Jaribu la hayati Rais Magufuli na jaribu la Ayubu

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
JARIBU LA HAYATI RAIS MAGUFULI NA JARIBU LA AYUBU.

Leo 13:15hrs 04/02/2023

Jaribu la Hayati Rais John Pombe Magufuli linakuja kwenye kutajwa kwake mara kwa mara,penye hoja na pasipokuwa na hoja,lakini jaribu hili linakuja akiwa hayupo,pengine angetamani awe hai ili aweze kujibu hoja zake,aliondoka akiacha uhakika kuwa yeye ni mmoja wa viongozi wachache sana wazalendo wa kweli kwa wananchi wanyonge Nchi nzima ya Tanzania,kwa namna hii hata mimi ningependa kumtaja lakini zaidi viongozi wengi wangependa kumtaja ili kujipima mbele za Wananchi wa Tanzania,ukitaka kukanekti na wananchi basi lazima umtaje Rais Magufuli ili kujiweka sawa kwenye uongozi na Wananchi waweze kukuelewa,bila kutaja jina la Rais Magufuli basi Wananchi hawawezi kukuelewa.

Ni dhahiri uwe na hoja usiwe na hoja utamtaja tu,iwe alikuziba mdomo wakati wa kula au hakukuziba mdomo utamtaja tu,uwe unampenda au haumpendi utamtaja tu,hivyo basi jaribu la Hayati Magufuli linakuja kwenye kutajwa tajwa kwake kwa kusifiwa na kwa kubagazwa ikiwa ametenda au hakutenda,hili ni jaribu ambalo Mungu ameliruhusu lije kwa Hayati Rais Magufuli akiwa amelala milele,jaribu hili lina utofauti na majaribu mengine kama jaribu lililoruhusiwa kwa Ayubu kwa maana ya uhai na umauti,jaribu la Ayubu lilimfanya ailaani siku aliyozaliwa na jaribu lile lilimfanya Ayubu atamani kufa lakini Mungu aliendelea kumuweka hai na baadae aliyashinda majaribu yale,lakini akiwa katikati ya jaribu alitamani atokee mtu wa kumtetea lakini hakutokea hadi baadae alishinda jaribu lile kwa sifa na utukufu wa Mungu,ebu tujikumbushe jaribu lililoruhusiwa kwa Ayubu akiwa angali bado yu hai na akalishinda.

-Jaribu la Ayubu na kutajwa tajwa kwake.

Siku moja wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Wana wa Mungu hawa wanaotajwa hapa ni malaika wa Mungu na ni neno linalotumika kwenye Agano la Kale kumaanisha malaika (Mwanzo 6:1-4; Ayubu 38:7). Tukio hilo lilifanyika mbinguni (Ayubu 6-12) Mungu anamsifia Ayubu mbele za Shetani, Anamwambia katika kuzunguka kwake duniani yupo mmoja ambaye anamcha Mungu licha ya kuwa dunia imejaa uovu. Shetani anapingana na Mungu kuwa si kweli kuwa Ayubu anamcha Mungu bure bure,Sababu anazotoa Shetani ni kuwa Ayubu anamcha Mungu kwa sababu Mungu amembariki sana,amemlinda pande zote,Hivyo ni baraka tu na ulinzi wa Mungu unaomfanya Ayubu amche Mungu.Shetani naye alijihudhurisha katikati yao. Shetani anamwambia Mungu kuwa uchaji wa Ayubu hautoki ndani bali ni kwa sababu anabarikiwa na analindwa na Mungu. Hivyo anamwambia Mungu anyooshe mkono wake na kuyagusa (kuyaondoa/kuyaharibu) yote aliyobarikiwa na Mungu na ndipo Ayubu atamkufuru Mungu,Mungu anamruhusu Shetani kutenda hayo aliyoyapendekeza kwa kuwa yamo mikononi mwake,Hapa tunaona kuwa mtenda maovu na mleta maovu ni Shetani. Mungu huwa anaruhusu tu, na kuondoa ulinzi waka ndipo Shetani anapata nafasi ya kufanya uharibifu.

-Marafiki wa Ayubu,Bildadi,Sofari na Elifazi wamtuhumu Ayub kutenda dhambi,

Majibu na Lawama za Elifazi kwa Ayubu (Ayub 4: 1-6),Elifazi anamshutumu Ayubu kuwa maneno yake anayoyasema kuwa ni maneno matupu tu yasiyo na maana yoyote ile,Hivyo hawakuwa wakiyatilia maanani kwa kuwa yalitoka midomoni mwa mtu aliyekuwa akijihesabia haki wakati alikuwa ni mwovu tu,Anamshutumu Ayubu kukosa hofu ya Mungu na pia kutompa Mungu ibada anayostahili,Zaidi anamwona Ayubu kuwa ni mtu ambaye dhambi zake alizofanya ndizo zinampa maneno ya kujitetea. Yaani kakosea ila anajaribu kujitetea ili kuficha maovu yake,Hivyo basi wanamwona Ayubu kuwa hata kinywa chake kinamhukumu yeye mwenyewe kutokana na hayo anayoyasema.

Bildadi anamkemea Ayubu (Ayub 8: 1-7),Huu ni ushauri wa kwanza wa Bildadi Mshushi kwenda kwa Ayubu. Huyu Bildadi anadhaniwa kuwa ni wa uzao wa Sua ambaye alikuwa ni mtoto wa Ibrahimu (Mwanzo 25:1-2),Anamkemea Ayubu kutokana na majibu yake kwa Elifazi. Anayataja maneno ya Ayubu kama upepo mkuu. Aliyaona maneno ya Ayubu kuwa ni makali na yenye nguvu,Bildadi anamwambia Ayubu ajaribu kuwaza na kutafakari kuhusu Mungu. Je, Mungu huwa anapotosha hukumu? Anasema Mungu ni mwenye haki kabisa,Hata vifo vya watoto wake Ayubu, tunaona Bildadi anadhani ni kwa sababu ya dhambi zao na wala si kingine chochote kile,Wazo la Bildadi ni lile lile kama la wenzake kuwa ni kwa sababu ya dhambi ndiyo maana Ayubu anapitia mateso. Mungu mwenye haki hawezi kumhukumu hivi hivi bila kosa lolote lile,Bildadi anamwambia kama Ayubu angemtafuta Mungu kwa bidii na kumwomba na pia kama angekuwa safi na mwelekevu wa moyo basi Mungu angesimama na kumtetea (Ayubu 8. 5-6). Kwa kusema hivi Bildadi anamshuku Ayubu kuwa kuna dhambi ameifanya tu.

Maneno ya Sofari kwa Ayubu,Sofari anamwambia Ayubu kuwa alistahili mapigo zaidi ya hayo (Ayub 11: 1-6),Sofari alikuwa miongoni mwa marafiki zake na Ayubu. Huyu aliongea kidogo sana kulinganisha na wenzake, lakini maneno yake yalikuwa makali sana na yasiyo na huruma kwa Ayubu,Sofari anamwambia Ayubu kuwa ni mwingi wa maneno na mwenye kujivuna/kujihesabia haki. Hivyo inapaswa ajibiwe kikamilifu kabisa,Marafiki watatu wa Ayubu walikuwa wakimsisitiza kuwa kuna dhambi nyuma yake aliyoifanya na yeye Ayubu alikuwa akikana. Namna walivyokazia zaidi na Ayubu alikana zaidi hivyo kupelekea sasa majibizano kuwa makali,Sofari anamwambia Ayubu kuwa kutokana na kujihesabia haki na kutotaka kukiri uovu wake basi alistahili adhabu kali zaidi ya hiyo.

Sofari anamfundisha Ayubu Theolojia (Ayubu 7-12) hii ilikuwa sawa na Chekea kumfundisha form six,Sofari anamweleza kuhusu ukuu wa Mungu na upeo wake mkubwa na kuinuliwa juu sana (transcendence). Hivyo Ayubu hawezi kumzidi Mungu maarifa. Ayubu hakupaswa kumuuliza Mungu chochote kile,Pia anamweleza kuhusu nguvu za Mungu kuwa Yeye ana mamlaka kamili kabisa na hana wa kumzuia chochote kile (sovereignty). Hivyo Ayubu anapaswa akubaliane tu na adhabu hiyo,Pia anamweleza kuhusu uwezo wa Mungu kujua mambo yote kabisa (omniscient). Kwamba anafahamu mambo hata ambayo hatuyajui. Anaona uovu na anawajua waovu pia. Hivyo hata Ayubu akijificha kuwa hana dhambi machoni pao, Mungu bado anamtambua na ndiyo maana kamuadhibu,Sofari anamwona Ayubu kama mjinga ambaye atapata ufahamu endapo punda mwitu wataanza kuzaa wanadamu.

Maisha yana majaribu na changamoto za aina mbalimbali. Kushinda jaribu la kwanza siyo mwisho wa kujaribiwa,Ukishinda jaribu jua litakuja lingine tena, maadamu upo hapa duniani. Kikubwa sana ni kuendelea kusimama kwa imani na kusonga mbele kwa msaada wa Mungu,Ayubu alipewa tena jaribu lingine kubwa lililougusa mwili wake moja kwa moja baada ya kushinda lile lililotangulia,Hata Yesu alipojaribiwa mara ya kwanza kule mlimani, maandiko yanasema aliposhinda yale majaribu , Shetani aliondoka *na kumwacha kwa muda tu,ikiwa na maana alikuja tena huko mbeleni kumjaribu tena na tena (Luka 4:13),Neno la msingi ni hili *“Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.” - Zaburi 34:19 (Biblia Takatifu,Shetani anaweza kuleta magonjwa na kutesa watu kwa magonjwa,Huu ni ukweli usiopingika. Si kila ugonjwa unaletwa na natural causes (sababu za kawaida), mwingine ni Shetani kabisa anawapiga watu kwa ugonjwa,Kisa cha mwanamke huyu,Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa,Luka 13:11 (Biblia Takatifu),Ukiangalia hapo unaona chanzo cha ugonjwa wake kilikuwa ni mapepo yalivaa sura ya ugonjwa na yakamfanya aonekane mgonjwa. Bwana Yesu alipomwombea na kumkemea yule pepo, huyo mama aliponywa papo hapo.

Hakuna chochote kiwezacho kuondoa dhambi isipokuwa damu ya Yesu Kristo,Ayubu anasema ingawaje atajiosha kwa maji ya theluji na sabuni lakini uovu wake hauwezi kuondoka,Huo ni ukweli kabisa hakuna kitu chochote kiwezacho kuondoa dhambi isipokuwa damu ya Yesu Kristo,“bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi,na damu yake Yesu, Mwana wake,yatusafisha dhambi yote,1 Yohana 1:7 (Biblia Takatifu)Tunayo ahadi ya mwombezi/mpatanishi ambaye ni Yesu Kristo,Ayubu hakujua kuhusu ufunuo huu. Tunaye mwombezi/mpatanishi anayeweza kusimama kwa ajili yetu katika maombi na kutupatanisha mbele za Mungu,Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu naso wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;1 Timotheo 2:5 (Biblia Takatifu),Mpatanishi wetu Yesu Kristo anazo sifa zote za upatanishi na anafaa kuwa mpatanishi wetu,Mapatanishi lazima akubalike na pande zote,Mpatanishi lazima aruhusiwe kutatua tatizo lote kikamilifu,Mpatanishi lazima awe na uwezo wa kuhusiana na pande zote mbili,Mpatanishi lazima awe na shauku ya kuona mwisho mwema wa upatanishi wake,Hayo yote Bwana Yesu aliyatimiza. Na hata sasa ndiye mpatanishi wetu na Mungu,Tumwendee Yeye pale tunapomkosea Mungu Ili tupatanishwe na Yeye.

1 Yohana 2 (Biblia Takatifu)¹ Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,² naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Nimalizie kwa neema ya toba,Kuna uhusiano mkubwa kati ya damu inayomwagika juu ya nchi (ardhi) pasipo hatia na hali ya nchi (ardhi) ambayo imepokea damu hiyo,Maombi ya Ayubu yalikuwa ni kwamba damu yake isifunikwe na nchi. Isisahaulike. Iendelee kunena na kudai haki yake,Ukitazama maneno haya yanafanana na yale ambayo Mungu alisema kwa Kaini kwenye,Akasema, Umefanya nini? *Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi,Mwanzo 4:10 (Biblia Takatifu),Damu ya Habili ilikuwa inamlilia Mungu juu ya kisasi,Damu ni uhai. Na Mungu alikataza damu ya mtu asiye na hatia isimwagwe juu ya nchi kwa kuwa italeta laana,isije ikamwagika damu ya asiye makosa kati ya nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi, ikawa na damu juu yako,Kumbukumbu la Torati 19:10 (Biblia Takatifu),Kuna wakati taifa la Israeli lilipata shida miaka mitatu kwa sababu ya shida kama hiyo ambapo damu ya watu wasio na hatia ilimwagika,Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni,2 Samweli 21:1 (Biblia Takatifu)

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Magufuli alikataliwa na Mungu mwenyewe kwa sababu alipopata madaraka kidogo akajifanya mungu-mtu.

Huwezi kuiba uchaguzi wa 2020 wote, unauwa wapinzani, unafukuza watu kazi, unaiba fedha za wafanya biashara halafu Mungu akakuacha.

Ile ni TAKA TAKA iache iendelee kuoza huko Chato
 
Magufuli alikayataliwa na Mungu mwenyewe kwa sababu alipopata madaraka kidogo akajifanya mungu-mtu.

Upuuzi wako ufiche
 
Laiti mngejua mnamchongea huyo jamaa kwa Mungu muumba kwa kulinganisha matendo na maneno matakatifu na maushenzi wa huyo jamaa! Mnapata dhambi na huyo jamaa yenu anachomeka huko na nyie mnamchongea tu
 
Acha wapumbavu waendelee kuhukumu,lkn mungu ndie anajua,magufuli kwa mda mfupi alifanikiwa kujitengeneazea maadui wengi sana,na hii ni kwa aababu ya uadilifu wake,
 
Katibu Wa Itikadi Na Uenezi
Nimempa Number Yako Angalau Upewe Mkoa Wa Shinyanga Uache Kupiga Kelele JF
 
Ficha upumbavu wako
Umeandika pumba tupu halafu nakushauri unamiambia nifiche upumbavu.

Angalia mada Ina masaa takriban mawili ila ina posts 8 kutoka kwa wachangiaji 3.

HIZI ni PUMBA tu peleka kwa NGURUWE au kwa wanao wale
 
Umeandika pumba tupu halafu nakushauri unamiambia nifiche upumbavu.

Angalia mada Ina masaa takeinan mawili Ina posts 8 kutoka kwa wachangiaji 3.

HIZI ni PUMBA tu peleka kwa NGURUWE au kwa wanao wale
Nasema ficha upumbavu wako
 
Watu awa waliokimbia zaidi ya kilomita kumpa heshima ya mwisho Rais Magufuli,kama hawakuwa binadamu basi walikuwa ni Malaika waliotumwa na Mungu na ipo siku watu hao au Malaika hao watakuja tena kumtetea Hayati Rais Magufuli.
 
Attachments

  • VID-20230204-WA0358.mp4
    17.6 MB
JARIBU LA HAYATI RAIS MAGUFULI NA JARIBU LA AYUBU.

Leo 13:15hrs 04/02/2023

Jaribu la Hayati Rais John Pombe Magufuli linakuja kwenye kutajwa kwake mara kwa mara,penye hoja na pasipokuwa na hoja,lakini jaribu hili linakuja akiwa hayupo,pengine angetamani awe hai ili aweze kujibu hoja zake,aliondoka akiacha uhakika kuwa yeye ni mmoja wa viongozi wachache sana wazalendo wa kweli kwa wananchi wanyonge Nchi nzima ya Tanzania,kwa namna hii hata mimi ningependa kumtaja lakini zaidi viongozi wengi wangependa kumtaja ili kujipima mbele za Wananchi wa Tanzania,ukitaka kukanekti na wananchi basi lazima umtaje Rais Magufuli ili kujiweka sawa kwenye uongozi na Wananchi waweze kukuelewa,bila kutaja jina la Rais Magufuli basi Wananchi hawawezi kukuelewa.

Ni dhahiri uwe na hoja usiwe na hoja utamtaja tu,iwe alikuziba mdomo wakati wa kula au hakukuziba mdomo utamtaja tu,uwe unampenda au haumpendi utamtaja tu,hivyo basi jaribu la Hayati Magufuli linakuja kwenye kutajwa tajwa kwake kwa kusifiwa na kwa kubagazwa ikiwa ametenda au hakutenda,hili ni jaribu ambalo Mungu ameliruhusu lije kwa Hayati Rais Magufuli akiwa amelala milele,jaribu hili lina utofauti na majaribu mengine kama jaribu lililoruhusiwa kwa Ayubu kwa maana ya uhai na umauti,jaribu la Ayubu lilimfanya ailaani siku aliyozaliwa na jaribu lile lilimfanya Ayubu atamani kufa lakini Mungu aliendelea kumuweka hai na baadae aliyashinda majaribu yale,lakini akiwa katikati ya jaribu alitamani atokee mtu wa kumtetea lakini hakutokea hadi baadae alishinda jaribu lile kwa sifa na utukufu wa Mungu,ebu tujikumbushe jaribu lililoruhusiwa kwa Ayubu akiwa angali bado yu hai na akalishinda.

-Jaribu la Ayubu na kutajwa tajwa kwake.

Siku moja wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Wana wa Mungu hawa wanaotajwa hapa ni malaika wa Mungu na ni neno linalotumika kwenye Agano la Kale kumaanisha malaika (Mwanzo 6:1-4; Ayubu 38:7). Tukio hilo lilifanyika mbinguni (Ayubu 6-12) Mungu anamsifia Ayubu mbele za Shetani,Anamwambia katika kuzunguka kwake duniani yupo mmoja ambaye anamcha Mungu licha ya kuwa dunia imejaa uovu.Shetani anapingana na Mungu kuwa si kweli kuwa Ayubu anamcha Mungu bure bure,Sababu anazotoa Shetani ni kuwa Ayubu anamcha Mungu kwa sababu Mungu amembariki sana,amemlinda pande zote,Hivyo ni baraka tu na ulinzi wa Mungu unaomfanya Ayubu amche Mungu.Shetani naye alijihudhurisha katikati yao. Shetani anamwambia Mungu kuwa uchaji wa Ayubu hautoki ndani bali ni kwa sababu anabarikiwa na analindwa na Mungu. Hivyo anamwambia Mungu anyooshe mkono wake na kuyagusa (kuyaondoa/kuyaharibu) yote aliyobarikiwa na Mungu na ndipo Ayubu atamkufuru Mungu,Mungu anamruhusu Shetani kutenda hayo aliyoyapendekeza kwa kuwa yamo mikononi mwake,Hapa tunaona kuwa mtenda maovu na mleta maovu ni Shetani. Mungu huwa anaruhusu tu, na kuondoa ulinzi waka ndipo Shetani anapata nafasi ya kufanya uharibifu.

-Marafiki wa Ayubu,Bildadi,Sofari na Elifazi wamtuhumu Ayub kutenda dhambi,

Majibu na Lawama za Elifazi kwa Ayubu (Ayub 4: 1-6),Elifazi anamshutumu Ayubu kuwa maneno yake anayoyasema kuwa ni maneno matupu tu yasiyo na maana yoyote ile,Hivyo hawakuwa wakiyatilia maanani kwa kuwa yalitoka midomoni mwa mtu aliyekuwa akijihesabia haki wakati alikuwa ni mwovu tu,Anamshutumu Ayubu kukosa hofu ya Mungu na pia kutompa Mungu ibada anayostahili,Zaidi anamwona Ayubu kuwa ni mtu ambaye dhambi zake alizofanya ndizo zinampa maneno ya kujitetea. Yaani kakosea ila anajaribu kujitetea ili kuficha maovu yake,Hivyo basi wanamwona Ayubu kuwa hata kinywa chake kinamhukumu yeye mwenyewe kutokana na hayo anayoyasema.

Bildadi anamkemea Ayubu (Ayub 8: 1-7),Huu ni ushauri wa kwanza wa Bildadi Mshushi kwenda kwa Ayubu. Huyu Bildadi anadhaniwa kuwa ni wa uzao wa Sua ambaye alikuwa ni mtoto wa Ibrahimu (Mwanzo 25:1-2),Anamkemea Ayubu kutokana na majibu yake kwa Elifazi. Anayataja maneno ya Ayubu kama upepo mkuu. Aliyaona maneno ya Ayubu kuwa ni makali na yenye nguvu,Bildadi anamwambia Ayubu ajaribu kuwaza na kutafakari kuhusu Mungu. Je, Mungu huwa anapotosha hukumu? Anasema Mungu ni mwenye haki kabisa,Hata vifo vya watoto wake Ayubu, tunaona Bildadi anadhani ni kwa sababu ya dhambi zao na wala si kingine chochote kile,Wazo la Bildadi ni lile lile kama la wenzake kuwa ni kwa sababu ya dhambi ndiyo maana Ayubu anapitia mateso. Mungu mwenye haki hawezi kumhukumu hivi hivi bila kosa lolote lile,Bildadi anamwambia kama Ayubu angemtafuta Mungu kwa bidii na kumwomba na pia kama angekuwa safi na mwelekevu wa moyo basi Mungu angesimama na kumtetea (Ayubu 8. 5-6). Kwa kusema hivi Bildadi anamshuku Ayubu kuwa kuna dhambi ameifanya tu.

Maneno ya Sofari kwa Ayubu,Sofari anamwambia Ayubu kuwa alistahili mapigo zaidi ya hayo (Ayub 11: 1-6),Sofari alikuwa miongoni mwa marafiki zake na Ayubu. Huyu aliongea kidogo sana kulinganisha na wenzake, lakini maneno yake yalikuwa makali sana na yasiyo na huruma kwa Ayubu,Sofari anamwambia Ayubu kuwa ni mwingi wa maneno na mwenye kujivuna/kujihesabia haki. Hivyo inapaswa ajibiwe kikamilifu kabisa,Marafiki watatu wa Ayubu walikuwa wakimsisitiza kuwa kuna dhambi nyuma yake aliyoifanya na yeye Ayubu alikuwa akikana. Namna walivyokazia zaidi na Ayubu alikana zaidi hivyo kupelekea sasa majibizano kuwa makali,Sofari anamwambia Ayubu kuwa kutokana na kujihesabia haki na kutotaka kukiri uovu wake basi alistahili adhabu kali zaidi ya hiyo.

Sofari anamfundisha Ayubu Theolojia (Ayubu 7-12) hii ilikuwa sawa na Chekea kumfundisha form six,Sofari anamweleza kuhusu ukuu wa Mungu na upeo wake mkubwa na kuinuliwa juu sana (transcendence). Hivyo Ayubu hawezi kumzidi Mungu maarifa. Ayubu hakupaswa kumuuliza Mungu chochote kile,Pia anamweleza kuhusu nguvu za Mungu kuwa Yeye ana mamlaka kamili kabisa na hana wa kumzuia chochote kile (sovereignty). Hivyo Ayubu anapaswa akubaliane tu na adhabu hiyo,Pia anamweleza kuhusu uwezo wa Mungu kujua mambo yote kabisa (omniscient). Kwamba anafahamu mambo hata ambayo hatuyajui. Anaona uovu na anawajua waovu pia. Hivyo hata Ayubu akijificha kuwa hana dhambi machoni pao, Mungu bado anamtambua na ndiyo maana kamuadhibu,Sofari anamwona Ayubu kama mjinga ambaye atapata ufahamu endapo punda mwitu wataanza kuzaa wanadamu.

Maisha yana majaribu na changamoto za aina mbalimbali. Kushinda jaribu la kwanza siyo mwisho wa kujaribiwa,Ukishinda jaribu jua litakuja lingine tena, maadamu upo hapa duniani. Kikubwa sana ni kuendelea kusimama kwa imani na kusonga mbele kwa msaada wa Mungu,Ayubu alipewa tena jaribu lingine kubwa lililougusa mwili wake moja kwa moja baada ya kushinda lile lililotangulia,Hata Yesu alipojaribiwa mara ya kwanza kule mlimani, maandiko yanasema aliposhinda yale majaribu , Shetani aliondoka *na kumwacha kwa muda tu,ikiwa na maana alikuja tena huko mbeleni kumjaribu tena na tena (Luka 4:13),Neno la msingi ni hili *“Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.” - Zaburi 34:19 (Biblia Takatifu,Shetani anaweza kuleta magonjwa na kutesa watu kwa magonjwa,Huu ni ukweli usiopingika. Si kila ugonjwa unaletwa na natural causes (sababu za kawaida), mwingine ni Shetani kabisa anawapiga watu kwa ugonjwa,Kisa cha mwanamke huyu,Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa,Luka 13:11 (Biblia Takatifu),Ukiangalia hapo unaona chanzo cha ugonjwa wake kilikuwa ni mapepo yalivaa sura ya ugonjwa na yakamfanya aonekane mgonjwa. Bwana Yesu alipomwombea na kumkemea yule pepo, huyo mama aliponywa papo hapo.

Hakuna chochote kiwezacho kuondoa dhambi isipokuwa damu ya Yesu Kristo,Ayubu anasema ingawaje atajiosha kwa maji ya theluji na sabuni lakini uovu wake hauwezi kuondoka,Huo ni ukweli kabisa hakuna kitu chochote kiwezacho kuondoa dhambi isipokuwa damu ya Yesu Kristo,“bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi,na damu yake Yesu, Mwana wake,yatusafisha dhambi yote,1 Yohana 1:7 (Biblia Takatifu)Tunayo ahadi ya mwombezi/mpatanishi ambaye ni Yesu Kristo,Ayubu hakujua kuhusu ufunuo huu. Tunaye mwombezi/mpatanishi anayeweza kusimama kwa ajili yetu katika maombi na kutupatanisha mbele za Mungu,Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu naso wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;1 Timotheo 2:5 (Biblia Takatifu),Mpatanishi wetu Yesu Kristo anazo sifa zote za upatanishi na anafaa kuwa mpatanishi wetu,Mapatanishi lazima akubalike na pande zote,Mpatanishi lazima aruhusiwe kutatua tatizo lote kikamilifu,Mpatanishi lazima awe na uwezo wa kuhusiana na pande zote mbili,Mpatanishi lazima awe na shauku ya kuona mwisho mwema wa upatanishi wake,Hayo yote Bwana Yesu aliyatimiza. Na hata sasa ndiye mpatanishi wetu na Mungu,Tumwendee Yeye pale tunapomkosea Mungu Ili tupatanishwe na Yeye.
1 Yohana 2 (Biblia Takatifu)¹ Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,² naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Nimalizie kwa neema ya toba,Kuna uhusiano mkubwa kati ya damu inayomwagika juu ya nchi (ardhi) pasipo hatia na hali ya nchi (ardhi) ambayo imepokea damu hiyo,Maombi ya Ayubu yalikuwa ni kwamba damu yake isifunikwe na nchi. Isisahaulike. Iendelee kunena na kudai haki yake,Ukitazama maneno haya yanafanana na yale ambayo Mungu alisema kwa Kaini kwenye,Akasema, Umefanya nini? *Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi,Mwanzo 4:10 (Biblia Takatifu),Damu ya Habili ilikuwa inamlilia Mungu juu ya kisasi,Damu ni uhai. Na Mungu alikataza damu ya mtu asiye na hatia isimwagwe juu ya nchi kwa kuwa italeta laana,isije ikamwagika damu ya asiye makosa kati ya nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi, ikawa na damu juu yako,Kumbukumbu la Torati 19:10 (Biblia Takatifu),Kuna wakati taifa la Israeli lilipata shida miaka mitatu kwa sababu ya shida kama hiyo ambapo damu ya watu wasio na hatia ilimwagika,Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni,2 Samweli 21:1 (Biblia Takatifu)

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Umeandika upimbi mtupu , sema tu hongera kwa kujipatia buku 7 hapo Lumumba... Mtu aliye wadhulumu wahanga wa tetemeko la aridhi bukoba unamfananisha na Ayubu ... Ni wp uliwahi kusoma Ayubu alikula lambi lambi ?? Mnyambuda weee

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yako mama/baba angefungwa kwenye sandarusi umkute mtoni usingeandika hivi.Alitaka kumuua mwenzake ila alitangulia yeye.Sijui huko aliko yupo wapi but namuombea apate msamaha maana ule haukuwa ubinadamu.Hakujua kutenganisha siasa na maisha ya kawaida alishindwa kuiga mfano wa mzee wa Msega akajikuta anafanya mambo ya ajabu.Kuna maisha baada ya siasa/uongozi na kuna maisha baada ya kifo yote yatategemea na matendo yako
 
Kwenye udc hujaambulia chochote?
 
Kuna maisha baada ya siasa 100%
 
Magufuli alikayataliwa na Mungu mwenyewe kwa sababu alipopata madaraka kidogo akajifanya mungu-mtu.

Huwezi kuiba uchaguzi wa 2020 wote, unauwa wapinzani, unafukuza watu kazi, unaiba fedha za wafanya biashara halafu Mungu akakuacha.

Ile ni TAKA TAKA iache iendelee kuoza huko Chato

Una uhakika kuwa Mungu ndiye aliyemuua?
 
Back
Top Bottom