Kwanini Ikulu inaendelea kuudanganya ulimwengu?

Kwanini Ikulu inaendelea kuudanganya ulimwengu?

hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

ni vema kama hujui vizuri uulize kwa upole utafahamishwa. jaribu kuficha umburula wako japo kidogo.

Kabila alianza harakati za kumng'oa Mobutu siku nyingi, miaka ya 60. Hii ya miaka ya 90 ilikuwa ni jaribio la mara ya pili ambapo alifanikiwa akisaidiwa na USA na Kagame. Vinginevyo jibidiishe kusoma historia ya Africa kijana. Vijana wa siku hizi mmekaa ki komedi komedi, hamtaki kushughulisha bongo zenu.
 
ndugu yericko nyerere haya ndo mwl nyerere aliyokuwa akihubiri akiwa pale ikulu kwa zaidi ya miaka 21. je, uko tayari kupingana na nyerere?

Historia ina nadharia ya ajabu sana, haitofautiani na nadharia ya hisabati,

Ikulu ya Dar es Salaam inaendelea kuaminisha watu kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliongozwa na Sheikh Karume ama mwanaharakati mashuhuru kutoka kundi la makuli ndani ya Bandari ya Zanzibar,

Na mwendelezo huo umo katika lamgambo lililo tawazwa leo mbele ya kadamnasi ya walimwengu.

Hili hapa:

Hebu tujikumbushe ukweli unaouma kwa ikulu ya Jamhuri,

Kwanini Ikulu inadanganya? Karume hakuongoza mapinduzi wala hakuyaona mapinduzi yale ndani ya miezi mitatu, yeye alikuwa Dar, Muasisi halisi na aliyeweza kuwanyoosha wabwanyenye ni Field Marshal John Okello, akaitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma ndani ya miezi mitatu, na zaidi John Okello ndie Mwenyeiti wa kwanza wa baraza la Mapinduzi,

Abdulhman Babu ndie aliyepewa idara ya propaganda kuutangazia umma kuwa Karumena ASP ndio waliofanya mapinduzi, ni uongo mtupu, historia huwa haifichiki, Karume alikabidhiwa Zanzibar na Julius Nyerere hapa Uwanja wa Ndege wa Dar ule wa Zamani, tena kwa makubaliano kuwa Okello atakuwa Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi na Karume atakuwa Rais wa Zanzibar. Baada ya siku tatu Okello alipigwa ambushi na mtaalamu wa shabaha Emilio Mzena (TISS) au wengine katika idara walipenda kumuita the snake, huyu alimteka Okello kwa agizo la Nyerere na Karume kisha wakampeleka Kenya, walifika Nairobi Kenyatta akakataa kuwa huyo sio Mkenya, ndipo akarudishwa rasmi kwao Uganda, Huyo ndie Baba HALISI wa taifa la Zanzibar.

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.

Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.

Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka, 2000. Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.
 
1 said:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.​
Mimi hapa pia huwa nashindwa kupaelewa!
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

Waswahili husema kuwa usilolijua ni usiku wa giza!! Che Guevara alikuja na kuingia Congo na kujaribu kuwasaidia wakina Laurent Kabila waikomboe nchi yao lakini wao badala ya kushabikia ukombozi wa nchi yao wakaona NGONO na ULABU ndio dili!!!
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

April 24 1965 CHE Guevala aliingia Congo na Afro Cuban 100 kutoa mafunzo ya ukombozi wa kumngoa Mobutu wakishiriana na Laurent Kabila,baada ya Kumpindua Patrice lumumba.Akiwa congo alipata msaada wa lunga ya kiswahili na lugha za jadi kutoka kwa kijana freddy Ilanga.kwa hiyo usidhan tu Kabila mkubwa alianza harakati miaaka ya karibuni,ni soon tu baada ya uhuru.
NAPENDA NIKUJULISHE LITTLE KNOWLEDGE IS VERY DANGEROUS,shida yako unajua vitu nunsunusu,zaidi tembelea google na jitahidi kushirikisha ubongo in doing simple research!
 
Hivi ni Sheikh gani mwenye uwezo wa kukaa UN na wazungu kudai uhuru? Tuwe wakweli pale UN hakuna hadithi za mahakama ya kadhi.

We SUKULE ulikua wapi cc ASHA mohamed Ritz
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo hapa ni mla mbwa Yericko na wewe mla panya mmakonde jinga kuliko wote na gesi ndio hio inaelekea bagamoyo, bana pua tea haitokiii!!

mkuu eti unamchukuliaje dume zima na mivuzi mpaka mku.... halafu anajilegeza na id ya kike ?? CC ASHA mohammed
 
Last edited by a moderator:
ndugu yericko nyerere haya ndo mwl nyerere aliyokuwa akihubiri akiwa pale ikulu kwa zaidi ya miaka 21. je, uko tayari kupingana na nyerere?

Kichwa cha mada hii kinasema, "Kwanini Ikulu inaendelea kuudanganya ulimwengu?"

Tafsiri ya kichwa hicho ni kuwa taasisi ya urais imeendelea kuudanganya ulimwengu kuhusu ukweli huo wa mapinduzi tangu yalipotukia,
 
April 24 1965 CHE Guevala aliingia Congo na Afro Cuban 100 kutoa mafunzo ya ukombozi wa kumngoa Mobutu wakishiriana na Laurent Kabila,baada ya Kumpindua Patrice lumumba.Akiwa congo alipata msaada wa lunga ya kiswahili na lugha za jadi kutoka kwa kijana freddy Ilanga.kwa hiyo usidhan tu Kabila mkubwa alianza harakati miaaka ya karibuni,ni soon tu baada ya uhuru.
NAPENDA NIKUJULISHE LITTLE KNOWLEDGE IS VERY DANGEROUS,shida yako unajua vitu nunsunusu,zaidi tembelea google na jitahidi kushirikisha ubongo in doing simple research!

Nakushukuru sana mkuu kwakumpa darasa huyo ndugu.
 
Historia ina nadharia ya ajabu sana, haitofautiani na nadharia ya hisabati,

Ikulu ya Dar es Salaam inaendelea kuaminisha watu kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliongozwa na Sheikh Karume ama mwanaharakati mashuhuru kutoka kundi la makuli ndani ya Bandari ya Zanzibar,

Na mwendelezo huo umo katika lamgambo lililo tawazwa leo mbele ya kadamnasi ya walimwengu.

Hili hapa:

Hebu tujikumbushe ukweli unaouma kwa ikulu ya Jamhuri,

Kwanini Ikulu inadanganya? Karume hakuongoza mapinduzi wala hakuyaona mapinduzi yale ndani ya miezi mitatu, yeye alikuwa Dar, Muasisi halisi na aliyeweza kuwanyoosha wabwanyenye ni Field Marshal John Okello, akaitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma ndani ya miezi mitatu, na zaidi John Okello ndie Mwenyeiti wa kwanza wa baraza la Mapinduzi,

Abdulhman Babu ndie aliyepewa idara ya propaganda kuutangazia umma kuwa Karume na ASP ndio waliofanya mapinduzi, ni uongo mtupu, historia huwa haifichiki, Karume alikabidhiwa Zanzibar na Julius Nyerere hapa Uwanja wa Ndege wa Dar ule wa Zamani, tena kwa makubaliano kuwa Okello atakuwa Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi na Karume atakuwa Rais wa Zanzibar. Baada ya siku tatu Okello alipigwa ambushi na mtaalamu wa shabaha Emilio Mzena (TISS) au wengine katika idara walipenda kumuita the snake, huyu alimteka Okello kwa agizo la Nyerere na Karume kisha wakampeleka Kenya, walifika Nairobi Kenyatta akakataa kuwa huyo sio Mkenya, ndipo akarudishwa rasmi kwao Uganda, Huyo ndie Baba HALISI wa taifa la Zanzibar.
Sio siri kabisa kwamba Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar serikali imeipotosha na wewe Yericko unaipotosha tena kwa makusudi! Kwanza kabisa nitaendelea kukuambia tena na tena kwamba si kweli kwamba muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ni John Okello ingawaje si kweli vilevile kwamba muasisi wa mapinduzi hayo ni Karume! Nadhani unatakiwa kuelewa nini maana ya kuasisi kitu! Hakuna shaka hata kidogo kwamba John Okello alikuwa mstari wa mbele kabisa katika kuongoza mapinduzi lakini ni uongo kupita kiasi kusema kwamba ndie muasisi wa mapinduzi hayo! Kama hufahamu nini maana ya kuasisi, rejea kamusi kisha nijuze ikiwa bado unaamini kwamba Okello ndie muaisisi!!

Historia ipo wazi, tusione taabu kuisoma ama kuitafuta! Wakati Okello anaingia Unguja kutokea Pemba tayari alikuta harakati za hapa na pale za kutaka kuupindua utawala wa Sultani...harakati hizi zilikuwa zinafanywa chini kwa chini na baadhi ya vijana wa Kikomunist wa ASP na wale wa Umma Party. Kimsingi, harakati za Mapinduzi Zanzibar zilianza hata kabla Okello hajaingia Unguja! Hata hivyo, wakati Babu kiongozi wa Umma Party alikuwa anafahamu juu ya harakati hizi Karume kwa upande wake (wa ASP) yeye alifichwa kwavile alikuwa ni mpinzani wa matumizi ya nguvu ingawaje alikuwa na support ya kutosha kutoka kwa vijana makuli na mabaharia.

Harakati hizi za mapinduzi ziliasisiwa na Wazanzibari wenyewe wakati wakiwa masomoni nchi za ng'ambo kwahiyo ni kichekesho kusema kwamba mapinduzi "yaliasisiwa" na Okello unless kama hufahamu nini maana ya kuasisi. Tusisahau kwamba haya yalitokea wakati mtu kama Abdulrahman Babu akiwa ameshapatwa kuwekwa ndani si mara moja kwa madai ya uhaini na kuchochea vurugu. Ni mapinduzi ambayo yalitokea wakati vijana kibao wa Umma Party walikuwa wameshapata mafunzo ya kijeshi kutoka Cuba na waliporejea Zanzibar hakuna walichohubiri zaidi ya Ukomunist hali ambayo iliwatisha hata Wamarekani wenyewe kwa kuhofia kile walichoita kuzaliwa kwa Cuba ya Afrika na hatimae kuu-frame Muungano kwa hofu ile ile ya kuwa na Cuba ya Afrika!

Hivyo basi, wakati Okello anaingia Unguja alikuta tayari kuna harakati za chini kwa chini kwahiyo alichofanya yeye ni kuwahamasisha watu. Kusema kwamba yeye ndie aliasisi ni sawa na kusema kwamba Zanzibar hakukuwa na harakati zozote za kutaka kufanya mapinduzi bali alipokuja Okello ndipo alipoanzisha harakati hizo...huo ni udanganyifu usio na maana yoyote hasa nikizingatia kwamba wakati unainanga Ikulu kwa kudanganya nawe tena unachukua mkondo ule ule wa kudanganya!
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi
Duu, kweli hili jukwaa limevamiwa na wavivu wa kujisomea!? Kwahiyo unadhani Kabila alianza harakati za kumng'oa Mabuto miaka ya 90 sio? Uliisha wahi kujiuliza ni nini kilicho mleta Kabila Tanzania? Na alikuja mwaka gani? Well, kwanini hata jina lake alibadirisha akiwa hapa Tanzania!? Sorry siwezi kumsaidia bwn Yerico Nyerere kwenye uzi wake but umenisikitisha sana kupinga kitu usicho kijua, bora ungeuliza!
 
Yericko Sometime uwe mzalendo mambo mengine ni ya ndani ya nyumba mezea. Acha kukusoa kila jambo ambalao hata nadharia yake hata hatuijui, maana hakuna mwenye historia ya kweli ya juu bya mapinduzi .
 
Sio siri kabisa kwamba Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar serikali imeipotosha na wewe Yericko unaipotosha tena kwa makusudi! Kwanza kabisa nitaendelea kukuambia tena na tena kwamba si kweli kwamba muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ni John Okello ingawaje si kweli vilevile kwamba muasisi wa mapinduzi hayo ni Karume! Nadhani unatakiwa kuelewa nini maana ya kuasisi kitu! Hakuna shaka hata kidogo kwamba John Okello alikuwa mstari wa mbele kabisa katika kuongoza mapinduzi lakini ni uongo kupita kiasi kusema kwamba ndie muasisi wa mapinduzi hayo! Kama hufahamu nini maana ya kuasisi, rejea kamusi kisha nijuze ikiwa bado unaamini kwamba Okello ndie muaisisi!!

Historia ipo wazi, tusione taabu kuisoma ama kuitafuta! Wakati Okello anaingia Unguja kutokea Pemba tayari alikuta harakati za hapa na pale za kutaka kuupindua utawala wa Sultani...harakati hizi zilikuwa zinafanywa chini kwa chini na baadhi ya vijana wa Kikomunist wa ASP na wale wa Umma Party. Kimsingi, harakati za Mapinduzi Zanzibar zilianza hata kabla Okello hajaingia Unguja! Hata hivyo, wakati Babu kiongozi wa Umma Party alikuwa anafahamu juu ya harakati hizi Karume kwa upande wake (wa ASP) yeye alifichwa kwavile alikuwa ni mpinzani wa matumizi ya nguvu ingawaje alikuwa na support ya kutosha kutoka kwa vijana makuli na mabaharia.

Harakati hizi za mapinduzi ziliasisiwa na Wazanzibari wenyewe wakati wakiwa masomoni nchi za ng'ambo kwahiyo ni kichekesho kusema kwamba mapinduzi "yaliasisiwa" na Okello unless kama hufahamu nini maana ya kuasisi. Tusisahau kwamba haya yalitokea wakati mtu kama Abdulrahman Babu akiwa ameshapatwa kuwekwa ndani si mara moja kwa madai ya uhaini na kuchochea vurugu. Ni mapinduzi ambayo yalitokea wakati vijana kibao wa Umma Party walikuwa wameshapata mafunzo ya kijeshi kutoka Cuba na waliporejea Zanzibar hakuna walichohubiri zaidi ya Ukomunist hali ambayo iliwatisha hata Wamarekani wenyewe kwa kuhofia kile walichoita kuzaliwa kwa Cuba ya Afrika na hatimae kuu-frame Muungano kwa hofu ile ile ya kuwa na Cuba ya Afrika!

Hivyo basi, wakati Okello anaingia Unguja alikuta tayari kuna harakati za chini kwa chini kwahiyo alichofanya yeye ni kuwahamasisha watu. Kusema kwamba yeye ndie aliasisi ni sawa na kusema kwamba Zanzibar hakukuwa na harakati zozote za kutaka kufanya mapinduzi bali alipokuja Okello ndipo alipoanzisha harakati hizo...huo ni udanganyifu usio na maana yoyote hasa nikizingatia kwamba wakati unainanga Ikulu kwa kudanganya nawe tena unachukua mkondo ule ule wa kudanganya!

Mkuu,

Kwanza habari za siku,

Hapa katika mada hii kinachotutenga ni tafsiri ya lugha tu,

"Uasisi wa mapindizi"

Kwakawaida neno uasisi husimama baada ya kitu kutukia, na hapo ndipo ndipo huanza kusomwa kuwa uasisi.

Katika dhana ya mapinduzi ya Zanzibar John Okello ndiye muasisi, haijalishi aliukuta wapi mpango wa mapinduzi, jambo kuu ni kuwa yeye ndie aliongoza mapinduzi hadi 12/01/1964 na tukio zima likatukia.
 
okello hakuwa mzanzibar wewe.yule alikuwa gaidi.hawezi kuingia kwenye historia ya zanzibar.mapinduzi yaliongozwa na karume. mbona wewe unatudanganya ni mtoto wa nyerere
Ulivyo M..ji....nga na ushamba sijui ulimaliza shule ya kata au vipi,yaani Mkiona jina la Nyerere tu mnaona alikuwa mmoja tu kuitwa jina hilo lol kazi kweli kweli,kama hutaki alichoandika Yeriko Nyerere nenda Library then tafuta alichokisema au nenda kwa mtandao lakini kwa kuwa Wabongo wengi ni wavivu wa kusoma utaendelea kubishana kwa kuwa umekuwa mvivu wa kuchambua mambo.Wake up man
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

pole sana na urudi darasani ukamsome che guevara tena, ndio msaada wa kukupatia kwa sasa
 
hivi harakati za kumng'oa mabutu zilianza lini?kabila aliingia lini madarakani?acha uongo kabila hajawahi kusaidiwa na che guevara hata siku moja wewe.harakati za kumtoa kabila zilianza wakati che guevara ameshakufa siku nyingi

Duh! Sorry mkuu kwani una umri gani?
 
Teh teh mla mbwa wa ifunda anaeleza historia ya zanzibar...
 
Yericko nyerere nimeamini sasa siasa zimekufumba macho umekuwa kipofu asiyetarajia kuona tena. Kila atakachosema raisi kikwete basi wewe kwako ni hoja. Historia ya nchi husika inaandikwa na wenye nchi wenyewe. Wenyewe wazanzibari wanasema karume ndiye aliyefanya mapinduzi, unataka kubishana nao? Heshimu historia ya wahusika huyo john okelo wakati anafanya mapinduzi ulikuwepo? Acha kuamini historia za kusimuliwa. Kuna wazee walioshiriki mapinduzi takatifu ya zanzibar mpaka leo wapo na hawamtaji john okelo kama kiongozi iweje wewe wa kutoka bara ushikilie issue isiyokuhusu. Sawa unatofautiana kiitikadi na aliyesema hayo lakini isiwe sababu ya kutuaminisha uongo na kuleta mada za kutugawa. Heshimu historia ya watu na kumbuka kuwa upinzani haimaniishi kupinga hata mazuri anayofanya mwenzio wa upande wa pili.
 
Back
Top Bottom