutsi zaidi ya 100,000 waliouawa na Wahutu.
Hata katika miaka iliyofuata mauaji dhidi ya Watutsi iliendelea. Wanasiasa Wahutu walizoea kuita Watusi ndio "Wadudu". Kila kitu kilichokuwa si sawa kilielezwa ni kosa la Watutsi waliokuwa raia bila haki. Idadi kubwa ya Watutsi walikimbia Burundi, Uganda na Tanzania.

Mwaka 1973 Generali Habariyama alimpindua rais Kayibanda na kuanzisha serikali ya kijeshi akijaribu kupatanisha vikundi ndani ya taifa. Lakini hata mwaka uliofuata 1974 mauaji ya Watutsi yalitokea tena.

Mnamo 1990 ilikuwa wazi ya kwamba Rwanda ilikuwa na hali ngumu. Kwa upande moja nchi za mataifa zilisukuma serikali za Afrika kuruhusu kura huru za kisiasa.

Katika Rwanda ongezeko la wakazi lilileta msongamano mkubwa na uhaba wa ardhi ya kilimo na Ufugaji. Uchumi ulikuwa duni, Wakati huohuo wapinzani Wahutu walikusanyika nje ya nchi hiyo kudai demokrasia. Na katika makumi elfu ya watoto wa Watutsi waliokuwa nje ya nchi hiyo, sauti zikasikika zilizodai warudi tena kuijenga Rwanda.

Habyarimana alijaribu kutafuta suluhisho na ungamano wa kitaifa, akaanza kujadiliana na Watutsi wa nje lakini alikutana na upinzani kwa upande wa Wahutu wakali waliochukia uelewano na Watutsi.

Safari ya Kagame na RPF kurudu Rwanda kutoka Uganda.

Oktoba 1990 Watutsi waliokaa Uganda walianzisha chama cha RPF (Rwanda Patriotic Front) wakiwa na wafuasi wahutu wachache wakavamia Rwanda kwa silaha. Kiongozi wao alikuwa Paul Kagame aliyeondoka Rwanda akiwa mtoto wa miaka minne. Alikuwa amejiunga na jeshi la Yoweri Museveni na kupanda ngazi katika jeshi la Uganda hadi kuwa mkuu wa huduma ya usalama ya kijeshi ya Uganda. Walitaka kulazimisha serikali ibadilishe hali ya Watutsi kuwa raia bila haki. Lakini uvamizi huu ulisababisha kuongezeka kwa ukali wa Wahutu dhidi ya Watutsi ndani ya Rwanda na siasa kali kwa upande wa viongozi Wahutu. Kikundi cha kihutu cha Interahamwe kilipewa silaha kujibu mapigo dhidi ya uvamizi wa Kagame, Maelfu ya Watutsi Warwanda waliuawa. Vita kati ya wapinzani kutoka Uganda na jeshi la serikali iliendelea mpakani hadi pande zote mbili zilikutana hapa Arusha Tanzania na kupatana kukoma kwa vita 1992 chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Sehemu ya viongozi Warwanda walijiandaa kutafuta utaratibu mpya lakini wengine walifanya mipango ya kumaliza swali la Watutsi kabisa wakipanga kuua Watutsi wote nchini.

Tarehe. 06.04.1994 rais Habariyama akirudi nchini kutoka safari ya Tanzania, Ndege yake ilipigwa kombora kabla ya kutua ikaanguka chini akafariki. Uwezekano ni mkubwa ya kwamba ni Wahutu wenye msimamo mkali ndio waliomua, lakini wengine walisema ni Jenerali Paul Kagame na RPF yake.

Tendo hili ilikuwa mwanzo wa mauaji ambayo hayakuwahi kutokea Afrika. Viongozi wa Interahamwe, wa jeshi la kitaifa na vikundi vikali vya Kihutu walitekeleza mipango ya kukusanya Watutsi kila mahali na kuwaua. Haiwezekani kuwa na idadi kamili lakini makadirio ya chini yanataja Watutsi 750.000 na Wahutu wasio wakali zaidi ya 100.000 waliuawa na Interahamwe na wanajeshi wa serikali ya Kihutu. Watu walikimbilia na kutafuta hifadhi makanisani lakini hata huko walichinjwa bila neema. Wahutu waliokataa kushiriki katika mauaji waliuawa pia.

RPF chini ya uongozi wa Paul Kagame iliamua kutumia nguvu zote kusimamisha machinjo haya. Kwa miezi miwili mauaji na vita yalienda sambamba hadi RPF iliposhinda Julai 1994 na kuchukua madaraka ya serikali.

Jeshi, Waparmehutu na serikali ya Kihutu walikimbilia Kongo wakiwalazimisha wakazi wengi kuongozana nao hali iliyosababisha kutokea kwa makambi ya wakimbizi makubwa sana katika Kongo ya mashariki yaliyokuwa na idadi ya Wahutu milioni mbili. Walio wengi wamerudi baada ya kuimarika kwa serikali mpya.

Tangu ushindi wa kijeshi mwaka 1994, RPF walianzisha serikali ya umoja wa kitaifa. Rais alikuwa Pasteur Bizimungu mwanasiasa Mhutu aliyeshikamana na RPF Kagame akiwa makamu wake. Baada ya kupinduliwa kwa Bizimungu mwaka 2000 Kagame akawa Rais. 2003 palitokea uchaguzi wa kwanza wa kirai ambapo chama cha RPF chimi ya Jenerali Paul Kagame kilishinda.

Jeshi la Rwanda limeendelea kuwa na vita ndani ya Kongo likipigana na mabaki ya Interahamwe waliokuwa wanashambulia Rwanda mara kwa mara kutoka Kongo.

Kutokana na mauaji hayo ya 1994, mahakama ya kimataifa iliyopo nchini Uholanzi imeendesha hukumu nyingi kwa wahusika wake, vilevile mahaka ya kimataifa ya Arusha nchini Tanzania nayo imeendesha huku stahiki kwa wahusika,

Ndani ya Rwanda mahakama za vijijini zinazoitwa "gachacha" vilevile zimejaribu kutoa hukuma juu ya waliohusija na mauaji ya mwaka 1994.
Mapatano ndani ya Rwanda yamezidi kushamiri, huku Paul Kagame akionsha kuijenga vema Rwanda kwa mkono wa chuma, Mathalani: D.Gasangwa wa EACU arisisitiza kwamba "Sometime in April(2004)" movie, ilikuwa "ETHNIC CLEASING", si HOLOCOSTI!, kama ilivyoandikwa na Wazungu wa Magazeti ya Ulaya. Watu karibu 600,000 waliuawa Rwanda, na hapo Mkoa wa Kivu, Congo.

Afrika ina ujuzi sasa; kama ujuzi wa Kiarabu, Kiswahili, Kilingala, Kiwolof, Kiamharic. Utengamano wa siasa mpya rasima utatupa na fasi ya kujenga inchi mpya kama EACU na Rwanda Kazembe.

Lakini huku mapambazuko mema yakitamalaki Rwanda, Kiongozi wa utawala wa nchi hiyo ndogo, anatajwa kuwa ni miongozi mwa viongozi makupe barani Afrika, ukupe wake sio waufisadi bali ukwasi wenye chembe za kiyunani

Lakini leo yale mabaki ya vikundi vile vya Interahamwe vilivyokimbilia uhamishoni kaskazini mwa Kongo mji wa Goma na Kivu si vikundi vya uasi dhidi ya Rwanda tena bali ni vitendea kazi muhimu dhidi ya upanuzi wa miliki mpya ya Watusi,

Wale watusi waliokimbilia Uganda enzi za Mwami Kigeri V, Inatajwa na kuaminika kuwa Jenerali Paul Kagame, Yoweri Mseveni na Watutsi waliokimbilia Goma baada ya kushika dola zao, walikuja na malengo mujarabu yanayotekelezwa kwa hatua na kwa vipindi virefu sana,

Mpango huo ulikuwa ni kusimika dola imara la Watutsi barani Afrika hasa nchini Kongo katika Goma-Kivu ya Kasiskani mpango siri walioupa jina la "Nchi mpya ya ahadi ya Watutsi". Ni mpango endelevu ulio na lengo la kuwakusanya Watutsi duniani kote na kuwaweka pamoja wakimiliki ardhi na rasilimali zake!

Hili linathibitika katika kile walicho "Mkataba wa kuigawa Kongo" ulisainiwa na Yoweri Mseveni, Paul Kagame na Laurent Kabila akiomba msaada wa kuingia madarakani kwa mtutu wa bunduki,

Naam baada ya Laurent Kabila kuingia madarakani kwamsaada wa Kagame na Mseveni kupitia ule mkataba, Kabila alikataa kuheshimu mkataba ule nakusema yale yalikuwa ni maneno ya porini tu hivyo hawezi kuiuza nchi kwa karatasi za mstuni!

Hapo sasa ndipo tunapoingia kwenye madhila ya Kongo tuliyoyaona tangu mauaji ya L. Kabila na tunayoyashuhudia hii leo chini ya J. Kabila, M23, Kagame na Mseveni.

MKATABA WA KUIGAWA na KUIUZA KONGO

Kinachoitwa vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa kuliko yoyote ile Afrika Mashariki na Kati.

Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutoka utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo.

Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.

Taarifa zilizopo zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu. Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Rwanda “kwa ukombozi wa Kongo.”

Desire Kabila alikuwa tayari amechoka. Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko. Alikuwa amefikia hatua ya kukata tamaa na kutulia jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.” Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo.

Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando; askari mtaalam wa kusomea. Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho.

Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Mungu akupe nini! Hakuna uthibitisho wowote, lakini taarifa zinaeleza kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere “ambaye aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.”

Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.”

Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika mkoa wa Kivu Kusini. Makabila ya asili ya hapa ni Wavira na Wafuliro. Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda wakuja.

Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo; inawanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji.

Wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.

Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za mkoa huo, wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda.

Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali – magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka – hatua ambayo ilielezwa kuwa uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.

Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamwasi Ngando.

Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji. Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga.

Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa na majibu tofauti. Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai.

Baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu. Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.

Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama – AFDL – Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo.

Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji.

Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa. Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo. Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa “Makubaliano ya Lemera.”

Kuna madai kwamba viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo. Miongoni mwa nchi hizo ni Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani.

Imeelezwa kuwa makubaliano ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda; na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, “taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa” na wavamizi.
Imeelezwa kuwa hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda. Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa.

Makubaliano yanadaiwa kueleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza.

Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera; na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa “majeshi ya ushirikiano” ya Rwanda na Kongo.

Kwa mujibu wa masimulizi juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.

Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni – Kongo.

Imeelezwa kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu: Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote; Mungu au shetani.

Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo mkuu wa sasa wa majeshi wa Rwanda, James Kabarebe.

Baada ya kuingia ikulu, Kabila anadaiwa kuwageuka wenzake. Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alikuwa tayari amesoma mwelekeo wa makubaliano yake na kuona kuwa yanatoa mwanya kwa kile kilichoitwa “Nchi ya Ahadi” ya Watutsi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Tanzania.

Alitakiwa atangaze, akiwa rais, kuwa Kivu mbili zote ni makazi ya Watutsi; ili hata wananchi wa Kongo watakaobaki humo, wawe wanafahamu kwamba siyo kwao.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi – kupitia bungeni – ili wananchi wenyewe waamue.”

Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto).
Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?”

Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na sasa mkuu wa majeshi ya Rwanda. Hatua hizi na nyingine, ndizo zilisababisha kutotekelezwa kwa Makubaliano ya Lemera.

Lakini wachunguzi na wafuatiliaji wa mahusiano ya nchi hizi mbili wanasema, makubaliano yameandikwa na yapo; hayajafutika. Kilichofanyika ni “ukaidi wa Kabila” wa kutotaka kutimiza ahadi yake baada ya kuingia ikulu.

Kabila anasemekana alikuwa amesoma kitabu cha Raphael Ntibazokiza kikieleza mahusiano ya Watutsi na wabantu, kiitwacho Plan de la colonisation tutsi au Kivu et region centrale de l’Afrique – Mpango wa ukoloni wa Kitusi katika Kivu na eneo la Afrika ya Kati.

Raphael anaandika, “Mhutu ameumbwa kufanyia kazi watu wengine; hawezi hata kujaribu kupata uongozi. Chukua nafasi zote za mikoa na wilaya na atakayekuwa mtawala ahakikishe kuwa analinda maslahi yetu... Baadaye watakapokuja kustuka, watakuwa wamechelewa…”

Mmoja wa waliokuwa karibu na Laurent Kabila amenukuliwa akisema hakuna kitu kilichomsononesha Kabila kama kauli ifuatayo ndani ya kitabu cha Raphael:
“Tutumie ukarimu wao. Tujinyenyekeze kwao kama sisi ni watumishi wao.

Tukiishachukua nafasi zao tuwatelekeze na ‘kuwalipa ujira wa nyani’- payez-les en monnaie de singe pour montrer leur incapacite – ili kudhihirisha kuwa hawana uwezo.”

Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa “watoto” wake – vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni.

Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake. Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera; lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi.

Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika wiki moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa; hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa.

Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kunaonekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako “baba” yake alikataa.
Kinachoitwa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na ile ya Kongo kinaonekana wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa.

Aidha, kukamatwa kwa Jenerali Laurent Nkundabatware na kuhifadhiwa nchini Rwanda kunaelezwa kuwa sura kamili ya “kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo.”

Kuna madai kuwa Nkundabatware, Mnyarwanda kutoka Rwanda, lakini Rwanda inasema ni Mkongomani, hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo. Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingilia kwa kisingizio cha “kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani.”

“Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda Jenerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti,” kimeeleza chanzo cha habari hizi mjini Goma.

Rwanda imeingia Kongo. Nani ataiondoa? Baadhi ya nchi jirani zimekuwa watazamaji tu wakati nyingine zikiwa katika maandalizi ya kunufaika kutokana na mgogoro wa nchi hii.

Moses Byaruhanga, waziri katika ofisi ya rais (Siasa) nchini Uganda, amesema nchi yake inaunga mkono “shirikisho la Kivu na Kisangani” na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya muungano wa Jamhuri ya Kivu.

Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda inaongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Kisangani ambako majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA).

Kiongozi wa LRA, Joseph Kony amekuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 15. Uganda sasa inadai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao.

Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam ilikaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo.

Jumuiya ya kimataifa imetekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.

Isipokuwa Barrack Obama ambaye angalau amesema anataka Kongo tulivu na kwamba atasaidia kuleta hilo, mataifa mengine, pamoja na Ufaransa, yanataka kuimega Kongo.

Vielelezo:

Moabi KKK/BKK
Yunani
Wikipedia
Tutsi
Hutu
Twa
Paul Kagame
Laurant Kabila
Yoweri Mseveni

Imeandikwa na:
YERICKO NYERERE
 
Ukweli mchungu.mapinduzi yaliongozwa na john okello.
che guavara alishirikiana na l kabila katika harakati za kumng
'oa mobutu.
waislamu ndio waliopigania uhuru wa tanganyika.
thabit kombo ndiye aliyefanikisha muungano wa tanganyika na zanzibar.
 
Yericko huo upuuzi ulioandika hapo juu utawadanganya vilaza wenzako lakini hili suala la John Okello tulisha kuelimisha muda mrefu sana .
 
Hapo kwenye red: Kitaalamu ni kosa kubwa mno kwa dola kutumia generic email servers kama hizi, wakati kuna sever ya serikali. Hii inamaanisha hata hackers wa kawaida anaweza akaingia kwenye inbox na akachukua siri za nchi kirahisi tu. Wataalamu wa IT hili inabidi walifanyie kazi, tuna servers zetu, why yahoomail anyway?

Hawaambiliki kwa mambo yote kama ZZK
 
Ukweli mchungu.mapinduzi yaliongozwa na john okello.
che guavara alishirikiana na l kabila katika harakati za kumng
'oa mobutu.
waislamu ndio waliopigania uhuru wa tanganyika.
thabit kombo ndiye aliyefanikisha muungano wa tanganyika na zanzibar.

Upo sahihi kiasi,

Uhuru wa Tanganyika haukupiganiwa kwa turufu ya dini, bali uafrika na dhamira thabiti tu,

Uwingi wa waamini wa dini ya kiislamu katika TAA na TANU sio tiketi ya uislamu kuongoza ukombozi,

Tuache uchochezi wa aina hiyo,

Mfano mzuri ni ccm ya leo ambayo 88% ya viongozi wa juu ni waslamu, lakini hatuwezi kuiita ccm ni chama cha waislamu, labda katika nyanja za kipropaganda za siasa za ndani tu
 
ya zitto yamekushinda sasa umeona uhamie kwa wazenji? hebu tueleze ukweli pia wa shekh suleiman taqdiir na akina bilal waikela walivyopigania uhuru wa tanganyika na nyerere akaitwa baba wa taifa wakati si kweli? nyani haoni ....

Hivi ni Sheikh gani mwenye uwezo wa kukaa UN na wazungu kudai uhuru? Tuwe wakweli pale UN hakuna hadithi za mahakama ya kadhi.
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

mkuu bora uulize kuliko kujianika hivi, hebu tumia hata Google kum-search Che-Guevara kama hujaona alishiriki vita ya Congo na kina Kabila.
 
Vita ya kumng'oa mabutu haikuanza miaka ya 90's ilikuwa imeanza kitambo toka Comrade CHE hakiwa hai na CHE aliingia Congo na kupigana vita upande wa kina Kabila Laurent lkn alibaini kuwa hawakuwa Wanamapinduzi bali wataka madaraka tu, maana alipata kuwaambia "mwanamapinduzi wa kweli anapaswa onekana ktk mapambano akiwa mstari wa mbele na si kuwa mstari wa mbele kwenye vyombo vya habari na kuwaacha vijana porini wakiendesha mapambano" hapo alikuwa amechukizwa na vitendo vya kabila mkubwa na timu yake kutokuwepo ktk mapambano na kudai wanatafuta msaada kwa nchi wafadhili ili uwasaidie ktk mapambano na kuwa vita inahitaji propaganda hivyo lzm waongee ktk vyombo vya habari. Comrade CHE alipobaini kuwa jamaa ni wachumoa tumbo na wanawatoa vijana kafara porini ili wakishinda vita wao ndio wale neema ya nchi akaondoka na kuwaachia vita yao. Hivyo Comrade CHE alipigana vita huko Congo na alichokiona ktk mapambano na kuamua kuonsoka ndio kilikuja kutimia baada ya Watutsi wa Kinyamulenge na warwanda walipomsaidia kumtoa Mabutu madarakani, kujinufaisha,ngono na pombe vikatawala maisha hadi wakageukana wwnyewe kwa wenyewe na Lauerent Kabila akauwawa. Embu google kuhusu Comrade CHE unaweza kuona uahiriki wake ktk mapambano ya kimapinduzi huko CONGO KINSHASA
 
mkuu bora uulize kuliko kujianika hivi, hebu tumia hata Google kum-search Che-Guevara kama hujaona alishiriki vita ya Congo na kina Kabila.

hivi unaziamini sana habari za google?kuna vitabu vingi vinavyoelezea kwa undani zaidi.che guevara hakupigans vita vya congo.mobutu alikuwa na nguvu sana pamoja na backup na mataifa ya nje hawa ndio walimuweka mobutu madarakani.baada ya kumuua lumumba mzalendo aliepigania maslahi ya congo. bila kusaidiwa na rwanda kabila asingeweza kufanya mapinduzi.
 
Back
Top Bottom