Kwanini Graphics Designer Wanashindwa Kutengeneza Pesa?

HabariTech

Member
Sep 1, 2019
8
21
Kama umewahi kujaribu kuanzisha biashara wewe mwenyewe utakuwa unaelewa ilivyo ngumu kuanzisha biashara yenye mafanikio. Aina ya biashara unaweza kuanzisha ni nyingi mno, kiasi kwamba wengi huwa hawajui wanaanzia wapi. Tukiongelea creators kama graphics designers, wanapoanza huwa wanakubali kazi ya kila aina, ili kupata walau kiasi kidogo cha pesa.

Lengo la wengi linaeleweka ni kupata pesa, lakini shida ni ambapo hupati wateja wa mara kwa mara au wateja ulio wahi kufanya nao kazi, hawarudi tena kwako. Baada ya muda unaweza kuta huna kabisa wateja.

Unadhani ni kwanini unashindwa kufikia malengo wewe kama graphics designer?

Leo nataka ufahamu baadhi ya sababu za graphics designer kushindwa fikia ubora wao unaowaruhusu kutengeneza pesa mara kwa mara kwa kiasi kikubwa.

Husikilizi Wateja​

Designers huwa na hali kujiona wanajua kuzidi mteja, kwa kuwa mteja ndiye kamtafuta huyu designer. Hivyo lengo la designer huwa ni kutengeneza design nzuri zinazovutia machoni kwa mtazamaji. Wanachosahau ni kwamba mteja hatafuti kuwa na design ya kuambiwa, “Hii design ni nzuri.”, mteja anataka design inayotatuta matatizo yake.

Lengo la mteja wako ni kuifikia hadhira fulani, ili aweze kukamilisha lengo lake, hivyo wewe kama designer wajibu wako ni kuhakikisha unamsikiliza zaidi yeye sio unachotaka wewe. Kama hujamsikiliza mteja unategemea utaweza vipi kumpa kile anataka?

Kuchelewesha Kazi​

Ukitaka kuwakosa kabisa wateja wako, chelewesha kazi zao. Mteja amekutafuta utengeneza deisgns kwa ajili ya kampeni yake binafsi ambayo ina udhibiti wa muda alafu wewe unachelewesha. Ni lazima huyu mteja ataenda kutafuta mtu mwingine afanye kazi zake anapohitaji tena hiyo huduma.

Hivyo hakikisha unapanga muda wako vizuri uweze kamilisha kazi za wateja wako ndani ya muda mlio kubaliana.

Kukosa Ubunifu Mpya​

Mteja anakufuata wewe kwa kuwa ameona una kazi zenye ubunifu mzuri. Angehitaji kazi zenye design zile zile za kila siku angetafuta designer wa kila siku. Hivyo wewe kama Designer usimuangushe mteja wako kwa kumpa kazi ya kawaida.

Jitahidi umpe kazi inayotatua matatizo yake katika namna ya kipekee.

Hujafanya tafiti ya kutosha kuelewa industry ya mteja wako​

Sifa ya graphics designers ni kuweza fanya tafiti kabla ya kuandaa design ya aina yoyote ile. Hii ni kwa sababu kila mteja anakuja kwako akitokea katika industry yake mwenyewe. Huwezi tumia aina ya designs za mafuta ya gari kwa mteja anayepigania kuokoa mazingira.

Ulinganisho wa Thamani na kile unatoa haupo​

Ushawahi kwenda nunua kitu ukauziwa bei kubwa, unalipia lakini unajua kabisa hiyo bei imezidi mno kuliko thamani ya kile umepata?

Hata mteja wako atajisikia hivyo akiona anacholipa na anachopata kuna utofauti wa thamani. Hii itafanya upoteze wateja kwa mshindani wako. Ili kuendelea kubaki kama mshindani sokoni ni lazima uonyesha kwamba unatoa thamani kuzidi wengine. Hii ni njia moja nzuri sana ya kuhakikisha mteja anabaki kwako.

Ni ngumu kufanya kazi na Wewe​

Wewe sio Leonardo Da Vinci au Picasso, hivyo hakuna nafasi ya wewe kujiona ni wa muhimu sana kuzidi wengine au wateja wako. Hali ya kujiona wewe ni bora kuliko mteja wako, iache kitandani unapoamka.

Mteja hana bahati ya kufanya kazi na wewe ila wewe ndiye una bahati ya kufanya kazi na huyo mteja. Jenga uhusiano mzuri na mteja wako, kiasi kwamba akitaka kutoa kazi kwa mwingine aone kama anakuibia hivi kuto leta hiyo kazi kwako.

Sababu Nyingine za Kushindwa Kama Designer ni Hizi​

Hujitangazi​

Kumbuka unafanya biashara kama ilivyo biashara nyingine. Siri ya mafanikio ya biashara ni kujitangaza ili watu wajue kuhusu biashara yako. Tumia vizuri mitandao ya kijamii kutangaza kazi zako.

Unapanga bei ndogo mno​

Hili ni eneo linasumbua designers wengi wanaoanza. Wengi hujikuta wanaumia kwa kufanya kazi nyingi kwa malipo kidogo. Hii inatokana na kutojenga jamii na designers wengine na kutofanya tafiti ya kutosha kujua njia sahihi ya upangaji wa bei.’

Hauna njia sahihi za malipo​

Sio kila mteja anatumia njia ya malipo uliyo nayo. Mteja wa Tanzania anakuuliza, “Nitumie Njia Ipi kufanya Malipo?” wewe unamwambia paypal. Unasahau kwamba hiyo haitumiki Tanzania. Jitahidi kuwa na zaidi ya njia 3 za malipo zinazotofautiana, ili usipishane na pesa anapokuja mteja.

Hujajiweka kama professional​

Kuwa na muonekano wa professional ni muhimu kwa kuwa ni kitu cha kwanza mteja anaona kutoka kwako. Mteja anataka kukuona kama ni mtu anayeweza kukuamini. Sio unaenda kuonana na mteja muonekano wako upo kama wa kibaka, hata mteja atapata wasiwasi kukukabidhi pesa yake.

Vaa vizuri na ujitahidi kuwa nadhifu mara kwa mara itasaidia kujenga imani kwa wateja wako.

Mwisho​

Graphics Designing sasa hivi ni eneo lenye uhitaji sana hapa Tanzania. Kama ni hivyo ina maana ya kwamba ni eneo lenye pesa ya kutosha wote waliopo katika tasnia hii. Hivyo hakuna sababu ya wewe kama designer kushindwa fikia ubora wako uweze kujipatia kipato.

Muhimu kumbuka kwamba kila unachokifanya kinaelezea biashara/kazi yako. Pia ni muhimu uelewe kwamba tasnia ya designing inahitaji mazoezi ya kutosha ili kuendelea kujiweka vizuri sokoni. Kwa sababu hiyo ni muhimu kufanya ubunifu mara kwa mara.
 
Cha kwanza ni creativity yako wewe mwenyewe Mtoa huduma maana kuna wengine skrill ziko below sana na pili ni jinsi ya kubargain malipo na mteja, hapa ndio pakubwa wanapofeli...
 
Sikupingi katika hili. Wengi wanafeli hasa katika ubora wa skills zao. Unakuta mtu anatumia premium pricing, lakini anatoa kazi za hovyo sana.
 
Umeandika mengi ila tambua haya.

Graphics designer mwenye mafanikio kibongo bongo ni yule anaefanya uwekezaji kwenye vitendea kazi na si ujuzi pekee.

Tafuta printer, mashine za tshirt press, ukiweza large format printer, na nyinginezo hapo ndio utaona faida na wateja walipo.

Usipokua na hivyo vitu utajikuta unapokea hata 5000 ku design logo na stickers.
 
Umeongeza kitu cha muhimu sana mtaalamu
 
Pia biashara haina formula, cha muhimu hakikisha tatizo lipo wapi, then solve tatizo utapata wateja. Kuna watu wajeuri na biashara zao watu wanapanga foleni.
Nadhani itakuwa ni namna unazungumza na wateja na package zako zinabeba offer ipi.
 
Back
Top Bottom