Historia ina nadharia ya ajabu sana, haitofautiani na nadharia ya hisabati,
Ikulu ya Dar es Salaam inaendelea kuaminisha watu kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliongozwa na Sheikh Karume ama mwanaharakati mashuhuru kutoka kundi la makuli ndani ya Bandari ya Zanzibar,
Na mwendelezo huo umo latika lamgambo lililo tawazwa leo mbele ya kadamnasi ya walimwengu.
Hili hapa:
Hebu tujikumbushe ukweli unaouma kwa ikulu ya Jamhuri,
Kwanini Ikulu inadanganya? Karume hakuongoza mapinduzi wala hakuyaona mapinduzi yale ndani ya miezi mitatu, yeye alikuwa Dar, Muasisi halisi na aliyeweza kuwanyoosha wabwanyenye ni Field Marshal John Okello, akaitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma ndani ya miezi mitatu, na zaidi John Okello ndie Mwenyeiti wa kwanza wa baraza la Mapinduzi,
Abdulhman Babu ndie aliyepewa idara ya propaganda kuutangazia umma kuwa Karumena ASP ndio waliofanya mapinduzi, ni uongo mtupu, historia huwa haifichiki, Karume alikabidhiwa Zanzibar na Julius Nyerere hapa Uwanja wa Ndege wa Dar ule wa Zamani, tena kwa makubaliano kuwa Okello atakuwa Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi na Karume atakuwa Rais wa Zanzibar. Baada ya siku tatu Okello alipigwa ambushi na mtaalamu wa shabaha Daudi Mzena (TISS) au wengine katika idara walipenda kumuita the snake, huyu alimteka Okello kwa agizo la Nyerere na Karume kisha wakampeleka Kenya, walifika Nairobi Kenyatta akakataa kuwa huyo sio Mkenya, ndipo akarudishwa rasmi kwao Uganda, Huyo ndie Baba HALISI wa taifa la Zanzibar.
Mungu Ibariki Zanzibar, Mungu Ibariki