Kwanini Dkt. Kalemani alipokuwa ofisi za TANESCO - Geita alivaa barakoa na alipoenda kanisani kujumuika na Rais Magufuli akaivua?

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Hili Jambo limenishangaza kidogo.!

Dr. Kaleman leo akiwa Ofisi za TANESCO-GEITA alivaa Barakoa pamoja na wote waliokuwa nae lakini ameenda Kanisani kujumuika na Raisi akavua na kuonesha hali ni shwari na wale wote waliokuwa Kanisani leo hawakuwa na Wala hawakuvaa Barakoa, kuna kitu kilipangwa au?
 
Hili Jambo limenishangaza kidogo.!

Dr. Kaleman leo akiwa Ofisi za TANESCO-GEITA alivaa Barakoa lakini ameenda Kanisani kujumuika na Raisi akavua na kuonesha hali ni shwari wale wote waliokuwa Kanisani leo hawakuwa na Wala hawakuvaa Barakoa, kuna kitu kilipangwa au?
Kalemani na wengine kama yeye wanaishi kwa kujipendekeza kwa John. Hata wakiambiwa walambe viatu vya John, wapo tayari muda wowote.
Uoga mbaya sana
 
Kanisani kuna ulinzi wa Mungu barakoa za nini?!
Mungu kwa nini hakuwapaisha wanaisrael kutoka Misri kwenda Kanani badala yake wakatembea kwa miaka 40 Jangwani tena kwa miguu na wengine wakifia humo humo Jangwani?

Na ni kwa nini Yesu alipoambiwa na shetani ageuze jiwe liwe mkate alikataa kwa hoja kwamba imeandikwa "usimjaribu bwana Mungu wako"?
 
Kumkubalia shetani ndio kumjaribu Mungu... Corona ni shetani!
 
Inaonekana kulikuwa na maagizo hapo kanisani watu wasivae..
Haiwezekani asiwepo mtu hata mmoja alievaa..

Kwahiyo hata hotuba yake ilikuwa well scripted..
Kaongea kama bahati mbaya but ilikuwa planned
 
Shetani alipojiudhurisha mbele ya Mungu pamoja na wana wa Mungu shetani alikuwa amekubaliwa na MUNGU? Kwani ule mfano wa Yesu wa "msamaria mwema" zile sio tiba? Kristo ni badala ya maelekezo madaktari?
Yesu anatibu roho na automatically mwili pia unapona.

Barakoa haitibu chochote ni ushuhuda wa uwoga mbele za Mungu..... Lakini ukiwa Bar vaa barakoa maana huko ni makao ya shetani!
 
Hili Jambo limenishangaza kidogo.!

Dr. Kaleman leo akiwa Ofisi za TANESCO-GEITA alivaa Barakoa pamoja na wote waliokuwa nae lakini ameenda Kanisani kujumuika na Raisi akavua na kuonesha hali ni shwari na wale wote waliokuwa Kanisani leo hawakuwa na Wala hawakuvaa Barakoa, kuna kitu kilipangwa au?
Ni kwasababu Dr.Kalemani anaipenda kazi yake kuliko anavyoupenda uhai wake.
 
Back
Top Bottom