Christopher Wallace
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,397
- 3,492
Bado naendelea kumkumbuka Rais wetu wa awamu ya tano, Field Marshall John Pombe Magufuli. Hakika maisha yake yaliwagusa watanzania wengi sana na hata kuondoka kwake kumeacha simanzi kubwa sana.
Enzi za uhai wake, hayati Magufuli alikuwa na majina mengi ya utani, kama vile Tingatinga, Chuma, Mwamba, nk hayo yote alipewa na wananchi katika kutambua uchapaji kazi wake.
Siku moja akiwa Singida (akiwa Rais tayari) akajipa jina la utani yeye mwenyewe kwa kujiita JIWE. Ni kama aliongea kwa utani lakini jina la Jiwe linaishi mpaka leo.
Kwanini alijiita jiwe? Na aliposema " sitishwi wala sitishiki" aliwalenga akina nani waliokuwa wanamtishia?